TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

Marehemu apumzike kwa amani...
Lakini huyu makongoro alikuwa mtoto wa mjini haswaa!!! Linda bezdui jina lake analijua mwenyewe.,.....
Alijua anatoka na mtoto kigogo iseee kumbe kaangua pua na uzuri wote ule
Alipata Heshima zote Kama Mtoto wa Nyerere lakini. Alisomeshwa USA na alikuwa afanye Kazi World Bank ila sikumbuki nini kilimsibu.
Mimi nilimuona miaka ya 90 mwanzonj, alikuwa ni Mbabe sana hapo Interchick na BANDAG.
 
Kwa hiyo alikua anadanga!?..hebu nimuone alivyo mzuri!!
Humjui Linda??? Fanya ku search habari
zake!!!
Alikuwa mdada wa mjini enzi hizo na alikuwa akimiliki salon ambayo ilikuwa hot pia wasanii hasa wa nje walitumia salon yake kufanya make up! Kwa sasa Yuko marekani akifanya tailoring.
 
Hilo nalijua,,,
though mimi si wa umri huo nakumbuka walikuwa wakija na makongoro mtoto wa Nyerere nyumbani kwetu kwa mama yangu mdogo ambae alikuwa anatoka na makongoro halisi na Linda alikuwa rafiki yake .
Maisha yanaenda Kasi hao wazee nimekula sana biscuits zao.
 
Marehemu apumzike kwa amani...
Lakini huyu makongoro alikuwa mtoto wa mjini haswaa!!! Linda bezdui jina lake analijua mwenyewe.,.....
Alijua anatoka na mtoto kigogo iseee kumbe kaangua pua na uzuri wote ule
Wewe hujielewi, aliangukia pua vipi wakati mtu mambo safi ana nyumba Bahari Beach, anaishi Mikocheni,, anakwenda mamtoni anavyotaka, anafanyakazi na wazungu unadhani hata watoto wa kuwazaa Nyerere mwenyewe wanamfikia huyu marehemu?

Sasa angetoka na mtoto wa Nyerere Andrew Nyerere si angeambulia vitabu tu?

Ujinga wa mademu wa Kibongo ni kubabaika na majina, mbona huyo mtoto wake Linda hakumpa ubini wa marehemu?
 
Hata sisi tunafiwa pia.

Na hatuleti misiba mitandaoni.

Matatizo yenu na watu wenu wa karibu, msifikiri matatozo hayo ninya kila mtu.

Mnapopata misiba, siyo kwamba inamhusu kila mtu.
Kuna wengine wanamjua na kupitia uzi huu wamepata taarifa za msiba huo, siyo vibaya kutoa taarifa. Kama wewe humjui usingeangaika kuufungua uzi wenyewe. Siyo taarifa zote zinawahusu watu wote.
 
Kwa hiyo alikua anadanga!?..hebu nimuone alivyo mzuri!!
Hapa ndio amezeeka sasa hivi ana 50 plus.
FB_IMG_1747914028303.jpg
FB_IMG_1747914126698.jpg
FB_IMG_1747914028303.jpg
FB_IMG_1747914126698.jpg
FB_IMG_1747914188941.jpg
FB_IMG_1747914188941.jpg
 
Wewe hujielewi, aliangukia pua vipi wakati mtu mambo safi ana nyumba Bahari Beach, anaishi Mikocheni,, anakwenda mamtoni anavyotaka, anafanyakazi na wazungu unadhani hata watoto wa kuwazaa Nyerere mwenyewe wanamfikia huyu marehemu?

Sasa angetoka na mtoto wa Nyerere Andrew Nyerere si angeambulia vitabu tu?

Ujinga wa mademu wa Kibongo ni kubabaika na majina, mbona huyo mtoto wake Linda hakumpa ubini wa marehemu?
Aisee!! Mie sijielewi kweli......
Mabishano hayana nafasi kwangu kuanzia kwenye maisha halisi mpaka mitandaoni.
Pumua kidogo kapate lunch.
 
MAGAMBO MAKONGORO AMEFARIKI DUNIA

Kwa wanaomfahamu Magambo Makongoro amefariki leo hospitali ya muhimbili, maziko kesho Kisutu Alasiri.

Msiba upo nyumbani kwake Msasani opp na nyumba ya Mzee Rais Mwinyi Mikocheni.
Nimepokea taarifa hiyo hapo juu hivi punde.

Magambo tunajuana toka udogo wetu ni mtoto wa Chief Makongoro.

Tulipokuwa shule tukifanya picnic yeye akitupeleka Kigamboni nyumba ya mapumziko iliyokuwa ya Gavana wakati wa ukoloni na kwa wakati ule baada ya uhuru ikawa iko chini ya Mwalimu Nyerere kama Rais wa Tanzania.

Mwalimu alikuwa haitumii nyumba hii na Magambo yeye kwa ule usuhuba uliokuwa baina ya baba yake na Nyerere alikuwa mtoto wa nyumbani State House.

Nakumbuka siku zile hata jina hili la Ikulu lilikuwa bado.

Magambo alikuwa mwenzetu na mchezo wetu ulikuwa mmoja pamoja na Kleist na mdogo wake Ebby, Yusuf Zialor, Wendo Mwapachu, Bubby Bokhari, Christopher Faraj, Abdallah Mohamed Saleh (Tambaza), Abdul Mtemvu, Edward Makwaia (sasa Chief wa Siha), Abdallah Mgambo, Eyshe na Mariam Max, Erica Kisa, Janet Zebedayo, Haitham Rashid, Esther Mzena wenzetu wengine wengi siwakumbuki.

Wenyewe tukijiita Scorpions na wengi tulikuwa wanafunzi St. Joseph's Convent.
Baadhi wemetangulia mbele ya haki.

Miaka ya kati Magambo alikuwa akifanya kazi Inter King iko Mbezi wanafuga kuku.

Mara ya mwisho miaka michache nyuma mwezi wa Ramadhani tulikutana Masjid Ngazija alikuwa na Abraham Sykes.

Nakumbuka siku ile walinishambulia sana kwa kunichangia ati mie najidai sana na Msikiti Ngazija nauona kama mali yangu nikiwaona wao wanakuja kusali pale roho inaniuma.

Haya ndiyo yalikuwa mapenzi yetu tulikutana lazima tubwatizane huku tunacheka.
Nilipoteana na Magambo kwa muda hatujaonana.

Allah amsamehe na amtie Firdaus.
Amin.

View attachment 3339866
Magambo Makongoro
siku nyingine muwe mnatufahamisha wakiwa hai cyo tu wakiwa wafu
 
Aisee!! Mie sijielewi kweli......
Mabishano hayana nafasi kwangu kuanzia kwenye maisha halisi mpaka mitandaoni.
Pumua kidogo kapate lunch.
Lunch gani? Unajuwa niko wapi? Kwanza kwa saa za Tanzania huu siyo muda wa lunch hata restaurant zinafungwa wanaandaa dinner.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Humjui Linda??? Fanya ku search habari
zake!!!
Alikuwa mdada wa mjini enzi hizo na alikuwa akimiliki salon ambayo ilikuwa hot pia wasanii hasa wa nje walitumia salon yake kufanya make up! Kwa sasa Yuko marekani akifanya tailoring.
Simjui,mi mjini mshamba,nilikuja 2000
 
Huko mara mbona uislam upo kitambo tu,angalia machifu walivyokua wakivaa,wakamuathiri hadi mkono kuvaa tunga, pitia kitabu cha Thomas molony,nyerere the early days
Zanaki hakuna Uislamu, labda huko Ikizu kwa kina Magambo Makongoro.

Ile kofia ya Nimrod Mkono ni tarabushi siyo vazi la kiislamu.

Vazi la heshima la Wahaya ni kanzu nyeupe na koti, kuna vitu tunachanganya.
 
Ni mavazi ya waislam,na buganda empire ilikua dola ya kiislam mahakama zikitumia sharia,we unadhani mavazi ya waarabu yatafika tu Mara,kagera bila dini ya mwarabu!?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hilo nalijua,,,
though mimi si wa umri huo nakumbuka walikuwa wakija na makongoro mtoto wa Nyerere nyumbani kwetu kwa mama yangu mdogo ambae alikuwa anatoka na makongoro halisi na Linda alikuwa rafiki yake .
Maisha yanaenda Kasi hao wazee nimekula sana biscuits zao.
Kumbe wewe ulimfahamu kwa ukaribu zaidi hadi kula Biscuits. Mimi nilimfahamu Kama Mkurugenzi. Alikuwa anatisha na Mbabe kwelikweli. Tulimuogopa mno.
Ila sema alikuwa hata hana muda na Sisi watu wa Chini na hivyo hata hakunifahamu. Ila walifahamiana na ndugu yangu kwani ilibidi amuone ili baadhi ya mipango yake yafanikiwe.

Nilivyomfahamu na nikiona hiyo Picha nabaki kusema Ujana ni Maji ya Moto.
Ujana wote kwisha....

RIP Mkurugenzi.
 
inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Nimesoma mama mtoto wake akimuombolezea. Mwenyeze Mungu awape subra familia na wote walioguswa na msiba huu
Screenshot_20250522_152100_Instagram.jpg
Screenshot_20250522_152145_Instagram.jpg
Screenshot_20250522_152216_Instagram.jpg
Screenshot_20250522_152256_Instagram.jpg

Ni jambo jema sana kukumbukwa kwa wema haswa na mzazi mwenza
 
Kumbe wewe ulimfahamu kwa ukaribu zaidi hadi kula Biscuits. Mimi nilimfahamu Kama Mkurugenzi. Alikuwa anatisha na Mbabe kwelikweli. Tulimuogopa mno.
Ila sema alikuwa hata hana muda na Sisi watu wa Chini na hivyo hata hakunifahamu. Ila walifahamiana na ndugu yangu kwani ilibidi amuone ili baadhi ya mipango yake yafanikiwe.

Nilivyomfahamu na nikiona hiyo Picha nabaki kusema Ujana ni Maji ya Moto.
Ujana wote kwisha....

RIP Mkurugenzi.
Ningeweza kuandika lakini kwa heshima a mamdogo nikae kimya..
Kwa u babe ilikuwa ni zaidi ya hapo na Kuna baadhi ya viongozi walisoma namba ile kauli unajua mi nani haijaanza leo.
Ni kweli Kuna vitu nimefaidi zaidi ya biscuits nadhani unajua kama watoto wa viongozi huwa wana package zao.
Miaka kadhaa alikosa ile hadhi ya vip sijui kilitokea nini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom