figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,888
Magufuli amesema Serikali katika kupambana na foleni Jijini dar es Salaam wameamua Kujenga flyover maeneo ya daraja la salenda. Kasema daraja lililopo halitabomolewa bali daraja jipya litajengwa upande wa baharini.
Kasema mkataba wa awali umeshasainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Korea tayari kwa maandalizi ya Kujenga.
Daraja litakua na urefu wa zaidi ya km7.
Magufuli akiongea na TBC1 alisema;
MiaTuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri Chief Executive wa TANROADs hivi karibuni na wataalamu wenzake walienda South Korea.. Serikali ya South Korea imekubali kutufadhili kujenga flyover nyingine pale.. na barabara yenyewe itakuwa na urefu wa karibu kilomita 7.2 na barabara itaanzia Coco Beach, itapita baharini itakuja kutokea Agakhan Hospital na kuja ku-join na barabara nyingine hii ya Alli Hassan Mwinyi…"
".. Tumepanua maeneo pengine kote.. tuna mradi wa BRT ambao una-involve kilometa zaidi ya ishirini na moja na karibu sasa hivi unaisha chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, lakini tunapofika pale Salenda pamekuwa na tatizo kubwa na kwa sasa hivi katika traffic count ya magari yanayopita pale kwa siku yamezidi zaidi ya magari hamsini na moja elfu kwa hiyo hawawezi wakaya-accommodate magari yote yanayoweza kupita sehemu hiyo.