Magufuli bila madaraka yukoje?


Heshima Mkuu! Mimi nilivyomwelewa MM, ni vigumu sana kujua msimamo wa Magufuli, anasimamia nini hasa katika masuala ya kitaifa. sawa, anaonekana mchapa kazi sana, lakini so far ukipiga picha, anaonekana kufaulu akiwa katika madaraka tu. sasa MM amejenga hoja hapo, na binafsi nimeikubali. conclusion yake pia, kwamba kwa maana hiyo itakuwa ni vigumu sana Magufuli kujiuzulu, kwa sababu hawezi kusimama kama yeye na msimamo wake, aka-flourish. na hoja hii ya MM inakuwa urgent kwa sababu kama asemavyo MM, PM na JK wamemlima jamaa kisawasawa, kiasi kwamba unabaki unashangaa huyu jamaa bado yupo. nadhani kwa mtu mwenye msimamo hasa, alitakiwa ajiuzulu na kama ni mtu mwenye misimamo inayojitokeza kitaifa, bado anaweza kuwa relevant and effective katika kusimamia yale anayoyaamini katika taifa hili. ndivyo anavyofanya Dr. Slaa, kwa mfano. sasa hivi sio mbunge, lakini akisimama mahala akaongea, watu wanamsikiliza na serikali inatetemeka
 
mkuu, hapo kwenye red umenikuna hasaaaaa!
 
Kwa upande wangu sijui kama nitamweka wapi huyu mheshimiwa. Naweza nikasema kuwa ni "mtendaji" anayetaka kuacha legacy kila aendako.Haijalishi ni aina gani ya legacy!
Namkumbuka vizuri sana kwenye maswala yafuatayo:

  • Kufuatilia "uporaji" wa magari ya serikali alipokuwa wizara inayohusika na Ujenzi na magari ya serikali.Alitetemesha watu pale alipothubutu kuwanyang'anya magari wazito walioandikisha magari ya serikali namba za binafsi na kuwapa wapendwa wao!
  • Aliposimamia uvuvi haramu hadi kukamata tani kadhaa za samaki waliovuliwa pasipo uhalali ndani ya maji yaliyomo ndani ya mipaka ya Tanzania - alipokuwa katika wizara inayohusika na uvuvi ( sijui kama mwisho wa sekeseke hili ulikuwa mzuri ama la hii ni ishu nyingine!)
  • Aliposimamia uuzwaji wa nyumba za serikali kwa watumishi wa umma ( wengine hawakuwa watumishi wa umma bali walikuwa wako karibu na watumishi wa umma) bila kujali malalamiko yaliyokuwa yakitokea ndani ya jamii - huenda kwa vile Serikali nzima iliunga mkono uamuzi huu na hivyo kupata confidence kuendelea bila kutetereka.
  • Uamuzi wake wa sasa wa kubomoaboamoa majengo ya watu binafsi na hata ya umma ya gharama kubwa kwa vile anasimamia sheria - japo hapa kuna kukosekana kwa support ya bosi wake.
Kitu kimoja ninachoona ni kuwa bila kujali "public policy" ya wakati husika, huyu kiongozi hufanya maamuzi ambayo wakati mwingine huwaacha watu wabaki wakijiuliza maswali mengi mno.Inawezekana anasimamia sheria na taratibu.Lakini kama anaonyesha double standards siwezi kumtafsiri na kumweka upande wowote.Kama ni msimamizi wa haki - ingetegemewa asitishe lile zoezi la kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa kwa kisingizio cha kuwasaidia watakapostaafu wasiadhirike wapate makazi.Siyo siri nyumba nyingi zimeuzwa kwa wahindi na wamejenga ma apartments - apartment moja yenye vyumba vitatu vya kulala kwa mfano Masaki inauzwa kuanzia dola za kimarekani 200,000 hadi 700,000 na hii ndio bei wenzetu waliouziwa kwa bei ya kutupa wameuza nyumba zile.Jengo moja linaweza kuwa na apartment hata 20! Piga hesabu.Ingetegemewa basi awe sharp zaidi kuona hili na kuhakikisha serikali hapati hasara kwa uuzwaji wa mali zake! Simuelewi kabisa huyu Mheshimiwa!
 
Kimsingi magufuli ataonesha taswira ya uzalendo na upiganaji wa haki ya matumizi endelevu ya rasilimali za taifa kwa maslahi ya watanzania pale ambapo atajiuzulu-kuonesha ishara ya kukerwa na wakubwa wake! Vinginevyo: Bado hana taswira ya uzalendo, kimsingi akishindwa kujiuzulu ni ishara tosha kuwa ..yeye bila "pazia la madaraka hawezi kuzuia upepo na vumbi kuingia ndani"
 
Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.


you are right absolutely! Na mimi ni miongoni mwa watu ambao nilikuwa ninaamini Magufuli ni kiongozi wa principle... lakini hili bado linanisumbua.
 


ni wazi kwamba haya aliyoyafanya hivi karibuni hayakuwa sahihi - kwa mtazamo wa viongozi wake wa juu kitu ambacho kikanuni ilimpasa kuachia ngazi.
 

Neno la leo.
 
Ndugu MM, topic yako hii, inaweza kukuweka mahali pabaya hata wewe, kwa sababu inaonekana kama kumjadili mtu. Tukumbuke kuwa simple minds discuss people... .

Utaona kumbe hatumjadili mtu kama mtu bali mtu na kanuni inayomuongoza; ndiyo maana sijasema "Magufuli yukoje?"; swali ni Magufuli bila ya madaraka. Na utaona wachangiaji karibu wote wanachangia - ukiwemo wewe- kwa kuangalia kiongozi aitwaye magufuli akiwa na madaraka au pasi na madaraka. Huku si kumjadili mtu kama mtu.
 

MMKJJ sijakuelewa una maana gani kusema magufuri anatete maslahi ya Umma, labda uende detail kuelezea kama ikiwa maana yako ni kuwa kubomoa hizo nyumba ndio maslahi ya Umma kwako wewe, si mbaya pia ukatwambia hiyo tafsiri una-evidence wapi?

Labda kama kuna kitu mnajadili kuhusu magufuri hamja kiweka wazi pia ni vyema mkatwambia na sisi maana kama ni swala la Bomobomoa Mimi na Jatropha tumelieleza kinagaubaga na kihalisia pia tumeanisha taratibu ambazo zilitakiwa zifuatwe ambazo Magufuri alizikiuka, tokea awali tumejitahidi na kujitolea kufafanua hili swala kwa upana wake hadi sasa hamna mtu aliyediriki kuzijibu hata hoja moja. Jana nilisoma comments zako katika thread ya "Magufuri tumeelewa" Nilikuandia na kukuomba kupata muda usome michango ya Jatropha na yangu binafsi katika threads zote za magufuri humu ndani ukianzia na ile "PM anatumiwa kumchafuwa Magufuri" hadi ile ya "Serikali ya kanusha kujizuru kwa Magufuri" nilikwambia usome hizo threads na pia kama utaweza tafuta "legal Opion" nilikushauri kama una fahamiana na Mhe.Lissu muombe ushauri wake maana lazima atakuwa Live cases za Bomobomo za Magufuri, nilikuwa naamini kuwa hujapitia michango ya baadhi ya members na hivyo nilidhani ingekusaidia sana. Hii threads yako imenioyesha au bado hujazisoma hizo hoja au la kama umeyasoma basi kuna jambo juu ya magufuri ambalo labda mnalijadili kwa kutumia neno bomoabomoa, na hivyo kutuacha kwenye mataa sisi tunaochangia na kutoa ushahidi kuwa Magufuri alikosea katika hili la kutaka kubomoa nyumba za watu wenye haki kisheria bila kufuata utaratibu na kwa mabavu.

Tunaomba mtwambie kuna nini? maana hata hivyo hizi threads za Magufuri zinafurika humu kila baada ya dk.5 na Mods pia hawaoni kama zinarudiwa bila tija yoyote wakati wanazileta wamegoma kujibu wala kutoa hoja yoyote.

Pia Naami unajua mambo mengi na wewe ni mfuatiliaji, kama utapata muda na kusoma hizo threads nilizokuomba kusoma naomba uje tena hapa katika hii threads yako utusaidie mambo yafuatayo:

  1. Magufuri anasimamia sheria ipi ya nchni inayompa mamlaka ya kuvunja nyumba za halali za raia tena wenye haki milki ya ardhi bila notice na fidia yeyote?
  2. Uje tushauriane katika hii nchni yetu nani ana mamlaka ya kupanga na kugawa matumizi ya ardhi, kama ukiwa na hisia kama zangu kuwa mwenye mamlaka ya kugawa ardhi ni Wizara ya Ardhi, basi tushauriane pia kuwa inakuwaje mwenye mamlaka agawie mlalahoi ardhi, ateseke kuuza mchicha karikoo na kujenga nyumba yake then aje mwingine katika serikali hiyohiyo iliyokupa ardhi aje tena nyuma kuibuka na kubomoa nyumba yako kwa ubabe na lazima bila taarifa wala fidia yeyote? Huku akinadi kuwa haijui wala haitambui hiyo sheria iliyokupa ardhi, tushauriane kama ikiwa tafsi ya sheria kwenu wenzetu ndio hiyo.
  3. Lakini cha Msingi kinacho pindisha hapa ambalo na hitaji tujadiliane Mkuu, ni iwapo Magufuri ana simamia sheria au ana chukua sheria mikono mwake? nataka tufafanue na kuchambua iwapo kumchoma moto kibaka ni kusimamia sheria au ni kuchukua sheria mikononi!? na inatofauti gani kwa upande wa shillingi katika hili Magufuri?

Mkuu nashukuru sana, naamini wote tunajenga nyumba moja ila tofauti ni kuwa Mimi na changanya ugongo na Wewe unakata fito, nasubiri fito uje nazo.
 
you are right absolutely! Na mimi ni miongoni mwa watu ambao nilikuwa ninaamini Magufuli ni kiongozi wa principle... lakini hili bado linanisumbua.
Magufuli sio kiongozi wa Principle, na hii imejidhihiriasha sasa. Magufuli ni kama robbot unaliprogram halafu linafanya kazi kulingana na ulivyo liprogram, nasema hivyo kwa sababu kila wizara anayoenda anakariri sheria na miongozo yake na kuanza kutekeleza bila kuipa nafasi akili yake kupambanua. Na ndio maana nje ya uongozi hana kitu anachoweza kufanya. Hana principle zake anazozisimamia.
 

sn2139 - ndio maana naamini ya haya maswali na uchokozi wangu hapa.. of course tunajua mawaziri wanafanya kazi at the pleasure of the president.. kwa hiyo upande mmoja ni kuwa ili aweze kuendelea kuwa madarakani na kufanya anayotaka hana budi kulamba miguu ya bosi wake. Swali langu ambalo ndio msingi wa hoja (natumaini Waberoya naye ataliona) ni kuwa viongozi hawa wanapotofautiana hivi ni nani ajiuzulu on principle? Swali langu halihusiani na upiganaji n.k linahusu kutawala na kuwabika kama kiongozi pale tofauti za msingi zinapotokea.
 

Hapo kwenye bold, naomba ufafanue.

Nijuavyo mimi, Waziri ana majukumu 1. Kusimamia sera za serikali iliyomweka madarakani 2. Ni political commissar hivyo anasimamia sera za chama na ilani ya uchaguzi ya chama chake. Ina maana hawezi kutenda nje ya mandates hizi.

Swali linakuja hivi: Je ni kazi yake kwenda frontline na kusimamia kama afanyavyo? Je katika kusimamia sera ( pamoja na Sheria) huyu waziri angeweza kuwa tofauti kiutendaji na akawa na tija? Kuna nafasi ipi itakayomwezesha kutenda effectively nje ya 'madaraka" yake?( madaraka ilivyotumiwa na MMKJJ ni sawa na mandate?)
 
Kimsingi hii inaonyesha kwa namna fulani viongozi anaowatumikia JPM hawana imani nae au hawakubaliani na jinsi anavyo endesha mambo yake, inapofikia kwamba kiongozi wako anaonyesha kutokubaliana na wewe hadharani ina maana aliisha kaa na wewe pembeni akakushauri na hukusikiliza ushauri wake. Sitaki kuamini kwamba JK na PM waliamua kumkosoa hadharani bila kuwa waliisha kaa nae na kumpa muongozo wao, huenda anachofanya JPM sicho walichokubaliana kwenye baraza la mawaziri na vikao vyo vingine na hivyo wameamua kumtolea uvivu hadharani. Kama kweli JPM is the man of principle ilibidi awaachie wizara yao, ili asije akaongo wizara kinyume na kile anacho amini.
 

Hapana; mandate is more a political notion ya kile mtu anachotarajiwa kufanya na inakuwa na nguvu pale inapoanishwa. Ninapozungumzia madaraka ninazungumzia - nguvu zinazotokana na mamlaka ya cheo au ofisi fulani - powers that comes with the authority of a rank or authority. Kwa hiyo Waziri wa Miundo Mbinu - ni cheo - na kutoka hapo kinakuja na nguvu fulani (kama Waziri generally, na kama Waziri wa Miundo Mbinu specifically).
 
Ninacho zungumzia ni kwamba nje ya madaraka hajawahi kuwa mwanaharakati/mkereketwa katika kuonyesha kuisukuma serikali iendeshe mambo kulingana na sheria zake
 
Dr. Magufuli atakumbukwa kwa misimamo ya KIJINGA eti anasimamia SHERIA kwa kuwafanya watu wazidi kuwa mafukara...tayari zaidi ya nusu yetu tunatumia CHINI YA DOLA MOJA kwa siku.....anampango sasa tutumiae CHINI YA NUSU DOLA kwa siku....

Hapa sijakuelewa, unaweza kufafanua tafadhali.
 
Kwa maelezo uliyoyatoa,he will make a good president pindi tukishabadili katiba...Kwasababu ameonyesha sifa nzuri ya usimamiaji wa sheria,then tubadili katiba halafu kama atasimama kwa sera nzuri,then he will make a good contender for presidency.Good kwa maana ya good for the country.
 
mkuu mwanakijiji kuna maswali mazuri ya waberoya ambayo majibu yake yatakuwa elimu tosha na pengine mjadala kutoa changamoto zaidi.
 

Mimi mwenyewe namfagilia sana huyu jamaa aisee.....nilitamani sasa awe waziri mkuu ingekuwa powa sana inaonekana kazi zake mkuu mwenyewe anakubali na hafichi huyu jamaa......zaidi atarudi tu madarakani....ni mchapa kazi wa kweli....
 

MwanaKijiji,

Kwa hali ilivyo ya nchi yetu kama Rais, Waziri mkuu na wazari wa kawaida wanapisha wadhania kuwa ni kuwa magufuli hana uwezoooo? Just think wide to that matter,

Nchi viongozi kama rais anashindwa kuitetea katiba ya nchi JK kama yeye tu hana maaamuzi mazito at least kwa magufuli aamabaye anajitahidi kukaa kwenye sheria lakini serikali inazipindisha tena na kumwona magufuli ni mbaya kwanini ?? nikuwa nchi haina KATIBA imara na hakuna usimamizi makini wa sheria zilizopo na ndio kunakuwa na hali hiyo kama rais anafika anawaambia watendaji jamani angalieni na Utu khaaaa wakati walipokuwa wakifanya mipango mini hakujua hilo huyo rais?? mbona viongozi wengi wameji patia mali kiholela na hajasema hawaionei huru pesa ya walipa kodi??

JK anaendekeza siasa na anashindwa kukaaa kwa maneno yake ambayo anawaambia wapinzani ati tuachane na siasa tufanye kazi sasa hapo ndio anafanya nini kwa kuwa piga mkwara wizara ya miundombinu?? Hapo ni Rais JK na Pinda ndio hawna msimamo its simple calculation watanzania sio mazuzu please

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…