Maghorofa Magomeni kumbukumbu inayoishi ya John Pombe Magufuli

Nilikuwa nafuatilia runingani namna Rais Samia anavyowakabidhi majengo wale wananchi walioahidiwa kujengewa na hayati JPM. Alipoanza kuongea yule Bibi aliyekuwa ameongozana na Babu kama ndio wawakilishi wa wakazi 644 akawa mzalendo katika kutoa shukrani zake.

Kasimama mbele ya Rais SSH lakini akaanza kwanza kumshukuru JPM kwa maamuzi ya kizalendo ya kuamua kutumia kodi za wananchi kwa faida yao wenyewe ya kuwajengea majengo yatakayowasitiri wao na familia zao na yatakayokuwa ni sehemu ya mapambo ya kisasa ya jiji la Dar.

Kwamba Mungu amemchukua, ni maamuzi ya Mungu mwenyewe hakuna mwenye jeuri ya kuyapinga siku yake ikifika. Lakini kushukuru aliyekuwa na ujasiri wa kuyafanya ni deni ambalo bibi ameweza kulilipa vyema mbele ya Rais wa sasa.

JPM angeweza kutumia pesa iliyotumika katika kuhudumia anasa za tabaka la wenye vyeo, akaona hapana, ni lazima awajengee wakazi wa Magomeni makazi ya maana yatakayodumu kwa miaka mingi ijayo.

Angeweza kabisa kutumia pesa zilizotumika pale Magomeni katika kulipia safari za anasa za kwenda Dubai na kurudi kila mwisho wa wiki, angeweza kabisa kuzitumia zile pesa katika kuendeleza matanuzi yasiyodumu ya kibinadamu yanayofanywa kila siku na viongozi wengi wa kiafrika wa mataifa ya bara hili na hakuna mtu ambaye angeweza kumfanya lolote.

Kivitendo ilikuwa ni vigumu sana kwake kumtimizia kila aliyekuwa akimlilia njiani ili aweze kumtatulia shida zake mbalimbali, asingeweza kuwa na uwezo wa kufanya yote ya wasaidizi wake kwa wakati wote akiwa pale ikulu. Lakini hili la nyumba za kisasa kwa kaya 644 ni kielelezo au ni ishara ya utayari wake wa kuwasaidia wote wenye shida mbalimbali aliokuwa akikutana nao kila mara safarini.

Jukumu la kijasiri la kuyajenga makazi lilifanywa na JPM lakini jukumu la kuyatunza makazi hayo yasigeuke kuwa ni uchafu ulio karibu kabisa na katikati ya jiji, ni la wakazi wenyewe wa Magomeni wakiongozwa na yule Bibi aliyemshukuru hayati JPM mbele ya SSH.

Kimwili JPM alitutoka mwaka mmoja uliopita na siku chache. Lakini kila tutakapokuwa tukikatiza tukiwa ndani ya vyombo vya usafiri maeneo yale ya Magomeni tutakuwa tukimkumbuka hayati. Ataendelea kuishi kupitia ujasiri wa maamuzi ya kujenga makazi ambaye kila mtazamaji atakuwa akimkumbuka.

Alichokifanya JPM ni sawa na kile alichokifanya Hayati Karume kule Michenzani Unguja. Kwamba alikwisha kuondoka duniani tangu april 1972 lakini ushahidi wa upendo aliokuwa nao bado upo hai mpaka leo hii.

JPM alikuwa ni populist leader, na alitamka wazi bungeni siku ya kwanza kabisa alipohutubia. Kwamba anajivunia wingi wa wapiga kura waliompigia kura na atakuwa nao bega kwa bega. Ni maamuzi magumu sana kujenga majengo ya kisasa, kwani ni kama amekubali kuziba riziki nyingi za wasomi wenye kumsaidia kazi mbalimbali.

Ni kama alijua kuwa hana muda mrefu juu ya uso wa dunia, hivyo akaamua kuacha amejenga makazi kwa wakazi wa Magomeni. Ni maamuzi ya kizalendo ambayo siku zote hayawezi kukosa wa kuyapinga.

Ulale pema peponi JPM.
Pamoja na sifa hizo zote kwa mwendaze, mapungu yoyote ya kitaalamu ambayo yatajitokeza katika majengo haya itampasa pia abebe lawama. Utetezi wa uwepo wa "expansion joints" hatutataka kuusikia.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom