Ni kweli. Lazima tuanzie hapa. Kwamba mtu anayetaka kuwa mtumishi wa umma lakini anafanya biashara aache biashara. Aweke kwenye 'blind trust' biashara zake katika kipindi chote cha utumishi wa uuma. Mataifa makubwa tena ya kibepari duniani yanafanya hivi. Sisi Taifa lililotoka kwenye ujamaa tunashindwa kuchukua hatua hii. Mara 3 nimepeleka muswada Bungeni kutaka kutungwa kwa sheria ambayo itadhibiti mgongano wa maslahi kati ya wafanyabiashara ambao ni wanasiasa na mra zote imekataliwa hata kuchapishwa kwenye gazeti la serikali (GN).
Nakubaliana na wewe kabisa kwamba hapa ndio mahala pa kuanzia. Kisha uwazi wa mali za viongozi. Hivi sasa tunatangaza mali lakini wananchi hawana access. Matokeo yake ni wananchi kuwa na mawazo tofauti kuhusu viongozi wao. Daftari la mali na madeni ya viongozi liwe wazi. Mfano kwa wabunge liwekwe pale ofisi za Bunge Dar na Dodoma. Daftari liwe wazi kwenye website ya Bunge. Ili kama kiongozi amedanganya iwe rahisi kwa wananchi kumsema na kuona kuona kama anamiliki mali zaidi ya kipato chake.
Uwazi ni msingi mkubwa sana wa kupambana na ufisadi. Uwazi utaondoa majungu na kuzushiana. Uwazi utawapa
nguvu wananchi juu ya viongozi wao.
Kama kweli wewe binafsi unakiri tumetoka kwenye UJAMAA na tuko kwenye UBEPARI unashangaa nini kuwa na Mafukara Milioni 30 na Mabilionea 30? Maana moja ya sifa kuu ya mfumo wa UBEPARI (Ambao wewe unadai tumo) ni kuwepo kwa matabaka tena kati ya walionacho na wasio nacho, mashindano bubu ya watu kuchuma fedha nk. nk.
Kitu ambacho kiko wazi ni kuwa, kwa sasa Siasa imewekwa kuwa njia kuu ya watu kuchuma fedha na kuupata utajiri wa haraka. No matter what, Siasa na Wanasiasa wako kwenye fursa kubwa ya kuchuma fedha watakavyo, kujilipa posho nono, kupokea rushwa kubwa kutoka kwa makampuni ya kibepari ili kulinda maslahi yao, kukwepa urasimu katika mahitaji mbalimbali ya kihuduma wanayoyahitaji na kupitisha biashara na maslahi yao binafsi.
Makala yako hii inataja uwepo wa mabilionea 30,hawa ni akina nani? Kuna Bilionea asiye mwanasiasa kwa sasa? Ni wachache. Jiulize kwa nini Ufisadi umekaa meza moja na Siasa yetu? Jibu ni rahisi sana, kuna ndoa ya Ufisadi baina ya Wanasiasa na Wafanyabiashara ambayo msingi wake ni huohuo kutengeneza mabilionea huku wakulima, wavuvi, wafugaji wakipigwa kumbo na kubaki kwenye lindi la ufukara.
Unasema tumeingia kwenye mfumo wa UPEBARI (Sijui ni lini?) hivyo, kubali tu uwepo wa Mabilionea hao 30 kati ya Mafukara Milioni 30, ndiyo sifa kuu ya UBEPARI, haiepukiki.Hata wewe kwa fursa uliyonayo una kila sababu ya kuchagua kundi la Mabilionea as far as UBEPARI unaruhusu Mashindano ya kuvuna utajiri baina ya watu, unaweza maana wenzako wameweza, pengine utakuwa umeanza, sijui.
Waumini wa dhati wa Mfumo wa Ujamaa kama (Karl Marx na Prof. Shivji ambaye unakiri ni mwalimu wako) muda wote wanalia na UBEPARI na sifa yake kuu ya matabaka katika jamii. Wamekuwa wakitoa wito wa kuyamaliza kama si kupunguza gape lililopo sasa.Prof. Shivji kila wakati amekuwa akipigania marejeo ya Sera ya Ujamaa na Kujitegemea.Hata Nyerere (RIP) alikufa akisisitiza kuwa haoni tatizo kwenye sera hii.
Ukweli ni kuwa, hata kama kutakuwa na utetezi wa namna gani dhidi ya Ufukara unaomtesa mwananchi wa kawaida huko kijijini bado Wanasiasa watabaki kuwa wa kwanza kulalamikiwa na Mafukara wanaotoka nchi ya KIJIJINI (Si nchi ya MJINI). Sheria zinapitishwa na wanasiasa, Bajeti za maendeleo zinapitishwa na Wanasiasa lakini Wanasiasa hawahawa (Hasa Wabunge(?)) ndiyo wenye fursa ya kuiwajibisha Serikali pale inaposhindwa kuwajibika ipasavyo.