Magufuli na ndege, siri nyuma ya pazia?

Magufuli na ndege, siri nyuma ya pazia?

Wewe ndo mjinga kuliko wote toka kwenu, ndege siyo kama Daladala itaokoteza abiria njiani kujazia. Dreamliner ya abiria 262 ikiondoka Dar na abiria 10 na hostages 10 itafika New York na wasafiri haohao na kurudi na wachache zaidi kwa sababu gharama za kulaza ndege na wafanyakazi kwa siku zisizojulikana kungoja abiria ni kubwa sana. Watalii wanaokuja Tanzania wengi wanatoka USA, Ulaya kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Asia kama Japan, China, India nk. Ebu mshauri Rais Wetu mpendwa atakavyowapata hao watalii na kuwaleta na kuwarudisha ukitilia maanani kuwa kila mtalii ana mipango yake. Hata wakija pamoja wote toka nchi moja, huyu atakaa Tanzania siku 5, yule wiki, mwingine siku 10, pamoja na madege yake mengi mshauri atawarudishaje kila mmoja akawahi shughuli zake. Madege yanakwenda kuleta watalii yanapeleka watu gani toka Tanzania watakaokuwa wamejaza madege na wanakwenda kufanya nini. Mwaka Jana au huu ndege aina ya Airbus 380, kubwa ya abiria kuliko zote ilitua Dar kwa dharura na wakazi wengi sana walikwenda uwanjani kuiona na kumsifu Rais wetu mpendwa kwa kuwezesha dege kubwa kama hilo kutua hapo ingawa Terminal III ilikuwa haijakamilika. Dege hilo lenye uwezo wa kuchukua abiria mpaka 800 likuwa limechukua watalii kwenda Mauritius, kisiwa kidogo sana hakina hata Big 5. Vilevile Shirika la Ndege la Ia Air Mauritius lina ndege zake nyingi zikisafiri Ulaya na kwingineko kuleta na kurudisha watalii. Dege lilikuwa la Shirika la EMIRATES ambalo linafanya safari zake Tanzania pia wakitumia ndege ndogo kuliko Dreamliner za Magufuli. Watanzania walivyo wajinga wakamsifu Magufuli kwa ujio wa dege hilo badala ya kujiuliza kuna nini huko kisiwa kidogo kuliko Wilaya yetu ndogo yoyote? Au nchi yetu kubwa sana yenye vivutio vingi vya kitalii, kwanini EMIRATES inaleta videge vidogo labda hata havijai? Tanzania hakuna biashara ya usafiri wa Anga.
Utakuha kuonge huu utopolo after 5 yrs ngoja kazi ifanyike. Kwa sisi wenye taarifa tunaona kazi inavofanyika na tunasupport ununuaji wa ndege zaidi, angalau zifike 15 ili ATCL iwe kampuni ya kati
 
Kwa bei ya kawaida kabisa kwa mashirika mengi ya ndege ni Masaa 17 hadi 20 hadi bongo. Hayo masaa 35 ujue huyo atakuwa ametafuta ya bei ndogo sana.

Ingekuwa vema kama ungesema hayo mabilion ya kununua ndege tungewekeza kwenye kujenga mabwawa na miundo mbinu ya umwagiliaji, kuimarisha soko zuri la mazao na bidhaa na mataifa ya nje wakiwamo majirani, kujenga viwanda kwa ajili ya usindikaji wa mazao na kuongezea thamani bidhaa zetu, kuongeza thamani kwenye ubunifu wa kijasiriamali kwa wajasiriamali, na kutoa mikopo nafuu kwa vijana, na ikiwezekana kufufua vyama vya ushirika kwa kuweka utaratibu wa uawajibikaji na uwazi kuhahakisha ushirika wenye tija na endelevu....na lingine tumia sehemu ya hiyo pesa kufanya marekebisho ya sera za uwekezaji kwa kuhakikisha mvuto na urahisi katika sekta ya uwekezaji hasa kwa kutatua utata na utitiri wa taasisi na tozo zenye kufanana zinazokandamiza spirit ya uwekezaji.

Sasa kama tunaanzisha shirika kwa kunyonga sekta binafsi...itachukua muda sana kupiga hatua. Tuheshimu sekta binfsi, ina mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya nchi.
Huko kwingine kunaendelea, kama vp 2025 gombea urais ili uimplement hoja zako, wenye akili wameona ndege zitaongeza watalii na wanafanya hayo ww kaa kulalamika tu
 
Heheheh usitumie nguvu saana..ukiona vipi potezea tu jomba. Unadhani haya yametokea hewani. Achana nayo fanya kazi nyingine
Naona unasepa kiaina. nimeask for ushahidi na evidence. Naona una dunk dunk pemben huko. Next time unapo mu accuse mtu au taasis fulani. Hakikisha una concrete evidence zinazo support allegation zako. Sio siasa everywhere .
 
Wacha rais ajenge nchi nyie jibidisheni na kusambaza ushoga tu

giphy.gif
 
Unachopinga nn hasa?? Kwamba hizo sio ajira?? Kwan aviation industry ni pilots tu na air hostages??, alfu muelewe kuwa kila awamu au serikali ina vipaumbele vyake, kwahyo Kama vipaumbele hivyo havikugusi moja kwa moja haimanishi kwamba hakuna anayenufaika navyo.
Umekiri kila awamu ina kipaumbele chake, the sad story ni kwamba hakuna namna SGR na Stigilaji kukamilika hata kama magufuli atapewa miaka mingine mitano, piga mahesabu kwa miaka mitano miradi yote hii miwili haijafikia hata robo ya lengo, kwa maana hiyo ili ikamilike inahitaji miaka mingine 15 (awamu ngapi hizi)

Kwasababu haitakamilika katika awamu ya magu na kila awamu ina kipaumbele chake, hivyo unatuambia akiingia mwingine ataachana na huu mradi uliokula mapesa mengi bila faida yoyote (kufikia lengo) ama tumuongezee awamu nyingine ili amalize hayo mamiradi yake?

Kama una akili timamu utaungana na wale wanaodai katiba mpya.
 
Wacha rais ajenge nchi nyie jibidisheni na kusambaza ushoga tu
Tumepigwa shekhe alimuita mtengeneza ndege wanakaa nae chumbani hapo ikulu huku akiwa Ameikalia sheria ya manunuzi ya Tanzania matakoni kwake aka 10% na kukuacha wewe unashindia kahawa na kashata hapo Lumumba.
 
Think twice,,,,,

Hizo ndege hazitoi ajira?


Mwenye chuki ni chuki tu hata jema halioni.

Hajui kwamba ndege zikiwa nyingi na zikizunguka duniani huko watalii watakuja kiurahisi na pato la utalii litaongezeka na ajira zitaongeza vile vile maana haiwezekani watalii wetu waje kwa kenya airways yani watue kenya na hajui kwamba ile mtalii tu kutua pale JNIA tayari ameisha tengeneza ajira kwa watu wanaohusika na hiyo chain kuanzia driver tax mpaka hotelini mpaka bundle atakalo tumia
 
Ndege inatoa ajira kiasi gani kutokana na uwekezaji wake? Kwa faida ipi kwanza? Unajua jinsi biashara ya ndege ilivyo na ushindani?

Tumia akili walau kidogo tu hivi unawezaje kua na vivutio vya kitalii vya kila namna hapa kwetu tanzania halafu unakosa kua na ndege ukitegemea ndege za jirani,je unajua utalii unaingizia pato taifa hili kiasi gani?

Tukiwa na usafiri madhubuti wa ndege jua wazi kabisa tutakuza utalii marudufu na hata kufikia pato la dollar za kimarekani billion 5 je unafikiri watu wangapi watapata ajira kwa hilo pato kama taifa.
 
Approximation:
Ndege moja ni bilioni 250 tsh.
Ndege tatu ni bilioni 750 tsh.
Ndege moja ajira za moja kwa moja ni 100.
Ndege tatu ajira za moja kwa moja ni 300.
Trekta moja (John Deere 5050D 4WD) ni milioni 30.
Tanzania kuna vijiji 12319.
Mil 30 X Vijiji 12,319 = bilioni 369.5
Tuseme 60 % ni Wakulima.
60% ya 60,000,000 = 36 milioni
Raia milioni 36 wanatumia matrekta.
Pembejeo nyingine ndio inatumia kwenye ile bilioni 400 iliyobaki.
Hapo kuna mbolea,mbegu,maghala,viuatilifu.
Hapo sasa ni bilioni 750.
Kati ya ajira 300 na ajira milioni 36 za moja kwa moja,unachagua ipi??

Kiwanda cha kuunga ma matractor mbona kipo pale kibaha au unadhani hivyo vitu havifanyiki uchumi wa tanzania unategemea sana kilimo ili kuupanua zaidi inabidi twende pia kwenye utalii ambapo ndege ndio msingi mkuu wa biashara ya utalii
 
Tumia akili walau kidogo tu hivi unawezaje kua na vivutio vya kitalii vya kila namna hapa kwetu tanzania halafu unakosa kua na ndege ukitegemea ndege za jirani,je unajua utalii unaingizia pato taifa hili kiasi gani?

Tukiwa na usafiri madhubuti wa ndege jua wazi kabisa tutakuza utalii marudufu na hata kufikia pato la dollar za kimarekani billion 5 je unafikiri watu wangapi watapata ajira kwa hilo pato kama taifa.

Utafanya nini na ndege tatu huku fly Emirates, Qatar airways zimepaki hapo pembeni? Au unadhani biashara
 
Wacha rais ajenge nchi nyie jibidisheni na kusambaza ushoga tu
Sera yenu siku hizi ni ushoga tu , tunahitaji majibu ajira kwa vijana ,elimu bure iliyo Bora, nyongeza kwa watumishi na wafanyakazi serikalini, kukuza sekta kilimo n.k siyo mtu akitoa hoja mnakimbilia kwenye ushoga , hatutaki kusikia hizo ngonjera mpo madarakani miaka karibia 60 tupeno majibu
 
Umekiri kila awamu ina kipaumbele chake, the sad story ni kwamba hakuna namna SGR na Stigilaji kukamilika hata kama magufuli atapewa miaka mingine mitano, piga mahesabu kwa miaka mitano miradi yote hii miwili haijafikia hata robo ya lengo, kwa maana hiyo ili ikamilike inahitaji miaka mingine 15 (awamu ngapi hizi)

Kwasababu haitakamilika katika awamu ya magu na kila awamu ina kipaumbele chake, hivyo unatuambia akiingia mwingine ataachana na huu mradi uliokula mapesa mengi bila faida yoyote (kufikia lengo) ama tumuongezee awamu nyingine ili amalize hayo mamiradi yake?

Kama una akili timamu utaungana na wale wanaodai katiba mpya.
Inasikitisha itabidi atakayemfuata aendelee na blue print ya huyu bwana. Na uhakika hii miradi ikikamilika basi watanzania wengi watakuwa hoi natabiri kuna baadhi ya watanzania wataanza kuikimbia nchi yao na kwenda nchi za jirani 😭
 
Utafanya nini na ndege tatu huku fly Emirates, Qatar airways zimepaki hapo pembeni? Au unadhani biashara

Kwa hiyo ulikua unataka kama taifa tusiwe na ndege kisa kuna emirates na kwanza hatuna ndege tatu na pili hivi unataka mtalii akitoka marekani apitie kwanza doha au dubai ndio aje hapa kwa nini asipande ndege ya air tanzania moja kwa moja toka newyork mpaka JNIA au KIA kwanza alikipitia dubai anakua kapoteza muda wake tu hapo tunacho kizungumza ni kua na direct flight kutoka europe na americas au asia(china),kwa hiyo ndege za ndani nazo tuogope quatar?
 
Umekiri kila awamu ina kipaumbele chake, the sad story ni kwamba hakuna namna SGR na Stigilaji kukamilika hata kama magufuli atapewa miaka mingine mitano, piga mahesabu kwa miaka mitano miradi yote hii miwili haijafikia hata robo ya lengo, kwa maana hiyo ili ikamilike inahitaji miaka mingine 15 (awamu ngapi hizi)

Kwasababu haitakamilika katika awamu ya magu na kila awamu ina kipaumbele chake, hivyo unatuambia akiingia mwingine ataachana na huu mradi uliokula mapesa mengi bila faida yoyote (kufikia lengo) ama tumuongezee awamu nyingine ili amalize hayo mamiradi yake?

Kama una akili timamu utaungana na wale wanaodai katiba mpya.

Utasubiri sana miradi itakamilika na utaona aibu sana na isitoshe mpaka umeme utautumia na kuufurahia
 
Katika vipaumbele vyote vya taifa, je, ndege ndicho hasa watanzania wanachohitaji?

Hizi ndege za magufuli zina malengo ya dhati ya kuinua maisha ya watanzania ama kuna ajenda nyingine isiyojulikana?

Watu wetu wanalia na umasikini, ajira, mifuko ya hifadhi ya jamii, mikopo, afya, maji, umeme, makazi duni, elimu duni, kilimo duni, mishahara kiduchu na mengine mengi, hayo yote hayana umuhimu kwake isipokuwa ndege tu?

Tunahitaji sera za magufuli ziguse watu. Miaka sita sasa ajira hakuna vijana wanahangaika tu mitaani kama yatima lakini yeye hana habari. Ati nendeni mkajiajiri!

Hizo ndege zina msaada gani kama haziweza kuinua maisha ya watu?? au ni kutafuta ujiko tu na kulimbuka?
View attachment 1553604
Heri hizo hela anazonunulia ndege angezielekeza kukamilisha Ujenzi wa SGR, hiyo reli ina multiplier effect kubwa kwenye Uchumi kuliko midege anayopanda yeye tu peke yake kwenda kula Krismas kijijini kwake
 
Hela za hizo ndege zingejenga hata kiwanda kimoja kingeajiri watu wengi zaidi kuliko hizo ndege!

Kiwanda kimoja na sector ya utalii kukua kipi ni bora na kipi kina ajiri watu wengi zaidi? Unajua kwamba utalii unachangia pato la taifa kwa 25% kwa ufupi ukiacha kilimo sector inayoafuata kwa pato la taifa ni utalii na ili uwe na utalii imara unahitaji shirika la anga madhubuti tena la kwako mwenyewe sio utegemee la mwenzako kama kenya airways au emirates!

Hivi shule mliendaga kusomea nini yani kweli karne ya ishirini na moja unaona kua ndege sio sawa?
 
Back
Top Bottom