Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Magufuli: Nikiondoka watakaokuja wataweza?

Kuingoza nchi na kuiletea maendeleo kama ilivyo sasa kutokana na kazi hiyo kuwa ngumu na kuhutaji viongozi kujitoa kwa moyo katika kufanikisha hilo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania sasa imekuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.

“Mara nyingi tumeambiwa kuwa Tanzania ni masikini, ninaomba neno hilo tulifute kwani nchi yetu ni tajiri lakini tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kututumia, kuna miradi imetumia matrilioni ya fedha saa nyingine ninajiuliza kweli hili limewezekana, tumeweza maana yake kila palipo na nia Mungu yupo pamoja na sisi,” amesema.

“Siwezi nikasimama mbele za watu nikasema haya ni kwasababu yangu kwani mimi ni dereva tu lakini pia huwa ninajiuliza ikitokea siku Mungu akanichukua hao watakaokuja watayamaliza kweli kwasababu panahitaji moyo, unafanya hivi huku unatukanwa lakini inabidi ufanye kwaajili ya Watanzania, inahitaji kujitoa sadaka ya kweli,” amesema.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kulisimamia taifa hili na ninawashukuru Watanzania wenzangu kwa kuendelea kuniombea na kunipa moyo, nchi yetu sasa imekuwa ya mfano watu wanatuogopa sasa, wapo wanaouliza mnapata wapi fedha mimi ninasema zilikuwa kwa mafisadi sasa zinaenda kwa Watanzania,” amesema.
#JamaaAmechanganyikiwa...
 
Huyu jamaa huwa si mkubali kwa syle yake ya udereva ila toka mwanzo nilisema at least kaona hili na sijui kwa kujua au imetokea tu kwa ile dhana ya kusema ‘sisi sio masikini , we are blessed kwa mali asili zetu’ hapa tu namkubali maana bila kuwa na ‘wealth mentality’ kama Taifa kutoboa ngumu na tujue maneno yanaumba pia kila siku sijui tupo masikini inatuumiza ki akili bila kujua na tunaumba hali hiyo

Ila kwa mengi nampa big no
 
Kwahiyo mpaka afe ndio tupate rais mwingine? Watanzania tuanze kujiandaa kisaikolojia.
Thubutu yaani asiote hilo ,kitanuka hajawahi fikiria yaani tukubali upuuzi wake huo wakati nchi imemshinda anataabisha watu kiuchumi ,vifo ,mateso,utekaji ,biashara hoi ,kila sekta hoi bin taaban hakuna hataamini hata Sara zetu zitapokelewa na mwenyezi Mungu .
 
Nani aendeleze mamiradi yake hayo yasiokuwa na kichaa wala miguu ,hayana faida yoyote kwa nchi zaidi ya hasara kama hayo mandege yake ,mtu kakalia ten pasenti .
 
Natumai alikumbushwa pia kwamba hilo jengo yeye amelikuta almost limeisha. Lakini ikamchukua four years just kufanya finishing! Pia ajue tu kwamba watanzania wapo 55m, na kila siku wanaendelea kuongezeka.
si mpaka awe na akili ya kuelewa
 
Kama CCM kiliweza Kumteua Yeye kuwa ' Flag Bearer ' wake na sasa anafanya hayo mambo makubwa na mazuri basi ni CCM hiyo hiyo tena itampata ' Flag Bearer ' mwingine na huenda akawa ni Mchapakazi, Mtu mzuri na Kipenzi cha Watanzania wengi kama siyo wote kuliko hata Yeye, hivyo nae ataweza Kuifanya Tanzania yetu hii mambo makubwa na ya Kimaendeleo. Alianza Hayati Mwalimu, akaja Mzee Mwinyi, akafuata Mzee Mkapa, halafu Mzee Kikwete na sasa Yeye na atakuja mwingine tena. CCM haikaukiwi Watu wazuri na haina rekodi ya Kukosea katika Kuteuwa Wagombea wake.
Tanzania itaanza kuendelea siku watu mkikombolewa toka utumwa wa fikra na mawazo wa ccm otherwise tutaendelea kushangilia ujinga,maana JK and then Magufuli ndo brain and best ccm personnel then kama nchi tunatatizo kubwa na tukiendelea na ccm zaidi tumekwisha
 
Mawazo ya ajabu kabisa, ni kweli kwamba ujinga wote unaoendelea sasa ifike mahali tuachane nao. Kwa mwendo wa sasa baada ya miaka kumi ni kama kurudi nyuma hadi precolonial period
 
Kikwete ni mpumbavu sana, Mwalimu Nyerere aliona mbali sana, alijua kabisa kuwa Kikwete hafai kuwa Rais alijua angeiacha nchi pabaya mno sasa nyote mmeona

Sasa mpumbavu au nyie Wajuaji mlioshindwa kumzuia yeye kuwa Rais
 
Huyu jamaa huwa si mkubali kwa syle yake ya udereva ila toka mwanzo nilisema at least kaona hili na sijui kwa kujua au imetokea tu kwa ile dhana ya kusema ‘sisi sio masikini , we are blessed kwa mali asili zetu’ hapa tu namkubali maana bila kuwa na ‘wealth mentality’ kama Taifa kutoboa ngumu na tujue maneno yanaumba pia kila siku sijui tupo masikini inatuumiza ki akili bila kujua na tunaumba hali hiyo

Ila kwa mengi nampa big no
mkuu we are blessed na mali asili nyingi,ila we are not blessed na akili kichwani,siasa safi na uongozi Bora mbaya zaidi tunalaana inaitwa ccm,so hata tungekuwa na wealth mentality ya aina gani hatuwezi kutoboa bila kwanza kuiua ccm,kuoverhaul mfumo wetu wa uongozi na upatikanaji wa viongozi na kuoverhaul elimu wanayopata watoto wa Tanzania
 
hahahaha umerukwa na akili wewe..ccm ina laana kwa sababu umebeba viongozi mahili wa upinzani au..sijaelewa..au labda kwa sababu inafanya.mambo makubwa nchi. hii...nashauri muwaambie mabwana zenu wazungu kule kwamba sasa nchi imeshika kasi..tunaenda kwenye uchumi wa kati..ccm ni philosophy na sio mtu..ina sera safi zenye.kuweza kuipeleka nchi popote kiuchumi..au unadhani ccm ni limtu liko pale ..hahahahaha mafisadi nawashauri kimbieni tu..hamtapata mwanya tena , wahini hata hapo Congo mchukue.dili zenu
 
Ukikua utagundua ulikuwa mjinga!
 
Huyu mzee hajui kuwa kuna watu wanalala bilabila
 
hahahaha umerukwa na akili wewe..ccm ina laana kwa sababu umebeba viongozi mahili wa upinzani au..sijaelewa..au labda kwa sababu inafanya.mambo makubwa nchi. hii...nashauri muwaambie mabwana zenu wazungu kule kwamba sasa nchi imeshika kasi..tunaenda kwenye uchumi wa kati..ccm ni philosophy na sio mtu..ina sera safi zenye.kuweza kuipeleka nchi popote kiuchumi..au unadhani ccm ni limtu liko pale ..hahahahaha mafisadi nawashauri kimbieni tu..hamtapata mwanya tena , wahini hata hapo Congo mchukue.dili zenu
Ungejua hao mabeberu wanaijua Tanzania kuliko hata magufuli wako na ungejua kuwa hayo unayoyaita maendeleo yamefanikiwa kwa pesa za mikopo kutoka kwao na kujengwa na makampuni yao usingejitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom