Magufuli kama Nebukadneza Mkuu wa Dola ya Babeli

Elisha Sarikiel

Verified Member
Aug 29, 2020
700
1,000
Mwaka 2015 niliandika habari iliyochapishwa na Gazeti la TAZAMA “Magufuli kama Nebukadneza mkuu wa dola ya Babeli” nairudia tena baada ya kusoma Gazeti la RAIA MWEMA. Mwandishi MWANA KIJIJI ameandika “sababu zilizowafanya mitume 11 wasimfuate Yesu majini”

Amemshambulia sana Rais Magufuli.
1. Mwandishi anadai mwaka 2015 walipopiga kura kumchagua Rais, hawakutarajia wawe na Askofu wa Tanzania, hawakufanya mabadiliko ili Magufuli awe Mwinjilisti mkazi wa Ikulu, Paroko wa kigango cha Magogoni.
Hawakutarajia Magufuli awe Mhubiri mwenye upako uliopitiliza mwenye cheo cha unabii na utume wa Kiraisi! Mwinjilisti mfawidhi mwenye kupigiwa saluti.

2. KWASABABU tu Rais anasisitizia Watanzania kumtanguliza Mungu, mwandishi anaona Magufuli amejigeuza Askofu, Shehe, Mchungaji, Nabii na Mwinjilisti.
Hivi karibuni Magufuli amewataka Watanzania kufunga tena kwa siku tatu ili kumsihi Mungu ainusuru Tanzania na COVID 19.

3. Sijui mwandishi huyo anaichukuliaje hatua ya kumtangaza Nyerere mtakatifu wa kanisa katoliki anayetoka Afrika? Maana Nyerere hakuwahi kuwa Askofu! Lakini mwandishi huyo hawagusi Watanzania wale wanaoihubiri “corona” kama kwamba hata Adamu na Hawa walikufa kwa COVID 19 .

4. Wapiga debe la corona wote siyo madaktari waliowatibu marehemu, siyo wasemaji wa familia za wafiwa wala siyo wasemaji wa Taasisi ambazo marehemu walifanyia kazi, lakini wamejipa majukumu ya kutangaza vifo vya watu ili tu kuiinua corona.
Wanatumia umaarufu wa marehemu kama tangazo la kibiashara ili kuinadai COVID 19 wakisema imerudi kwa kasi mpya na nguvu mpya.

5. Wapiga debe la corona wanafanana na waliohamasisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 walitumia vyombo vya habari kuchochea mauaji, ila wahubiri wa corona wanahamasisha mauaji ya kisaikolojia na kiroho.

6. Mahubiri yao hasi yatawaacha Watanzania wengi wakiwa hai kimwili lakini ndani wakiwa wafu kiimani, walioaminishwa kwamba corona iliyo duniani haishughulikiwi mbingunini, corona iliyotoka nje ya Afrika haisikii dawa yoyote iliyo ndani ya nchi, corona haitibiki kwa njia za kiafrika isipokuwa tiba zitokazo nje. Wanaoamini ugonjwa uliotoka nje, unaomuua hata mzungu suluhisho lake haliwezi kupatikana Tanzania, walioaminishwa corona iliyotoka nje suluhisho lake liko nje.

7. Mahubiri yao yameambatana na lawama wakimlaumu Rais Magufuli kwasababu amekuwa jasiri! Wanatamani angesalimu amri awatangazie hao “superiors” wao walioko nje kwamba Tanzania nayo inakiri kushindwa. Wanataka waitumie hali ya kushindwa kama sumaku ya kuvutia misaada.

8. Mwandishi anawasoma wapiga debe waliojiinua juu ya madaktari, waliowafunika wataalamu wa Afya na wanaoingilia hata familia za marehemu wakijigeuza wasemaji wao. Mwandishi haioni jinai yao bali anaona tu dosari ya Magufuli hadi anamfananisha na Mtume Petro aliyethubutu kutembea juu ya bahari lakini mitume wengine 11 hawakumfuata.

MAGUFULI NI ZAIDI YA NABII
9. Leo tunayemwita nabii zamani Waisraeli walimwita mwonaji, baadaye wakamwita mwenye kusema kabla hayajatokea, wengine wakasema anatabiri. Magufuli hasemi mambo kabla hayajatimia, mtu anayetimiza sifa ya kusema mambo kabla hayajatokea na baadaye yakatokea ni Julius Nyerere, alisema kabla wataibuka watetezi wa wanyonyaji, hayo yametimia “Advocates” wa “imperialism” waliibukia Bungeni, wakaacha kumbukumbu ya kudumu kwenye “Hansard” kuhusu utetezi wao. SASA tusubiri kutimia alilosema Nyerere kwamba ataibuka Rais ambaye kwa ulevi atajitangaza Rais wa maisha.

10. Rais Magufuli siyo Askofu, siyo Mwinjilisti, siyo Shehe, siyo mchungaji, siyo Paroko wala siyo Nabii bali ni zaidi ya Askofu, zaidi ya Shehe, zaidi ya Mwinjilisti, zaidi ya Paroko, zaidi ya Mchungaji na zaidi ya Nabii. Kwasababu ameinuliwa na Mungu kwa wakati wake ili afanye wasiyoyaweza kuyafanya hao Maaskofu na Mashehe na Wachungaji na Wainjilisti. Magufuli anamtumikia Mungu kwenye nafasi yake ya Urais.

11. Neno la Mungu linasema mshitaki wa wenye haki Ibilisi ni kama Simba angurumaye akitafuta mtu ili ammeze. Shetani kama simba aliyezeeka asiyeweza kumrukia mnyama, hujificha mahali akaunguruma ili wanyama watakaokimbia sauti yake wakutane na simba wakamataji.

12. David Camerun aliyekuwa Waziri mkuu wa Uingereza aliunguruma kwenye Jumuia ya madola akizitaka nchi za Afrika zibadilishe katiba zao kutambua ndoa za jinsia moja, Barack Obama wa US na Cameruni wa UK walisema wazi nchi isiyobadilisha katiba (isiyoukubali ushoga) isitarajie kupokea msaada wowote kutoka Jumuia ya Ulaya wala Marekani.

Tanzania kwasababu ilizitaka fedha za bure ilitikiswa, ikaanzisha mchakato wa katiba mpya.

14. Hao wababe walipounguruma kwa niaba ya Ibilisi hakuna Askofu, Mchungaji, Shehe, Nabii, Mtume wala Mwinjilisti aliyesimama upande wa Mungu kuwaambia hapana! Ni Robert Mugabe tu Rais wa Zimbabwe aliyekuwa jasiri kumwambia Obama “ukija Zimbabwe kuhamasisha ushoga itabidi kwanza mimi nikuoe wewe Obama ili tuonyeshe mfano.”

15. Lakini wengine wote hata hao wanaotamba kama wainjilisti wa kimataifa, hakuna yeyote aliyethubutu kuugusa (kuupinga) ufisadi huo ili kuinusuru Afrika. Hata Pope alinyamaza kimya hakuthubutu kuwapigania wakatoliki walioko Afrika, ikumbukwe Yesu alisema “atakaporudi tena mwana wa Adamu,JE, ataikuta imani duniani?” Yesu alimaanisha ataikuta imani ile ile aliyoasisi? Papa hadi leo hajajiweka wazi kwenye suala la ushoga ameshindwa kukiri kama alivyofundisha Yesu kwamba “ndiyo yenu iwe ndiyo na siyo yenu iwe siyo” lolote lisiloangukia kwenye "ndiyo" wala "hapana" linatoka kwa yule Mwovu.

16. KWANINI NAMFANANISHA MAGUFULI NA NEBUKADNEZA ?

17. KWASABABU Mwenyezi Mungu huwainua watu ili kutimiza makusudi yake ikiwa amemuinua Magufuli kuwafikishia ujumbe Walimwengu, Waafrika na Watanzania, hakuna mwenye ubavu kuzuia wala atakayemwambia Mungu huyo ni Rais wetu tuliyemchagua wenyewe kwa kura zetu, hawezi kutumika kama chombo chako wakati Mashehe na Maaskofu wapo!

18. Mungu alimtumia Punda akasema kama mwanadamu, baada ya Nabii Baalamu kutiwa wazimu na kiasi kikubwa cha fedha alichofungashiwa ili afanye waliyotaka wanadamu hakujali aliyoyataka Mungu. Hata leo dini “zikibiasharaishwa” (commercialized) wenye dini watapagawishwa na nguvu ya fedha, hadi kupoteza mamlaka ya kiroho “moral authority” mfano hai Askofu mkuu wa dhehebu la Anglican alijitangaza kuwa shoga, hakuna Mchungaji wala muumini wa Afrika aliyethubutu kujitenga na Anglikani ya Ulaya wala Marekani kuashiria kuuchukia uchafu huo! Hakuna mwenye jeuri ya kujitenga azikose dola za Marekani na Euro za Ulaya! Hawa ndio watakaofungisha ndoa za jinsia moja kwenye madhehebu yao, ni mtihani mgumu kati ya kuikiri nguvu ya Yesu kwa kushikamana naye ama kuikiri nguvu ya fedha na kumkana, ndio yaliyomshinda Nabii Baalamu hadi wazimu wake ukasababisha Punda aseme kama binaadamu.

19. Mwenyezi Mungu hafungwi na mifumo ya madhehebu ya dini, wala kwenye mapambano ya ukombozi Mungu hawekewa mipaka na wanadamu. Walioongoza TANU walimhusisha Mungu katika mapambano yao walipopigania uhuru, mashehe walimshurutisha Julius Nyerere kufunga pamoja nao licha ya kumfahamu hakuwa mwislamu.

20. Wakati huo wa mapambano Nyerere aliulizwa swali itakuwaje endapo Mwingereza atagoma kutoa uhuru? Waliomuuliza swali hilo walimtegea Nyerere aidha kujibu kama kiongozi mwoga ama kujibu kishujaa kwamba na Watanganyika nao watachukua msimamo wa Kenya. Mzee Jommo Kenyata alikuwa ameiingiza Kenya kwenye mapambano ya umwagaji damu waliyaita MAUMAU yaani Mzungu Arudi Ulaya Mwafrika Apate Uhuru.

21. Nyerere alijibu kwa utulivu kwamba Gavana akigoma kutoka, tutamshitakia Malkia, asipotusikiliza Malkia tutashitaki Umoja wa Mataifa, huo usipotusikiliza tutamshitakia Mungu. Huo ni uthibitisho kwamba tangu awali Watanganyika walimtanguliza Mungu walimwamini na kumkiri kwa kila gumu walilokutana nalo maishani, ndio maana baada ya uhuru kupatikana waasisi walikumbuka kumtaja Mungu (kumkiri) kwenye wimbo wetu wa Taifa.

22. Tunapoimba “Mungu ibariki Afrika, uwabariki viongozi wake, uwape hekima, kwakuwa hekima na umoja ndio ngao zetu ama kinga yetu sisi Afrika na watu wake” dua hili halielekezwi kwa Jabali wala sanamu la kufikirika lisilosikia, lisilojibu wala lisiloweza kufanya lolote, bali tunamwomba Mungu aliye hai.

23. Watanzania tunapoimba “Mungu ibariki Tanzania, dumisha uhuru na umoja kwa wote, wanawake, wanaume na watoto” hatuombi kwa HAKUNA, isiyoyosikia, isiyoitika wala isiyotenda. Tunamwomba yeye ambaye yuko, mwaminifu na wa haki, hao waliotetereka kiimani yaani wanaoamini kwamba maendeleo ya sayansi na tekinolojia yatakuwa mbadala wa Mungu wasitulazimishe kuikubali hiyo imani yao iliyompindua Mungu duniani, ikamgeuza aishie kuwa Mungu wa mbinguni tu, bado Mungu anatakiwa kutawala dunia 100%.
(i) Mungu kama alivyo Mungu huko Mbinguni ndivyo alivyo Mungu hapa duniani

(ii) Mungu kama anavyohusika Mbinguni anahusika pia na dunia yetu kwa kiasi kile kile anachohusika mbinguni.

(iii) Mungu ni yule yule wa zamani wa sasa na baadaye


24. Mtu anayeona binaadamu wa leo amesoma, ameelimika, ameendelea na kupiga hatua kubwa kisayansi na kitekinolojia na kwahiyo awe amepevuka kiasi kwamba upevu wake unatosha kumfanya asimtegemee tena Mungu maishani mwake, huyo tumwambie wazi uasi wake asiuingiza kwenye dola, kwasababu dola ni yetu wote tunaoamini na wasioamini. Rais wa nchi ni wetu wote, wasitokee wengine kulazimisha kwamba Rais wa Tanzania awe mali ya wasioamini tu.

25. Tanzania ni dola iliyoanza na Mungu tangu ikiitwa Tanganyika, imeendelea na Mungu hadi leo na itaendelea na Mungu hadi kiama, wanaweza kuibuka viongozi wakengeufu lakini bado hatakosekana japo Mtanzania mmoja mwenye kumcha Mungu.

26. NABII WA YEREMIA NA MFALME NEBUKADNEZA

27. Mwenyezi Mungu kwa kinywa cha Nabii Yeremia anamwita Nebukadneza mtumishi wangu, Nabii Yeremia amelirudia neno hilo “mtumishi wangu Nebukadneza” mara sita. Wakati Yeremia akimtaja Nebukadneza kama mtumishi wa Mungu, huyo Nebukadneza mwenyewe hakuwa akimjua Mungu wa Waisraeli. Nebukadneza alikuwa na miungu yake ya kibabeli, swali ilikuwaje Mungu asimwite mtumishi wangu Mfalme Sedekia wa dola ya kidini ya Israeli, badala yake amwite Nebukadneza ambaye mbele ya dini ya wayahudi alikuwa “kafiri?”

28. Ilikuwaje Mungu asiwaite Makuhani na viongozi wa dini ya kiyahudi watumishi wake bali amwite Nebuukadneza ambaye leo kwa viwango vya madhehebu yaliyotoka Ulaya ni “pagano” ama “gentiles?” Hapa ndipo unatakiwa uelewa kwamba Mungu hafugwi kwenye taratibu za wanadamu, Nebukadneza aliitwa mtumishi wa Mungu kwasababu aliitwa kulitumikia shauri la Mungu.

29. Nebukadneza aliitwa mtumishi wa Mungu kwasababu kwa nafasi yake kama Mfalme aliutimiza mpango wa Mungu, inabidi tukubali kwamba kuna mambo hapa duniani ambayo Mungu hawezi kuwatuma Malaika kuyafanya ili malengo (mapenzi) yake yatimizwe, bali atawatumia wanadamu kwa nafasi zao ama kaliba zao.

Mwandishi wa makala hii : Mtumishi mzee Kamara Kusupa
 

nduza

JF-Expert Member
Feb 7, 2019
972
1,000
Inafikirisha
Lakini Nina shida na aina ya uongozi wa huyu bwana katika vipaumbele vyake Kama angezingatia Sana kuhusu huduma za jamii elimu Bora na kutokomeza umasikini angekuwa bonge la kiongozi na angependwa Sana na kuungwa mkono na watu wengi zaidi

Tuliosoma mpaka mwisho Kama Mimi gonga like hapa
 

Cannibal OX

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,809
2,000
Noted.

Kamara Kusupa ni Mwandishi Nguli Jabali toka kitambo sana. Kongole zake, uzi umeenda Shule kama Katibu Mkuu Kiongozi Mteule Balozi Dkt Bashiru Ally Kakorwa.
 

HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,169
2,000
Kama wasingegawa hili Jimbo sasa hivi huyu Mwalimu angekuwa mstaafu
FB_IMG_1614373072495.jpg
 

simon2016

Senior Member
Oct 19, 2020
148
500
Huyu jamaa anajua na anatetea ugali wa wengi ana msimamo na matumaimi yapo mie namkubali sana na akimaliza hayo anayotutalajia hii nchi raisi anaefata na watumishi watakua miungu watu na uhuru utakua mkubwa.

Ila tatizo swala la ajira kabana sana na biashara hatuhemi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom