Magufuli ataiweza vita dhidi ya Karimjee Jivanjee Family?

Serikali haijasema kuwa haitanunua magari, bali watanunua kufustana na shughuli husika, mfano JPM ?kauliza mhandisi ana umuhimu wa kutumia v8
 
Kama hawatanunua mashangingi watanunua hardtop na rav 4 hapohapo Toyota Tanzania.
 
Kweli? Basi wewe ni kati ya wale walioburuzwa miaka nenda rudi huku wakishangilia na kushabikia tu bila kuuliza swali. Hivi uliposoma primary hukusikia methali iliyosema: "Mbio za sakafuni huishia ukingoni?" Ni nani muasisi wa uwozo wa nchi hii? Kama ni maraisi waliotangulia na familia zao unafikiri ni rahisi Magufuli kuwatumbua majipu kwa wepesi kama unavyofikiri? Majipu haya sii ya juujuu kama unavyodhani. Think twice! Magufuli anaweza kutumbukia kwenye shimo refu na akashindwa kabisa kutoka huko katika mbio hizi unazoshangilia. Fikiri! Uliza! changanua! Angalia kila fact na ujiridhishe kama mtu mzima!

Hakuna cha kuishia sakafuni,sehemu kubwa ya watanzania tunamuunga mkono,wewe tulia uone.Sasa ndio tumepata mtu anayejua kuyatumia mamlaka ya urais,haya tulikuwa tunayasikia kwa akina Kagame sasa tunajionea wenyewe,hii ndio namna ya kuongoza nchi iliyobobea kwenye ufisadi.Mafisadi wataisoma namba
 
urafiki wa JPM na mtu kama yule mzee aliyetufilisia shirika letu la ndege huwa inanifanya niamin dhamira ya JPM sio kututumikia sisi
 
Nilisikiliza Hotuba yake ya kufungua Bunge aisema kwamba pamoja na mambo mengine Serikali yake itaondoa matumizi ya magari ya kifahari maarufu kama, mashangingi", sasa hii ni kwamba ametangaza vita dhidi ya mabepari wakubwa nchi hii na hawa siyo wengine bali ni Karimjee Jivanjee Familiy ambao ndiyo wamiliki wa Toyota Tanzania ambao pia ni wauzaji wa Mashangingi yote serikalini na hawa jamaa wamekuwa na biashara ya uhakika tangu mwaka 1995, sasa Je, Magufuli wetu ataiweza hii familia ya Kipebari?

Na kama kweli amedhamiria kula nao sahani moja basi nashauri pia ajiimarishie ulinzi kwani na wao pia watakula naye sahani moja, hawa Karimjee Jivanjee family ni noma, wazungu walivyoondoka ndiyo waliowakabidhi nchi (kiuchumi) wako Afrika Mashariki yote!

Wananchi tuna nchi tuna Magufuli ninyi mko na mafisadi.

Aliondoka mkoloni atakuwa huyo mhindi!
 
mim mbna nimeagiza mwenyewe?kwan kuagiza gar ni kushindana na wakala?

Wewe utakuwa uliagiza gari iliyotumika, used car, sisi hapa tunazungumzia brand new cars, zero kilomita. Hata hiyo unaweza aagiza pia, ila hiyo kampuni watakaokuuzia ni lazima kwanza wainunue hiyo then iwe kwamba wanakuuzia iliyotumika hata kama ni zero kilomita. Soma vizuri sera za Toyota Japan
 
Mambo ya 10% ndo maana individual wanaweza agiza direct ila serikali hadi wakala, du!!!
Elewa basi. Hata wewe huwezi kuagiza gari jipya toka TOYOTA japan. Itabidi uliagize Toyota Tanzania. Kama serikali ina dalili mwingine hapo kati kama ilivyokuwa rada na ndge ya rais hapo 10% lazima. Fahamu tu kwamba ukiwa na mihela yako huwezi kuagiza toka Japan.
 
"Na kama kweli amedhamiria kula nao sahani moja basi nashauri pia ajiimarishie ulinzi kwani na wao pia watakula naye sahani moja, hawa Karimjee Jivanjee family ni noma, wazungu walivyoondoka ndiyo waliowakabidhi nchi (kiuchumi) wako Afrika Mashariki yote!"
Mwisho Wa kunukuu..


Watanzania tunajiita wasomi lkn baadhi yetu elimu zetu hazitusaidii. Mleta Uzi ameandika maneno hayo hapo juu. Ni ujuha na ujinga ndiyo vinamsumbua au amedhamiria makusudi kumdhalilisha Rais wetu.

Ubavu Wa kusema raia ATAKULA SAHANI MOJA na Muh. Rais Magufuli ameutoa wapi?

Mpumbavu sana wewe. Ili kuweka nidhamu mleta Uzi huu anafaa kufuatiliwa akamatwe na vyombo vya dola ili aeleze vizuri magabachori watakvyo kula sahani moja na rais. Anafaa kuswekwa ndani ili atambue mamlaka ya Rais ni yapi.

Umemdhalilisha Rais wetu

Lakini wewe huoni ni maoni yake? Au huoni anafikiri hivyo? Ulichoandika wewe ndio upuuzi mtupu maana hukuelewa kilichoandikwa maana pengine hujui kusoma vizuri.
 
Kwa kukusaidia tuu, last consignment ya magari ya serekali ni mashangingi 300, yamenunuliwa kwa bulk pocurement na GIPSA, na wameyanunua direct from kiwandani!, no middle men, no agent!. Wameyanunua kwa gharama ya half market price, na kumbe ukinunua more than 100 units, unasafirishiwa kwa half price na kushauriwa kufungua after sales service center yako!.

Pasco

Bila shaka report ya CAG umeiona ilichokisema kuhusiana na hao GPSA na uagizaji wa magari ya Toyota.

Naona kweli wameyaleta kwa half price kama ulivyosema mkuu,hahah.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom