Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

Magufuli, acha kujitafutia sifa kwa mfumo huu

CCM ni moja, na CCM ni wamoja.........bahati mbaya ni kuwa watu ni wasahaulifu sana.
 
Katika hali ilivyo nchini ambayo kwa kila mwenye akili iliyo huru na salama anaiona,yale aliyoyazungumza Rais Magufuli jana ndio ukweli wenyewe.Ndio kilio cha watanzania wengi.Kwa kiwango kikubwa kuna wizi,uzembe na urasimu mno Serikalini lakini mamlaka husika walikua kimya.Magufuli kazungumzia HALI HALISI bila kujali nani kasababisha,na huo ndio UONGOZI.Hajadhalilisha mtu wala kiongozi bali ni wao wenyewe wanaodaiwa kudhalilishwa hawakuwajibika ipasavyo kwenye nafasi zao.
 
Mleta mada elewa kwamba mh. Rais alikuwa analihutubia bunge kwa kuelezea mwelekeo na vipa umbele vya serikali yake kwamba hatafanya kazi kwa mazoea , kwa kueleza kwa uchache gharama ambazo kama taifa zinaweza kuepukwa ! Nimemkubali Rajs wetu ana hofu ya Mungu. Hapa kazi tu
 
Kitendo cha Rais, Dr John Pombe Magufuli, kuwadhalilisha Dr Jakaya Mrisho Kitwete na marais wa zamani mnamo tarehe 20/11/2015 wakati alipokuwa analihutubia bunge hakikubaliki hata kidogo. Kutumia udhaifu wa viongozi hao, huku akiwashambulia wazi wazi, hasa Dr Kikwete, hakikubaliki katika jamii ya watu wastaarabu na ambao wamejijengea misingi ya kuheshimiana. Kumpalaza Dr Kikwete hadharani, hasa katika suala la safari zake zilizoligharimu taifa hili mabilioni ya shilingi, sio jambo jema na halijengi sura nzuri katika jamii ya watu wanaoheshimiana na kulindiana heshima.

Hata kama JK katika utawala wake alifanikiwa kutalii karibu dunia nzima huku akiandamana na misururu ya wapambe, mimi binafsi naona kwamba Rais huyu anafaa kuheshimiwa na kuachwa apumzike pasipo kumsukasuka kwa namna yoyote ile. Sikuona haja ya Dr Magufuli kuishambulia serikali ya Kikwete kwa udhaifu wake wakati naye alikuwemo humo humo kwenye serikali pasipo kutoa ushauri jinsi ya kuendesha serikali kwa ufanisi. Sasa ameona mzee wa watu amejistaafia na kwenda Msoga kulea wajukuu na kulima mananasi anaanza kumshambulia huku akijua kwamba hawezi kumjibu wala kujitetea.

Kama Dr Magufuli anadhani ataperform vizuri zaidi ya Kikwete basi afanye hivyo kwa vitendo pasipo kugandamizia chochote kutoka serikali iliyopita, anayoiona ni dhaifu, ijapokuwa naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaunda baraza la mawaziri la Kikwete. Sipendi kabisa tabia hii ya kujikweza na kujiona maarufu kwa kutumia udhaifu wa watu wengine. Nadhani sio mimi tu, hata wadau wengi humu jukwaani mnaniunga mkono katika hili.

Mungu nibariki mimi, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki dunia nzima.

:yield:

CC: FaizaFoxy Ritz thatha MwanaDiwani jingalao TataMadiba Lizaboni Simiyu Yetu Mingoi MAHAkama ya katiba T 2015 CCM mwa4

Ndio maana tunaichukia CCM kwa sababu ya watu kama nyie,kwa hiyo ulitaka aseme nyekundu ni nyeupe wakati tunaona na tunajua?
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli

Mkapa alipoingia hakumtukana mwinyi ..Pamoja na kuwa alikuwa namalalamiko yake ya kuachiwa Hali Mbaya...alifanya kazi ...

Kuna Kosa MOJA jk alifanya ni kuacha mkap adhaliloshwe na wapambe ...TOFAUTI NA SASA NI KUWA HAIKUFIKIA MAHALA JK ..ALIINUA MDOMO WAKE KUMTUKANA AU KUMDHALILISHA MKAPA ..NAKUMBUKA AKIWA SONGEA MAADHIMISHO YA CCM ALIOMBA TU HATA KINAFIKI WATU WAche kumdhihaki mkapa KWA kuwa kamuachia Nchi yenye pesa za kutosha na Ndege iko run way yeye atapaaa

ITS A MATTER OF TIME MAY BE KIKWETE IS PAYING THE PRICE WE DONT KNOW .....WOTE YEYE NA RAFIKI YAKE LOWASSA ..WAKO ON RETIREMENT BILA FURAHA ..
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi ashaisoma # tayari na bado?
Kama mlishazoea kupakana powder hiyo hakuna tena?
 
