Kama kweli wewe binafsi unakiri tumetoka kwenye UJAMAA na tuko kwenye UBEPARI unashangaa nini kuwa na Mafukara Milioni 30 na Mabilionea 30? Maana moja ya sifa kuu ya mfumo wa UBEPARI (Ambao wewe unadai tumo) ni kuwepo kwa matabaka tena kati ya walionacho na wasio nacho, mashindano bubu ya watu kuchuma fedha nk. nk.
Kitu ambacho kiko wazi ni kuwa, kwa sasa Siasa imewekwa kuwa njia kuu ya watu kuchuma fedha na kuupata utajiri wa haraka. No matter what, Siasa na Wanasiasa wako kwenye fursa kubwa ya kuchuma fedha watakavyo, kujilipa posho nono, kupokea rushwa kubwa kutoka kwa makampuni ya kibepari ili kulinda maslahi yao, kukwepa urasimu katika mahitaji mbalimbali ya kihuduma wanayoyahitaji na kupitisha biashara na maslahi yao binafsi.
Makala yako hii inataja uwepo wa mabilionea 30,hawa ni akina nani? Kuna Bilionea asiye mwanasiasa kwa sasa? Ni wachache. Jiulize kwa nini Ufisadi umekaa meza moja na Siasa yetu? Jibu ni rahisi sana, kuna ndoa ya Ufisadi baina ya Wanasiasa na Wafanyabiashara ambayo msingi wake ni huohuo kutengeneza mabilionea huku wakulima, wavuvi, wafugaji wakipigwa kumbo na kubaki kwenye lindi la ufukara.
Unasema tumeingia kwenye mfumo wa UPEBARI (Sijui ni lini?) hivyo, kubali tu uwepo wa Mabilionea hao 30 kati ya Mafukara Milioni 30, ndiyo sifa kuu ya UBEPARI, haiepukiki.Hata wewe kwa fursa uliyonayo una kila sababu ya kuchagua kundi la Mabilionea as far as UBEPARI unaruhusu Mashindano ya kuvuna utajiri baina ya watu, unaweza maana wenzako wameweza, pengine utakuwa umeanza, sijui.
Waumini wa dhati wa Mfumo wa Ujamaa kama (Karl Marx na Prof. Shivji ambaye unakiri ni mwalimu wako) muda wote wanalia na UBEPARI na sifa yake kuu ya matabaka katika jamii. Wamekuwa wakitoa wito wa kuyamaliza kama si kupunguza gape lililopo sasa.Prof. Shivji kila wakati amekuwa akipigania marejeo ya Sera ya Ujamaa na Kujitegemea.Hata Nyerere (RIP) alikufa akisisitiza kuwa haoni tatizo kwenye sera hii.
Ukweli ni kuwa, hata kama kutakuwa na utetezi wa namna gani dhidi ya Ufukara unaomtesa mwananchi wa kawaida huko kijijini bado Wanasiasa watabaki kuwa wa kwanza kulalamikiwa na Mafukara wanaotoka nchi ya KIJIJINI (Si nchi ya MJINI). Sheria zinapitishwa na wanasiasa, Bajeti za maendeleo zinapitishwa na Wanasiasa lakini Wanasiasa hawahawa (Hasa Wabunge(?)) ndiyo wenye fursa ya kuiwajibisha Serikali pale inaposhindwa kuwajibika ipasavyo.