Magufuli versus Tundu Lissu; yupi unamwamini kwenye sakata la makinikia?

Magufuli ameongea kwa reference ya Tume ya wataalamu...lakini pia kumbuka ni mkemia mwanasayansi tofauti na ngwini Lissu.
Mkemia sawa kisheria je. Kati ya sheria na kemia kipi hakituletei hasara? Sasa ona inaonekana wewe ni ZUZU NAMBA MOJA CCM
 
Hili suala sioni wala silichukulii kimahakama huko unaenda mbali sana. Mfano observation za tume acacia anazipinga baadae serikali na Acacia wakubaliane warudie kupima under transparency grounds majibu yakikaribia au yakilingana na ya Tume hapo mahakama inaingia vipi. Watakubaliwna kuanzia siku hiyo waanze kulipa kwa terms za matokeo ya vipimo vipya ambavyo wote wameconcent. Ndicho pia acacia wanachosisitiza, mahakama zinaletwa na wanasiasa au zitakuja kama tukiendelea kushikilia huku tunagoma kumfanya muwekezaji aridhike kwa upandwake kupitia transparent sampling. Kwa baadae maana hikitulichofanya ni sahihi maana sisi ndio tulitaka kujilidhisha....
Unanipeleka kuanza kuona tatizo ndani yako. Unaonyesha hapa kwamba kumbe kuna room ya ACACIA na serikali kukaa na pengine kufanya upya huo unaouita "uchunguzi", sasa ni kwanini mnawaita wezi at this juncture?
 
Aliyesema ajira zitatangazwa baada ya mwezi namuamini maana ni mtu wa vitendo
 
ngwini kuitwa wakili msomi basi anadhani anajua kila kitu cha kwenye kila field...
Mbona hata mwanasheria wenu hajajitokeza kumpinga lisu kile alichoongelea juu ya accia. Anajua lisu yuko sahihi ila kwa sababu ya mfumo ananyamaza. Wewe bwege anashangilia nn. Fatilia siku lisu alipoongelea hili suala bungeni mwanasheria wenu alivyotulia kwa aibu hakusimama kutia neno. KIMYAAAAAA
 
Unanipeleka kuanza kuona tatizo ndani yako. Unaonyesha hapa kwamba kumbe kuna room ya ACACIA na serikali kukaa na pengine kufanya upya huo unaouita "uchunguzi", sasa ni kwanini mnawaita wezi at this juncture?
Nimekupa possibility Kuna room nyingi tu. Moja niserikali kuendelea mbele na yeye acacia afanye anachotaka ikibidi kwenda mahakamani kufanya kile unachokifikilia.
Kuna kufukuzwa kabisa
Kuna kumuonyesha kwamba tunachokisema ni sahihi na kama na yeye anapenda kujilidhisha tena tukiwa nae hakuna shida tumalize uchunguzi wetu tutampa nafasi

Mkuu Kuna possibility nyingi tu nashangaa unashangaa nini.

Kumbuka yote haya hadi hapa sio wala hayahusiani na mikataba. Maana hapo ni suala la Kuna nini na vingapi na ni kiasi gani.
 
Mbona hata mwanasheria wenu hajajitokeza kumpinga lisu kile alichoongelea juu ya accia. Anajua lisu yuko sahihi ila kwa sababu ya mfumo ananyamaza. Wewe bwege anashangilia nn. Fatilia siku lisu alipoongelea hili suala bungeni mwanasheria wenu alivyotulia kwa aibu hakusimama kutia neno. KIMYAAAAAA
Ampinge ili iweje wakati lisu anatoa comments kwenye non-legal issues huku akijua Kuna tume ya wabobezi wenzake wa sheria na uchumi bado wako jikoni. Anawahi nini?
 
Kumuamini Tundu Lissu unatakiwa uwe na kumbukumbu fupi sana. Lissu ndo mwaka juzi tu hapa alikiri kuwa alikuwa akiandaa data za uongo dhidi ya ufisadi wa kina Lowassa na Sumaye na kumpa Slaa. Baada ya kuona kuwa kumbe all the noise about ufisadi zilikuwa hila za uongo, Slaa akaamua kuachia ngazi na kina Lissu leo wapo na macho makavu.

Utafiti wa Kisayansi matokeo yake hupingwa na matokeo mengine ya Utafiti. Lissu anaongea kwa hisia tu bila kuwa na matokeo yoyote ya utafiti tumwaninije? Lissu huyo huyo wakati yuko LEAT alikuwa akilalamika wizi uko kwenye mchanga, leo analalamika wizi uko mgodini!!! Tunahitaji kuwa makini zaidi na wanasheria/siasa. Inakuwa vigumu kujua ni wakati gani anaongea kama mwanasheria na ni wakati gani anaongea kama mwanasiasa.

Matokeo ya tume yanasimama hadi utakapofanyika utafiti mwingine wa kisayansi na kuja na matokeo tofauti.
 
Fanyeni yote, ila mchanga lazima uondoke. Ttafuta maneno mazuri wakati wa kuruhusu mchanga kuondoka nchini ila ukweli ni kwamba, mpaka Sasa, mchanga lazima upelekwe Japan ukapembuliwe ili wachukue madini yao halafu mchanga wenyewe wajapan wabaki nao kwa ajili ya kufanyia land reclamation.
 
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

Mimi nitamwamini Tundu Lissu, kwa sababu sheria zinasema mali inayo chibwa ni mali ya mwekezaji, na serekali inachukua %4 ya mapato.
Hata kama ni ww upate %96 utatamani tena hata iyo 4? Mikataba mibovu ndiyo inayo tuibia pamoja na watu tulio wapa dhamana ya kisimamia..
 
Sio kumwamini Lissu bali namwelewa kwa kigezo cha hoja zake. Magufuli zaidi ya kofia ya u-Rais hana hoja wala hekima.

Suala la kusema "nina uchungu.....mimi ni mtetezi wa wanyonge......nina uzalendo..." ni extremely vague at best.
 
Mkemia sawa kisheria je. Kati ya sheria na kemia kipi hakituletei hasara? Sasa ona inaonekana wewe ni ZUZU NAMBA MOJA CCM
Unaongeleaje sheria wakati tume ya kisheria bado haijaleta matokeo yake?
Kilichowasilishwa so far ni matokeo ya kisayansi ya nini haswa kilichomo ndani ya Makinikia
 
Sintakuja nimwamin rais Magufuli maana mara nyingi hupenda kutumia uongo kama ngaz ya kuonekana mtendaji. Lejea haya hapa. Kasema kajenga majengo ya UDSM KWA B10 wakat ni uongo. Alienda bandarin akasema kuna meli 32 wakati kuna meli 16. Amewahi kusema hatachagua wapinzan Anna huyo hapo. Mambo kem kem utamwamin vip.
 
Nimekupa possibility Kuna room nyingi tu. Moja niserikali kuendelea mbele na yeye acacia afanye anachotaka ikibidi kwenda mahakamani kufanya kile unachokifikilia.
Kuna kufukuzwa kabisa
Kuna kumuonyesha kwamba tunachokisema ni sahihi na kama na yeye anapenda kujilidhisha tena tukiwa nae hakuna shida tumalize uchunguzi wetu tutampa nafasi

Mkuu Kuna possibility nyingi tu nashangaa unashangaa nini.

Kumbuka yote haya hadi hapa sio wala hayahusiani na mikataba. Maana hapo ni suala la Kuna nini na vingapi na ni kiasi gani.
Kwahiyo mko tayari kukaa chini na mwizi mjadiliane kama alikuwa anawaibia au la!
 
Hivi kuna mtu anamuamini Magufuli, kama yupo nitamshangaa sana maana hata profesa muhongo amesema raisi kadanganywa

This Professor is another hopeless case ya wasomi wetu Tanzania. Mbona hakuyasema alivyokuwa kwenye Uwaziri?? Mbona hakuchukua hatua yoyote?...hata kutudanganya kwamba serikali inafanya lolote alishindwa.

Mpaka leo sielewi watu wanaomsifia Mhongo! Sijaona kitu ambacho amekifanya angalau hata ku-risk kazi yake ya Uwaziri. Atleast Magufuli kwa hili is miles apart..ni mara kibao alichukua maamuzi ambayo yaliwauzi wakubwa..hata kama yalitenguliwa lakini unaona..alithubutu!

I am sorry, kwa Tanzania tulipofika.........nadhani ngoja twende na Magufuli tuu. Hakuna namna.

Angalia mtu kama Sumaye..ten years as Prime Minister (Mikataba mingi ya kifisadi ilisainiwa chini ya uongozi wake kama mtendaji Mkuu wa serikali)..leo analia na mikataba mibovu kweli???

Wanasiasa Mungu wa Mbinguni anawaona!
 
Lisu ni zero brain
Hajui hata symbols ya copper na zinc anatokwa povu la metals.

Yeye ale tu hela za mafisadi anaowatetea
Mbaya zaidi waliosomea symbol za Copper, Zinc, Brass na Bronze hawajawahi kuvumbua chochote nchi hii. Wapo tu bize kukariri symbols. Sasa ndugu yangu, mikataba inayotufilisi haitafsiriki kwa symbol za copper
 
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

Ninamuamini TL kwa 99% moja ya kwangu mwenyewe.Simuamini JPM sababu huwezi kuwapa MADARAKA makubwa wale waliotuingiza kwenye shida na kuhujumu uchumi wetu kwa kupewa viapnde 30 vya fedha!
 
Back
Top Bottom