Je Tanzania inahitaji Chama Dola au Dola Huru?

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,382
Reaction score
4,664
Habari za wakati huu;
Nachokoza mjadala kidogo ambao naamini kabisa ndio mjadala unaoendelea kwa sasa hapa nchini kwetu.

Mara nyingi nimekuwa nikisikia tuhuma kwamba Chama Tawala CCM kimeungana na serikali sana na hivyo kinaitwa chama dola.Katika siasa tunapozungumzia Chama Dola tunazungumzia chama cha siasa katika nchi ambacho ni Mamlaka ya Juu kabisa katika NCHI yaana-PARTY SUpremacy.Katika mfumo huu chama cha siasa kinakuwa ndicho chenye maamuzi ya mwisho kabisa katika mustakabali na uelekea owa nchi na kwamba maamuzi ya chama ndio maamuzi ya nchi na uongozi wa chama ndio uongozi wa nchi.

Katika mfumo ambapo DOLA ndio ina mamlaka ya mwisho yaani STATE Supremacy chama kinakuwa tu ni kama usafiri wa kumuingiza mtu kwenye DOLA akishaingia chama hakina uwezo wa kumfanya chochote kwa sabab sasa anakuwa ni sehemu ya DOLA na dola haiwezi kufanywa chochote kile na chama.

Kwa muktadha huu ina maana kwamba DOLA hata ikikosea Chama hakiwezi fanya jambo lolote lile.Ninapozungumzia DOLA ninazungumzia Mahakama,Bunge na Serikali.

Nimeona niliweke hili sawa ili tunapojadiliana basi tuelewe tunajadiliana nini.

Kwa upande wa TANZANIA tangu enzi za Nyerere kulikuwa na PARTY SUPREMACY kwamba chama ndio kilikuwa na mamlaka ya mwisho ila sasa ili kukwepa mivutano CCM ililiamua kwamba RAIS wa nchi ni lazima awe mwenyekiti wa Chama ili kuepuka MVURUGANO unaotokana na tofauti za kisiasa.Uamuzi huu ulifanyika kwa sababu hatukataka kukubali mfumo wa state supremacy kwa sababu ya uchanga wa demokrasia yetu na mifumo yetu.

Vilipokuja vyama vingi,Mfumo wa Party Supremacy uliendelea,Ndio maana kwa mujibu wa sheria,Mbunge lazima awe na chama na akiondolewa chamani basi na ubunge unakoma vivyo hivyo kwa RAIS n.k.

Sasa leo hii ningependa tujadiliana kwa utulivu na kwa HOJA Je sisi kama Tanzania Tunataka tuwe na mfumo ambao STATE Ndio Supreme Authority?Je kama tukifanya hivyo tutakuwa n hali njema?Au e tubaki na mfumo uliopo Je huu mfumo unatufaa?Je tuna mfumo mbadla ambao tunaweza utumia ambao unaweza kuwa na maslahi zaidi?

Tunaweza tafuta mifano kutoka nchi mbalimbali ili tuone uelekeo wa nchi yetu.
 
Nchi yetu bado haina taasisi imara za kusimamia state supremacy. Tukisema chama kisiwe na kauli, tutatengeneza madikteta serikalini ambao hakuna wa kuwahoji.

Chama angalau kina vikao vya ndani vya nidhamu, lakini serikali ikiwa na absolute power, nani atamfunga paka kengele?
 
Gentleman,
kwenye mfumo wa vyama vingi unatenganishaje chama tawala na dola vitu ambavyo vyote ni mali ya umma?

kwasababu,
dhamira, malengo na misingi ya kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa ni kushindanisha agenda, mipango na hoja za kisiasa, kijamii na kiuchumi, ili hatimae atakae shinda uchaguzi kwa kura nyingi, apewe dhamana ya umma kwa mujibu wa sheria, ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi wote.

hii ikimaamisha,
chama chochote cha siasa kitakachoshinda uchaguzi kwa mujibu wa katiba, kitakabidhiwa dhamana ya umma ya kukamata dola, kuunda serikali na kuongoza nchi kwa niaba ya wananchi wote.
Na karibu vyama vyote vya siasa hulenga hayo ukiachilia mbali vyama vichache vya mchongo ambavyo ni vitega uchumi vya watu.

Ni muujiza upi utatumika kutenganisha upacha huo wa chama tawala na dola? Kwasababu dola ndio nyenzo kuu ya chama chochote kile tawala ya kuongoza nchi na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama husika inatekelezwa kadiri ya vipaumbele vya wananchi waliokipa dhamana ya uongozi ya chama hicho.

Dola ni mali ya umma, na vyama vyote vya siasa pia ni mali ya umma. Hakuna namna ya kutenganisha upacha huo wa kihistoria ulimwenguni kisiasa 🐒
 
Labda nikupe mfano wa mfumo wa Marekani.Katika mfumo huu Serikali ni Supreme.Chama ni Ngazi tu kwa ajili ya kupata uongozi.Ukishapata uongozi kazi ya chama imeisha.Baada ya Hapo ni mambo ya kuendesha nchi ndio yanabaki.Ukienda China Chama ndio kinaamua kila kitu.Chama kina maamuzi ya mwisho kabisa katika uelekeo wa nchi.
 
Nchi yetu bado haina taasisi imara za kusimamia state supremacy. Tukisema chama kisiwe na kauli, tutatengeneza madikteta serikalini ambao hakuna wa kuwahoji.

Chama angalau kina vikao vya ndani vya nidhamu, lakini serikali ikiwa na absolute power, nani atamfunga paka kengele?
Tunajadiliana.Nidhamu inaweza simamiwa kwa mifumo ya kisheria na kikatiba ya nchi bila vikao vya chama.
 
Labda nikupe mfano wa mfumo wa Marekani.Katika mfumo huu Serikali ni Supreme.Chama ni Ngazi tu kwa ajili ya kupata uongozi.Ukishapata uongozi kazi ya chama imeisha.Baada ya Hapo ni mambo ya kuendesha nchi ndio yanabaki.Ukienda China Chama ndio kinaamua kila kitu.Chama kina maamuzi ya mwisho kabisa katika uelekeo wa nchi.
nadhani uko sambamba kabisa na maana ya maelezo yangu.
China ni kesi tofauti kabisa.

ndivyo demokrasia ya vyama vingi sehemu kubwa duniani huwa.

dola iko pale tayari na ni huru kusubiri chama cha siasa chochote kinachoshinda uchaguzi ili kitumie hiyo dola kuongoza nchi. Ukiondoka, unaondoka na chama chako, unaiacha dola na wengine waliopewa dhamana ya umma nao kuitumia kwasababu ni mali ya umma wa wote.

Na ndio maana kipindi cha kutafuta uongozi,
yaani kampeni, utakuta mngombea wa democratic anailaumu republican, na mngombea wa republican anailaumu democrats kwa matumizi holela ya dola. Vivyo hivyo Tanzania na maeneo mengine yenye mfumo wa kidemokrasia 🐒
 
Habari za wakati huu;
Nachokoza mjadala kidogo ambao naamini kabisa ndio mjadala unaoendelea kwa sasa hapa nchini kwetu.

Mara nyingi nimekuwa nikisikia tuhuma kwamba Chama Tawala CCM kimeungana na serikali sana na hivyo kinaitwa chama dola.Katika siasa tunapozungumzia Chama Dola tunazungumzia chama cha siasa katika nchi ambacho ni Mamlaka ya Juu kabisa katika NCHI yaana-PARTY SUpremacy.Katika mfumo huu chama cha siasa kinakuwa ndicho chenye maamuzi ya mwisho kabisa katika mustakabali na uelekea owa nchi na kwamba maamuzi ya chama ndio maamuzi ya nchi na uongozi wa chama ndio uongozi wa nchi.

Katika mfumo ambapo DOLA ndio ina mamlaka ya mwisho yaani STATE Supremacy chama kinakuwa tu ni kama usafiri wa kumuingiza mtu kwenye DOLA akishaingia chama hakina uwezo wa kumfanya chochote kwa sabab sasa anakuwa ni sehemu ya DOLA na dola haiwezi kufanywa chochote kile na chama.

Kwa muktadha huu ina maana kwamba DOLA hata ikikosea Chama hakiwezi fanya jambo lolote lile.Ninapozungumzia DOLA ninazungumzia Mahakama,Bunge na Serikali.

Nimeona niliweke hili sawa ili tunapojadiliana basi tuelewe tunajadiliana nini.

Kwa upande wa TANZANIA tangu enzi za Nyerere kulikuwa na PARTY SUPREMACY kwamba chama ndio kilikuwa na mamlaka ya mwisho ila sasa ili kukwepa mivutano CCM ililiamua kwamba RAIS wa nchi ni lazima awe mwenyekiti wa Chama ili kuepuka MVURUGANO unaotokana na tofauti za kisiasa.Uamuzi huu ulifanyika kwa sababu hatukataka kukubali mfumo wa state supremacy kwa sababu ya uchanga wa demokrasia yetu na mifumo yetu.

Vilipokuja vyama vingi,Mfumo wa Party Supremacy uliendelea,Ndio maana kwa mujibu wa sheria,Mbunge lazima awe na chama na akiondolewa chamani basi na ubunge unakoma vivyo hivyo kwa RAIS n.k.

Sasa leo hii ningependa tujadiliana kwa utulivu na kwa HOJA Je sisi kama Tanzania Tunataka tuwe na mfumo ambao STATE Ndio Supreme Authority?Je kama tukifanya hivyo tutakuwa n hali njema?Au e tubaki na mfumo uliopo Je huu mfumo unatufaa?Je tuna mfumo mbadla ambao tunaweza utumia ambao unaweza kuwa na maslahi zaidi?

Tunaweza tafuta mifano kutoka nchi mbalimbali ili tuone uelekeo wa nchi yetu.
Nchi Iwe na serikali 5, maraisi wa 5, itakayowakilishwa na Mfalme 1.
 
nadhani uko sambamba kabisa na maana ya maelezo yangu.
China ni kesi tofauti kabisa.

ndivyo demokrasia ya vyama vingi sehemu kubwa duniani huwa.

dola iko pale tayari na ni huru kusubiri chama cha siasa chochote kinachoshinda uchaguzi ili kitumie hiyo dola kuongoza nchi. Ukiondoka, unaondoka na chama chako, unaiacha dola na wengine waliopewa dhamana ya umma nao kuitumia kwasababu ni mali ya umma wa wote.

Na ndio maana kipindi cha kutafuta uongozi,
yaani kampeni, utakuta mngombea wa democratic anailaumu republican, na mngombea wa republican anailaumu democrats kwa matumizi holela ya dola. Vivyo hivyo Tanzania na maeneo mengine yenye mfumo wa kidemokrasia 🐒
Baada ya Kupata uongozi kati ya Party na State ni upande upi uwe Supreme?Maana wakati wa uchaguzi hakuna shida yoyote ila baada ya uchaguzi ndipo shida inaanza
 
Kitu pekee tanzania inaitaji ni katiba yenye mamlaka ya usimamizi wa misingi ya kitaifa, na ndio maana pendekezo langu la katiba lililopo kwenye www.katibampya.com linatoa jibu la swali lako.

Kwanza kabisa rasimu hiyo ina muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

Muundo huu unahakikisha uwazi, uwajibikaji na kutoingiliwa kwa mamlaka fulan kinyume na katiba na sheria za nchi.

Kwenye orodha hiyo limeongezeka baraza ambalo kwenye rasimu limetamkwa kuanzia ibara ya 98 mbaka 116, unaweza kwenda kulisoma na kulielewa kiundani.

Pili, tunapaswa kuwa na mamlaka ya Uwajibikaji wa lazima. Katika rasimu hiyo hiyo yapo mamlaka ya mwisho kabisa ya ulinzi wa katiba ambayo hata baraza lenyewe likitekwa au kudhoofushwa katika kulinda katiba basi Mamlaka hiyo uingia kwa mwisho kabisa, nayo ni Mamlaka ya kimapinduzi yaliyotamkwa katika ibara ya 255 mbaka 260 ya tasimu hiyo ya katiba.

Tembele tovuti www.katibampya.com hili ukajisomee mwenyewe, kisha rudi hapa kwa kuiunga mkono, kuihoji au kuikosoa kwa hoja zillizo wazi kabisa bila matusi wala kejeri.
 
Kwa mujibu wa katiba, Tanzania ni nchi inayofuata demokrasia ya vyama vingi.
Viongozi wa serikali huchaguliwa kupitia kwenye vyama vyao ili waongoze dola.
Watumishi wa Uma wakiwemo wale wa vyombo vya dola hawatakiwi kuonesha ushabiki au ufuasi wa vyama vya siasa.
Changamoto kubwa tuliyo nayo ni ujinga, fikra duni za kitumwa ambapo watumishi hao hujiingiza moja kwa moja kwenye siasa na hivyo kuingiza taifa kwenye misuguano isiyo ya lazima.
Ujinga huo huo hufanya viongozi wa kisiasa (rais na serikali yake) kupata misukosuko isiyokuwa ya lazima.
Bila watumishi wa Uma wenye akili huru, katiba na sheria hazina walinzi na hivyo kusababisha vurugu.
 
Asante, lakini nakuomba usome post iliyojuu ya post yako hii kipo kitu ambacho tanzania inapaswa kukipata hili kutatua matatizo yake.
 
Kitu pekee tanzania inaitaji ni katiba yenye mamlaka ya usimamizi wa misingi ya kitaifa, na ndio maana pendekezo langu la katiba lililopo kwenye www.katibampya.com linatoa jibu la swali lako.

Kwanza kabisa rasimu hiyo ina muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

Muundo huu unahakikisha uwazi, uwajibikaji na kutoingiliwa kwa mamlaka fulan kinyume na katiba na sheria za nchi.

Kwenye orodha hiyo limeongezeka baraza ambalo kwenye rasimu limetamkwa kuanzia ibara ya 98 mbaka 116, unaweza kwenda kulisoma na kulielewa kiundani.

Pili, tunapaswa kuwa na mamlaka ya Uwajibikaji wa lazima. Katika rasimu hiyo hiyo yapo mamlaka ya mwisho kabisa ya ulinzi wa katiba ambayo hata baraza lenyewe likitekwa au kudhoofushwa katika kulinda katiba basi Mamlaka hiyo uingia kwa mwisho kabisa, nayo ni Mamlaka ya kimapinduzi yaliyotamkwa katika ibara ya 255 mbaka 260 ya tasimu hiyo ya katiba.

Tembele tovuti www.katibampya.com hili ukajisomee mwenyewe, kisha rudi hapa kwa kuiunga mkono, kuihoji au kuikosoa kwa hoja zillizo wazi kabisa bila matusi wala kejeri.
Kabla sijaenda kuisoma Katiba yako naomba tutafakari kwa pamoja;
Kwa swali lililoulizwa Je Tunataka Chama Dola au Tunataka Dola Huru? Katiba yako inajibu swali hilo?

Pili Je Mihimili yako hiyo minne uliyopendekeza imezingatia Checks and Balance?Je katiba yako imezingatia Mamlaka ya Umma(People's Power) na namna hayo mamlaka yatakavyotumika?

Nimeambatanisha hapa picha ya muundo wa Tanzania uliyopendekeza ili tunapojadiliana basi tutazame kwa pamoja.

Ila tunapswa tukubaliane Jambo moja kwamba Hatuwezi kukwepa mjadala wa Party Supremacy vs State Supremacy kwa sababu tukiweza kuamua hapo basi tunaweza amua iwapo People's Power itumike wapi.Je itumike katika kuendesha Chama ama itumike katika kuendesha State?

Ni muhimu sana kwa sababu nionavyo mimi,hatuwezi kuwa taifa ambalo kila mtu anafanya anavyotaka lazima tuwe na utaratibu na utaratibu huo lazima uwe wazi na unaoeleweka kwa mfano kama tukizingatia Party Supremacy inamaana kwamba Mchakato wowote ule lazima uanzie katika Ngazi ya Chama kabla haujafika kwenye ngazi za maamuzi ya serikali.

Na iwapo tukiamua kwamba State Supremacy Ndio muhimu basi michakato yote lazima ianzie na kumalizikia kwenye Vyomba vya kiserikali ambavyo ni Bunge,Mahakama na Serikali Kuu.Kama ikiwa Hivyo ni lazima tuwe na Mahakama yenye Nguvu Kubwa,Bunge lenye Nguvu Kubwa na Serikali kuu Yenye Nguvu Kubwa. Sasa ili tutengeneze Hivi Vyombo Vikiwa na Nguvu Kubwa lazima tujiulize Central Power Atakuwa nayo nani? Je ni hili Baraza la Usimamizi wa Nchi?Kama ni hilo Je Baraza hili liundweje?Je liundwe na viongozi wa vyama vyote vya siasa?Kama ni Ndio Je Vyama Visajiliweje?Je Visajiliwe na Kusimamiwa na Sekretariat ya Hilo Baraza?Je Uchaguzi uendeshwe na nani?Je uendeshwe na Hilo Baraza la Usimamizi?

Je Gharama za uendeshaji wa hilo Baraza zitoke wpi?

Anyway uandishi wa Katiba unahitaji mambo mengi sana na ni mchakato mrefu sana.Tuendelee kujadiliana zaidi ili tujifunze na tupeleke nchi yetu mbele
 
Attachments

  • Muundo Picha.png
    Muundo Picha.png
    177.1 KB · Views: 6
Kabla sijaenda kuisoma Katiba yako naomba tutafakari kwa pamoja;
Kwa swali lililoulizwa Je Tunataka Chama Dola au Tunataka Dola Huru? Katiba yako inajibu swali hilo?
Ndio, Rasimu ya katiba kwenye Tovuti tajwa imejibu swali hili kwa kuweka muhimili wa nne wenye jukumu la kusimamia misingi yote ya kitaifa, yaani misingi kama bunge kutoingiliwa, misingi ya demokrasia ya kisiasa kutodhoofishwa, Tunu za taifa, Dira ya taifa ya maendeleo endelevu na ustawi wa jamii n.k
Kwa lugha ya Kimichezo naweza Kuliita baraza kama refa anaesimamia wachezaji wacheze kwa mujibu wa Sheria ya mchezo huo. Baraza ndie msimamizi wa ufuasi wa Katiba, yaani kuhakikisha taifa na mamlaka zote linaifuata katiba.

Pili Je Mihimili yako hiyo minne uliyopendekeza imezingatia Checks and Balance?Je katiba yako imezingatia Mamlaka ya Umma(People's Power) na namna hayo mamlaka yatakavyotumika?
Ndio, Katiba hiyo imetamka wazi kabisa mamlaka ya kila muhimili na mipaka yake, pia swali ulilosema People's power ndio Tena yametamkwa katika ibara ya 12 ya katiba na kuwekwa ngubu yake katika ibara 74 kwamba si tu yamewekwa kama kauli ya rohoni bali kama mamlaka inayoweza kutekelezeka, pia ibara ya 286(2) imeweka ufafanuzi wa jumla wa katiba yote ambapo mamlaka ya Wananvhi yamewekwa juu kabisa ya mamlaka zote, mihimili yote na yanatekelezwa kutia Haki ya sauti ya taifa ( ibara ya 74) naomba uisome kidogo hili uelewe hiyo haki ya sauti ya taifa ni nini..

Ila tunapswa tukubaliane Jambo moja kwamba Hatuwezi kukwepa mjadala wa Party Supremacy vs State Supremacy kwa sababu tukiweza kuamua hapo basi tunaweza amua iwapo People's Power itumike wapi.Je itumike katika kuendesha Chama ama itumike katika kuendesha State?
Kwenye Rasimu ya katiba niliyoitoa au pendekezo lilounganishwa na uzi huu ni kwa sababu swali lako linajibiwa kwamba Chama dola uzalisha udiktekta dhidi ya demokrasia, na Dola huru bila mamlaka ya usimamizi wa misingi yake dola ugeuka kuwa shamba la bibi lililokosa usimamizi, hapa sasa ndipo pendekezo langu la katiba yenye mihimili minne linaingia.
Pili kuhusu Mamlaka ya wananchi yatumike wapi..? Katika swali nililolijibu kwa asilimia zaidi ya 75% ni hili, kwenye rasimu hile. Swali hili alijajibiwa kwa ibara moja bali kwa mfumo mzima kwamba mamlaka hii hipo chini ya mamlaka gani, inawajibika kwa nani na kwa namna gani, pia falsafa ya katiba kuhusu mamlaka hiyo hipo tofauti kidogo na kwamba katiba nyingi au hata tuliyokuwa nayo sasa imetamka Mamlaka ya wananchi na kutokuweka inatekelezwa vipi, pendekezo langu limeipa mamlaka hiyo nguvu hasa ibara ya 74 na kuweka mamlaka nyingine iliyo chini ya mamlaka ya wananchi moja kwa moja kwenye ibara ya 255 isipokuwa kuna utaratibu wa kuthibitishwa kwamba hapa sasa mamlaka ya wananchi ingia, na kuchukuwa nguvu zake.
Jibu la moja kwa moja, Mamlaka ya wananchi hayawezi kuachwa kwenye mikono ya vyama vya siasa, wakati swali la kikatiba linaingia, Je Vyama hivyo hasa kile kilichotawala kikisema kinatekeleza matakwa ya mamlaka ya wananchi katika jambo la kuathili misingi ya taifa, nani anaweza kukizuia chama hicho...?

Ni muhimu sana kwa sababu nionavyo mimi,hatuwezi kuwa taifa ambalo kila mtu anafanya anavyotaka lazima tuwe na utaratibu na utaratibu huo lazima uwe wazi na unaoeleweka kwa mfano kama tukizingatia Party Supremacy inamaana kwamba Mchakato wowote ule lazima uanzie katika Ngazi ya Chama kabla haujafika kwenye ngazi za maamuzi ya serikali.
Exactly, Naomba nikujibu kwa ujasiri wa kisomi na kitaaluma kwamba Baraza la usimamizi wa Taifa ndio mamlaka iliyopewa dhamana ya kusimamia misingi ya kitaifa ambapo maadili ya taifa ni sehemu ya usimamizi wake.

Na iwapo tukiamua kwamba State Supremacy Ndio muhimu basi michakato yote lazima ianzie na kumalizikia kwenye Vyomba vya kiserikali ambavyo ni Bunge,Mahakama na Serikali Kuu.Kama ikiwa Hivyo ni lazima tuwe na Mahakama yenye Nguvu Kubwa,Bunge lenye Nguvu Kubwa na Serikali kuu Yenye Nguvu Kubwa. Sasa ili tutengeneze Hivi Vyombo Vikiwa na Nguvu Kubwa lazima tujiulize Central Power Atakuwa nayo nani? Je ni hili Baraza la Usimamizi wa Nchi?Kama ni hilo Je Baraza hili liundweje?Je liundwe na viongozi wa vyama vyote vya siasa?Kama ni Ndio Je Vyama Visajiliweje?Je Visajiliwe na Kusimamiwa na Sekretariat ya Hilo Baraza?Je Uchaguzi uendeshwe na nani?Je uendeshwe na Hilo Baraza la Usimamizi?
Kwanza kabisa naomba nikulekebishe neno dogo, Pale uliposema vyombo vya kiserikali Umechanganya Mihimili mingine kwamba hipo chini ya serikali na ulichotakiwa ni kutumia neno Dola. Kwenye rasimu hiyo ya katiba Kuna kanuni iliyowekwa inayoitwa "Kanuni ya ulinganigu wa nguvu za kikatiba" itakayowekwa ndani ya sheria ya usimamizi wa taifa kazi ya kanuni hiyo ni kupima hali nguvu ya mamlaka A kuwa juu ya mamlaka B kwa wakati C kisha mamlaka B kuwa juu ya mamlaka A kwa wakati D.

Kwanza kabisa Baraza la usimamizi wa taifa lina Marais wawili kutoka kila upande wa muungano, ambao hao si marais wenye serikali ya utendaji bali wenye dhamana ya usimamizi upande husika wa muungano, Misingi ya kitaifa na kama ilivyowekwa na katiba yenyewe. Marais wa baraza hawapatikani kwa mchakato wa kisiasa, bali ni weledi, ufanisi na masharti ya kikatiba pekee, pia ni kosa la kikatiba kwao kujihusishwa na siasa au kufanya maamuzi yenye upendeleo wa kisiasa kiasi cha kupitiliza dhamana yao ya usimamizi wa misingi ya taifa.

Marais wa baraza wa kila upande awajaacbwa wenyewe wamepewa wawakilishi wa kila upande wa muungano, yaani.
1. Baraza la mapinduzi zanzibar kwa upande wa zanzibar
2. Tanganyika social council kwa upande wa tanganyika.
Wawakilishi hawa na ni ndio taasisi za mwanzò za ushauri wa baraza pale baraza litakapoitaji ushauri au kushauriwa, basi hawa ukutana kwenye ofisi ya barqza iitwayo "Ofisi ya Maendeleo, Ushilikiano na Muungano" iliyo ndani ya Baraza lenyewe.

Baraza la usimamizi wa taifa limetamkwa kuanzia ibara ya 98 mbaka 116 ya katiba hiyo, hivyo basi mambo yote kuhusu muundo wake, majukumu yake n.k vimewekwa ndani ya ibara hizo.

Uchaguzi unaendeshwa na tume huru ya uchaguzi, Marais wa baraza wanapatikana kwa welwdi na sifa zao za kikatiba na pale sifa zao na weledi unapo kinzana kati ya wawili au zaidi kura ya maoni inaibuka kwa wananchi wa upande husika kumpigia kura ya maoni, hivyo marais wa baraza uchaguliwa kwa kura ya maoni na mchakago wa kura ya maoni inaendeshwa na Tume huru ya uchaguzi.
(Hapa naomba tuweke usahibi kwamba Marais wa baraza wanapatikana kwa mchakato huo na baadae baraza linakuwa na nguvu ya usimamizi, kilichofanyika hapa ni kuondoa maslahi ya kichama kwao hili wafanye maamuzi wakiwa wameweka maslahi ya pamoja mbele sio chama cha siasa) soma ibara nilizokuonyesha zinazohusu baraza kuanzia 98 mbaka 116 hili kupata picha kamili ya ninachokizungumza hapa.

Je Gharama za uendeshaji wa hilo Baraza zitoke wpi?
Kwenye nyoongeza ya katiba, yaani mwisho kabisa wa katiba na njee ya katiba yenyewe nimeweka Taratibu mbali mbali na kueleza ukweli wa gharama za uendeahaji lakini kwa ufupi kabisa baraza litaitaji 0.3% ya bajeti kuendeshwa lakini litaokoa 0.8% ya bajeti au zaidi iliyokuwa inapotea kwenye ubadhirìu, ufisadi na Wizi wa viongozi wa umma. Hili nalisema kwa ujasiri mkubwa sana kwamba ndio Muundo wa baraza unaweza kudhibiti Ufisadi na wizi wa mali ya umma kwa kiwango kikubwa.

Popote utakapoitaji ufafanuzi zaidi kipindi unasoma ibara hizo za katiba hasa 98 mbaka 116 nitakuwa tayari kutoa ufafanuzi.
 
Nchi yetu bado haina taasisi imara za kusimamia state supremacy. Tukisema chama kisiwe na kauli, tutatengeneza madikteta serikalini ambao hakuna wa kuwahoji.

Chama angalau kina vikao vya ndani vya nidhamu, lakini serikali ikiwa na absolute power, nani atamfunga paka kengele?
Exactly, Marcostilone nakumbuka kwenye uzi wangu mmoja tuliongea kuhusu muhimili wa nne wa kitaifa wenye jukumu la usimamizi wa misingi ya kitaifa na leo umeingia kwenye pendekezo langu la katiba moja kwa moja bila kujua kuwa unaingia humo, kwanza kabisa nikuombe usome ibara ya 98 mbaka 116 inayoeleza muundo, majukumu, mipaka na mengineyo kuhusu baraza la usimamizi wa taifa.

Naomba nichambue hiyo mihimili minne kwa majina.
1. Baraza la usimamizi wa taifa (mlinzi wa misingi yote ya taifa, mtoa tathmini ya hali za kitaifa na mtoa muongozo au amri pale "Kanuni ya ulinganifu wa nguvu za kikatiba zilizowekwa kwenye katiba hiyo na sheria ya usimamizi wa taifa inapooingia" ni nini hicho Kanuni za ulinganifu wa nguvu za kikatiba, ni kama mzani wa nguvu za kikatiba kulingana na hali ya taifa, mfano Pale usalama wa taifa unapolindwa kisha hapo hapo demokrasia ya kisiasa inachukuliwa, na maadui wa njee utumia jukwaa hilo hili kudhoofisha usalama wa nchi, hapa nguvu ya kikatiba italiweka kwamba Demokrasia ya kisiasa iendelee isipokuwa usalama wa taifa utawekwa mbele zaidi hili tuqe salama then turudi kwenye msingi wetu, naomba niseme wazi hapa kwamba maadui utumia njia nyingi kudhoofisha taifa fulani hivyo swala si kudhibi kile kilichokuwa ni miongoni mwa miaingi ya taifa swala ni kutambua kuwa mpaka ni huu pale hili linapotomea.

Pia naomba nisemw kwamba kwenye ibara zinazohusu usalama wa taifa imewekwa falsafa kwamba "Haki za msingi za kibinadamu si tishio kwa usalama wa taifa na kinyume chake tishio la usalama wa taifa linaqeza kufichwa chini au nyuma ya haki hizo hivyo basi TISS na kwa kuzingatia Tathmini ya Baraza kupitia ofisi yake ya Tathmini ya usalama wa taifa wana wajibu kutenganisha kwa umakini kile kinachoitwa haki a kile kinachoitwa tishio na hapo ndipo tishio litadhibitiwa na haki za msingi za kibinadamu kutokuvunjwa wala kudhoofishwa."

2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania ( ni serikali moja tu ya pamoja, yenye jukumu la utekelezqji wa sera za serikali na uendelwvu wa taifa)

3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania (lenye jukumu la uwakilishi wa wananchi, Kutunga sheria, kupitisha bajeti na mijadala ya uendelevu wa taifa ambapo katika dhamiri mbali mbali za wananchi na maoni yao ya namna taifa liende na dhamiri itakayopata kipaumbele zaidi kwa ndiyo itakayo tawala, "hapa maana yake dhamiri ni maoni ya nda kile ana amini kuwa ndio njia bora ya uendelwvu wa taifa hivyo wananvhi kuweka wawakilishi wao wa kibunge ni kwaajili ya kutafuta dhamiri itakayokuwa na hoja nzito za kupewa kipaumbele".

4. Mahakam ya jamhuri ya muungano wa tanzania (yenye jukumu la kutafasiri katiba na sheria za nchi, kutoa uhamuzi wa migogoro ya kikatiba na kisheria, na kutoa hukumu zote zinaloitaji mamlaka ya Mahakama,

muundo huu unafunga mianya yote ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma na mengineyo na hqpo ndipo uadilifu, uwazi na uwajibikaji utakapoibuka kwa asilimia zaidi ya 90%

Rasimu ya katiba yenye muundo uliotajwa hapo juu inapatikana katika tovuti ya www.katibampya.com

Nenda kaisome, kiaha njoo na hoja zako hapa za kuiunga mkono au kuikosoa kwa hoja na kwa uwazi kile unachoona kwenye ibara husika hakija wekwa sawa na si kukosoa kwa kejeri na matusi.
Karibuni kwa hoja mbaka tupate jibu je Party or state hipi ndio iwe na nguvu ya Dola zima.
 
Ni muujiza upi utatumika kutenganisha upacha huo wa chama tawala na dola? Kwasababu dola ndio nyenzo kuu ya chama chochote kile tawala ya kuongoza nchi na kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama husika inatekelezwa kadiri ya vipaumbele vya wananchi waliokipa dhamana ya uongozi ya chama hicho.

Dola ni mali ya umma, na vyama vyote vya siasa pia ni mali ya umma. Hakuna namna ya kutenganisha upacha huo wa kihistoria ulimwenguni kisiasa 🐒
naomba nijibu Swali lako.
Utengano huu unaitaji mamlaka huru ya usimamizi wa miaingi ya taifa, yaani kuwepo na muhimili kamili wenye kujumu la kusimqmia misingi ya kitaifa.

Kwanini nasema ni muhimu kuwepo na mubimili kamili, kwanza kabisa Chama kinachotawala chenyewe binafsi kisipojiwekea mipaka ya kutotumia dola kubaki kwenye dola kinazalisha udiktekta dhidi ya demokrasia na ni ukweli kwamba chama chochote hakitakubali kuruhusu chama kingine kichukuwe dola kisha kitumie dola kubaki kwenye dola kama wao wafanyavyo.

Jibu la swali hili ni uwepo wa muhimili wa nne wenye jukumu hilo na muhimili huo usiwe na chembe ya itikadi za kivyama bali weledi, ufanisi na sifa za kikatiba.

Naomba nipendekeze kwako Rasimu ya katiba iliyo kwenye www.katibampya.com ambapo rasimu hiyo ina muundo wa dola lenye mihimili minne, yaani.
1. Baraza la usimamizi wa taifa (linasimamia misingi yote ya taifa, kutoa tathmini na kutoa muongozo au amri ya muunvozo pale "Kanuni ya ulinganigu wa nguvu za kikatiba inapoingia"

2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania (lina jukumu la utekelezaji wa sera za serikali, Ulinzi wa taifa na uendelevu wa taifa)

3. Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania (lina jukumu la uwakiliahi wa wananchi, kutunga sheria, kupitisha bajeti na mijadala ya uendelevu wa taifa) hapa ndipo hoja yako hii inaingia,
dhamira, malengo na misingi ya kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa ni kushindanisha agenda, mipango na hoja za kisiasa, kijamii na kiuchumi, ili hatimae atakae shinda uchaguzi kwa kura nyingi, apewe dhamana ya umma kwa mujibu wa sheria, ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi wote.

Kwa lugha yepeai wananchi wanaweka mawazo yao kwa muwakilishi wao mmoja ndani ya bunge katika kila jimbo la uchaguzi na mawazo ya wabunge hao watakuwa na hoja nzito na kupewa kipaumbelw kwa hoja na hapo ndipo mjadala wa namna taifa liende litaenda, hivyo Mbunge wenye hoja nzito ndio uwakiliaha hoja za wananchi wa jimbo lake.

4. Mahakam ya jamhuri ya muungano wa tanzania (muhimili wenye jukumu la kufasiri katiba na sheria, kutoa hukumu ya migogoro ya kikatiba na sheria, na kutoa hukumu za jambo linaloitaji mamlaka ya mahakama)

Kwa unasiri mkubwa nasema kwamba muundo huu ndio muundo bora, na unaweza kuusoma kwenye tovuti tajwa hapo juu.
 
Nani anayesimamia hiyo mifumo ya kisheria? Si ni viongozi wale wale waliowekwa madarakani na chama?

Conflict of interest itaua hiyo nidhamu mapema mno.
Baraza halina kiongozi wa kisiasa hata mmoja, wote wanatokana na sifa, weledi na masharti ya kikatiba.
 
Back
Top Bottom