Magufuli versus Tundu Lissu; yupi unamwamini kwenye sakata la makinikia?

Usiwaite tena ACACIA kuwa ni wezi kwa kutumia ripoti ya Prof. Mruma. Punguza jazba na mhemko kwa kuwa hata huna uhakika wa suala hili litamalizikaje!
nitaendelea kuwaita wezi. na nategemea riport ya pili kuibua mengi zaidi. ninaiamini tume ya mruma kwa sababu ni technical team. principle yangu ambayo ni non-negitiable, ni afadhali nigundue nilidanganywa na mtaalamu kuliko kugundua nilidanganywa na mwanasiasa. wale ni experts kwenya yale mambo na baadhi yao wamefanya hiyo kazi wakiwa acacia au abg contractors hiyo.
sina shaka mkuu endelea na lisu wako
 
Shida yenu ni hiyo! Ni wapi nimemtaja Lissu tangu nimeanza kubishana na wewe hapa? Inaonekana Lissu mnamwogopa sana eeh! Mimi na wewe ubishi wetu umeanza pale mimi nilipohoji uhalali wa wewe kuwaita ACACIA kuwa ni wadanganyifu na wezi kama wezi wengine kwa kutumia tu ripoti ya akina Pro. Mruma. Mabishano yetu mimi na wewe hayamuingizi hapa Lissu wala mkuu wa nchi kama sehemu ya mabishano. Nakushauri kwa mara ya mwisho sasa, jifunze kutohamaki kwenye mambo technical kama haya, usiwe kama wale walioigharimu serikali hii mabilioni kwa sababu tu ya mihemko na kutotafakari! Wizi au udanganyifu kama kosa la jinai hauthibitishwi na ripoti ya akina Prof. Mruma.
 
Bila kujua hizo symbol huwez kujua kilichopo mule, na huwezi kujua any reaction

Acheni kupotoshwa na wanasiasa uchwara kina lissu
sikiliza walosign mikataba ya madini wanazijua symbol? walotufikisha hapa wato wanazijua symbol? ww endelea kujua halaf watu wanapiga mpunga ww endelea kukaa na symbol mfukon halaf watu wanakaa na dhahbu kwenye makontena tuone nani mjanja
 
Usitutoe njia kuu hatukubali. Chenge na Werema watajijua
njia gani ulotolewa? unatafta correctness huna unachokijua bas sikiliza wanaojua na angalia wanavokinzana thn una conclud kupata jibu haihitaj diploma mkuu akili ya kawaida wengi wapewe
 
Magufuli akiongozwa na Tume yake mwenyewe ya Professa Mruma wanadai makonteina yamejaa dhahabu, shaba na fedha zilizochanganyikana na udongo na hazijawahi kusafishwa!

Tundu Lissu anadai makinikia kwenye makonteina ni mabaki baada ya ukekenuaji uliofanyika mgodini Bulyanhulu. Pia 95% ya dhahabu iliyochimbwa huvunwa mgodini na kusafirishwa na ndege huku 5% ndizo huwemo kwenye makinikia.

Serikali inadai hakuna usafishaji wa dhahabu kwa sababu hatuna mitambo ya kusafishia.

Maelezo ya pande mbili ni dhahiri yanakinzana na upande mmoja uko sahihi na mwingine unaongopa.

Ni upande upi unauamini na kwa sababu zipi?

Hili sawali linaonyesha uelewa wako du
 
Wote wako sahihi. Magu amefanya maamuzi kwa kufuata reference ya tume aliyoiunda na ilikuwa maalumu kwa ajili ya mchanga uliokamatwa bandarini. Lisu bila shaka kuna reference anazo kutokana na historia yake kuhusiana na madini tangu 1998, hivyo basi ushauri wake na ukosoaji wake juu ya hatua zilizochukuliwa, jinsi tunavyoibiwa madini mengi zaidi ya Yale yaliyomo kwenye makinikia na masuala ya kisheria ni mhimu sana kwa taifa ili kumfanya rais afuatilie zaidi ya hatua alizochukua. Hakuna wa kumbeza, wote wanafanya kazi kulingana na nafasi zao.
 
Hatareee!... Namuamini mkulu kwasababu anaongea vutu facts. Wamefanya research na wakagundua...reference ipo dhahiri. Lisu anaongea mambo ya kwenye makaratasi ambayo ktk uhalisia yamedanganywa.....kwahiyo Lisu ni muongo maana hajafanya research kuhusu yale makinikia...kitu cha kumshangaa ni kwamba anajitokeza hadharani bila aibu kupinga kitu ambacho kipo na kimehakikiwa na vipimo halisi.
 
Kalele zote zanini kwani hii serikali haiweki wazi himakataba yote ya madini tujipange upya tuanze moja ccm kuweni majasiri misione aibu na serikali yenu kwa masilah ya taifa mkileta ubishi huko tuendako sio kuzuri kwa kuficha mambo mahimu kama hizi mali asili zetu wajukuu zetu watakuja kutucheka ujinga
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom