Magufuli didn’t ban all forms of politics...

Magufuli didn’t ban all forms of politics...

.
Ni haki kwa chama cha siasa kuzunguka nchi kikieneza habari za uwongo kwamba Rais Magufuli hakushinda kihalali? Jitazame tena.

Dah kaka....be sure of what you levarage in...hapo unatoka nje ya mstari na kuwa kada perse..!!!! Nilidhani unasimamia kwenye hoja tu....

Politics have never been a good game ukizipa promo nzito kihiiivooooo..just be like Mzee John Malecela...the wise person....

Wewe ni msomi.mzuri.and you are intelligent...you can make.the world the better place to live....not that way bro...
 
.
Umetumia maneno makali 'waandishi uchwara." Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford University Press, 1980) neno "uchwara" ni kivumishi kinachomaanisha "-enye kutokuwa na thamani, -a kudharaulika, duni." Kwa hiyo unasema, hiyo thread yangu hapo juu ni yenye kutokuwa na thamani, ya kudharaulika, na duni. Kama hilo ndilo hitimisho lako, basi wewe unao ubongo uchwara.

Deus;
I can tell yu ma brother, nilikuwa follower wako sana lakini, nilipoisoma thread yako hii kuonesha kuwa ati wewe ndio tuu uliyeweza kumuelewa JPM na tamko lake hilo hivyo wengineo woote Tz hawakumwelewa!! Nimeshangaa. Bora tu nibaki na bongo langu uchwara kuliko kukubaliana na uandishi uchwara unaoonesha kutaka kujikomba ili mtu akumbukwe hata kwa U DC. Nisamehe bureeeee. Huwezi halalisha mkutano huu wa ccm wakati polisi wameweka msimamo tofauti na hayo mawazo yako. Waelimishe kwanza polisi
 
Halafu Social media zinawatoa watu sana, akina polepole walipiga kelele wakasikiwa, na wengine wengi, inaonekana macho ya serikali yapo sana mitandaoni!

Ila Magufuli ana kauli tata balaa, cheki hii, "Kwa sasa hivi, iwe kwa bahati nzuri au kwa bahati mbaya, serikali inayoongozwa ni ya Chama cha mapinduzi.."

Hapo kwenye bahati mbaya ndo ukweli. Ni kwa bahati mbaya kwa sababu madudu yote.Sijui "wafanyakazi hewa" sijui

"barabara hewa" vyote vimefanyika chini ya serikali hiyo hiyo ya CCM na yeye akiwa mmojawapo kama kiongozi miaka zaidi ya 20.

Kwa sasa wanasiasa wanajua kucheza na media kwakuwa wanajua huko ndiko vyeo vinapatikana.Rejea DC wa

Iringa.Makonda.Polepole.Mwampamba. Kwa kutaja wachache...
 
OK now you show the true color.

Kama alizuiwa yeye na serikali imeshaundwa kwanini mikutano inazuiwa tena?

Imefika mahali hata mahafali inawatia hofu viongozi

Lakini pia, ilikuwa nafasi nzuri ya kumkamata Mamvi kwa uchochezi.
Si Magufuli ana dola , nini kinamtisha

Pili, mkutano wa ACT ulizuiwa, tena wa ndani! kulikuwa na sababu gani?

Tatu, Polisi na serikali wazuia hata mkusanyiko wa mazishi kule Mwanza. Ni sawa hiyo?

Nne, tueleze ni wajibu wa jeshi la Polisi kutangaza kipindu pindu na kuzuia mikutano?

Tano, Jeshi la Polisi lina uwezo gani wa kubaini maradhi yasiyhitaji mikutano?

Sita, tueleze kwanini waziri mkuu alizuia mikutano akisema ni wakati wa kazi?

Utaona kuwa Polisi hawakujua CCM itakuwa na mkutano.

Serikali ilisahau wananchi wa leo si wa jana na kwamba hawawezi kudanganywa na sababu za kitoto zisizo na mashiko

Tamko la Magufuli kupiga mikutano marufuku liekiuka katiba na uhuru wa kukusanyika na kutoa mawazo ndani ya sheria.

Ni tamko lililochagua makundi ya jamii na hivyo kuleta 'discrimination'

Rais ni kiongozi wa Taifa, hatakiwi kubagua CCM na Wapinzani.

Akishatangazwa anakuwa wa wote, wezi, wafanyabaishara wapinzani na WanaCCM.

Ni jambo la hatari kutenga CCM na makundi mengine. Ni kujenga matabaka

Ndio maana nasema kama ni mawazo huru naheshimu sana mawazo yako, kama umeagizwa au kutumwa, kwakweli tafuta mahali pa kunawa, uso umejaa taka

Na huyu ndiye alitaka

Amesema haiwezekani kila siku ni siasa, watu watalima saa ngapi? Unamaanisha kilimo kinaweza kufanyika bila siasa? Au kwa maana nyingine kwenye kilimo hakuna siasa?
 
Hapo kwenye bahati mbaya ndo ukweli. Ni kwa bahati mbaya kwa sababu madudu yote.Sijui "wafanyakazi hewa" sijui

"barabara hewa" vyote vimefanyika chini ya serikali hiyo hiyo ya CCM na yeye akiwa mmojawapo kama kiongozi miaka zaidi ya 20.

Kwa sasa wanasiasa wanajua kucheza na media kwakuwa wanajua huko ndiko vyeo vinapatikana.Rejea DC wa

Iringa.Makonda.Polepole.Mwampamba. Kwa kutaja wachache...

Hili neno "iwe kwa bahati mbaya au nzuri" ni Utata mtu linaleta hisihisi za wasiwasi ukirejea jinsi uchaguzi ulivyoenda! Huyu jamaa kuna siku atakuja kutamka jambo tusilolitegemea hadharani, tusubiri tu!
 
.
Jibu ni rahisi: Rais hana mamlaka ya kikatiba ya kuzuia "any form of politics in Tanzania."

Safi sana kwa hilo jibu lako.

Kichwa cha habari cha uzi wako kinasema hivi "Magufuli didn’t ban all forms of politics''

Zile forms zingine za siasa alizoban, alifanya hivyo kwa mjibu wa nini?
 
Hili neno "iwe kwa bahati mbaya au nzuri" ni Utata mtu linaleta hisihisi za wasiwasi ukirejea jinsi uchaguzi ulivyoenda! Huyu jamaa kuna siku atakuja kutamka jambo tusilolitegemea hadharani, tusubiri tu!

Kuna siku alisema polisi makao makuu walikula mabilioni zaidi ya 25 bilioni wakati wa uchaguzi.Polisi walitakiwa wanunuliwe sare. Jamaa juu wakazitafuna. Polisi wadogo wakawawanaambiwa waende kwa Mhindi kuchukua.Lugumi.

Na anajua uchaguzi ulivyokwenda."Ma-rope" anaujua mchezo vizuri. Ndo mana haguswi na mtumbua majipu....
 
Mkuu mimi siungi mkono chama chochote na sina unazi wa mambo ya kisiasa yasiyokuwa na hoja... Lakini pia naunga mkono hoja yako ya kutaka Mh.Raisi atoe ufafanuzi kwa kauli yake!!

ila hizi double standard mbona zipo ata kwa CHADEMA pia... CHASO Dar es salaam na CHASO Iringa walifanya mikutano yao bila polisi kuwazuia... Je wao walifuata taratibu zipi??

kama lengo la Mh.Raisi ni kuzuia mikutano ya kisiasa ambayo haivunji taratibu zozote apo mimi simuungi mkono maana kufanya ivyo ni kuminya Demokrasia... ila kama vyama vya siasa vinakiuka taratibu kwanini visidhibitiwe??!!

Siku zote UHURU bila NIDHAMU ni UWENDAZIMU na NIDHAMU bila UHURU ni UTUMWA... lazima tujifunze kutumia uhuru wetu vizuri.

Mkuu Aminato;
Naomba nieleweke vizuri tu hapa. Kwanza sitaki kuunga mkono upuuzi wowote ule unaomuwezesha mtu mmoja au kikundi kuumiza wengine. Nasema sipendi na sintaunga mkono.
Nikiisha eleweka hivyo nataka niseme hivi; Polisi wetu, wameingizwa katikati ya wanasiasa. Wapo wanaowafaidi na wapo ambao wanawaona maadui. Sasa, wajitahidi kujiondoa kwenye huu mtego.
Endapo kutatokea majeruhi Dodoma, lawama hazitawaendea wanasiasa naamini zitawaangukia polisi. Sasa, kwa nini, kama huko nyuma polisi walizuia hayo makongamano na mikusanyiko kwa neno lao tu, leo kimewashinda nini kutamka kwamba, Kutokana na hali hii kuwa tete, ccm ahirisheni mkutano wenu till hali iwe nzuri?? Ni wazo tu, sijasema naamuru.
 
No Political activities till 2020 or else you will talking to Police force.
 
Kuna siku alisema polisi makao makuu walikula mabilioni zaidi ya 25 bilioni wakati wa uchaguzi.Polisi walitakiwa wanunuliwe sare. Jamaa juu wakazitafuna. Polisi wadogo wakawawanaambiwa waende kwa Mhindi kuchukua.Lugumi.

Na anajua uchaguzi ulivyokwenda."Ma-rope" anaujua mchezo vizuri. Ndo mana haguswi na mtumbua majipu....

Ninachompendea jamaa ni kauli zake tata, huwa anazirusha kama bomu, halafu anaanza kutabasamu, huku akichekicheki pembeni! Muda unavyoenda hii kazi ya kuwa prezidaa inakuwa ngumu vibaya mno, sasa kichwa kikifikia degree za moto kama ilivyokuwa kwa Jeikei, ndipo utegemee kauli tata zaidi!
 
Mkuu Aminato;
Naomba nieleweke vizuri tu hapa. Kwanza sitaki kuunga mkono upuuzi wowote ule unaomuwezesha mtu mmoja au kikundi kuumiza wengine. Nasema sipendi na sintaunga mkono.
Nikiisha eleweka hivyo nataka niseme hivi; Polisi wetu, wameingizwa katikati ya wanasiasa. Wapo wanaowafaidi na wapo ambao wanawaona maadui. Sasa, wajitahidi kujiondoa kwenye huu mtego.
Endapo kutatokea majeruhi Dodoma, lawama hazitawaendea wanasiasa naamini zitawaangukia polisi. Sasa, kwa nini, kama huko nyuma polisi walizuia hayo makongamano na mikusanyiko kwa neno lao tu, leo kimewashinda nini kutamka kwamba, Kutokana na hali hii kuwa tete, ccm ahirisheni mkutano wenu till hali iwe nzuri?? Ni wazo tu, sijasema naamuru.
Kujichanganya kwa Polisi kunatokana na ukweli kuwa CCM wana mkutano mkuu na hawawezi kuwazuia.
Wapinzani wana hoja, kama lipo tamko la kupiga marufuku mikutano kwanini linachagua makundi ya jamii? Polisi hawakuwahi kutoa ufafanuzi kuhusu mikutano ya ndani na nje ya kisheria na 'haramu'

Katiba inaeleza wazi watu wana haki ya kukusanyika kwa kufuata sharia.
Haki ya kuzuia mikutano ya baadhi ya makundi ya jamii ipo wapi kikatiba?

Ukisoma bandiko la huyu bwana, inaonekana ni yeye na Polisi ndio walioelewa tangazo.
Ikiwa hi hivyo, kuna hatari tukizingatia hata vyombo vya habari havikuelewa

Hapa ikubalike tu kuwa tamko la marufuku linaibana serikali na CCM. Zinatafutwa hoja ndeefu kuhalalisha jambo hili ambalo lina uhalali wa kikatiba.

Wanasimamia sharia wanazipinga kwa mkono mwingine
 
Kitu gani?

Mkuu nilikuwa nakualert kwamba jamaa anasema Magufuli hakuban aina zote za siasa, ameulizwa swali kama rais ana uwezo wowote wa kimamlaka kuzuia aina yoyote ya siasa au lah, akajibu hana! Sasa wewe umemwuuliza utetezi wake umebase kwenye nini, ndio nilikuwa nakuweka sawa usikilizie jinsi mtaalamu aliyebobea kwenye siasa atakavyojibu!
 
Nimekuelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom