.
Kwa ufahamu wangu, mikutano iliyopigwa marufuku ni ile ya Bwana mvi kwenda kuwashukuru wananchi na kuwambia kwamba "nilishinda, nikaporwa ushindi, Magufuli sio Rais halali, lakini nimekubali yaishe ili damu isimwagike." Huu ni uhalifu chini ya Kanuni ya Adhabu CAP 16 RE 2002. Wewe huoni jambo hili?
OK now you show the true color.
Kama alizuiwa yeye na serikali imeshaundwa kwanini mikutano inazuiwa tena?
Imefika mahali hata mahafali inawatia hofu viongozi
Lakini pia, ilikuwa nafasi nzuri ya kumkamata Mamvi kwa uchochezi.
Si Magufuli ana dola , nini kinamtisha
Pili, mkutano wa ACT ulizuiwa, tena wa ndani! kulikuwa na sababu gani?
Tatu, Polisi na serikali wazuia hata mkusanyiko wa mazishi kule Mwanza. Ni sawa hiyo?
Nne, tueleze ni wajibu wa jeshi la Polisi kutangaza kipindu pindu na kuzuia mikutano?
Tano, Jeshi la Polisi lina uwezo gani wa kubaini maradhi yasiyhitaji mikutano?
Sita, tueleze kwanini waziri mkuu alizuia mikutano akisema ni wakati wa kazi?
Utaona kuwa Polisi hawakujua CCM itakuwa na mkutano.
Serikali ilisahau wananchi wa leo si wa jana na kwamba hawawezi kudanganywa na sababu za kitoto zisizo na mashiko
Tamko la Magufuli kupiga mikutano marufuku liekiuka katiba na uhuru wa kukusanyika na kutoa mawazo ndani ya sheria.
Ni tamko lililochagua makundi ya jamii na hivyo kuleta 'discrimination'
Rais ni kiongozi wa Taifa, hatakiwi kubagua CCM na Wapinzani.
Akishatangazwa anakuwa wa wote, wezi, wafanyabaishara wapinzani na WanaCCM.
Ni jambo la hatari kutenga CCM na makundi mengine. Ni kujenga matabaka
Ndio maana nasema kama ni mawazo huru naheshimu sana mawazo yako, kama umeagizwa au kutumwa, kwakweli tafuta mahali pa kunawa, uso umejaa taka