TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

Baba yake (au babu yake?) Magambo, Chifu Makongoro, ndiye mtu aliyemuambia baba yake Julius Nyerere, Chifu Nyerere Burito, kwamba huyu mtoto (Kambarage Nyerere) ana akili sana, anafaa kupelekwa shule.

Yule Chifu Makongoro alipokuwa anamtembelea Chifu Nyerere Burito, alikuwa anapata nafasi ya kucheza bao na mtoto wa rafiki yake na Chifu mwenzake, mtoto mwenyewe ndiye Kambarage Nyerere. Chifu Makongoro akaona kuwa huyu mtoto Kambarage anajua sana kucheza bao, anamshinda hata yeye mtu mzima. Chifu Makongoro akamwambia rafiki yake Chifu Nyerere Burito ampeleke huyu mtoto kusoma shule, kwa sababu anaonekana ana akili sana.

Chifu Burito Nyerere kwanza alisita, lakini kaka yake Nyerere aliyeitwa Edward Wanzagi (aliyekuja kuwa Chifu Wanzagi baada ya Chief Burito kufariki) naye pia akamsisitiza Chifu Nyerere Burito (baba yake Edward Wanzagi na Kambarage Nyerere) amuandikishe kuanza shule Kambarage Nyerere. Edward Wanzagi alimpenda sana mdogo wake Kambarage Nyerere.

Hiyo ndiyo historia ya Julius Kambarage Nyerere kuandikishwa shule. Chifu Makongoro alikuwa mtu aliyemshawishi baba yake Kambarage Nyerere ampeleke shule huyu Kambarage Nyerere aliyekuja kuwa rais wa Tanganyika na Tanzania.

Kwa hiyo, utaona familia ya Makongoro imekuwa na ukaribu sana na famikia ya Nyerere tangu enzi za wazee walivyokuwa machifu huko.

Na kwa hwshima ya Chifu Makongoro, Julius Kambarage Nyerere alimuita mmoja wa watoto wake jina hilo la Makongoro, Charles Makongoro Nyerwre. Baba yake Magambo Mako giro ndiyo chanzo cha jina la Charles Makongoro Nyerere, aka "kaka Mako".

Kwa historia zaidi ya uhusiano huu wa famikia za Nyerere na Makongoro soma "Nyerere: The Early Years" cha Profesa Timothy Molony (Edinburgh University).

Poppy Hatonn
Asante kwa ufafanuzi.
Tangu namuona Interchick, niliambiwa kwamba alitunzwa kwenye Familia ya Nyerere ila hawana Undugu.
Interchick alikuwepo pia Matare Joseph Nyerere kama sijachanganya Sirname na hivyo wengi walikuwa wanajua ukweli huo.
Ila nilikuwa sijajua uhusiano wao hadi kukaa na Nyerere yeye na Dr Abdallah (Mhaya) sijui?
Hata hivyo sijawahi kuifuatilia kwa ukaribu historia ya JK Nyerere na hivyo siwezi kusema lolote. Leo walau nimepata somo zaidi maana nilikuwa najua JKN na yeye ni kutoka Familia ya Mtemi.
 
Snakes and Chiefs​

Some 20 kilometres from Butiama on the road to the Serengeti National Park that passes through Fort Ikoma a traveler comes across the village of Nyamuswa, the seat of the late Chief Mohamed Makongoro Matutu of the Ikizu ethnic group who died in 1958.

I have recently visited Chief Makongoro's homestead on several occasions and have been informed that there is a huge snake at an area with a granite rock outcrop near the homestead. One of the Chief's sons who took me around the area in an attempt to locate the snake said the snake has been around for a long time. He recalls seeing the snake from his childhood days. I estimate the son is close to 60 years old today.

Although our attempts to locate the snake were unsuccessful I am told the snake was allowed to stay in the area by the specific instructions of Chief Makongoro and for that reason those who live there today, mostly members of his family, do not harm the snake. Occasionally, the snake emerges from the tall grass and granite rocks to soak in the warmth of the sun in the mornings. Sometimes, the snake wanders farther and into the residential area where members of the Chief's family live. The snake is so old that witnesses report grass has grown on its head.

At Butiama, in the area where the late Chief Nyerere Burito of the Zanaki ethnic group used to live, residents regularly report seeing another large snake that I have not have had the fortune of sighting. That snake sometimes moves into one of the residents of Mwalimu Nyerere, a house that remains uninhabited for lengthy periods. The snake leaves the house when people move in, but returns when they leave.

The beliefs and treatment of some animals and snakes of the Ikizu and the Zanaki could be similar. The Zanaki do not harm animals, particuarly those living near
Hii story ameandika nani?
 
Ukoo mkubwa una watu wengi hauwezi kukosa characters wa kila aina.

Kuna mmoja yupo New York machachari sana, injinia mzuri lakini Unyamwezii sasa, wee. Mwingine binti yupo Ireland ukitaka kupigana naye mseme vibaya babu yake.

Kaka Mako naye ndiyo hivyo inabidi apewe comedy show kabisaa.

Mwana mwenyewe kaka mkubwa huwa namfurahia sana kwa sababu hatabiriki kama hali ya hewa ya pwani za Monsoon.
First born Andrew Nyerere akili zimezidi zinampa shida.

Ile kichwa inatafsiri vitabu vya buddhism
 
First born Andrew Nyerere akili zimezidi zinampa shida.

Ile kichwa inatafsiri vitabu vya buddhism
Naam,

Andrew nilitafsiri naye Dhamapada kwenda Kiswahili nikamuachia kazi hiyo mimi nilipokwenda kusoma chuo New York City.

Dhamapada is a very nice Buddhist text, even my aunt, who is a Christian and knew nothing about Buddhism, when she read it, she loved the wisdom it carried.

Dhamapada ya Kiswahili nafikiri ipo pale kwa Rev. Pannasekara Buddhist Temple, Mindu Street, Upanga Dar es salaam.

Poppy Hatonn
 
Mzee nakuheshimu, lakini hayo ni mapungufu yako, pembe la ng'ombe halifichiki.
Dr. Matola upungufu upi?

Mimi nimesahihisha historia ya Mwalimu Julius Nyerere iliyokuwa na upungufu mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Umesoma kitabu hiki: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press London 1998?

Unajua historia ya kitabu hiki na athari yake katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika?

Unajua wasomi wangapi mabingwa wa historia ya Afrika wamekifanyia mapitio na mapitio hayo kuchapwa katika Cambridge Journal of African History?

Unajua maana ya kitabu kuingizwa kwenye Journal of African History?

View: https://youtu.be/bgMxDNdCv64?si=0K-TpgnRoygaskaz
 
Naam,

Andrew nilitafsiri naye Dhamapada kwenda Kiswahili nikamuachia kazi hiyo mimi nilipokwenda kusoma chuo New York City.

Dhamapada is a very nice Buddhist text, even my aunt, who is a Christian and knew nothing about Buddhism, when she read it, she loved the wisdom it carried.

Dhamapada ya Kiswahili nafikiri ipo pale kwa Rev. Pannasekara Buddhist Temple, Mindu Street, Upanga Dar es salaam.

Poppy Hatonn
Mwamba Andrew Nyerere ametambulisha rosary yake mpya na siyo Necklase, ni rosary ya 1008 beads.
FB_IMG_1747975805717.jpg
 
MAGAMBO MAKONGORO AMEFARIKI DUNIA

Kwa wanaomfahamu Magambo Makongoro amefariki leo hospitali ya muhimbili, maziko kesho Kisutu Alasiri.

Msiba upo nyumbani kwake Msasani opp na nyumba ya Mzee Rais Mwinyi Mikocheni.
Nimepokea taarifa hiyo hapo juu hivi punde.

Magambo tunajuana toka udogo wetu ni mtoto wa Chief Makongoro.

Tulipokuwa shule tukifanya picnic yeye akitupeleka Kigamboni nyumba ya mapumziko iliyokuwa ya Gavana wakati wa ukoloni na kwa wakati ule baada ya uhuru ikawa iko chini ya Mwalimu Nyerere kama Rais wa Tanzania.

Mwalimu alikuwa haitumii nyumba hii na Magambo yeye kwa ule usuhuba uliokuwa baina ya baba yake na Nyerere alikuwa mtoto wa nyumbani State House.

Nakumbuka siku zile hata jina hili la Ikulu lilikuwa bado.

Magambo alikuwa mwenzetu na mchezo wetu ulikuwa mmoja pamoja na Kleist na mdogo wake Ebby, Yusuf Zialor, Wendo Mwapachu, Bubby Bokhari, Christopher Faraj, Abdallah Mohamed Saleh (Tambaza), Abdul Mtemvu, Edward Makwaia (sasa Chief wa Siha), Abdallah Mgambo, Eyshe na Mariam Max, Erica Kisa, Janet Zebedayo, Haitham Rashid, Esther Mzena wenzetu wengine wengi siwakumbuki.

Wenyewe tukijiita Scorpions na wengi tulikuwa wanafunzi St. Joseph's Convent.
Baadhi wemetangulia mbele ya haki.

Miaka ya kati Magambo alikuwa akifanya kazi Inter King iko Mbezi wanafuga kuku.

Mara ya mwisho miaka michache nyuma mwezi wa Ramadhani tulikutana Masjid Ngazija alikuwa na Abraham Sykes.

Nakumbuka siku ile walinishambulia sana kwa kunichangia ati mie najidai sana na Msikiti Ngazija nauona kama mali yangu nikiwaona wao wanakuja kusali pale roho inaniuma.

Haya ndiyo yalikuwa mapenzi yetu tulikutana lazima tubwatizane huku tunacheka.
Nilipoteana na Magambo kwa muda hatujaonana.

Allah amsamehe na amtie Firdaus.
Amin.

View attachment 3339866
Magambo Makongoro
Habari mimi ni Mtoto wa Makongoro marehemu naomba nipate contacts zako tunashida kidogo kwenye upande wa mirathi mke wa Marehemu anataka kutu dhulumu Mali za marehemu
 
Hivi una marafiki wakristo?
 
Ni nani aliyetangaza kifo cha Magambo?
Ni Mohammed Said yule historian?
The last time nimemwona Magambo ilikuwa katika msiba wa Rose Nyerere hapa Msasani.
Nilikuwa nimefika,at the same time Magambo akafika na bajaji
Tukaingia wote getini.
Halafu walikuwepo wanafamilia pale wanafanya kikao kuhusu maziko.
Nikawaambia,"Mtayarishie Magambo kiti hapo"
 
Habari mimi ni Mtoto wa Makongoro marehemu naomba nipate contacts zako tunashida kidogo kwenye upande wa mirathi mke wa Marehemu anataka kutu dhulumu Mali za marehemu
Mkuu ni mke mkubwa au mdogo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom