TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

Ningeweza kuandika lakini kwa heshima a mamdogo nikae kimya..
Kwa u babe ilikuwa ni zaidi ya hapo na Kuna baadhi ya viongozi walisoma namba ile kauli unajua mi nani haijaanza leo.
Ni kweli Kuna vitu nimefaidi zaidi ya biscuits nadhani unajua kama watoto wa viongozi huwa wana package zao.
Miaka kadhaa alikosa ile hadhi ya vip sijui kilitokea nini.
Ya ndani usiandike. Haitakuwa vizuri. Ila yale yalifanyika Public hayo waweza kutumegea 😀😀
 
Hata sisi tunafiwa pia.

Na hatuleti misiba mitandaoni.

Matatizo yenu na watu wenu wa karibu, msifikiri ni matatizo hayo ni ya kila mtu.

Mnapopata misiba, siyo kwamba inamhusu kila mtu.
Boss, JF ni social media ya kupashana habari pia kama vile instagram, FB, Twitter....don't take it personal....!
 
MAGAMBO MAKONGORO AMEFARIKI DUNIA

Kwa wanaomfahamu Magambo Makongoro amefariki leo hospitali ya muhimbili, maziko kesho Kisutu Alasiri.

Msiba upo nyumbani kwake Msasani opp na nyumba ya Mzee Rais Mwinyi Mikocheni.
Nimepokea taarifa hiyo hapo juu hivi punde.

Magambo tunajuana toka udogo wetu ni mtoto wa Chief Makongoro.

Tulipokuwa shule tukifanya picnic yeye akitupeleka Kigamboni nyumba ya mapumziko iliyokuwa ya Gavana wakati wa ukoloni na kwa wakati ule baada ya uhuru ikawa iko chini ya Mwalimu Nyerere kama Rais wa Tanzania.

Mwalimu alikuwa haitumii nyumba hii na Magambo yeye kwa ule usuhuba uliokuwa baina ya baba yake na Nyerere alikuwa mtoto wa nyumbani State House.

Nakumbuka siku zile hata jina hili la Ikulu lilikuwa bado.

Magambo alikuwa mwenzetu na mchezo wetu ulikuwa mmoja pamoja na Kleist na mdogo wake Ebby, Yusuf Zialor, Wendo Mwapachu, Bubby Bokhari, Christopher Faraj, Abdallah Mohamed Saleh (Tambaza), Abdul Mtemvu, Edward Makwaia (sasa Chief wa Siha), Abdallah Mgambo, Eyshe na Mariam Max, Erica Kisa, Janet Zebedayo, Haitham Rashid, Esther Mzena wenzetu wengine wengi siwakumbuki.

Wenyewe tukijiita Scorpions na wengi tulikuwa wanafunzi St. Joseph's Convent.
Baadhi wemetangulia mbele ya haki.

Miaka ya kati Magambo alikuwa akifanya kazi Inter King iko Mbezi wanafuga kuku.

Mara ya mwisho miaka michache nyuma mwezi wa Ramadhani tulikutana Masjid Ngazija alikuwa na Abraham Sykes.

Nakumbuka siku ile walinishambulia sana kwa kunichangia ati mie najidai sana na Msikiti Ngazija nauona kama mali yangu nikiwaona wao wanakuja kusali pale roho inaniuma.

Haya ndiyo yalikuwa mapenzi yetu tulikutana lazima tubwatizane huku tunacheka.
Nilipoteana na Magambo kwa muda hatujaonana.

Allah amsamehe na amtie Firdaus.
Amin.

View attachment 3339866
Magambo Makongoro
Pole mzee wangu kwa msiba wa swahiba wako....Allah amlipe Firdaus.

Nimesikia pahala leo hii, kumbe ni ndugu na mzee Isa Makongoro alikuwa katika viongozi wa Yanga miaka ya nyuma...nimeweza ku relate.
 
Kumbe alipata Stroke?
Magonjwa ya Moyo yanauwa sana Watu kwa sasa. Tupime afya zetu hasa Pressure na kuangalia Mafuta kwenye damu yaani Cholesterol. Hii kitu inaondoa sana watu Duniani kwa sasa hasa Sisi Weusi.
Nilikuwa naambiwa Makongoro ana Mke Mrembo sana, kweli nimekubali.

inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Nimesoma mama mtoto wake akimuombolezea. Mwenyeze Mungu awape subra familia na wote walioguswa na msiba huu
View attachment 3342049View attachment 3342050View attachment 3342051View attachment 3342052

Ni jambo jema sana kukumbukwa kwa wema haswa na mzazi mwenza
 
Alipata Heshima zote Kama Mtoto wa Nyerere lakini. Alisomeshwa USA na alikuwa afanye Kazi World Bank ila sikumbuki nini kilimsibu.
Mimi nilimuona miaka ya 90 mwanzonj, alikuwa ni Mbabe sana hapo Interchick na BANDAG.
Baba yake (au babu yake?) Magambo, Chifu Makongoro, ndiye mtu aliyemuambia baba yake Julius Nyerere, Chifu Nyerere Burito, kwamba huyu mtoto (Kambarage Nyerere) ana akili sana, anafaa kupelekwa shule.

Yule Chifu Makongoro alipokuwa anamtembelea Chifu Nyerere Burito (baba yake Kambarage Nyerere), alikuwa anapata nafasi ya kucheza bao na mtoto wa rafiki yake na Chifu mwenzake, mtoto mwenyewe ndiye Kambarage Nyerere. Chifu Makongoro akaona kuwa huyu mtoto Kambarage anajua sana kucheza bao, anamshinda hata yeye mtu mzima. Chifu Makongoro akamwambia rafiki yake Chifu Nyerere Burito ampeleke huyu mtoto kusoma shule, kwa sababu anaonekana ana akili sana.

Chifu Burito Nyerere kwanza alisita, lakini kaka yake Nyerere aliyeitwa Edward Wanzagi (aliyekuja kuwa Chifu Wanzagi baada ya Chief Burito kufariki) naye pia akamsisitiza Chifu Nyerere Burito (baba yake Edward Wanzagi na Kambarage Nyerere) amuandikishe kuanza shule Kambarage Nyerere. Edward Wanzagi alimpenda sana mdogo wake Kambarage Nyerere.

Hiyo ndiyo historia ya Julius Kambarage Nyerere kuandikishwa shule. Chifu Makongoro alikuwa mtu aliyemshawishi baba yake Kambarage Nyerere ampeleke shule huyu Kambarage Nyerere aliyekuja kuwa rais wa Tanganyika na Tanzania.

Kwa hiyo, utaona familia ya Makongoro imekuwa na ukaribu sana na familia ya Nyerere tangu enzi za wazee walivyokuwa machifu huko.

Na kwa heshima ya Chifu Makongoro, Julius Kambarage Nyerere alimuita mmoja wa watoto wake jina hilo la Makongoro, Charles Makongoro Nyerere. Baba (babu?) yake Magambo Makongoro ndiyo chanzo cha jina la Charles Makongoro Nyerere, aka "kaka Mako".

Kwa historia zaidi ya uhusiano huu wa familia za Nyerere na Makongoro soma "Nyerere: The Early Years" cha Profesa Timothy Molony (Edinburgh University).

Poppy Hatonn
 
Bado hujajibu swali langu, umeongelea dhana tu, hapo Ikizu na Zanaki hakukuwa na Uislamu kabisa, kuna watu wa asili sijui ndio mnawaita wapagani na Wakristo, makao makuu ya Wasabato Tanzania yalijengwa Zanaki pale Busegwe kwa kina Nimrod Mkono.

Hapa nieleweke sina interest na dini yoyote, lakini najaribu kutafiti huyu marehemu chimbuko la uislamu wake, nataka kujuwa tu maanda yule Linda aliyezaa naye najuwa alikuwa mkristo akasilimu sasa ni mwislamu.
Huyo jamaa actually sijawahi kumsikia kabla ya uzi huu,,ila Nina uhakika ukoo wa makwaia kina kidaha waliokuwa ni waislamu,sema baadae waingereza walikua wanamuundaa kidaha kuwa kiongozi wa nchi,wakambatiza na kumwita David kidaha makwaia Kama sikosei,
So nahisi hata chief makongoro alikuwa ukoo wa makwaia
 
Ila mpaka leo watoto, wajukuu za nyerere huwa siwaelewielewi 😄

Ova
 
Kama umefiwa na unataka msiba wako ujulikane, na wewe una haki ya kuleta uzi wa nsiba wako mtandaoni.

Kwa nini unaona vibaya watu wakiomboleza misiba ya watu wanaowajua hapa JF?
Kwasababu huzuni zao siyo huzuni za kila mtu.
 
Huyo jamaa actually sijawahi kumsikia kabla ya uzi huu,,ila Nina uhakika ukoo wa makwaia kina kidaha waliokuwa ni waislamu,sema baadae waingereza walikua wanamuundaa kidaha kuwa kiongozi wa nchi,wakambatiza na kumwita David kidaha makwaia Kama sikosei,
So nahisi hata chief makongoro alikuwa ukoo wa makwaia
Mkuu,

Makongoro ni watu wa Mara na Makwaia ni watu wa Shinyanga ni familia mbili za kichifu lakini ni uchifu tofauti.

Mimi najua hilo kwa sababu Makwaia ni family.
 
Kwasababu huzuni zao siyo huzuni za kila mtu.
Huzuni zao si huzuni za kila mtu.

Ndiyo maana hujalazimishwa kuhuzunika nao umejipendekeza wewe mwenyewe kuingilia uzi wa huzuni za watu na kuwafanyia fujo.

Hawa watu hawajakulazimisha uhuzunike. Unaweza usi conment chochote kwenye uzi wa huzuni zao.

Watu kibao wamesoma wakaona uzi wa Magambo Mak9ngoro, mtu hawamjui, labda hawaoni haja ya kumjua, wakasepa, hawaja comment.

Wengine wamejiuliza huyu nani, wamesoma, wakaona mtu hawamjui, hawaja commebt.

Sasa wewe mtu humjui, humjali, hakuhusu, hakuongezei kitu, hakupunguzii kitu, kimbelembele cha ku comment cha nini?

Wakihuzunika kwa kumpoteza mpendwa wao bila wewe kuhuzunika hilo halitawapunguzia kitu, wala halitakupunguzia kitu wewe.

Sasa kwa nini unajilazimisha ku comment hapa na kuleta fujo kwenye uzi wa msiba wa watu?
 
Ni namba zinazogawanyika kwa moja na zenyewe tu 😂😂😂
Kuna mmoja alikuwaga denmark alirudi bongo kutokana na 1,2,3 chenga
Kuna wale jamaa zangu pale msasani wana kibar chao na chenga alafu lile eneo la wazi
La mama nyerere, wale akili zao nao wanazijua wenyewe
Kuna shida mahali naona 😄

Ova
 

Snakes and Chiefs​



Some 20 kilometres from Butiama on the road to the Serengeti National Park that passes through Fort Ikoma a traveler comes across the village of Nyamuswa, the seat of the late Chief Mohamed Makongoro Matutu of the Ikizu ethnic group who died in 1958.

I have recently visited Chief Makongoro's homestead on several occasions and have been informed that there is a huge snake at an area with a granite rock outcrop near the homestead. One of the Chief's sons who took me around the area in an attempt to locate the snake said the snake has been around for a long time. He recalls seeing the snake from his childhood days. I estimate the son is close to 60 years old today.

Although our attempts to locate the snake were unsuccessful I am told the snake was allowed to stay in the area by the specific instructions of Chief Makongoro and for that reason those who live there today, mostly members of his family, do not harm the snake. Occasionally, the snake emerges from the tall grass and granite rocks to soak in the warmth of the sun in the mornings. Sometimes, the snake wanders farther and into the residential area where members of the Chief's family live. The snake is so old that witnesses report grass has grown on its head.

At Butiama, in the area where the late Chief Nyerere Burito of the Zanaki ethnic group used to live, residents regularly report seeing another large snake that I have not have had the fortune of sighting. That snake sometimes moves into one of the residents of Mwalimu Nyerere, a house that remains uninhabited for lengthy periods. The snake leaves the house when people move in, but returns when they leave.

The beliefs and treatment of some animals and snakes of the Ikizu and the Zanaki could be similar. The Zanaki do not harm animals, particuarly those living near
 
Kuna mmoja alikuwaga denmark alirudi bongo kutokana na 1,2,3 chenga
Kuna wale jamaa zangu pale msasani wana kibar chao na chenga alafu lile eneo la wazi
La mama nyerere, wale akili zao nao wanazijua wenyewe
Kuna shida mahali naona 😄

Ova
Ukoo mkubwa una watu wengi hauwezi kukosa characters wa kila aina.

Kuna mmoja yupo New York machachari sana, injinia mzuri lakini Unyamwezii sasa, wee. Mwingine binti yupo Ireland ukitaka kupigana naye mseme vibaya babu yake.

Kaka Mako naye ndiyo hivyo inabidi apewe comedy show kabisaa.

Mwana mwenyewe kaka mkubwa huwa namfurahia sana kwa sababu hatabiriki kama hali ya hewa ya pwani za Monsoon.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom