Kikundi cha kijeshi cha Houthi cha Yemen kimetangaza Vita dhidi ya Israel na kufanya mashambulizi

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,056
8,710
Kikundi cha Houthi kutokea Yemen kimetangaza vita rasmi na Israel katika kuiunga mkono na kimefanya mashambulizi ya makombora ya masafa marefu na kurusha drones za mashambulizi kuelekea Israel kutokea Yemen.

Kikundi hiki kinashikilia maeneo kadhaa ya nchi ya Yemen na kimekua kwenye mapigano pia dhidi ya Saudia kwenye mgogoro wa vita wa Yemen na Saudia na pia mgogoro wa ndani wa Yemen yenyewe.

Tazama tamko la mmoja wa viongozi wa jeshi lao na tazama makombora na drones zilizorushwa umbali wa takaribani 1600km ili kuishambulia Israel.

Makombora hayo na mashambulizi hayo itabidi yasafiri anga ya Yemen na Saudia ili kufikia kupiga shabaha Israel. Kwa umbali wa makadirio ni kama kutoka Zanzibar mpaka Zambia ama Malawi.



Naiona hatari ya vita iliyoanzisha na Israel kusambaa Mashariki ya Kati nzima hivi punde kama Israel haitasitisha mashambulizi yake.

Kwa mashambulizi haya ya kikundi kidogo kama hiki ambacho kwa clip hii kinaonyesha kina uwezo mkubwa wa silaha za kivita kushinda HAMAS,kinaweza kuanza kushambulia meli za mafuta na kuhatarisha usalama wa biashara ya mafuta hali itakayopelekea dunia nzima mfumuko wa bei.

Pia kikundi kikuu hasimu cha Hizbullah dhidi Israel chenye asili ya Palestine lakini chenye makazi yake nchini Lebanon, kiongozi wao Mkuu yupo mbioni kutoa tamko rasmi siku ya tarehe 3,ambayo ni ijumaa, kikundi hiki nacho kinauwezo mkubwa wa kijeshi kushinda HAMAS,ieleweke HAMAS ni kama chama cha siasa ambacho chenyewe kina mlengo mkali kushinda PLO ya marehemu Yasser Arafat na wengi wa wanajeshi wao ni watoto wa marehemu ambao waliuliwa na Israel kwenye Vita vyao dhidi ya Palestine kugombea ardhi. Ni kama Leo hii watoto wanaobaki yatima kutokana na vita hii wanakuja kuunda umoja na kuuita jeshi!
 
Marekani ilipoanza kusogeza silaha hamkuelewa?
Mlidhani wanaenda kuwa waangalizi wa uchaguzi?

Waache Waarabu wote waingie vitani tu
 
Makundi ya meli kama hizi yapo yasiyopungua manne kwenye huo ukanda ili kuisaidia Israel, waarabu wataishia tu kubweka na kurusha hivyo vikombora ila hakuna mbwa atakayethubutu kuingia mzima mzima dhidi ya Israel.
1200px-US_Navy_031130-N-3653A-002_USS_George_Washington_(CVN_73)_Carrier_Strike_Group_formatio...jpg
 
Inakadiriwa Israel ana tactical nuclear weapons zisizopungua 80.

Sasa muarabu ajizime data akamguse Muisrael moja kwa moja wakati ela za mafuta ni tamu?
 
Mzayuni alivyohana ile yatumsifu yesu kristo wao nijino kwajino nakwambia kuna mtu atakula nuclear mchana kweupe
 
Back
Top Bottom