Magari Ya Umeme:ISRAEL YAANZA KUTUMIKA

Bubu Ataka Kusema Marafiki zangu watatu (wamenunua magari mapya hivi karibuni) walifanya utafiti wa magari haya kabla ya kuamua ama wanunue ya kutumia petroli au ya umeme na wote waliamua kununua ya petroli kwa kudai kwamba walikosa info zilizojitosheleza hivyo wakaamua kuyakwepa. Kama nilivyosema yanaingia taratibu ukilinganisha na ilivyotegemewa na hii bei ya petroli ilivyo juu labda wateja wengi wanaweza kuamua kuyanunua kwa wingi. Kikubwa ni bei ambayo unakuta unalipa hata $5,000 au zaidi kwa gari la umeme.


Ni pole pole hata huko kwetu yatafika na bei itashuka na Wabongo navyowajuwa si mda watakuwa nayo.

http://www.chevrolet.com/volt/?seo=...ase&utm_content=Search&utm_term=electric_cars
 
  • Gharama ya magari yanayotumia umeme bei yake ni mrara tatu au nne ya magari yanayotumie fuel. kwa Tanzania ni serikali tu na waneemeka wachache sana wanaweza kuyamudu.

  • Waafrika na watanzania tunapenda kuonekana tunaendesha migari mikubwa. Kwa kasumba ya viongozi wetu Sidhani kama kuna waziri yuko tayari kutumia gari linalotumia umeme lenye sura kama ya bito.
Kwetu wengi kuwa ndani ya gari kama VX ndo status. Sasa problem inakuja magari mengi ya umeme sababu ya energy efficiency ni madogo madogo sana. Sasa kama serikali yenyewe yeye uwezo wa kunnua magari mapya inaona hata waziri kutumia vitara ni kosa ndo ije kuwa gari la kutimia umeme linalofananaa na bito.

Hizi tutabaki tunasoma tu maana viongozi wetu ni waongeaji wazuri. Tooo much poltics hawaonyeshi mfano.......

Mkuu uankumbuka Computer in 1995 ilikuwa bei gani?
 
Mkuu uankumbuka Computer in 1995 ilikuwa bei gani?

kompyuta mwaka 1995 ilikuwa bei gari lakini serikali ilikuwa inanunua tena mpya.

Nachosema kwa sassa serikali yetu ambayo ina uwezo kama kweli ingekuwa na watu wasio na mawazo mgando wangekuwa nazo elctric car japo mjoja au mbili a majaribio.
 
mbona wachina walianza toka mwaka jana! niliyaona shanghai .. wanavituo maalum! .. ila talikuwa madogo yalikwenda kwa jina la SMART
 
Hii technolojia ni nzuri sana, itasaidia na petrol kushuka bei watu wakiamua kuhamia kwenye magari ya umeme

Hapa bongo bado tatizo litakuwepo, maana mgao wa umeme unaongeza makali kila siku. Utalaza gari njiani kla siku maana mgao wa masaa 18 ni issue!
 
Du Wajamani,

Magari ya umeme yapo siku nyingi kidogo na labda tu ungeliandika kuwa Waizrael nao wameanza kutengeneza na si kugundua.

Soma historia yake hapa: Electric car - Wikipedia, the free encyclopedia

Nchi zilizoendelea, wanatumia sana Umeme kwenye Matrain, trams, Metro na Mabasi ya umeme. Ni kitu kilekile ila sema kuwa kwenye gari, inabidi uwe na Mtungi wa kutunzia huo umeme (Batteries).

Hata Train za Tanzania zinazotumia Mafuta, zinatumia umeme yaani kile kichwa hakitengenezi Torque moja kwa moja kama kwenye gari. Kile kichwa ni GENERATOR la umeme. Ule umeme ukishazalishwa, ndiyo unakwenda kwenye MOTORS zilizopo kwenye matairi moja kwa moja na kuanza kuyazungusha. Ndiyo maana train za mafuta zilipofika, watu kudandia na kuruka waliumia sana au kufa maana hawakujua kuwa linachukua speed kubwa kwa muda mfupi sana.
 
Kwa umeme huu wa kupima na kibaba wa bongo wala sinunui hilo gari chaji ikiniishia njiani na tanesco wakawa wame-switch off itakuwaje?
 
LABDA TUOMBE CHAMA KIMOJAWAPO CHA SIASA (BE IT; CHADEMA,CCM,TLP,CUF,DP,UDP,UPDP,NCCR,SAU,PPT,NRA,UMD,NPF,MAREJESHO,NDUTA,JAHAZI,CHUDEWAMA,CHAUSTA,MAKINI,FORD,TADEA)
Ambacho kiamue kufanya majaribio,ya kununua.....NITAKIUNGA MKONO......KIHESABU KINA KURA YANGU MOJA ISIYO NA MASHAKA.....NA PIA ...KIWE NA SERA YA UPANDAJI MITI (sifa ya kujiunga na chama hiki cha siasa ni kupanda miti kwa kwenda mbele) NASEMA HIVIII NITASHIRIKIANA NAO BEGA KWA BEGA
 
Kwa umeme huu wa kupima na kibaba wa bongo wala sinunui hilo gari chaji ikiniishia njiani na tanesco wakawa wame-switch off itakuwaje?


Excuse kama hizi ni za kisiasa sababu na wala si sabau ya msingi kushindwa kununua. Sababu gari likishakuwa na chaji linatembea km nyingi kadhaa eg 100 Km . Sio kwamba linahitaji umeme muda wote.

Mbona magari ya fuel yanakwenda vijijini na kule hakuna vituo vya mafuta na yanarudi mjini.

Na hata ikitokea bahati mbaya likaishiwa charge basi mbinu utazotumia ni kama vile utayoshiwa mafuta porini. Utafayaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom