Magufuli bila madaraka yukoje?

Magufuli bila madaraka yukoje?

Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty

!
!
hii iliandikwa lini hii? huyu mwandishi alifunuliwa aiswe
 
Mwanakijiji alishasahau kama aliwahi kuandika kuhusu Magufuli. Saizi ameside nae. Njia moja saizi. Usimwamini mwanadamu kabla hajafa.
Hivi nyie chadema mmekuwa na akili gani? Kwani kuna kitu gani kibaya mwanakijiji kaandika kuhusu Magufuli? Alichosisitiza ndio kinaonekana leo.. Kapewa rungu na mnaisoma namba vibaka wote.
 
Ulitaka nje ya madaraka yap wakati tokea mwaka 1995 yuko ndan ya madaraka
 
Mwanakijiji alishasahau kama aliwahi kuandika kuhusu Magufuli. Saizi ameside nae. Njia moja saizi. Usimwamini mwanadamu kabla hajafa.
The most likely scenario ni kuwa kuna mahali amepata kutuliza njaa katika serikali hii. Kuna mahali humu amesema kuwa ukiwa na njaa unaweza kula bila kunawa! MWKJJ akaunga mkono sana. Please MWKJJ can you flashback your memories to this thread!
 
MM,siku hizi anazikana nyuzi zake kafika bei..lakini vitu vyake alivyokuwa akiongea ndo vinatimia kwa sasa ila yeye bado anajipinga kama Lipumba
 
Ndiyo maana tunamshangaa. He was a man of critical analysis of issues! Njaa mbaya! It might be kama siyo yeye, kuna ndugu zake wamepata madaraka makubwa hivyoo njaa imepata mahali pa kuiganga! IT IS A PITY KUWA HANA TOFAUTI NA CHEYO NA MREMA NA BANA
 
Ninadhani humjui unayemzungumzia ndugu, jaribu kutafuta mada zake katika kipindi hiki cha utawala wa Uncle Magufuli utaelewa ninamaanisha nini.
Wewe ndio hujamwelewa mleta uzi. anaongea kwa lugha ya kinyume...
 
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?

Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?

Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?

Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?

Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?

Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:

a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.

b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.

Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:

a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.

b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.

my two cents plus the other fifty

Mmmm...enzi hizo. Ni vema tukapata update ya hii mada kutoka kwa MMM mwenyewe...
 
Ndiyo maana tunamshangaa. He was a man of critical analysis of issues! Njaa mbaya! It might be kama siyo yeye, kuna ndugu zake wamepata madaraka makubwa hivyoo njaa imepata mahali pa kuiganga! IT IS A PITY KUWA HANA TOFAUTI NA CHEYO NA MREMA NA BANA
Katika vitu ambavyo vinanifanya nimkumbuke Nyerere ni kupinga UKANDA na UKABILA .
 
Mimi naamini kabisa mtu tofauti na MMKJJ sasa hivi akii copy hii thread na kuiweka kama thread mpya huyu huyu MMKJJ anaweza kuwa wa mwanzo kuipinga!

Pamoja na weight ya kutosha iliyobebwa na ujumbe huu bado huyo mzee kwa sasa ataipinga. Thanks kwa aliyeichimbua makala hii angalau inatukumbusha MMKJJ asiyechakachukuliwa anafananaje. We really miss him.
 
Msimamizi wangu wa ndoa aliasa kuwa " MWAMINI YESU PEKE YAKE" . Kweli mwanadamu si wa kuamini
 
Wala si uongo mkuu. Katika surprises kubwa kabisa katika uchambuzi wa siasa nchini ya MMKJJ ni namba moja yangu. Mwakyembe hana la kunisurprise kabisa.
 
Back
Top Bottom