Maghorofa ya Magomeni Kota hayana Viwango?

Maghorofa ya Magomeni Kota hayana Viwango?

SOMA HII HAPA...

Kwanza hao wahusika wapo hapa after deal, kabla ya kuingia tunahakikisha kila kitu na kukiwepo na kasoro tunawapa taarifa waje kutatua ila wanakwambia "
hilo ni tatizo dogo ingia tutakuja kulifanyia kazi"

Haya kanzia floor ya kwanza kwenda juu madirisha yetu yalipaswa kuwekwa nondo au flat bar si kwa ajili ya urembo tu, bali usalama.

Kama ni mfuatiliaji wa taarifa ni kuwa kuna jirani yangu alidondoka kutoka floor ya juu kabisa mpaka chini na akaondoka duniani (kufa) na hata hapo kabla tuliliongelea hilo, but majibu ni "
hiyo haipo kwenye budget ya kazi ukiweza toa pesa tukuwekee"
Huko kuanguka kwa jirani yako kulisababishwa na ujenzi wa hayo majengo?
 
Angalia hii kitu hapa chini, hizi ni nyumba au magorofa yanayoitwa Magomeni Kota, humu ni sehemu ambayo nimekabidhiwa kuishi kama mmoja wa wanaostahili kuishi kutokana na kuwepo eneo hili baada ya vita ya Kagera.

Nilipita kuangalia kwa majirani wenzangu hali ni hiyo hiyo, baada ya kuuliza naambiwa baada ya yule baba kufariki basi ikawa ni mwendo kasi ili kukamilisha ujenzi.
View attachment 2309201
☝🏾Huo ni mlango haupo balance na mwenzake, yaani mtu ukiwa umefunga unaweza kupitisha mkono.

View attachment 2309207

☝🏾Sehemu ya ubao unaoshika ukuta, yaani hapo walishamaliza kazi na ndiyo maisha yanaeneelea hapa tunaishi.

View attachment 2309214
☝🏾Yaani hiyo ni sakafu, tayari kuna ufa soon naweza kumchungulia aliye floor ya chini akiwa kalala na family yake!.

Ukiondoa hayo, tulipewa miezi sita tutumie maji, umeme, ulinzi, watu wa usafi bure ili kupima matumizi yetu yatakuwaje ila sasa, kwa hali iliyopo maji yanazidi unga, soon tunafukuzwa humu. (JPM)
Mkuu kwan hawaja weka sakafu ya tiles ?
 
We nae huna shukrani Kwanza umepewa ukae bure alafu unajifanya mjuzi wa ujenzi
Jenga yako yenye viwango achana na vya bure
 
Akili ndogo hawawezi kukuelewa
SASA BROTHER, HIYO CRACK YA FLOOR TATIZO TANGIA MWANZO WA UJENZI NA SIO FINISHING?.
MAREHEMU ALIKUWA HAI KWENYE HIZO STAGE ZOTE ZA MWANZO KUANZIA STRUCTURE NAFIKIRI ALIONDOKA IKIWA IMEBAKIA SEHEMU NDOGO SANA.
HAYA NI MADHARA YA KUHARAKISHA MAMBO YA KITAALUM NA KUFORCE BUDGET NDOGO IFANYE KAZI.
 
Huku kwenye barabara hali ni mbaya sana
Anashangaa majengo yaliyojengwa awamu ya 5!

Shangaa pia barabara zilizojengwa awamu ya 5 zinavyoharibika mapema wakati kuna barabara zilijengwa awamu za nyuma bado ziko imara. Mfano barabara ya Chalinze - Morogoro ilijengwa awamu ya 3 lakini mpaka leo bado ni imara.
 
Magufuli aliwachukulia hatua gani wale waliojenga Magufuli Hostel?
Kawatafute watakuambia kuwa jpm ni shetani ...kisha watakuambia bora alivyo kufa ...kisha utawasikia wakikuambia kama unampenda kazikwe naye chato ...hapo ndiyo ujue kuna kitu mbaya aliwatenda wahuni wote wasiopenda uzalendo.
Ila kwenye swala la magufuli mimi naona bado alikuwa mpole sana alitakiwa kuwa mkali na mkatili ili nchi inyoooke ....WATANZANIA TINATAKA FULLCAPACITY DICTATOR MZALENDO
 
Sasa hivyo vitu si unarekebisha tu mwenyewe huko ndani?
Yaani vidogo hivyo mpaka ufanyiwe
 
Nahisi hata wote mliopewa hizo flati huko mna kadi za ccm...
Mbanane hukohuko, msituletee shombo hapa...
 
zile nyumba ukiziangalia ni special kwa watu wenye kazi na biashara zao,unalipia service charge unafanyiwa usafi na garden pia genereta ili kulifanya jengo kubaki na usafi wake muda wote,ila hao wakazi wa pale wengi wao ni waswahili sana
Wataondoka wenyewe..hawana uwezo wa kumaintain hali ya usafi na utilities zingine katika hizo kota..mbona wataziachia wenyewe..tangulini msawahili akaishi kwenye magorofa..soon watarudi mwanayamala ndio makazi yao yaliko wakacheze vigodoro.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizo lawama zishaanza naona kuna uzi wa kulalamikia kutozwa gharama za usafi na garden.
Hao watu wapuuzi sana wanafkiri bado maisha yatakua km wapo kota za zamani,
Hawachukui round hapo wasipobadilika
 
Tatizo unasoma huku unawaza utakula nini, ndiyo maana hujaelewa, -Pole.
Umelalamika kuwa hawajaweka nondo au flat bars ndipo ukaleta hiyo habari ya jirani kuanguka. Basi kama ni hivyo mtaanguka sana nyie watu.
 
Back
Top Bottom