MAGARI YA UMEME: Fahamu Faida Zake, Aina na Namna Yanavyofanya Kazi

Kama yule mhindi wa Kenya amenunua Tesla model X kwa Kes 20 mill sawa na tz mill 420 sasa wadhani mtu wa kawaida ataiweza hiyo gharama?

 
hutaki kukaa kwa saa moja (dakika 60) kuchaji betri ya gari... Kwa madai ni upotevu wa your precious time.
Yaani nilifikiri utakuja na hoja za maana. Kukaa barazani nikaiga story huwezi kufananisha na kuwa nimetoka nataka niwahi kufika sehemu flani lakini gari ikahitaji chaji njiani.

Vipi simu yako nayo huwa unaichaji kwa muda gani? Vipi na hiyo siyo upotevu wa your precious time.
Kiukweli, hujui kulinganisha vitu. Simu na Gari? Mpaka unatumia gari basi ujue unauhitaji wa kutoka point A-B. Simu unaweza ukaitumia huku unachaji, gari utatembea na charging station?

Hata hizi electric vehicles kama ukitaka zitoe sauti kubwa hilo linawezekana sana tu mbona.
Unamaanisha u mimic sounds? :D Yaani nisikie sauti feki kwenye spika? Unataka niishi kwa kujidanganya?
 
Yaani nilifikiri utakuja na hoja za maana. Kukaa barazani nikaiga story huwezi kufananisha na kuwa nimetoka nataka niwahi kufika sehemu flani lakini gari ikahitaji chaji njiani...
vipi zile mashine za kusaga nafaka, je huwa zinatoa sound fake eeh?

Maana nazo zinatumia motor, kama vile tu ambavyo gari za umeme zinavyotumia motor.

Na motor inavyozunguka huwa inatoa sauti, hata kama sauti ni mdogo lakini ukweli unabaki pale pale kuwa inatoa sauti.

Na ukitaka sauti iwe kubwa inawezekana pia, kwani zile sauti za kwenye mashine ya kusaga nafaka vipi je zile nazo utaita ni sauti feki?

NB:
Kazi ya Motor ni kubadili nishati ya umeme (electrical energy) ili iwe nishati ya kimakenika (mechanical energy).

Mechanical Energy ndiyo inayofanya vitu vijongee.

Gari za Umeme pia nazo zinazo Motor.
Hivyo nimeweka mfano wa motor ya mashine kwa makusudi.
Hata Feni nazo ni motor, zipo Feni ambazo pia zinazotoa sauti kubwa na zingine zinatoa sauti ndogo.
Na Kitaalamu, ukitaka hiyo sauti iwe kubwa inawezekana mbona.

Hata gari zenye Combustion Engine za Diesel au Petrol, zipo zinazotoa sauti kubwa na zingine sauti ni mdogo sanaaaaa!

Gari za Petroli au Diesel nazo vile vile ukitaka sauti iwe kubwa au ndogo inawezekana pia.
 
Yaani nilifikiri utakuja na hoja za maana. Kukaa barazani nikaiga story huwezi kufananisha na kuwa nimetoka nataka niwahi kufika sehemu flani lakini gari ikahitaji chaji njiani...
the thing ni kwamba, tutake au tusitake... The electric vehicles are here to stay. Therefore, we should get prepared!

Kama unayo safari ndefu, nununua betri mbili zijaze zote chaji na zibebe kwenye gari.

Muda tunapoteza sana tu hata kwenye mambo mengine wala siyo kuchaji betri tu pekee. Mwanadamu hawezi kuwa na efficiency ya 100%.

Mpaka muda hizi electric vehicles ziwe ndiyo gari pekee duniani kote, hapo ni zaidi ya miaka 20 ijayo.
Muda huo teknolojia ya Betri nayo itakuwa imepiga hatua sana, hata kuchaji nayo itakuwa ni muda mchache ukilinganisha na sasa.. Pia muda huo inawezekana kwa single full charge gari likatembea mpaka Kilometers 500 au zaidi.

Kilometres hizo kwa safari za town humu ndani zinatosha sana!

Badala ya Petroleum Stations kutakuwa na Charging Stations.

Kama unapiga route ndefu, DSM to Arusha, Mwanza to DSM. Morogoro to Kigoma, Mbeya to Dodoma.
Kote huko mambo yatakuwa safi..

Maana gari ikiwa inatembea pia muda huo huo itakuwa inajichaji pia. Wanaweza kutengeneza onboard Dynamo itakayokuwa ina-supply power na kuchaji betri wakati gari likiwa linatembea.


Kama unapenda sauti ya gari, basi nishaelezea kuwa gari ya umeme lazma iwe na motor, motor ndiyo inayofanya gari lijongee.

ikiwa Motor ya mashine ya kusaga nafaka inatoa sauti, basi hata Motor ya gari la umeme nayo inaweza kutoa sauti kubwa. (na nieleweke hapo wala sijasema ni mimic sound au fake sound, na wala haitahitaji speaker)

Kingine ni kwamba, tusiishi kwa mazoea, tujiandae na ujio wa electric vehicles.
 
vipi zile mashine za kusaga nafaka, je huwa zinatoa sound fake eeh?

Maana nazo zinatumia motor, kama vile tu ambavyo gari za umeme zinavyotumia moto...
Usifananishe sauti ya combustion engine na sauti ya motor ya umeme.... Unaandika tu kwamba ilimradi umeandika. Unajua kwanini gari za umeme wanajitahidi kuzipa sound ya combustion engine kupitia speakers? Au ungewauliza Lexus LFA waliwahitaji Yamaha kufanya nini exactly kwenye V10 yao.

Unaandika maelezo marefu kutaka kutushawishi tusikilize sauti motor ya kupandishia maji ukiifaninishe na sauti ya miripuko ya engine.
 
Nissan leaf.... 0cc car, bei chee
Screenshot_20210307-194851.jpg
 
Teknolojia inayokuja barabara zitakuwa na umeme na gari itakuwa inacharge kwa wireless yaan mbele kuna virtual switch inafungua hivo umeme unaflow then nyuma kuna virtual switch ya kuuzima umeme ili usidhuru watumiaji wengine, bado haijaanza kutumika ila china wanaifanyia utafiti
 
Gari kama Prius nyingi sana zimefika mpk zaidi ya km 300,000 bila shida yoyote ile ya battery, lkn pia battery ikizingua unatumia mafuta kawaida tu maana engine yake ni ya kawaida tu1nz-fxe ingawa gari itakua weak kiaina.
Hybrid inafanyaje kaz?
 
Simaanishi hio system ilokuwemo kwenye hybrid, nazungumzia full electric car. Wakati maringi yanazunguka, kwanini mzunguko wa hayo maringi usitumike kuzalisha umeme na kurudisha chaji kwenye betri? Windmill inazunguka ndio inatowa umeme, Hydro Elctric Power turbines zinazunguka na kuzalisha umeme, vipi maringi ya gari yanazunguka lakini hayazalishi umeme?
Unataka lisiwe linaisha?? Hakuna free energy duniani...
 
Hybrid gari inakuwa na mifumo miwili, ya umeme na injini ya mafuta, kwenye mwendo mdogo gari inatumia umeme(batri) tu, kwenye mwendo mkubwa au betri ikiisha chaji injini inajiwasha kuendelea kuliendesha gari na pia kujaza chaji kwanye betrii. Hiki ndio kidogo ninachojua kuhusu magari ya hybrid kama toyota prius. Hii husaidia kwenye utumiaji wa mafuta kuwa mdogo kwa kilometa
 
Tafiti ndio hazija maliza, kwa sasa wanatumia lithium na wanaendelea kuproduce lithium batteries na kuharibu mazingira vile vile.

Kweli wanataka battery iwe future.

Kuna swali najiuliza, hivi gari za electric zinapotembea wakati yale maringi yanazunguka kwanini hayarudishi chaji kwenye battery?
Unawaza free energy 😁😁 assume unataka rudisha 1000w ..hivo kwenye matairi resistance itakuepo kubwa sana ili iweze suka 1000w sasa hapo kuna kutembea kweli
 
Say hio electric car ina motors za nyuma kupush gari. Wakati wa kuendeshe gari maringi ya mbele yanazungushwa kutokana na ile push ya maringi ya nyuma. Vipi maringi ya mbele hayatumiki kuzalisha umeme kutokana na huo mzunguko
Mbna haiitaji akili kubwa sana kujua haiwezekani!! Swali je unataka zizalishe umeme kiasi gani hizo dynamo ( motor) za mbele tuseme je unajua hata ukinyanyua gari juu hizo motor za nyuma mfano ziwe ni za 1hp hazizaweza zungusha motor ya 1.5hp ikiwa full loaded? Kama haziwezi how come unataka na gari litembee
 
Hybrid gari inakuwa na mifumo miwili, ya umeme na injini ya mafuta, kwenye mwendo mdogo gari inatumia umeme(batri) tu, kwenye mwendo mkubwa au betri ikiisha chaji injini inajiwasha kuendelea kuliendesha gari na pia kujaza chaji kwanye betrii. Hiki ndio kidogo ninachojua kuhusu magari ya hybrid kama toyota prius. Hii husaidia kwenye utumiaji wa mafuta kuwa mdogo kwa kilometa
Ushuru wake sunatisha Sana

Sent from my Nokia 5.3 using JamiiForums mobile app
 
Mbna haiitaji akili kubwa sana kujua haiwezekani!! Swali je unataka zizalishe umeme kiasi gani hizo dynamo ( motor) za mbele tuseme je unajua hata ukinyanyua gari juu hizo motor za nyuma mfano ziwe ni za 1hp hazizaweza zungusha motor ya 1.5hp ikiwa full loaded? Kama haziwezi how come unataka na gari litembee
Kwani Tesla roadster in HP ngap?
 
Back
Top Bottom