Magufuli versus Tundu Lissu; yupi unamwamini kwenye sakata la makinikia?

This Professor is another hopeless case ya wasomi wetu Tanzania. Mbona hakuyasema alivyokuwa kwenye Uwaziri?? Mbona hakuchukua hatua yoyote?...hata kutudanganya kwamba serikali inafanya lolote alishindwa.

Mpaka leo sielewi watu wanaomsifia Mhongo! Sijaona kitu ambacho amekifanya angalau hata ku-risk kazi yake ya Uwaziri. Atleast Magufuli kwa hili is miles apart..ni mara kibao alichukua maamuzi ambayo yaliwauzi wakubwa..hata kama yalitenguliwa lakini unaona..alithubutu!

I am sorry, kwa Tanzania tulipofika.........nadhani ngoja twende na Magufuli tuu. Hakuna namna.

Angalia mtu kama Sumaye..ten years as Prime Minister (Mikataba mingi ya kifisadi ilisainiwa chini ya uongozi wake kama mtendaji Mkuu wa serikali)..leo analia na mikataba mibovu kweli???

Wanasiasa Mungu wa Mbinguni anawaona!

Unajua kwanini tunashindwa kuwachukulia hatua STAHIKI?Ukimshika Sumaye,kule juu kutaguswa,ukigusa Lowassa utagusa matawi ya juu kabisa.Leo tunaona Kalemani na Yamungu waliokuwa kwenye Bodi ya makinikia na waliokuwa sababu ya kukubali upuuzi wa mikataba mibovu wamepewa ULAJI.Halafu unasubiri Meli ya kwenda Zanzibar airport
 
Nitakuwa sina akili nzuri kumwamini magufuli.Nguli wa miamba na madini mwenyewe profesa Muhongo amesema magufuli kaingizwa chaka!
 
Dhahabu inavhenjuliwa migodini na ndio maana TMAA wanakagua na TRA wanachukua kodi zao. Mchanga unaobaki hupelekwa nje kuchenjuliwa zaidi
 
Bandari ya Tanga ilitaka kununua kontena kwa M40 Acacia wakagoma
Sasa wewe ACACIA wanasema kila kontena lina dhahabu kama kilo 4 sasa hiyo 40 million inanunua 4 kg za gold?
Kilo moja ya dhahabu kwa bei ya kwetu hapa Tanzania ni 90 million ungekuwa wewe ungeuza 4 kg kwa 40 million?
 
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

ngoja niweke kumbukumbu sawa kwanza.
 
Swali jepesi sana kuwahi kutokea hapa jf!
lissu: `lowasa ni fisadi' ametamka mwenyewe kwa miaka nane,lakini amegeuka kuwa mtetezi wake mkuu.
Lisu:`CCM wamempa fomu FISADI agombee uraisi' lakini akashiriki kumptisha kuwania urais!
lisu:`hongera kwa kaz nzr iliyofanywa na tume ya prf. Mruma'...
 
Nakereka sana kuona vijana walikofika,MTU anashindwa kujibu maswali bila matusi,NANI KAWALOGA VIJANA? jenga hoja kujibu swali ueleweke,tusiwe kisiasa nchi hii yetu tutabaki.
 
Kumwamini mwanasiasa yeyote inahitaji uwe na roho ngumu kama ya paka.
 
Back
Top Bottom