Dar itakuwa nzuri sana
Wamekopa tena ili kujenga dar wakati kuna barabara za mikoa/wilaya hazina lami,mikoani hospitali ni mbovu kupita maelezo lakini wao wanajenga dar tu kana kwamba matatizo ya watz ni dar ..nakumbuka Jk aliahidi meli mpya Kagera yenye thamani ya 40bn lakini mpaka leo si pesa wala meli ambacho wamekifanya juu ya meli hii na hivi juzi imezimika ziwani kwa masaa 6 watu wakiwa majini,hiyo haingolewi ila wako busy na kujenga dar kuwaonesha wazungu eti Tz nzuri wakati mikoani umaskini wa kutisha ..kwa hali hii ndo maana naunga mkono sera ya majimbo ili maendeleo yafike kote kuliko kuichuma mikoa alafu kodi zote ziishie dar
Jana nilimsikiliza kwa makini na kugundua hana tafsiri sahihi ya daraja na "flyover"hata kule kigamboni amesema kutakuwa na "flyover" tatuHivi daraja la bahari ndo lina flyover? kwa hiyo na lile kigamboni ni flyover????????
Magufuli ni jembe kama Prof Muhongo
![]()
Magufuli amesema Serikali katika kupambana na foleni Jijini dar es Salaam wameamua Kujenga flyover maeneo ya daraja la salenda. Kasema daraja lililopo halitabomolewa bali daraja jipya litajengwa upande wa baharini.
Kasema mkataba wa awali umeshasainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Korea tayari kwa maandalizi ya Kujenga.
Daraja litakua na urefu wa zaidi ya km7.
Magufuli akiongea na TBC1 alisema;
Mia
Kwanza miradi ya kitanzania huwa ya kukurupuka, pili, nilidhani kama kusudio lilikuwa ni kuondoa foleni "basing kwenye hoja yako kuwa huu mradi ni mdogo sana kwa wakorea japo sijajua ni kwa nini" basi serikali ingefikiria hio flyover ingeanzia kwenye makutano ya Barbara za Mandela na Kilwa na ipitie huko huko baharini na utokee hapo aghakhan hadi huko Toure Drive/ koko beach, kwa mradi huu naona kama umekusudia kuwa favour watumishi wa magogoni wawahi majumbani kwao,Tatu, jana saa 2 usiku TBC walisema huyu mradi unafadhiliwa na Korea Kaskazini ila vyombo vingine vinasema Korea kusini.Nimeshangaa sana.Siamini kama Magufuli amefanya tathmini ya kutosha kujua kama hili daraja litakuwa na tija.kutoka Aghakan hadi Cockcock beach maana yake ni kwa wale wanaoelekea Masaki,Osterbay kidogo na Msasani kidogo. Sasa kwa kiasi cha mabilioni zaidi ya 100 sioni tija yake.
Lakini kwa kutengenezeka wakorea hilo daraja la km 7 kwao ni kazi ndogo mno.Korea kuna hadi daraja la km 20 na hili daraja limeshikiliwa na nguzo ndefu za kimo cha mita 70.hayo ya km 7,2,4,6 ni kitu cha kawaida sana kwa kuwa kule ni nchi ya vimilima.
Uhai ndio utakaojenga Flyover?
Na hilo ndo sulujisho la foleni dar?
Nchi hii ina viazi vingi sijui kwanini tusiviuze china na uturuki.
Mkuu daraja Litaanzia maeneo ya coco beach hadi mataa ya agha khan. MiaUmbali wa Selander hadi COCO sio 7km, kuna makosa ya namba hapo, labda 700m, maximum pale ni 1km.Gharama haziwezi kuwa kubwa sana kwa kuwa pale hakuna kina kirefu.hivyo nguzo ambazo ndio sehemu kubwa ya gharama za daraja hazitakuwa ndefu sana.