Mkuu
Nguruvi3, nilikuwa nimepania sana kuwa na mnakasha wa maana na huyu limbukeni
Deus J. Kahangwa lakini ghafla nikagutuka niliposoma namna anavyotoa majibu ya kipuuzi. Hivyo nikaamua kukaa kimya isije ikawa taabu kututofautisha...
yupi anamkimbiza yupi! Kwamba ni yeye tu anao uwezo wa kututafsiria alichosema Magufuli, kulinipa picha kamili ya uwezo wake wa kufikiri ulipofikia.
Mkuu hawa watu tumewakalia kimya wanadhani nchi nzima imejaa wendawazimu na wana uwezo wa kufanya na kusema watakalo tutaitikia na kuimba nyimbo walizotunga za kuhadaa
Nilisoma nikidhani kuna substance. Nilipomaliza nikahitimisha article 'imeandaliwa'
Ushahidi ni majibu yasiyolingana na hoja
Think about this, anasema Magufuli hakupiga marufuku mikutano.
Kwamba media houses hazikumwelewa isipokuwa yeye na Polisi
Tumemueleza si Magufuli tu, aliyeanza ni waziri mkuuMagufuli akapigilia msumari.
Tukamuonyesha aliposema mikutano ya kisiasa hadi 2020 ili atekeleza agenda zake.
Ingawa haieleweki mikutano inazuia vipi utekelezaji hiyo ndiyo kauli inayosemwa
Mada ikageuzwa, hatukumuelewa, kuna 'any form' ya mikutano na 'specific form'
Hakueleza ni aina gani ambayo Polisi na serikali na CCM wamezuia kati ya hizo form mbili
Polisi wamezuia 'any form' si za mikutano bali mikusanyiko.
Mazishi , kipindu pindu Mwanza, mahafali,ugonjwa Dodoma, mikutano ya siasa n.k.
Hivyo walichozuia ni 'any Form'
Kama ni 'specific form' Zitto na ACT alikuwa na mkutano specific kwa mujibu wa sheria ambao ulikuwa wa ndani. Polisi wakazuia. wakazuia kukutana na waandishi ofisini.
Polisi wamezuia 'specific form' ya mikutano
Kwa mantiki hiyo Polisi na serikali wamezuia 'any form na specific form'
CCM wamepewa ruhusa ya mikutano kwa vile ni 'specific form' ya mikutano.
Haki iliyowapa CCM wamenyimwa ACT-Wazalendo pale millennium tower
Katika double std ya namna hii, Polisi hawana majibu. Wamejikuta wakiulizwa maagizo hayo yanatoka kwa nani na kwanini kama chombo cha umma inaonekana kutumiwa .
Hoja ya wanaokwenda 'kusaidia' Polisi kama ulinzi jamii imeletwa na Polisi na CCM
CCM/ Serikali wametangeneza mazingira hayo sasa wanaruka kama si wao.
Mkuu, hawa watu waelezwe ukweli wakae wakijua nchi hii ni yetu sote, haina umiliki
Siasa za namna hii zinajenga chuki katika jamii isiyo na ulazima
Tunamshauri Deus ambaye 'apparently' ni msomi, apeleke habari hii gazeti la Uhuru
na ikajadiliwe Radio Uhuru.Hapa JF amekwama, amekimbia na ahsante akirudi, aje na kitu cha maana chenye mashiko na akili
Nilimwambia toka mwanzo, kama ni mawazo huru tunayaheshim, kama ametumwa akanawe uso, umejaa taka na harufu. Akajisafishe arudi jamvini akiwa msafi.
Deus J. Kahangwa Wasalimie huko na karibu tena jamvini
Masalaam