Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli bila madaraka yukoje?

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty

Nini maoni yako leo hii Mzee Mwanakijiji katika hiyo para nyekundu?
 
Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.

Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.

J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.
Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango. Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa. Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.

J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.

Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.

Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.

La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.

Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.
Uliongea powa
 
Magufuli ni wa ajabu kidogo kwangu. Amewahi kusimamia kwa nguvu zote uuzwaji wa nyumba za serikali. Atwambie hii nisheria ipi alikuwa anasimamia.

Juzi hapa kashikilia mabango yote yaliyoko pembeni mwa barabara za TANROADS yaondolewe. Hajatuambia ni sheria ipi alikuwa anasimamia. Mabango haya mwaka jana yalisheheni picha za kampeni za bosi wake JK na yalikuwepo tangu akiwa wizara hiyo enzi za Mkapa. Anajua sana kucheza na vyombo vya habari na hasa TV.

Kwa hili hana tofauti na Lowasa.
Kwahiyo magufuli na lowassa saw?
 
MIMI UPINZANI ila toka kampeni zianze MAGUFURI NAMKUBALI nilimpa kura yangu Lowassa kwa ajili ya katiba tu sio utendaji JPM hata ongea yake tu inatosha kukuthibitishia kwamba hayumbishwi na mtu NA MSIMPIME KWA YAKE YA KALE TUMPIME SAIVI KIPINDI KILE ALIKUWA CHINI YA SHERIA NAE
mbona tumeona mengi hamishwa yake wizara ya uvuvi wangapi hawajui chanzo chake WATANZANIA HEBU TUBADILIKE TUKUBALI PALE YATOKEAPO MAZURI
 
MIMI UPINZANI ila toka kampeni zianze MAGUFURI NAMKUBALI nilimpa kura yangu Lowassa kwa ajili ya katiba tu sio utendaji JPM hata ongea yake tu inatosha kukuthibitishia kwamba hayumbishwi na mtu NA MSIMPIME KWA YAKE YA KALE TUMPIME SAIVI KIPINDI KILE ALIKUWA CHINI YA SHERIA NAE
mbona tumeona mengi hamishwa yake wizara ya uvuvi wangapi hawajui chanzo chake WATANZANIA HEBU TUBADILIKE TUKUBALI PALE YATOKEAPO MAZURI
 
b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty

Hakika hili linatokea sasa!
 
Hivi mnamjua Magufuli Jimboni kwake?
Nyie magufuli mnanjadili katika dhana ya utendaji wake kitaifa lakini katika ngazi ya jimbo mtu huyu ni mchafu kupitia kiasi .

Mfano :Mafgufuli aliteka viwanja chato,akajenga majumba mtaa mzima,kanisa,hotel nk kisha akashinikiza Serikali ili Jimbo la chato kujitenga kutoka Biharamulo ili iwe wilaya na Halmshaurui inayojitegemea ,Akafanikiwa.Sasa watumishi wa Halmshauri ya Chato wakapanga kwake.

Hivyo hadi sasa idara zote za halmshauri ya chato zinapanga kwake pamoja na kuishi hata Waziri mkuu alipofika chato alilama Kwenye nyumba zilizo na hasdhi kama ikulu(mali ya magufuli).

Kwa ufupi Serikali nzima katika hslmshuri ya chato inapanga kwa Magufuli.
Inawezekana alitafuta kwa uwezo wake lakini si msafi kama wengi wanavyodhani .

Kwa siku za usoni nitaanzisha thread mpya kuhusu huyu Bwana.
Hehehe uhongo mwingine bwana hehehe ni nacheka tu
 
Back
Top Bottom