Magufuli akagua daraja la Kigamboni

Magufuli akagua daraja la Kigamboni

Camalillo

Member
Joined
Oct 12, 2013
Posts
90
Reaction score
83
Nimeshangaa hata kutoamini macho yangu kipindi tupo twasikiliza redio kutangazwa baraza la Mawaziri , Dr. Magufuli alikuwa hapa kwenye Ujenzi wa daraja la Kigamboni na tena akiwa peke yake kavaa casual alikuwa anadrive Gari lake mwenyewe. Watu wamecheka na kufurahi kwa vile kaondoka pale kwenda kukagua eneo lenye utata wa kupisha Ujenzi , inaonekana hata hajui kinachoendelea Ikulu!

Pata picha zake:
image-1.png

image_5.jpeg image_8.jpeg image_3.jpeg image_10.jpeg image_11.jpeg image_7.jpeg
Source: mimi mwenye, fundi mchundo darajani
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    71.4 KB · Views: 4,583
  • image.jpg
    image.jpg
    69.2 KB · Views: 4,576
  • image.jpg
    image.jpg
    92.9 KB · Views: 4,608
  • image.jpg
    image.jpg
    79.6 KB · Views: 1,262
  • image.jpg
    image.jpg
    55 KB · Views: 1,435
Kwa kweli nimeipenda hii. Kudrive gari lake mwenyewe, kuvalia casual, kukagua daraja wakati macho na masikio ya wote wakiwa Ikulu.

Huyu mtu anastahili kuwa sehemu fulani zaidi ya hapa. Pengine uwaziri mkuu unamfaa kabisa. Uchapa kazi wake ni wachache sana wanao, na wenye nao hawaishi Tanzania.
 
Afanye kazi kwa moyo nina hakika Watanzania
daima watakuwa nae pamoja muda wote.
Sio hao Mawaziri wavimba macho hakuna
wanalofanya zaidi ni kupeperusha bendera tu.
 
wakati wengine muda huo ndo walikuwa wanapigwa dose ya mwisho mwisho na sangoma,
wakati wengine wapo na vimada pale white sand,
wakati wengine wakiwa wanaangalia mahekaru yao,
wakati wengine wakiwa wanabeza report za kamati ya tokomeza ujangili,
Yeye jumapili hii siku ya mapumziko anawatumikia watanzania,
Hivi huyu hawezi kuingia na kuwatumikia watanzania pale ikulu?
naam majibu yapo kwetu watanzania!
uchaguzi wa mizigo au wawajibikaji ni juu yetu 2015,
 
I hope we see exactly what the portrait show! Usanii upo upo pia!
 
Alikuwa hana shida ya kujua kinachoendela Ikulu maana alisha tonywa na fast jet kwamba hahamishwi wala kutupwa kama Mulugo. Hivyo alionelea vema kwenda kukamilisha yale ambayo hakukamilisha wakati alipohitajika kuyakamilisha. Ni maoni yangu tu wanajamvi
 
wakati wengine muda huo ndo walikuwa wanapigwa dose ya mwisho mwisho na sangoma,
wakati wengine wapo na vimada pale white sand,
wakati wengine wakiwa wanaangalia mahekaru yao,
wakati wengine wakiwa wanabeza report za kamati ya tokomeza ujangili,
Yeye jumapili hii siku ya mapumziko anawatumikia watanzania,
Hivi huyu hawezi kuingia na kuwatumikia watanzania pale ikulu?
naam majibu yapo kwetu watanzania!
uchaguzi wa mizigo au wawajibikaji ni juu yetu 2015,[/QUOTE

Umesema vema mkuu,ila je CC na NEC watampitisha? kazi kuwa kwetu ni mpaka tuletewe labda awe
na uthubutu wa kugombea binafsi.
Hofu yangu kama huna hata harufu ya upanya,kupewa uongozi
kwenye kizazi cha panya ni ndoto.
 
Heko mwanafunzi wa babaangu rubabangwe primary
 
Hapo ni site ya ujenzi, mbona hajavaa PPE? Ni mfano gani kwa makandarasi kuhusu usalama kazini?
 
Back
Top Bottom