Uchaguzi 2020 Magufuli si mgombea wa Tanzania pekee bali Afrika nzima inamuhitaji

Ina maana Nchi kuharibika mpaka uwepo wa vita!?
Ama kweli kujibizana na Mataga ni kujipotezea mda.

Vipi kuhusu rushwa ilivyotamalaki huku TAKUKURU wakiufyata mkia?

Vipi kuhusu ufisadi papa wa serikali ya Mr. Tanzania mpya (refer 1.5T)?

Vipi kuhusu ongezeko la umasikini kwa Watanzania?

Vipi kuhusu ubaguzi wa kikanda na wapinzani?

Vipi kuhusu ukosefu wa ajira kwa WaTz?

Vipi kuhusu dhuruma kwa wastaafu na wakulima (refer wakulima wa korosho)?

Vipi kuhusu Mauji, unyanyasaji na ubambikiziaji kesi kwa wapinzani?

N.k,

Mambo ni mengi, nimechoka kutype.

Jiwe atupishe tu, Tano inatosha.
Hakuna nchi duniani yenye imemaliza hayo mambo msiionee Tanzania
 
Tanzania IPO katika nchakato wa Uchaguzi Mkuu, miongoni mwa wagombea URAIS ni Mheshimiwa Daktari John Joseph Pombe Magufuli.

Rekodi alizovunja Mheshimiwa JPM nchini Tanzania, Afrika na dunia nzima, zinamfanya asiwe mgombea wa Tanzania pekee Bali tegemeo LA Afrika kama mfano wa Kiongozi bora, shupavu, jasiri, Mzalendo na Mchapakazi.

Katika nchi nyingi, RAIA na viongozi wanamtazama Magufuli kama kiongozi bora wa mfano wa kuigwa katika ulinzi wa Rasilimali na Maendeleo ya nchi.

Tungekuwa na uchaguzi wa RAIS wa Afrika, JPM angeshinda kwa kura nyingi maana Afrika inamhitaji kuliko yeye anavyoihitaji Afrika.

Hizi rekodi zake haziwezi kufikiwa na Rais mwingine yeyote wa Afrika hivyo kumpambanua kama kiongozi bora wa karne hii:
1. Kuongoza nchi ya kiafrika kwa miaka mitano bila kukanyaga Ulaya, Amerika wala Asia
2. Kuzuia safari za nje kwa viongozi na watumishi wa umma ili viongozi wawatumikie wananchi
3. Kudhibiti biashara ya kulevya nchini
4. Kudhibiti ujangili
5. Kujenga ukuta ili kulinda rasilimali madini
6. Kutumia wasomi na Elimu zao kwa maendeleo ya nchi bila kujali itikadi
7. Kufufua shirika LA ndege kwa kutumia cash money
8. Kubadili mfumo wa mashirika ya umma kutoka kuomba ruzuku hadi kutoa gawio
9. Kusimamia uwajibikaji wa viongozi wa umma
10. Kuwaminya mabeberu hadi kukubali kukaa meza ya mazungumzo ili kutupatia Hisa na gawio LA mapato ya madini
11. Kuboresha miundo mbinu na usafiri wa anga, barabara, majini na reli
12. Kukomesha mgao wa umeme na kuongeza uzalishaji wa umeme
13. Kupambana na Covid-19 kidete hadi kuirejesha Tanzania katika hali ya kawaida na sasa maisha yanaendelea vyema
14. Kuimarisha mifumo ya Uthibiti ubora wa Elimu kwa kuimarisha NACTE, NECTA, SQA, TCU n.k
15. Kuimarisha huduma za afya na Bima ya Afya, sasa hivi wenye bima wanapokelewa kama wafalme hospitalini, zamani tuliwekwa benchi
16. Kuimarisha michezo na usimamizi hivyo wachezaji wananufaika na jasho lao na timu zetu zinafanya vizuri. Ndani ya miaka mitano ya JPM Tanzania imecheza AFCON, ilifuzu CHAN, simba ilifika robo fainali
17. Heshima ya Tanzania kama Taifa imerejea, hakuna Nchi inayotuchezea tena
18. Kilimo kimeimarishwa hivyo nchi imeongeza uzalishaji, hakuna njaa tena nchini.
19. Imani ya wananchi kwa CCM imeongezeka na sasa wana CCM wanazaa sare zao hadharani tofauti na 2013-2014 ambako MTU angepita na sare ya CCM, angezomewa au ingechanwa.

Kwa sababu hizo na zinginezo, Waafrika wanatutegemea sana watanzania tumpe Ushindi wa Kishindo DR. JPM kwa ustawi wa Tanzania na Afrika nzima. CHAGUA JPM, CHAGUA MAENDELEO

Burundi anakubalika sana.

Akagombee huko.
 
Mnamzungumzia Raisi JPM anayesubiri kuapishwa Kwa mara nyingine mwishoni mwa mwaka huu siyo?

Huyu ni Baadhi ya watu wachache duniani ambao hupatikana Kwa nadra sana! Huyu anapaswa kulazimishwa aongoze nji yetu hata baada ya matakwa ya kikatiba kumlimiti

Atake asitake tutamlazimisha,. Haiwezekani bajameni, ni Uongozi wake tu ambapo Korona Nayo imekubali kuongozwa na JPM, lakini kote huko Corona imekuwa kiongozi wa nji hizo

Ni JPM pekee Hadi barozi wa USA anaweza kuvua barakoa lake mbele yake hata hajaambiwa, inamaana Mabeberu wanaweza kumhoji kama hajakutana nao Tu, wakikutana naye lazima washushe kofia kichwani
nyie ndio mnaolea upumbavu itafikia kila mtu atakae ingia ikulu anabadili katiba akae mpaka kifo huuu ni ujinga na hauvumiliki na utaleta migogoro isio lazima nonsense nyie ma CCM akili hamna nyie
 
Kama Africa inamhitaji aende Zimbabwe kuwakuzia uchumi, sisi Tz hatumhitaji, mitano yake inatosha.
SASA BASII.
Zimbabwe hawezi kwenda watamtukana mara ya pili arudi mbio kama safari ile alipowauthi kwa kumsifia Kiongozi wao ambaye hajawafanyia lolote. Amezoea kusifiwa for doing nothing anafikiri Waafrika wote ni wajinga kama Wabongo wanaodai anapendwa dunia nzimà bila kutaja hata nchi moja. Hata hapa walimfukizia kwa kujisifu amewafanyia mengi mazuri kumbe kawatia umasikini. Huu ni msalaba wetu hakuna nchi inayoutaka!
 
Wamchukue wanako muhitaji tena tunawapa buree
Hakuna wanakomhitaji hata bure maana atakuwa mzigo usiobebeka. Ni Chama chake ndo kinatubebesha mzigo usio na manufaa yoyote ulitakiwa utupwe mahali uchomwe Moto majivu yatupwe baharini. Hafai kuishi kati ya watu!
 
Back
Top Bottom