Katika vipaumbele vyote vya taifa, je, ndege ndicho hasa watanzania wanachohitaji?
Hizi ndege za magufuli zina malengo ya dhati ya kuinua maisha ya watanzania ama kuna ajenda nyingine isiyojulikana?
Watu wetu wanalia na umasikini, ajira, mifuko ya hifadhi ya jamii, mikopo, afya, maji, umeme, makazi duni, elimu duni, kilimo duni, mishahara kiduchu na mengine mengi, hayo yote hayana umuhimu kwake isipokuwa ndege tu?
Tunahitaji sera za magufuli ziguse watu. Miaka sita sasa ajira hakuna vijana wanahangaika tu mitaani kama yatima lakini yeye hana habari. Ati nendeni mkajiajiri!
Hizo ndege zina msaada gani kama haziweza kuinua maisha ya watu?? au ni kutafuta ujiko tu na kulimbuka?