Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Mratibu wa msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ambaye ni Katibu Mkuu BAVICHA (Bara) Yohana Kaunya, wanaoendelea na ziara ya 'Operesheni +255 Katiba Mpya, Okoa Bandari Zetu', amesema kuwa licha ya awali kukubaliwa na familia ombi lao la kwenda kudhuru kwenye kaburi la Rais Magufuli amedai kuwa wamepokea maelekezo wakiwataka wasiende.
Tulikuwa na ratiba ya kwenda kuona familia ya Rais Magufuli na kutembelea kaburi lake na tulienda kwenye familia wakatukubalia lakini baada ya tukio la (gari kuungua moto) lakini asubuhi tumepata mrejesho kuwa hatupaswi kwenda lakini kufika jana familia ilikuwa imetukubalia" Mratibu wa Msafara wa Tundu Lissu, Yohana Kaunya
Kaunya amesema kuwa walikusudia kabla ya mkutano ambao ulipangwa kufanyika Chato saa nane mchana wangeazia kuzuru kwenye kaburi la Rais Magufuli kama alivyotamka Tundu Lissu akiwa Mkoani Kagera wakati wa uzinduzi wa Oparesheni hiyo.
Kuhusu tukio la gari kuungua moto amesema wametoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, huku akisisitiza kuwa wahusika wanatakiwa kuchukuliwa hatua ili kuondoa taharuki.
Ikumbukwe Tundu Lissu alitangaza kuwa ataenda kudhuru kwenye kaburi la Rais Magufuli na 'kumuamsha' akidai ili aone vitendo vinavyofanyika nchini ikiwemo sakata la Mkataba wa uwekezaji wa Bandari, ambao Lissu alidai kuwa Magufuli asingeweza kuingia mkataba wa aina hiyo.