. But note this: the political parties act says that electroral politics shall be engaged in within a specific time frame as defined by NEC--Ratibu ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu. So there is nothing new in the words of the President when he says, "electoral politics are over." Umeonae?
Hapa ndipo ndugu yetu anapodanganya na kupotosha umma. Hoja yake inakosa mashiko na ni ya uongo kwa sababu zifuatazo
1. Nimepitia Political parties act, hakuna kipengele kinachosema siasa za uchaguzi ni za muda maalumu.
Mleta mada anachanganya Political parties act na sheria za tume ya uchaguzi.
Ratiba ya uchaguzi hai define political process katika nchi.
Ratiba ya uchaguzi ina eleza hatua za uchaguzi katika msimu uliotajwa kikatiba.
Kwamba, kutakuwa na uchaguzi kila baada ya miaka 5.
Tume ya uchaguzi inatoa ratiba hiyo kama ambavyo sheria imeiwezesha.
Shuguli za kisiasa kwa mujibu wa ''Political parties act'' inatoa fursa za kufanya siasa bila muda kwa kifungu Sehemu ya Pili 4-(1) inayoeleza ushiriki wa vyama na haki za mikutano n.k.
Hakuna mahali popote pale sheria ya vyama vya siasa au tume ya usajili imeeleza mwisho wa msimu wa siasa, narudia msimu wa siasa.
NEC walikabidhi ripoti ya kukamilisha uchaguzi si kumaliza msimu wa siasa.
Hivyo kazi ya NEC ni kuratibu chaguzi si kumaliza muda wa siasa nchini.
Kazi ya msajili wa vyama kwa mujibu wa sheria ni kusimamia shughuli za vyama vya kisiasa vlivyoandikishwa bila kuweka msimu,
Huyu ndugu haoni jambo jipya alilosema Rais, pengine tumkumbushe kifungu 18 cha katiba ya JMT na sehemu ya pili na ya tatu ya sheria ya vyama vya siasa nchini zinavyoeleza.
Atueleze Rais alitumia utaratibu gani kupiga marufuku juu ya sheria zilizopo?
Deus hatengenisha shughuli za msajili na NEC anawezaje kutueleza mambo ya siasa?
Siasa ni shughuli endelevu katika jamii ndiyo maana imewekewa act.
Uchaguzi ni shughuli inayokamilisha sehemu ya shughuli za kila siku za siasa inasheria zake