Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Kwamba Mungu akimchukua,aiseee. Hivyo tunae mpaka majaaliwa.
 
Hii sasa kaiona kama nchi yake yani hafikirii mtu mwingine kuongoza yeye akiwa hai.
Mkuu Badilisha haraka hiyo katiba yako.Isomeke marekebisho ya kifungu no.........Rais ataongoza milele.Inawezekana
 
Kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
kwahiyo mpaka Mungu akuchukuwe ndio utaachia nchi. watanzania twafyaa. naogopa kutekwa
 
Ngoja Kwanza nitakuja tz mwakani,nipo Malimali huku.


 
Piga kazi usijali au kusikiliza comment zisizo na maana na maneno yao matupu ya watu,tunakuombea
 
Hahahahahhaha "mungu akinichukua" na sio Muda wake ukiisha, jamani huyu mtu huyu eeeeeh haya
 
Back
Top Bottom