Ukiingia kwenye siasa, unatakiwa pia uangalie mlango wa kutokea siku ukipigwa chini, wanasiasa wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu katika hili, maana wamekuwa wakiamini ya kuwa, watakuwa kwenye madaraka siku zote, na hivyo kujisahau kutengeza njia ya maisha mapema, wahenga walisema, cheo ni dhamana na kwa mantiki hiyo unatakiwa ufahamu ya kuwa siku moja utarudi kule ulipokuwa mwanzo, na ndo kimefanyika katika serikali hii ya awamu ya tano, hasa kwa wakuu wa wilaya, ombi langu kwao, najua wengi walikuwa hawatarajii ya kuwa wataachwq nje ya mfumo, hivyo badi ni wakati mwafaka kwao kutimia kile walichopata kwa kipindi chote cha uongozi wao kujiendeleza ili kukidhi maisha ya hapo baadae
