VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Magesa Mulongo,aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mara ametokea mbali. Kabla ya kupelekwa Mara, Mulongo alikuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na hata Mwanza.
Kihistoria,Magesa Mulongo ametokea chini hasa kusikojulikana kama akina Waziri Simbachawene na Waziri Lukuvi. Ukada ukambeba. Ukampa vyeo. Ukampandisha hapa hadi pale. Sasa,ukada unamshusha.
Kwa kutenguliwa ukuu wake wa mkoa,Mulongo namfananisha na mpandamti upindao. Mti upindao,ukipandwa hupinda na kukurejesha chini tena kwa kasi isiyo hasi wala nafasi.
Hatahivyo,kote alikopita Magesa Mulongo alikuwa akisifiwa na kulalamikiwa. Kutenguliwa kwake,kwahiyo kutahuzunisha na kufurahisha. Ndiyo maisha ya siasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)