Katika hali ilivyo nchini ambayo kwa kila mwenye akili iliyo huru na salama anaiona,yale aliyoyazungumza Rais Magufuli jana ndio ukweli wenyewe.Ndio kilio cha watanzania wengi.Kwa kiwango kikubwa kuna wizi,uzembe na urasimu mno Serikalini lakini mamlaka husika walikua kimya.Magufuli kazungumzia HALI HALISI bila kujali nani kasababisha,na huo ndio UONGOZI.Hajadhalilisha mtu wala kiongozi bali ni wao wenyewe wanaodaiwa kudhalilishwa hawakuwajibika ipasavyo kwenye nafasi zao.

kwani yeye (magufuli) hakuwamo katika serikali hizo zilizowaibia na kuwadhurumu wananchi? yeye alifanya nini kurekebisha hali hiyo? toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utakiona kibanzi kwenye jijo la mwenzako.
 
JPM bado yuko kwenye kampeni akitafuta uungwaji mk?no na wananchi. Teh teh teh.
 
Tumezoa sana kuficha uozo na kumsifia mtu aklwapo huku pembeni tukilalamika. He put the point straight na nafikiri alipaswa kufanya hivyo. Taabu aliyoipata kwenye campaign hakuwa na it is black or white. Amesema wanayosema wananchi, wapinzani, wafadhiri, etc. tumuombee na kumsaidia lengo litimie! Kawa jasiri
 
Sasa kama mtu kafanya fyongo asiambiwe kisa kulinda heshima...

Ifike mahali wtz kama tunaona tabu kuacha unafki basi
tupunguze walau.
 
Magufuli hana hekima angejifunza kwa Lowassa pamoja na kushambuliwa hata na JK yeye hakumjibu. Hata hvyo malipo hapa hapa duniani na JK alimshambulia Lowassa kwa hiyo asikasirike.

Kweli mkuu atulie tuli km ananyolewa, rais wangu Lowassa kadhalilishwa sana aisee, na bado kitaeleweka tu kwa dua tunazoomba kwa alichofanyiwa lowasa
 
Safari za Rais bajet yake ipo Foreign Affairs!? Kwa hiyo JPM alimpiga JK za uso mbele ya Kadamnasi tena mbaya zaidi kwenye Hotuba ambayo dunia nzima ilikuwa inafuatilia. Nadhani JK inabidi achague na hafla ghani anatakiwa kuhudhuria akiwepo JPM. JK alivyo atamrudishia za uso kwenye vikao vya CC
 
Kamati zote za Wabunge huwa zinaenda nchi mbalimbali eti kujifunza wenzao wanafanya nini huko. Mambo waliyojifunza ni kuzomea na vijembe! Pesa zetu zinaliwa kama mchwa!
 
Mleta uzi ashaisoma # tayari na bado?
Kama mlishazoea kupakana powder hiyo hakuna tena?

mimi sijakataa suala la usomaji namba...kama ni kuisoma namba kila mtanzania anaisoma...ama uwe UKAWA, CCM au nyumbu! kama ni kufa kwa kukosa huduma bora za kijamii kama vile matibabu bora, nk, kila mtanzania anakufa pasipo kujali kabila, dini, rangi, chama au kitu chochote.

ninachokikataa mie ni kitendo cha magufuli kutafuta CHEAP POPULARITY kwa kuwachafua viongozi waliomtangulia. wewe unadhani kama mkapa asingesimama kidete kumzuia membe, leo hii magufuli angekuwa rais wa nchi hii? halafu anakuja kumdhalilisha mzee mkapa hadharani wakati yeye ndiye aliyemuokotea magufuli embe dodo chini ya mchongoma...hii ni sawa?

kwa staili hii sitashangaa kama magufuli atafufua upya skandali ya ununuzi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira....wewe unadhani akifufua skandali hii atakuwa namtendea haki mzee mkapa aliyemfikisha hapo alipo? think twice mkuu.
 
Wapi amemsema Kikwete,Magufuli alikuwa anazungumzia ngazi za chini sio ngazi ya uraisi

tulia juha wewe aliyezurura mara nyingi nje ya nchi zaid ya kikwete ni nani?
 
Back
Top Bottom