Magenge ya utapeli Tanzania: Tupe stori kama umekumbana na kadhia zao

Haya magenge huwa kati ya watu wawili mpaka watano
Viongozi wao huwa ni watu wenye elimu kubwa lakini hawana ajira na watumishi wa uma waliofutwa kazi kwa sababu mbalimbali
Wamo
Wanajeshi
Polisi
Wafamasia
Madaktari
Wanasheria
Walimu
Makarani nknk

Hawa wana makundi yao kulingana na fani zao lakini pia wamo mult purpose wanaocheza kote kote na nyanja zao ni
Ishu za madini
Ishu za ajira
Ishu za kupata nyaraka na vibali mbalimbali
Ishu za tenda na mikataba
Ishu za mashamba, viwanja na nyumba
Ishu za uwekezaji
Ishu za biashara mbalimbali
Masomo , ajira na biashara nje ya nchi

Ndani yao wana wataalam wa
Madini
Nyaraka
Lugha
Madawa
Fedha
Na kwenye idara zote za serikali wana watu wao kabisa ambao wako kwenye payroll yao
ni kweli kabisa..
 
Matapeli wakikuletea mchongo wanasisitiza uwe msiri kwakua wamekupa a lifetime opportunity so usitangaze tangaze.
Ha ha hapo ndo watu wanapopigwa, na huwezi kusema mpka upigwe.
 
Kuna jamaa alikuwa amepiga hatua sana kwenye biashara huko Mbeya, matapeli wakaanza kumchekecha zaidi ya miaka miwili.
Cha kwanza wakamuamisha Mbeya wakamleta Dsm, na biashara akabadili..
Wakaanza kumkopesha mzigo mpka wa mil 200,siku anakuja kupigwa aliliwa zaid ya mil 500..
Saiz hana kitu anapiga mpka mizinga ya buku 10. Ila huko Mbeya waswahili wanadai alikosea masharti wengine et mganga wake kafa.
 
Hajamchulia hatua yoyote wanadai wanaundugu nae mimi inanishangaza sana mtu haoni hata aibu kuwatapeli watu wa karibu hata kama ni familia rafiki na siyo undugu wa damu lakin yule jamaa ni mtu bure kabisa nilianza kumshtukia baada ya kula 200k ya dogo alaf akaanza kuomba na hela zingine zingine mara kwa Mara alimfanya dogo kama mradi wake
Utapeli wa kumuamini ndugu ni rahisi sana kwa mtu yeyote kutapeliwa.
Kuna story hata wazazi wanaweza mtapeli mtoto wao. Mtoto yupo Ulaya anatuma hela wazazi wamjengee lakini unakuta mdingi anazitumia hizo hela kwa mambo yake mengine.
Akirudi anakuta patupu labda tu tofali trip mbili zimewekwa kiwanjani.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Ushuhuda wangu kwenye utapeli,nilitapeliwa 4,500 TZS

Nakumbuka after chuo ile kuapply kazi , kuna post niliiona nikavutiwa kuapply, few days later nikaona email nimekua shortlisted for an interview na itafanyikia posta,i was excited ila nilishangaa hiyo interview eti itakua na part ya Refreshment yaani ni coffee sijui so tunatakiwa kutuma just 4,500/= kabla ya siku hiyo mmh nilisita ila home wakasema we tuma mbona ni kiasi kidogo tu basi nikatuma na nikaanza kujiandaa na nondo za interview 🤪 siku ikafika mapema nipo Posta nikakuta watu kibao nikiwauliza wanasema ni hiyo interview na wameshatuma hizo 4,500/= kama waliambiwa , basi tukaendelea kusubiri tunaona mda wa interview umefika ila ofisi hata haijafunguliwa wapo walinzi tu mmh, tukawauliza leo kuna interview hapa mbona kama hatuelewi eh walinzi wanashangaa na wanasema hawana taarifa yoyote kama kungekua na interview leo. Basi kuwapigia simu sasa hawapokei. Ndiyo tukajua tumetapeliwa. Nilimind kupotezewa muda na ila huruma wengine walikua wametoka mbali Bukoba, Mwanza huko nauli+accomodation ,dah fresh gradutes tunapitia magumu, na walipata pesa nyingi tu maana ni kiasi kidogo sawa ila kwa watu wengii😬

Now nimekua over conscious hata mtu aniambie lete buku tu tukusaidie nini nampiga mkwara namreport TCRA ni tapeli 😀😃
 
K
Utapeli wa kumuamini ndugu ni rahisi sana kwa mtu yeyote kutapeliwa.
Kuna story hata wazazi wanaweza mtapeli mtoto wao. Mtoto yupo Ulaya anatuma hela wazazi wamjengee lakini unakuta mdingi anazitumia hizo hela kwa mambo yake mengine.
Akirudi anakuta patupu labda tu tofali trip mbili zimewekwa kiwanjani.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kisa kama hicho kimetokea juzi Uganda. Jamaa alikua mission Sudani malakwamala anatuma pesa nyumbani ya ujenzi wa nyumbani, ikatokea akaumwa ghafla ikabidi wamrudishe nyumbani. Jamaa kufika nyumbani anakuta nyumba ileile ya miti, udongo na nyasi na wazazi hawana hata senti iliyobaki na wanachoongea hakifahamiki, siku iliyofuata jamaa walimkuta kajinyonga
 
Utapeli wa kumuamini ndugu ni rahisi sana kwa mtu yeyote kutapeliwa.
Kuna story hata wazazi wanaweza mtapeli mtoto wao. Mtoto yupo Ulaya anatuma hela wazazi wamjengee lakini unakuta mdingi anazitumia hizo hela kwa mambo yake mengine.
Akirudi anakuta patupu labda tu tofali trip mbili zimewekwa kiwanjani.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
unamtumia hela ya ujenzi na hela yake ya matumizi pemben ila wanaipiga yote unateseka huko ng'ambo ukirud unakuta kiwanja kimejaa majani na trip moja ya mawe yametawanyika kiwanja kizima ni bora u save pesa yako mwnyewe hata kweny accnt ukirud ndo uamshe mjengo wako
 
Kuna utapeli mwingine ni biashara ndani ya biashara..... Nakumbuka kwenye miaka ya 2012 mabango ya biashara kwenye nguzo za umeme yalijaa sana na ahadi ya mshahara wa 350k...basi rafiki yangu mmoja akanitafuta tuende maana kiukwel tulikua hatuna job kipindi hiko... Binafsi huwa naogopa sana kazi za kuitwa kwa matangazo ya wazwaz maana naamini zitakuwa na vikwazo vingi sana na applicants watakuwa wengi sana, ila kutokana na ushawishi wa rafiki yangu ilibidi niende(kwa sasa ni marehemu-RIP to him, alikua mpambanaji sana na kifo chake nafikir ni kwa sababu za kihpambanaji tu maana kilikua hakielewek mara baada ga kupata kaz nzuri)

So tulienda kufika pale tulikuta vijana wengi sana, wote walikua wanasubir kufanyiwa interview.Kulikua na watu zaid ya mia tatu(ilikua ni maeneo ya ilala)
Kama kawaida nikaanza kukusanya taarifa za kina kichwan mwangu kwa kuangalia mazingira jinsi yalivyo bila kuulizana na mtu...
Mazingira ni ya nyumba ya mtu, inawezekan walikodi nyumba yote, kulikuwa na masecretary wawili, chapchap kuangalia aina ya watu walioingia kwa usahili wengi ni wahitimu wa kidato cha nne, sita na baadhi vyuo hasa hivi vya kati...maana stori zilikua zikiendelea na hapo ndipo nilijua majority ni watu wa aina gani.

Ghafla tulitangaziwa kulipia form kiasi cha kama 3500tsh na tuliijaza pale chap maana hakuna aliyeitaji kuondoka kwa kushindwa kutoa kiasi hicho kidogo. Baada ya hapo tuliwekwa kwa namba ili tuweze Kuingia kufanyiwa usahili individually

Wengi waliingia na mm zamu yangu ilifika, kama kawaida niliendelea kupita huku nikicgunguza mazingira ya ile nyumba nikielekea chumba cha usahili, akilini nikiwa na kimuemue kuwa nitakutana na jopo limekaa, nilipoingia ndani nakutana na jamaa mmoja tu amekaa kwenye kiti na meza lake kubwaaaa mbele ana simu ya mezani anazuga kuongea na mtu, nilipokaa yeye ananioji maswali huku naendelea kumtafakari na kumchunguza

Muvi linaanza kwa kuthaminisha mavazi jamaa kavaa suti ya kuunga unga pale karume, suruali na koti haviendani chini ana kobaz zimeisha sio poa, tai kubwa kuliko muonekano wa mwili wake, yaani kifupi physical appearance yake iliniambia kuwa huyu mtu sio boss, ni mpigaji tu.
Basi baada ya kuhojiwa hojiwa akaniambia kuwa turudi kesho yake ashbui kwa ajili ya hatua ya pili ya usahili na vitu vingi kweli kweli
-barua ya utamvulisho wa mtaa
-uniform shati jeupe na suruali nyeusi
-passport kama sita
-barua ya mdhamini

Nk

Halafu wakatutoa pale saa tisa jioni, yan nilipotoka tuu jamaa yangu anankambia inabidi awai akakusanye hivo vigu ili awai kesho aubui, nikamwambia tu tumepigwa

Tumeagizwa vitu vingi ili tushindwe kwenye usahili ujao maana washakusanya zaid ya 500k kwa ada ya usahili, hawa ni matapeli tu
Baadae sikurudi na jamaa hakurud maana mpaka tunaondoka hatukujua kaz gani tutafanya japo tayar nilihisi ilikua ni kaz ya promotion kutembea na mabakuli.... Mjini shule yan majamaaa wanapiga hela kwa technique nyepec sana

So utapelu ni mwingi mjini hapa na makundi haya yamejizatiti,na yanawalengwa wake, kama hili linalenga sana watu wanaohitimu wanaokuja kitaa na moto wa kaz....
 
Ushuhuda wangu kwenye utapeli,nilitapeliwa 4,500 TZS

Nakumbuka after chuo ile kuapply kazi , kuna post niliiona nikavutiwa kuapply, few days later nikaona email nimekua shortlisted for an interview na itafanyikia posta,i was excited ila nilishangaa hiyo interview eti itakua na part ya Refreshment yaani ni coffee sijui so tunatakiwa kutuma just 4,500/= kabla ya siku hiyo mmh nilisita ila home wakasema we tuma mbona ni kiasi kidogo tu basi nikatuma na nikaanza kujiandaa na nondo za interview siku ikafika mapema nipo Posta nikakuta watu kibao nikiwauliza wanasema ni hiyo interview na wameshatuma hizo 4,500/= kama waliambiwa , basi tukaendelea kusubiri tunaona mda wa interview umefika ila ofisi hata haijafunguliwa wapo walinzi tu mmh, tukawauliza leo kuna interview hapa mbona kama hatuelewi eh walinzi wanashangaa na wanasema hawana taarifa yoyote kama kungekua na interview leo. Basi kuwapigia simu sasa hawapokei. Ndiyo tukajua tumetapeliwa. Nilimind kupotezewa muda na ila huruma wengine walikua wametoka mbali Bukoba, Mwanza huko nauli+accomodation ,dah fresh gradutes tunapitia magumu, na walipata pesa nyingi tu maana ni kiasi kidogo sawa ila kwa watu wengii

Now nimekua over conscious hata mtu aniambie lete buku tu tukusaidie nini nampiga mkwara namreport TCRA ni tapeli
We nishajua weakness yako

Lazima nikukule hela
 
Nimetapeliwa na likishoka la tanesco upande wa REA sina hamu kabisa limejifanya kwenda home kufanya survey kwa ajiri ya kuunganishiwa umeme likamukuta dogo niliyemuacha pale kulinda nyumba hayupo likaandika namba getini pale. Dogo kurudi kakuta namba ikabidi aitafute ndiyo likasema sisi tanesco tumepita hapo tunahitaji majina matatu na namba za mida chapu tufanye mchakato wa kulipia.
Dogo akaniunga na jamaa kilichonitokea basi tu.
 
Matapeli bana, eti anajifanya yeye ni kamishna wa polisi na ana siku chache sana kabla hajastaafu Ila serikali imempa mchongo mwingine wa yeye kuwa mkuu wa usalama katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta huko Tanga. So amepewa nafasi mbili za kutafuta madereva! Ili kuipata hiyo nafas akataka laki tatu na nusu Ila kwanza apewe laki, halafu nyingine itafuata. Basi bana tulikuwa Mimi na mwenzangu, jamaa yangu akanishawishi nikaingia king. Tukatoa laki laki! Baada ya hapo lile tapeli likawa linafos limaliziwe kiasi kilichobaki. Mmh nikaanza kupata wasiwasi, nilarudi nyuma! Mwenzangu akamalizia 250k iliyobaki. Mpaka Leo jamaa kapotea!
Dah huyo mzee noma
 
Ndama mutoto ya Ng'ombe, huyu jamaa alishawahi hadi kutengeneza wizara feki ya ardhi pale masaki ili kumuingiza kingi 'Ngo'mbe' kutoka uarabuni na akafanikiwa kumuuzia kiwanja hewa pale magomeni kotaz. Ana mizizi mirefu serikalini, Serikali ya Chuma ilitaka kumpoteza kabisa ila kaingia mama naona kaishamuachia huru.
Alimpa chuma 200milion akatoka kupitia utaratibu wa kinyang'anyi wa dpp usimsingizie bimdash
 
Ndama mutoto ya Ng'ombe, huyu jamaa alishawahi hadi kutengeneza wizara feki ya ardhi pale masaki ili kumuingiza kingi 'Ngo'mbe' kutoka uarabuni na akafanikiwa kumuuzia kiwanja hewa pale magomeni kotaz. Ana mizizi mirefu serikalini, Serikali ya Chuma ilitaka kumpoteza kabisa ila kaingia mama naona kaishamuachia huru.
Si ametoa mlungula yani awamu hii matapeli wote wanaachiwa
 
Back
Top Bottom