MAGARI YA UMEME: Fahamu Faida Zake, Aina na Namna Yanavyofanya Kazi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,798
EV-charging.jpg

Magari ya umeme ndiyo magari yanayotazamiwa kutumika zaidi siku za usoni. Serikali nyingi barani Ulaya zinaahidi kusaidia utengenezaji wa magari yenye kiwango cha chini cha uzalishaji wa hewa sumu, huku makampuni ya Mazda na Maserati yakiwa tayari yametengeneza au kuweka mipango ya kutengeneza magari ya umeme.

Suala la utengenezaji wa magari yatumiayo umeme si jipya kama inavyodhaniwa na wengi. Gari la kwanza la umeme lilitengenezwa mnamo 1837 huko Aberdeen, Uskochi. Teknolojia hiyo ilipata mafanikio kiasi ya kwamba teksi zilizotumia betri za umeme zilianza kutumika katika mitaa ya London na New York mwishoni mwa karne ya 19.

Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kuwa umaarufu wake haukudumu kwani bei ya mafuta ilipungua na hivyo kuyafanya magari ya petroli na dizeli kutawala barabara mpaka leo hii.

Sasa enzi mpya ya magari ya umeme imekuja. Pamoja na teknolojia kukua haraka, miundo inazidi kuvutia macho na ulimwengu unazidi kuwa na ufahamu zaidi wa mazingira.

Mnamo 2008 Tesla Roadster ilifikia kiwango cha kilomita 350 na kutoa msukumo kwa makampuni mengine ya utengenezaji wa magari kuingia katika soko hilo. Hivi sasa kampuni kama Volvo imetangaza kuwa kila gari wazalishalo kuanzia 2019 litatumia kabisa au litahusisha angalau mfumo kidogo wa kutumia umeme.

Hata hivyo ripoti zanadai kuwa mpaka kufikia mwaka 2035 magari yote mapya yatakayouzwa barani Ulaya yatakuwa yale yatumiayo umeme.

Je, magari ya umeme hufanya vipi kazi?
Badala ya tanki la mafuta, gari la umeme lina betri ya ndani ambayo huchajiwa kupitia usambazaji wa umeme na kisha huhifadhi na kutumia nguvu hiyo kuwezesha mota ya umeme na kusukuma magurudumu. Inamaanisha kuwa magari haya hayana haja ya clutch na mfumo wa gia au bomba la kutolea moshi, jambo linaloyafanya yawe yasiyotoa sauti kubwa kama yale ya mafuta. Waendeshaji wengi wa magari haya wanasema ni laini sana kuendesha.

Likiwa fully charged, gari la kawaida la umeme sasa linaweza kwenda zaidi ya kilomita 400 kabla ya kuhitaji kuchajiwa tena. Hiyo inaweza isiwe umbali unaopata kutoka kwenye magari ya petroli, lakini safari nyingi bado zinaweza kutekelezwa kwa urahisi kwenye gari la umeme.

Je, kuna faida gani za kutumia gari la umeme?
Kuna sababu nyingi kwanini mtu angetaka kuwa na gari la umeme. Moja ya sababu kubwa zaidi ni utunzaji wa mazingira. Magari haya yanazalisha kiasi kidogo cha hewa chafu na yana ufanisi zaidi kwani 95% ya nishati inayozalishwa hutumika katika mfumo wa kusukuma gari, wakati injini za mafuta zikiwa na ufanisi wa 30% tu -- nishati inayobaki inapotea kama joto au kelele.

Lakini kuna faida zingine pia. Kuna gharama za chini za uendeshaji kwani kuchaji betri hadi kujaa kabisa hutumia gharama za chini zaidi kulinganisha na kujaza tanki la petroli.

Kumbuka kuwa, ingawa kwa sasa ni gharama zaidi kununua gari la umeme kuliko gari la kawaida, kuna motisha na mipango maalumu ya serikali nyingi duniani iliyowekwa ili kukabiliana na hii.

Je, ni zipi aina tofauti za magari ya umeme?
Kwa ujumla kuna aina tatu za magari ambayo huchukuliwa kama 'ya umeme'.
  • Conventional Hybrids kama vile Toyota Prius ambayo yanahitaji tanki la petroli lakini pia ina mota ya umeme inayotumiwa na betri ambayo huchaji wakati gari linapofunga breki.
  • Plug-in Hybrids ambayo pia yana injini za petroli na mota za umeme lakini inaweza kuingizwa ili kuchaji na kwa ujumla inaweza kukimbia kwa muda mfupi kwa nguvu ya umeme kabla ya betri kuishiwa chaji.
  • Battery Electric Vehicles ndio huenda unafikiria zaidi unapofikiria magari ya umeme. Magari haya yanaendeshwa kwa umeme tu. Watengenezaji wengi wakubwa wa magari hutengeneza haya -- kuanzia Renault hadi wazalishaji wataalam wa magari ya umeme kama Tesla.
Je, unachaji vipi gari la umeme?
Tutachaji magari yetu kama vile tunachaji simu zetu kabla ya kwenda kulala ama wakati zinapoishiwa chaji, kwa kutumia soketi zile zile unazotumia kuwasha televisheni yako au mashine ya kunyolea.

Kasi ya kuchaji hutegemea aina ya gari ulilo nalo na aina ya usambazaji wa umeme ulioliunganisha nao.

Lakini, kawaida kuna aina tatu za kuchaji:
  • Kuchaji polepole (slow charging): hii inachukua kama masaa 5 mpaka kujaa kabisa.
  • Kuchaji haraka (fast charging): hii huchukua saa moja.
  • Kuchaji haraka zaidi (rapid charging): hii unaweza kuchaji gari lako kwa dakika 20 tu. Sehemu za huduma za kuchaji zinapatikana karibu na barabara kuu au kwenye vituo vya huduma za magari karibu na barabara.
Enzi mpya ya magari ya umeme
Ni wazi kwamba tunaingia kwenye enzi mpya ya magari ya umeme. Miundombinu ya huduma za magari haya zitakuwa zimeboreshwa sana katika miaka michache ijayo. Kuendesha gari la umeme itakuwa kawaida kwa wengi katika miaka ijayo na serikali na makampuni ya kuzalisha nishati yanaweka malengo makubwa kusaidia hilo kutekelezeka.
  • Nchini Ujerumani, serikali inaangalia uwezekano wa kuhama kabisa kutoka matumizi ya dizeli na petroli hadi umeme katika siku za usoni.
  • Ufaransa na Uingereza tayari wamepanga kupiga marufuku uuzaji wote wa magari ya petroli na dizeli ifikapo mwaka 2040.
  • Denmark sasa ina vituo vingi zaidi vya kuchaji magari ya umeme kuliko vituo vya mafuta.
  • Italia imesamehe wamiliki wa magari ya umeme ushuru wa kila mwaka na ushuru wa umiliki kwa miaka mitano tangu tarehe ya usajili wao wa kwanza.

Credits: E.ON
 
Hiyo hapo

Kaka hiyo gari bei ni nafuu Ila kununua Electric Vehicles iliyotembea 129443km ni janga kubwa. Kama hybrid car jamii ya kina Toyota Prius ukikuta ina high mileage Betri yake unakuta imezeeka kinachofata ni pesa kukutoka na kuwaneemesha mafundi.

Ni Bora Toyota GX100 ambayo itatembea mara 2 Kwa wiki , kuliko Nissan Leaf ambayo hutoenda sheli na kutembelea miezi michache kisha ukawa mteja wa kudumu wa Betri zake.
 
Hayo magari ya umeme hayana Raha yoyote.
Mkuu gari za injini (internal engine combustion) ya petrol/diesel zina utamu wake. Wakina Rudolf Diesel waliumiza vichwa hasa kutengeneza Diesel engines.

Hao wazungu wanapenda mazingira Ila wakisikia sound za V8/V10/V12 akili zinawahama.
Nakubali mkuu,ukiisikia kitu kama Lexus LFA iko inapiga mluzi ukija kulinganisha na Gari za umeme unaona ni bure kabisa.
 
Hili suala la ukitumia gari za umeme unaokoa mazingira nalo lina changamoto zake.

Battery za hizo gari zinatengenezwa kutokana na madini yanayochimbwa ardhini kama lithium,cobalt etc kwa hio hayo magari yakitengenezwa kwa mamilioni maana yake hapo kunaenda kufanyika uharibifu wa kufa mtu wa mazingira.
 
Kaka hiyo gari bei ni nafuu Ila kununua Electric Vehicles iliyotembea 129443km ni janga kubwa. Kama hybrid car jamii ya kina Toyota Prius ukikuta ina high mileage Betri yake unakuta imezeeka kinachofata ni pesa kukutoka na kuwaneemesha mafundi.

Ni Bora Toyota GX100 ambayo itatembea mara 2 Kwa wiki , kuliko Nissan Leaf ambayo hutoenda sheli na kutembelea miezi michache kisha ukawa mteja wa kudumu wa Betri zake.
Gari kama Prius nyingi sana zimefika mpk zaidi ya km 300,000 bila shida yoyote ile ya battery, lkn pia battery ikizingua unatumia mafuta kawaida tu maana engine yake ni ya kawaida tu1nz-fxe ingawa gari itakua weak kiaina.
 
Hayo magari ya umeme hayana Raha yoyote.

Mkuu gari za injini (internal engine combustion) ya petrol/diesel zina utamu wake. Wakina Rudolf Diesel waliumiza vichwa hasa kutengeneza Diesel engines.

Hao wazungu wanapenda mazingira Ila wakisikia sound za V8/V10/V12 akili zinawahama.
Umenikumbusha mbali sana.
Huwa nikimfikiria Rudolf nabaki namwacha kama alivyo.
129119197_369262647499577_2047263609240894221_n.jpg
 
Hili suala la ukitumia gari za umeme unaokoa mazingira nalo lina changamoto zake.

Battery za hizo gari zinatengenezwa kutokana na madini yanayochimbwa ardhini kama lithium,cobalt etc kwa hio hayo magari yakitengenezwa kwa mamilioni maana yake hapo kunaenda kufanyika uharibifu wa kufa mtu wa mazingira.
Umefikilia mbali

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha mbali sana.
Huwa nikimfikiria Rudolf nabaki namwacha kama alivyo.View attachment 1674324
Rudolf Diesel aliumiza Sana kichwa na matunda yake tutayafaidi hata gari za umeme zikipewa kipaumbele.

Hizo electric vehicle ni Kwa ajili ya town trip, uwezi ukawa na safari ya kutoka Mbeya-Mpanda-Kigoma au Moro-Ifakara- Malinyi hapo akili itakurudi na kukumbuka nishati ya mafuta
 
Kibongobongo hata town trip ni shida.

Hizo ni gari za ulaya wenye mtandao mpana wa charging stations.
 
Mazingira gani yanayotunzwa na magari ya umeme! Hio Lithium inapatikana vipi na huo umeme wa kuchajia izo betry unapatikana vipi! kuzidisha load tu kwenye grid.

Ili ujue kama umeendesha gari, usikie engine inavonguruma! other than that utakuwa unaendesha scooter ya maringi manne na cabin tu.
 
Mkuu upo dunia gani? Mbona sa izi kuna magari ukiwa ndani husii hata mlio wa gari
 
Dada yake Britney Spears, Jamie Lynn Spears anamlalamikia Elon Musk kwamba magari ya umeme ya Tesla yanaua paka wake, kwa sababu paka wanakuwa hawasikii gari linavyokuja.

Magari ya umeme hayana kelele kama magari ya mafuta.

Hiyo ni moja ya kasoro ya magari ya umeme.

Back
Top Bottom