Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Kaanza kupanda seed ya kutaka aongeze muda kwa kisingizio kwamba watakaokuja hawatakuwa wazalendo enough kumalizia miradi aliyoianzisha. If we try to go that route, we are finished
 
kagoda, meremeta, kilimo kwanza, escrow m EPA, ujenzi wa chuo kikuu cha cha dodoma, HESLB, Nssf ,Twiga bankcorp, Gas ya mtwara, NBC, TPB, radar, richmond, when combined together unajia ni bei gan ilipigwa? au hata hizo zilipotea JPM akiwa rais?

Kwa taarifa yako huo upigaji wote uliotaja haufikii hiyo 2.4t. Tena zenyewe zilipigwa ndani ya miaka 30, hii 2.4 imepigwa within 4 yrs!
 
Anadanganywa na wanaomzunguka kwa maslahi yao, maana kuwepo kwake madarakani ndio kuneemeka kwao. Watanzania tujipange kisaikolojia nchi inatuponyoka hii!
 
Ninaomba mungu iwe hivyo. Akae sana tupate maendeleo. Hii ndivyo ilikuwa kwa Singapore ilipo mpata kiongozi wake aliyewaletea maendeleo. Alikaa zaidi ya miaka 10. Malaysia vile vile. Nyie mnafuata hao wazungu wanaofadika tukiendelea kuwa masikini. Wanaohusudu na kushangilia viongozi wetu (wa kiAfrica) wakiwa mafisadi. Hao wanawasifia sana na kuwalinda! Hawaandiki mabaya yao kwenye magazeti yao. Tumeisha mpata mkombozi kwanini tumutake afuate mi

Usijali hata akitoka madarakani hakatazwi kuleta maendeleo. Bado anaruhusiwa kuleta maendeleo maana huwa anasema ili tupate maendeleo tunatakiwa kuchapa kazi sana, na sio ili kuleta maendeleo lazima uwe rais.
 
Bora deni likue tu lakini tunaona miradi kama hiyo, kwani hakuna nchi isiyodaiwa waulize USA wana deni kiasi gani kwa wachina.
Hivi kwa akili yako unaamini maskini mwenye kipato cha laki 1 kwa mwezi akawa na deni la laki 5 ( 5 times) ni sawa na tajiri mwenye kipato cha 1 Billion kwa mwezi lakini akawa anadaiwa bilioni 20 ( 20 times) ?!
 
Raisi Yuko sahihi mtu mwingine akija so lazima aendeleze hayo hayo anayofanya.Mfano kazindua uwanja mpya wa ndege na kanunua ndege anayekuja aweza Sasa fanya kazi ya kuwawezesha watanzania kwa kuwapa ajira wengi , kuongeza mishahara wafanyakazi na Bei za mazao ili watanzania wengi Wawe na Uwezo wa kupanda hizo ndege alizonunua na kuutumia huo uwanja .Pia mwingine akija so lazima ajenge mabarabara yeye aweza kuja na mkakati wa mfano kuondoa ushuru wa magari au kupunguza Kodi ili watanzania wengi waweze kumudu kumiliki magari binafsi mengi watumie kwenye hizo barabara alizojenga.Hospitali na zahanati nyingi aluzijenga mwingine akija so lazima ajenge aweza kipau mbele chake kujaza ajira za madaktari na manesi na madawa kwenye hizo hospitali alizojenga kuhakikisha zinakuwa na madaktari na manesi was kutosha .Uraisi kila moja hufanya kivyake hakuna was KU.kopi kwa mwenzie.Yeye akiondoka anatakiwa ajue kabisa kuwa ajaye nyuma yake SI lazima afanye Kama alivyofanya yeye.Yeye Kama Raisi afanye chake ya mengine akiondoka awaachie wengine.

Hapa nakuunga mkono kwa asilimia 100. Yeye amejikita kwenye miundombinu tu, huku akiacha kubalance maeneo mengine, ikiwemo kilimo, uchumi, ajira na hata demokrasia. Atakapokuja mwingine anaweza kukuta kuna miundo mbinu ya kutosha na kuamua kubalance mambo mengine. Ukweli ni kuwa Magufuli sio rais mzuri bali ni rais anayeamini kwenye miundo mbinu tu.
 
Bora deni likue tu lakini tunaona miradi kama hiyo, kwani hakuna nchi isiyodaiwa waulize USA wana deni kiasi gani kwa wachina.
Deni linakuwa vpi wakati mnatutangazia kwamba mnajenga kwa hela za ndani.

Halafu hivi unazijua athari za kukua kwa deni ww. Siku tukifika stage ambayo hatuwezi kukopesheka tena ndo utajua athari za madeni zipo vp...
 
Kwahiyo hataki kuondoka?
Akwende zake hukoooo! Asitake kutuaminisha kwamba yeye.ndiye.atakuwa wa mwisho.hatutapata mwenye akili! Eti naye kwa.akili yake anaona anafanya maajabu! Asitake kutudanganya eti tunatumia pesa yetu, mbona deni la taifa linapaa kama tunatumia pesa ya mafisadi? Aache upotoshaji huyu Mzee!
 
Kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
Mambo ya niombee yamerudi tena, muda mrefu sana sujasikia Mniombee!
 
kwa haya mema anayotumwagia akae tu

Hapana, atoke ataingia mwingine atakaelinda demokrasia, atatoa ajira, atakuwa kilimo na kujenga miundombinu pia.
 
Ata mimi kwakweli simuoni mtu atakae vaa viatu vyake akitoka na ujasiri wake katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

Tatizo kubwa ninaloliona kwake ni hofu ambazo hazipo, watu wasiojulikana, democracy; na hizi ni values ambazo kwakweli sio za ku compromise you can’t overlook those values pamoja na yote mazuri anayofanya.

Hila mwisho wa siku kutokana na kauli yake huyu bwana amebakiza miaka 5 ni nani unaweza sema serikarini mwenye ‘can do attitude’ kama ya Magu ambayo imefikia ata nusu, binafsi sijaona.
 
Hapa nakuunga mkono kwa asilimia 100. Yeye amejikita kwenye miundombinu tu, huku akiacha kubalance maeneo mengine, ikiwemo kilimo, uchumi, ajira na hata demokrasia. Atakapokuja mwingine anaweza kukuta kuna miundo mbinu ya kutosha na kuamua kubalance mambo mengine. Ukweli ni kuwa Magufuli sio rais mzuri bali ni rais anayeamini kwenye miundo mbinu tu.
Awamu ya nne na ya tano maraisi walihama na wizara zao ikulu.Kikwete alikuwa waziri wa mambo ya nchi za nje kabla ya kuwa Raisi .Aliipenda Sana ile kazi ya uwaziri wa mambo ya nchi za nje aliposhika uraisi alikuwa akisafiri Sana kwa mambo ya nchi za nje.Raisi Magufuli alipokuwa waziri wa ujenzi aliipenda Sana hiyo wizara na aliposhika uraisi anafanya kazi zaidi ya wizara ya ujenzi na miundombinu Yake aliyokuwa akiipenda Sana akiwa waziri wa ujenzi.Wakati wa Kikwete waziri wa mambo ya nchi za nje alifunikwa na Kikwete wakati huu waziri wa ujenzi kafunikwa na Magufuli.
 
Hahhahaha kanogewa sijui kama kunakuondoka hapa kazi tunayo
 
Back
Top Bottom