Maghorofa Magomeni kumbukumbu inayoishi ya John Pombe Magufuli

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Nilikuwa nafuatilia runingani namna Rais Samia anavyowakabidhi majengo wale wananchi walioahidiwa kujengewa na hayati JPM. Alipoanza kuongea yule Bibi aliyekuwa ameongozana na Babu kama ndio wawakilishi wa wakazi 644 akawa mzalendo katika kutoa shukrani zake.

Kasimama mbele ya Rais SSH lakini akaanza kwanza kumshukuru JPM kwa maamuzi ya kizalendo ya kuamua kutumia kodi za wananchi kwa faida yao wenyewe ya kuwajengea majengo yatakayowasitiri wao na familia zao na yatakayokuwa ni sehemu ya mapambo ya kisasa ya jiji la Dar.

Kwamba Mungu amemchukua, ni maamuzi ya Mungu mwenyewe hakuna mwenye jeuri ya kuyapinga siku yake ikifika. Lakini kushukuru aliyekuwa na ujasiri wa kuyafanya ni deni ambalo bibi ameweza kulilipa vyema mbele ya Rais wa sasa.

JPM angeweza kutumia pesa iliyotumika katika kuhudumia anasa za tabaka la wenye vyeo, akaona hapana, ni lazima awajengee wakazi wa Magomeni makazi ya maana yatakayodumu kwa miaka mingi ijayo.

Angeweza kabisa kutumia pesa zilizotumika pale Magomeni katika kulipia safari za anasa za kwenda Dubai na kurudi kila mwisho wa wiki, angeweza kabisa kuzitumia zile pesa katika kuendeleza matanuzi yasiyodumu ya kibinadamu yanayofanywa kila siku na viongozi wengi wa kiafrika wa mataifa ya bara hili na hakuna mtu ambaye angeweza kumfanya lolote.

Kivitendo ilikuwa ni vigumu sana kwake kumtimizia kila aliyekuwa akimlilia njiani ili aweze kumtatulia shida zake mbalimbali, asingeweza kuwa na uwezo wa kufanya yote ya wasaidizi wake kwa wakati wote akiwa pale ikulu. Lakini hili la nyumba za kisasa kwa kaya 644 ni kielelezo au ni ishara ya utayari wake wa kuwasaidia wote wenye shida mbalimbali aliokuwa akikutana nao kila mara safarini.

Jukumu la kijasiri la kuyajenga makazi lilifanywa na JPM lakini jukumu la kuyatunza makazi hayo yasigeuke kuwa ni uchafu ulio karibu kabisa na katikati ya jiji, ni la wakazi wenyewe wa Magomeni wakiongozwa na yule Bibi aliyemshukuru hayati JPM mbele ya SSH.

Kimwili JPM alitutoka mwaka mmoja uliopita na siku chache. Lakini kila tutakapokuwa tukikatiza tukiwa ndani ya vyombo vya usafiri maeneo yale ya Magomeni tutakuwa tukimkumbuka hayati. Ataendelea kuishi kupitia ujasiri wa maamuzi ya kujenga makazi ambaye kila mtazamaji atakuwa akimkumbuka.

Alichokifanya JPM ni sawa na kile alichokifanya Hayati Karume kule Michenzani Unguja. Kwamba alikwisha kuondoka duniani tangu april 1972 lakini ushahidi wa upendo aliokuwa nao bado upo hai mpaka leo hii.

JPM alikuwa ni populist leader, na alitamka wazi bungeni siku ya kwanza kabisa alipohutubia. Kwamba anajivunia wingi wa wapiga kura waliompigia kura na atakuwa nao bega kwa bega. Ni maamuzi magumu sana kujenga majengo ya kisasa, kwani ni kama amekubali kuziba riziki nyingi za wasomi wenye kumsaidia kazi mbalimbali.

Ni kama alijua kuwa hana muda mrefu juu ya uso wa dunia, hivyo akaamua kuacha amejenga makazi kwa wakazi wa Magomeni. Ni maamuzi ya kizalendo ambayo siku zote hayawezi kukosa wa kuyapinga.

Ulale pema peponi JPM.
 
Hayo yapo kila awamu mkuu Retired

Mkapa - Kombe
JK - Ulimboka/Kubenea
Nyerere - Wahaini waliofungwa maisha.

Huwa hayaondoi mema yanayokuwa yakifanyika yenye lengo la kuyagusa maisha ya wengi.
As long as it involved killing of innocent human beings, then all ghorofas go into the trush

Ndiyo maana napinga wakatoliki eti Nyerere ni mtakatifu! Huwezi kuwa kiongozi wa serikali ukawa mtakatifu maana A government is an instrument of oppression!
 
As long as it involved killing of innocent human beings, then all ghorofa go into the trust. Ndiyo maana napinga wakatoliki ti Nyerere ni mtakatifu! Huwezi kuwa kiongozi wa serikali ukawa mtakatifu maana A government is an istrument of oppression!
Teacher naye nasikia alikuwa mtu wa hovyo sn
 
As long as it involved killing of innocent human beings, then all ghorofa go into the trust. Ndiyo maana napinga wakatoliki ti Nyerere ni mtakatifu! Huwezi kuwa kiongozi wa serikali ukawa mtakatifu maana A government is an istrument of oppression!
Utakatifu ni siri ya Mungu Mkuu Retired. Mtume Paulo alikuwa katili sana akiua wakristo kama ingekuwa leo ungemlinganisha na hawa viongozi wanaonyoshewa vidole.

Lakini ni mtakatifu na amehubiri sana injili ndani ya Biblia. Utakatifu haupimwi kwa akili zetu za kibinadamu zenye mipaka ya maoni.

Utakatifu unaweza kusababishwa na tendo moja tu zito sana likafuta madhambi yote ya miaka ya nyuma.
 
Magufuli alikuwa jembe

Uliza sasa unit costs ya hizo nyumba, linganisha na za NHC kwa walengwa wa market segment hiyo hiyo.

If anything aliesimamia hii project ndio alitakiwa kupelekwa NHC.

Unit zaidi ya 600 kwa mkupuo sio mchezo NHC miaka 20 awajajenga idadi ya nyumba hizo kwenye project zao zote ukijumlisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom