Mafukara milioni 30, Mabilionea 30 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafukara milioni 30, Mabilionea 30

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zitto, Sep 20, 2012.

 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  TAIFA LA MAFUKARA MILIONI 30 NA MABILIONEA 30


  Zitto Kabwe

  Mwalimuwangu wa nje ya Darasa Issa Shivji hugawa Watanzania katika madaraja matatu; WalalaHoi, WalalaHeri na WalalaHai akimaanisha watu wenye kuishi kwenye dimbwila Umasikini, watu wenye ahueni na Matajiri. Katika mtandao wa kijamii(twitter) wakati naandika makala hii, mdogo wangu Michael Dalali akaniongezea daraja jipya ‘wakeshahoi'. Hawa wa mwisho nadhani ndio tunasema ‘masikini wakutupwa' kwa lugha ya mtaani. Sijapata fursa ya kumwuliza Michael ili anifafanulie hili daraja jipya. Leo ninatafakari na wasomaji kuhusu madaraja mawili tu, Walalahoi (Mafukara) na Walalahai (Matajiri).

  MweziJuni, 2012 niliandika andiko katika lugha ya Kiingereza (The Bottom 30M, www.zittokabwe.com) kujibu swali la kwa nini Watanzania ni masikini licha ya utajiri mkubwa ulioponchini. Katika makala hiyo ‘Mafukara 30M' nilihitimisha kwamba Watanzania ni masikini kwa sababu watawala wetu wameamua hivyo kwa kutunga na kutekeleza sera na mikakati ambayo inanufaisha watu wachache katika tabaka la juu la maisha ambao wengi wanaishi mijini na kuacha watu wengi wanaoishi vijijini wakiwa masikini zaidi. Katika tafakuri ya leo nafafanua zaidi huu mtazamo. Watawala wetu ninaamini wakiulizwa tena na wanahabari kwanini Tanzania ni masikini hawatajibu hawajui (Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda wamenukuliwa zaidi ya mara moja wakisema hawajui kwa nini nchi wanayoongoza ni masikini). Nimesema na kuandika mara kadhaa sababu za umasikini kuongezeka nchini licha ya kwambauchumi unaonekana kukua kwa kasi.

  Waziriwa Fedha ndugu William Mgimwa wiki iliyopita amerudia tunayoyasema kila sikukwamba Ukuaji wa Uchumi Tanzania haujapunguza umasikini. Tumekuwa tukisema kwamba mikakati ya kiuchumi tunayotekeleza haimsaidii Mtanzania wa kawaida maana hatuoni tofauti ya maisha yake. Serikali ikaendelea na inaendelea kutekeleza mikakati ile ile ikitegemea kupata matokeo tofauti.

  NduguMgimwa, Waziri wa Fedha, anasema, "Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi chamiaka 10 iliyopita uchumi umekua kwa wastani wa asilimia saba lakini umasikiniumepungua kwa asilimia 2.1 tu ambayo ni ndogo ikilinganishwa na asilimia yaukuaji wa uchumi". Akanukuliwa "Umasikini umepungua kwa asilimia 2.1 kutokaasilimia 35.6 mwaka 2001 hadi kufikia asilimia 33.4 mwishoni mwa mwaka janakatika kundi la masikini,". Hakuna kauli mpya hata moja. Kinachosikitisha ni kwamba Serikali imeendelea kuona MKUKUTA ndio mkakati pekee wa kuondoa umasikini nchini. Sera na mikakati ya Serikali ya kuondoa Umasikini imeshindwa. Taarifa ya Shirika la SID ya mwaka 2012 imeonyesha kuwa kati ya mwaka 2001 na2011 watanzania takribani milioni 5 zaidi wameingia katika dimbwi la umasikini.Kwa nini Uchumi unakua kwa kasi kubwa lakini ukuaji huu haupunguzi umasikini, unazalisha masikini zaidi?

  Taarifa za Serikali pia zinaonyesha kuwa ukuaji wauchumi hautengenezi ajira kwa watu. Kwa nini hali hii? Kama kawaida hatukosi majibu ya maswali haya. Tunayarudia majibu haya kila wakati tunapopata nafasi ya kueleza. Kwamba Sekta za Uchumi zinazokua hazina mahusiano yenye nguvu na wananchi wa kawaida – Madini, Utalii na Mawasiliano. Sekta yenye mahusiano makubwa na wananchi – sekta ya Kilimo - haikui kwa kiwango kinachoweza kupunguza umasikini. Ili kupunguzaumasikini Tanzania kwa kiwango kikubwa, sekta ya Kilimo inapaswa kukua kwaasilimia zaidi ya nane (8%) angalau kwa miaka mitatu mfululizo na kuendeleakukua kwa wastani wa asilimia sita (6%) kwa miaka kumi.

  Jibulipo na limeshasemwa sana lakini jawabu halisemwi. Labda tuulize tena. Kwaninisasa sekta ya Kilimo haikui kwa kiwango kinachotakiwa ili kuondoa umasikini Tanzania? Jawabu langu ni kwamba Watawala hawataki. Watawala wetu wamechagua Watanzania wengi wabakie mafukara.

  Umasikini wa Watanzania ni chaguo mahususila watawala kwa kuamua kutekeleza sera ambazo zinakuza kipato cha mwenye nachona kufukarisha wananchi wengi wa vijijini. Vile vile uamuzi wa watawala kushindwa kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa rasilimali za umma ni ufukarishwaji wa mwananchi wa vijijini ambaye anakoseshwa huduma za jamii na miundombinu ya kumpa fursa ya kufaidika na shughuli zake za kiuchumi. Ufukara wa mamilioni ya Watanzania ni matokeo ya chaguo la watawala kisera, kimkakatina kimatendo.

  Ufukarani tofauti na Umasikini ingawa tunatumia maneno haya tukiamini kuwa yana maana inayofanana. Wakati Umasikini (poverty) ni hali ya kukosa huduma za msingi kama Elimu, Afya, Chakula na Maji safi na salama kunakotokana na kukosa kipato au kuwa na kipato kidogo, Ufukara (impoverishment) ni hali ya kukoseshwa huduma za msingi za kibinaadamu hata kama kuna juhudi za dhati za kufanya kazi kwa bidii ili kupata uwezo wa kufikiahuduma hizo. Umasikini unaweza kusababishwa na masuala mbalimbali ikiwemo haliya kuwa masikini tu (‘we are poor because we are poor') au jiografia nk. Ufukara unatokana na kufukarishwa. Unatokana na maamuzi ya kisera ya Taifa husika (au mataifa ya nje) ambayo yananyonya juhudi za watu kupata maisha yenye kuwapa huduma zote za msingi kama Elimu, Afya Maji na muhimu zaidi chakula chauhakika. Mafukara wote ni masikini, ila Masikini wote sio mafukara. Nitafafanua.

  Mwaka1991 Watanzania masikini wanaoishi Dar es Salaam walikuwa ni takribani asilimia28.1 ya wakazi wote wa Jiji. Miaka 16 baadaye, asilimia 16 ya wakazi wa Jiji laDar es Salaam walikuwa wanaishi kwenye umasikini. Kwa upande wa Watanzania wanaoishi Vijijini, mwaka 1991 kulikuwa na masikini asilimia 40 ya wakazi wote wa Tanzania vijijini. Mwaka 2007, miaka 16 baadaye, asilimia 37 ya Watanzaniawa vijijini walikuwa wanaishi kwenye dimbwi la umasikini. Takwimu hizi unazipata kutoka Ofisi ya Takwimu na Shirika la Twaweza limerahisisha taarifa hizi kupitia chapisho lao ‘Growth in Tanzania: Is it reducing poverty?'

  Masikini wanaoishi Dar es Salaam na miji mingine nchini wanaweza kujikwamua kutoka umasikini kutokana na fursa zinazojitokeza mijini. Miundombinu ya usafiri nausafirishaji, viwanda vipya na fursa za ajira zinajengwa zaidi mijini kuliko vijijini. Huduma za Elimu na Afya zinaboreka zaidi mijini na hata Walimu naManesi wanakimbilia kufanya kazi mijini ambako wamerundikana kuliko vijijiniambapo kuna ukosefu wa kutisha wa wafanyakazi wa sekta hizo. Masikini wa mijinisio mafukara.

  Masikiniwanaoishi vijijini licha ya kufanya kazi kwa bidii na hasa kazi za Kilimo hawana fursa za kuondokana na umasikini. Mfumo wa Uchumi wa nchi umejengwa kwamisingi kwamba watu wa vijijini hupokea Bei za kuuza mazao yao kutoka mijini na vilevile hupokea bei za kununua bidhaa zinazotengenezwa mijini kutoka hukohuko. Barabara za vijijini zina hali mbaya au hazipo kabisa. Huduma za jamiikama Elimu, Maji na Afya ni mbaya. Huduma za nishati ya Umeme hazipo kabisa katika vijiji 96 kati ya vijiji 100 nchini. Masikini wa vijijini ni Mafukara.Wamefukarishwa kutokana na sera zinazonyonya jasho la kazi yao kwa upande mmojana sera zinazowanyima maendeleo ya miundombinu kwa upande mwingine. Asilimia 75ya Watanzania wanaishi vijijini hivi sasa na kwenye ufukara mkubwa sana. Kwamakadirio ya idadi ya watu Tanzania, Watanzania milioni thelathini waishiovijijini ni mafukara.

  Kufunguliwakwa miundombinu ya Vijijini kama Barabara, Maji na Nishati ya Umeme kunawezakuwaondoa watu wa Vijijini kwenye minyororo ya ufukara kwenda kwenye umasikini na hatimaye kutokomeza kabisa umasikini. Lakini Watawala wanaogawa rasilimaliya nchi hawataki. Wanasema hakuna rasilimali fedha za kutosha kusambaza umeme vijijini ili kukuza viwanda vidogo vidogo na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, kusambaza maji safi na salama ili kuboresha afya na kumpunguzia mwanamke wakijijini muda wa kutafuta maji na kujenga barabara za vijijini ili wakulimawafikishe mazao yao sokoni. Ikifika kujenga shule na zahanati na vituo vya afyawananchi wa vijijini wanaambiwa wajenge wenyewe, wajitolee. Ni kweli hakunafedha za kuwekeza vijijini?

  Ufisadi unatengeneza Mabilionea

  Itakumbukwa kwamba mwaka 2007 Bunge la Tisa liliibua kashfa mbalimbali zinazoonyesha namna ambavyo fedha za nchi zinavyoibwa na wenzetu wachache. Haina maana kwamba Mabunge ya nyuma hayakuwa na Wabunge wenye uwezo au ujasiri wa kuibua masualaya msingi kuhusu fedha za nchi, lakini nadhani wakati au mazingira hayakuwa yanaruhusu. Tulishuhudia Ufisadi uliofanywa Benki Kuu ya Tanzania kwa kuibwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 133 za malipo ya Nje (EPA), Utoroshaji mkubwa wafedha zilizofikia dola za kimarekani milioni 136 kupitia mradi wa Meremeta uliokuwa chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), Uingiaji wa Mkataba waMadini ya Dhahabu wa Buzwagi uliokuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni400 bila kuzingatia uhitaji wa kuboresha mazingira ya nchi kufaidika na utajiriwa Madini na Wizi mkubwa wa Fedha za msaada wa kuagiza bidhaa kutoka Serikaliya Japani (Commodity Import Support) ambapo zaidi za shilingi bilioni 40ziligawiwa kwa viongozi kadhaa wa Serikali na wafanyabiashara.

  Kashfachache zilijadiliwa sana ikiwemo ile ya Mkataba wa kununua Umeme wa Richmond ambao sasa unelekea kuliingiza hasara Taifa ya zaidi ya shilingi bilioni 90kutokana na hukumu ya Kampuni iliyorithi mkataba wa Richmond dhidi ya Shirikala Umeme TANESCO, ile ya Buzwagi ambayo ilipelekea kuundwa kwa Kamati ya Bomani iliyopelekea kuandikwa kwa Sera mpya ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 na ile ya EPA iliyopelekea baadhi ya watuhumiwa kufikishwamahakamani lakini kuacha kitendawili kikubwa kuhusu Kampuni ya KAGODA ambayoilikwapua zaidi ya shilingi bilioni 40 katika shilingi bilioni 133 zilizoibwa. Masuala ya MEREMETA na Import Support yamezimika na mshawasha wa wafuatiliaji wa mambo kufuatilia masuala haya umepungua sana.

  Masuala hayo machache yaliyoibuliwa katika Bunge la Tisa yanaonyesha kwamba kunarasilimali fedha nyingi katika Taifa ambayo ingeweza kutumika kuwekeza kwenye maendeleo ya watu wa vijijini. Hata hivyo rasilimali fedha hii inatumika kufanya Watanzania wachache kuwa mabilionea kwa njia haramu za kifisadi. Bungela Kumi, ninaamini, litaibua masuala mengine zaidi yanayoonyesha namna ambavyo tumeamua kuwafukarisha Watanzania wengi na kuwabilionesha wachache.

  Matrilioni ya shilingi yatoroshwa kila mwaka

  Katika Kitabu cha 'Africa's Odious debts: Howforeign loans and capital flight bled a continent' waandishi Leonce Ndikumana na James Boyce wameonyesha kwamba katika kipindi cha miaka 40 jumlacya dola za kimarekani 11.4 bilioni zimetoroshwa kutoka Tanzania kwa njia mbalimbali. Hizi ni sawa na wastani wa dola za kimarekani 285 milioni kutoroshwa kila mwaka kuanzia mwaka 1970 mpaka 2010. Sehemu kubwa ya fedha hizizinatoroshwa na Makampuni makubwa ya Kigeni yanayofanya biashara na kuwekeza hapa nchini (utoroshaji mkubwa umefanyika mara baada ya Tanzania kuanza kuzalisha dhahabu kwa wingi na makampuni makubwa ya nje kuanza kutafuta mafuta na gesi asilia kwenye bahari ya Tanzania) na sehemu nyingine ni bakshishi wanayopewa maafisa wa Serikali wanaofanikisha utoroshaji huu. Watanzania hawa (Wanasiasa, Watendaji, Maafisa wa Jeshi na Usalama wa Taifa na Wafanyabiashara) huficha fedha hizi chafu kwenye Mabenki ughaibuni na hasa Uswisi, Dubai, Mauritius, Afrika ya Kusini na maeneo mengine (Tax Havens/Offshore/TreasureIslands). Wengine wamewekeza kwenye mali zisizoondosheka kama majumba na zinazoondosheka kama hisa kwenye makampuni mbalimbali duniani.

  Taarifa rasmi ya Benki ya Taifa ya Uswisi inaonyesha kuwa Watanzania wameficha hukozaidi ya dola za Kimarekani 196 milioni. Uchunguzi unaoendelea unaonyesha kuwa takribani Watanzania 30 wameficha Fedha zao katika Mabenki ya Uswisi. Hii nibila kuhusisha wale ambao wameficha fedha zao kupitia majumba na hisa kwenye makampuni mbalimbali duniani na hasa katika nchi za Mauritius, Afrika Kusini naDubai. Uchunguzi pia unaonyesha kuwa Mtanzania mmoja ambaye hana rekodi yeyoteya Biashara zaidi ya utumishi wa Umma ameficha takribani dola milioni 56 katikaBenki mojawapo nchini Uswisi. Serikali ya Tanzania mpaka sasa imekataa kuchukuahatua za kuwajua Watanzania hawa na kuhakikisha kuwa mabilioni hayayanarejeshwa nchini na kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo vijijini. Serikaliya Senegal hivi karibuni imetuma maombi rasmi kwa Benki ya Dunia kuisaidiakufanya uchunguzi na kurejesha nchini mwao mabalioni ya fedha yaliyofichwakwenye mabenki ya nchi za Ulaya na hasa Uswisi.

  Ufisadi unafukarisha

  Tanzaniaina mtandao wa barabara wa zaidi ya kilometa 85,000 zikiwemo za vijijini nawilaya (zinazosimamiwa na Halmashauri za Wilaya) na za Mikoa na Barabara Kuu (zinazosimamiwa na TANROADS). Fedha zinazotoroshwa kila mwaka ni sawa sawa nakutorosha takribani kilometa 800 za babara za lami kila mwaka kwa kutumia gharama za sasa za ujenzi wa barabara. Fedha hizi pia zinaweza kuunganisha umeme kwenye vijiji 1300 (asilimia 10 ya vijiji vyote nchini) kila mwaka kwa gharama za sasa za kuunganisha umeme tena kwenye mikoa ambayo haipo kwenyegridi ya Taifa (REA wanatumia takribani shilingi bilioni saba kusambaza umemekatika vijiji 16 vya Jimbo la Kigoma Kaskazini). Fedha hizi pia zingeweza kuajiri walimu wengi zaidi wa vijijini na kwa kuwa miundombinu ya umeme, barabara na maji ingekuwa imeboreshwa walimu hawa wangekaa vijijini nakufundisha watoto wetu. Ufisadi kama huu umekosesha nchi rasilimali zakuendeleza watu wake.

  Rushwana Ufisadi inatengeneza Watanzania wachache kuwa mabilionea. Mabilionea hawaambao wana ushawishi mkubwa katika kuunda sera za nchi na utekelezaji wake wanapelekea kuundwa kwa sera na sharia zinazolinda utajiri wa walionacho na kuendelea kuhakikisha masikini wanaendelea kuwa mafukara. Rasilimali za nchizinaboresha maeneo ambayo mabilionea na wasaidizi wao wanaishi na kusahau kabisa kwamba Watanzania wengi wanaishi vijijini na huko ndipo kuna umasikini mkubwa. Umasikini wa vijijini kwa kiasi kikubwa unatokana na sera na matendo yanayofukarisha wananchi wengi.

  Ukuajiwa uchumi unaoambatana na ufisadi wa kiwango kinachotokea Tanzania unawafanya wenye nacho kupata zaidi na masikini kuwa mafukara zaidi. Tofauti ya kipato katika jamii imezidi kuongezeka na inaweza kuleta machafuko katika nchi. Takwimu za Pato la Taifa, kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa 2011, zinaonyesha kwamba asilimia 30 ya Watanzania (the richest 30%) wanamilikiasilimia 75 ya Pato la Taifa.

  Tumeonakwamba Watanzania mafukara wanaishi vijijini, asilimia 75 ya Watanzania, na hivyo takribani Watanzania milionithelathini wanaoishi vijijini wanaishi katika dimbwi la umasikini. Vile viletumeona kwamba asilimia 30 ya watanzania wanamiliki asilimia 75 ya Pato lote laTaifa. Pato la Taifa mwaka 2011 lilikuwa shilingi 40 trilioni na hivyo asilimia 30 ya Watanzania wanamiliki shilingi 30 trilioni katika jumla ya shilinig 40trilioni. Kutokana na muundo wa uchumi wetu ambapo sekta ya Huduma (Service sector) na ile ya Viwanda (Industrial sector) zinachangia zaidi ya asilimia 70ya Pato la Taifa na ukweli kwamba sekta zinazokua kwa kasi ni pamoja naMawasiliano, Madini, Ujenzi na Utalii, ni dhahiri Watanzania na Kampuni za Kitanzania zinamiliki zaidi ya shilingi trilioni moja hawazidi thelathini nakuna watu wanaweza kuwataja mmoja mmoja kwa majina yao au majina ya Kampunizao.

  Kwahiyo Watanzania milioni thelathini wamefukarishwa kwa kunyimwa fursa zakiuchumi na hivyo kumiliki sehemu ndogo sana ya Pato la Taifa. Wanafanya kazikwa bidii lakini mfumo wa kinyonyaji unawaweka katika umasikini daima dumu. Tumeona kuwa uchumi wa nchi unazalisha kundi dogo la watu wenye utajiri mkubwa ambao sehemu kubwa umepatikana kwa njia haramu. Watu hawa pia wanamiliki sekta zauchumi zinazokua kwa kasi na hivyo utajiri wao unazidi kuongezeka. Hawa wanashirikiana na Watanzania walio katikati (walalaheri) kuhakikisha wanaendelea kumiliki uchumi wa nchi. Hawa watu wa kati ndio wanasiasa, warasimu serikalini, wafanyakazi wa kada ya kati ya makampuni ya matajiri hawa au yanayofanya biashara na matajiri hawa. Badala ya watu wa kati kuweka sera madhubuti za kumkomboa Mtanzania wa chini aondokane na ufukara, wanaweka mazingira mazurikwa matajiri kutajirika zaidi.

  Hatimaye tunajenga Taifa la Watanzania Mafukara milioni Thelathini na Mabilionea Thelathini.

  Tukatae.
  Tunawezakujenga Taifa la watu wenye fursa sawa kwa kufanya maamuzi ya kubomoa mfumo wa kiuchumi wa kinyonyaji tunaoujenga tangu kupata uhuru kwa kuacha kubomoa mfumowa uchumi wa kikoloni licha ya Azimio la Arusha. Juhudi za kujenga Taifa lenye watu sawa ziliyeyuka mara baada ya kuamua kufuata sera za ubinafsishaji ambapo zilitafsiriwa kwa kukabidhi mali za Taifa kwa kundi dogo la watu na hivyo kutengeneza mfumo wa kifisadi ambao sasa umeota mizizi. Kazi iliyofanywa kwamiaka ishirini ya kujenga uchumi wa viwanda ziliyeyushwa katika kipindi chamiaka mitano tu ambapo viwanda vyote viligawanywa kwa watu binafsi na vingi leoni maghala tu ya kuhifadhia bidhaa nyingine.

  Ufisadi mkubwa ulishamiri kupitia sera ya ubinafsishaji ambapo watawala waliokuzwa kwa ‘kanuni' ya ‘kutosheka' walijawa na tamaa kubwa na uroho wa mali na kuanzakukusanya chochote kilichokuwa mbele yao. Hivi sasa nafasi yeyote ya uongoziimekuwa ni nafasi ya ulaji na sehemu kubwa ya tabaka la watawala kuanzia kwawenyeviti wa vijijiji, madiwani, Wabunge, Mawaziri na hata Marais wamekuwa ‘rent seekers' yaani watu ambao ni lazima kulimbikiza mali kutokana na nafasi za utawala walizo nazo. Mfano wa Wabunge kulilia nyongeza ya posho za kukaa kitako wakati walimu na madaktari wanaishi katika mazingira magumu ya kazi nimoja ya tabia za kutotosheka na tamaa zinazopamba viongozi wa kisiasa wa zamahizi.

  Kutochukuamaamuzi madhubuti ya kutokomeza ufisadi na mfumo wake ni kufukarisha Watanzania kwa sababu rasilimali ambayo inapotea kupitia vitendo vya kifisadi ingeweza kuwekezwa katika maendeleo ya watu wa vijijini, kwa kukuza shughuli za kiuchumi na kupanua mapato ya wananchi. Hivi sasa vita dhidi ya ufisadi imekuwa niturufu ya kisiasa tu na sio mchakato maalumu wa kuondoa kabisa mfumo wakifisadi. Ni lazima kuondoka kwenye hali ya kwamba wa ushujaa ni kutaja tu Fulani na Fulani ni fisadi, hali ambayo imefikia hata watu wasio na chembe yauadilifu kuchafua wengine, na kwenda mbele zaidi kwenye hatua za kubomoa mfumowa kifisadi.

  Hata uchumi ukue kwa kasi ya namna gani iwapo ukuaji huo unanufaisha kikundi kidogocha watu hauna maana na ni hatari kwa uwepo wa Taifa lenyewe. Ni lazima kuchukua maamuzi ya kujenga taasisi zenye nguvu ambazo zitaondoa hali hii yauchumi kutajirisha wachache na kufukarisha wengi. Taasisi na mfumo utakaohakikisha kuwa watawala wanawajibika kwa umma kwa wanayoyatenda na wasiyoyatenda. Mfumo utakaohakikisha kuwa rasilimali za nchi zinarudi kwa wananchi ili kujenga miundombinu vijijini ya barabara, maji, nishati ya umeme na huduma za kijamii hasa elimu na afya. Vinginevyo tutaendelea kuwa Taifa vipande vipande kutokana na tofauti kubwa ya kipato na fursa ndani ya jamii.

  Tanzania yenye Mafukara milioni Thelathini na Mabilionea Thelathini haikubaliki!

   
 2. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tunaishia kusema, kulalamika, kulaumu na kutoa takwimu lakini tumeshindwa kuchukua hatua za ki-vitendo. 'Tanzania yenye mafukara 30m na mabilionea 30m, haikubaliki', hiyo kauli haina mashiko hata kidogo, hizo kauli za 'haikubaliki' ni kauli za kisiasa au kinafiki. Sikia Mr. Zitto, tunachotaka kutoka kwako ni 'way forward', sema hivi jamani wananchi tuingie mitaani ili tuitoe hii serikali, tupe miundombinu ya kuingia mtaani na kuitoa hii serikali. You know what, enough is enough, tumechoka na porojo, matamko maandiko sasa tunataka kuingia mtaani...
   
 3. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Karibu jamvini Mkuu na pole na honeymoon! Najua Wana Jamvi Wana maswali mengi na wanatamani majibu ya kina kutoka kwako Ngoja niwape nafasi. Alafu fanya edit kidogo APo juu Mkuu usomeke vizuri kusoma nako kazi inapokuwa kwenye mpangilio m'bovu Kama huo
   
 4. S

  STIDE JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mh. Zitto, kwanza pole sana na majukumu. Pia asante sana kwa kutukumbuka wana jukwaa (nilidhani umekimbia missile)!!

  Mh. Zitto, ninayo mengi ningehitaji kuyafahamu kutoka kwako maadamu umekuja lakini naomba nianze na hili ili twende sawa:-

  Mh, umezungumza vizuri sana na kwa uyakinifu, ila naomba kabla hujaendelea utufafanulie juu ya tuhuma zinazo kukabili kuhusu "HATA WEWE PIA UMETOROSHA PESA KWENDA USWIS KIASI CHA $3.5mln." Je nikweli(unalizungumziaje)? Je huoni kwamba nawewe "UNAFUKARISHA" watz(kama ni kweli)!?
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  mkuu sidhani kama umefahamu tatizo si wingi wa mafukara na uchache wa mabilionea.Kwani hata ratio ya top layer ya matajiri wa India ambao wan arank kidunia katik top 20 kuinganisha na majority of very poor indians nimbaya kuliko sisi.

  Wapo watanzania wengi tuu hawaogopi umasikini ukiacha wale ambao roho zao hazijui kwanini Mungu kalaani "greed".Na ushahidi upo kwani wapo watu wengi wkipata hela kidogo shemu yake kubwa hutumiwa kwa makini katk starehe huku wakisema "Life is too short" au "we live only once".

  Mheshimiwa tatizo ni njia wanayoonekana kuzipata hizo hela, greed wanayoinyesha, mateso wanayowapa watu, kufuru wafanyazo na majibu ya kijinga wayatoayo.Na image wanayoproject kuwa "politics ndio biashara nzuri kuliko" huku wakiwatamanisha watu kuja halafu wanawafungia milango wasiingie.Thats why huwezi ona utajiri wa kina mengi, sabodo na wengine ukileta chuki.Ila huo wenu wa fujo na vurugu mnazozionyesha hapo juu zinapolarize watu.

  Sijui anajisikiaje mtu aliyetengeza hela kama mengi halafu akaingia katika siasa na kutengeneza hela km hiyo kwa mwaka mmoja?Pengine wanasiasa ni wapuuzi sana kutojua hela kama hiyo haina pride kama ilivyo kwa mtu aliyempata binti akiwa amelewa?
   
 6. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Hongera kwa makala nzuri mh zzk, wakati naisoma nimefika katikati ghafla ikanijia akilini ile kauli aliyoitoa mh rais wetu JK, KUWA" UKITAKA KUJUA UMASKINI TZ UMEPUNGUA,BASI KAANGALIE WINGI WA MAGARI NA FOLENI BARABARANI!"
  kauli hii imenipandisha hasira ghafla na kushindwa kuendelea kusoma!
  naahidi kumalizia kuisoma yote na kuchangia, baada ya muda mfupi, ngoja hasira zipungue kwanza!
   
 7. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Zitto,
  Good observation ingawaje hamna kipya ambacho hakijapata kuongewa huko nyuma. Tuchelee kuishia kuona matatizo na kutoa suluhisho za juu juu. Kwamba, miundombinu; hususani barabrara na reli ni nguzo muhimu ni jambo lisilo shaka toka hata kwa mtu mwenye uelewa mdogo.....issue, ni namna gani basi tunaweza kujenga hiyo miundo mbinu, na hapa nikizungumzia vyanzo mbadala vya mapato.

  Mifano ni mingi.

  Si hivyo tu, hakuna shaka kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu lakini, je Watanzania hao wa vijijini wanakichukulia vipi kama njia kuu ya uchumi?! Ni ukweli ulio wazi kwamba mamilioni ya Watanzania tunakichukulia kilimo kama sekta ya wale wasio na shughuli mbadala ya kiuchumi na ndio maana sio ajabu kuona mtu analima na pale anapopata visenti kiduchu, anaamua kujiingiza kwenye uchuuzi na kuachana na kilimo! In short, kutokana na nchi hii kutopata kuwa na mikakati endelevu juu ya kiuchumi, basi sekta hiyo muhimu inaonekana ni ya wale wasio na ajira!
  ni
  Tatizo la msingi ninaloliona hapa ni kilimo chetu kukosa nguvu kazi itakayojitoa kwenye shughuli hiyo....yaani commited work force. Endapo kilimo kingepatiwa commited workforce, basi sina shaka kilimo kingekuwa ni injini ya maendeleo yetu.

  Leo hii ningekuwa kwenye maamuzi basi ningekitengenezea kilimo a commited work force kwa kuanzisha Jeshi La Maendeleo ya Kilimo Nchini ambalo labda ningeliita Agricultural Development Army; ama ADA ukipenda. ADA, lingekuwa ni jeshi sawa na jeshi lingine lolote lile nchini huku likiwa na stahili na stahiki zote za kijeshi kuanzia katika kuajiri hadi maslahi. Tofauti na majeshi mengine, ADA lingekuwa ni jeshi ambalo waajiriwa wake ni vijana wenye elimu mbalimbali, hadi wale wa darasa la saba.....hawa wangekuwa ndio nguvukazi haswa ya ADA! Jeshi kama JKT ningevunja na wale wenye umri mkubwa wangeamishiwa kwenye majeshi mengine na wale wasio na utaalamu wowote(vijana) pamoja na wale wenye taaluma za kilimo wangehamishiwa ADA.

  Kwavile nchi yetu ni kubwa, basi ingegawanywa kwa kanda maalumu za kilimo; lakini kanda hizo hazitaangalia mipaka iliyopo hivi sasa bali ingeangalia sura ya nchi. Katika hili, sehemu kama za Kilombero, Rufiji, Kyela na zingine kama hizo zingekuwa katika kanda moja ya uzalishaji wa mpunga na kambi za ADA zingekuwa huko ili ku-boost kilimo cha mpunga. Sehemu kama Mbeya, Iringa, Kigoma na zingine kama hizo zingeweza kuwa kwenye kanda moja ya uzalishaji wa mahindi na kambi za ADA zingekuwa huko ktk ku-boost kilimo cha mahindi. Hali kama hiyo ingekuwa kwa mazao mengine pia hususani yale ya biashara na chakula kinachotumika sana ukanda wa Afrika Masharki na Maziwa Makuu. Kwa kuanzia, tungejikita kwenye mazao ya nafaka na mikunde mikunde na baadhi ya mazao ya biashara husasani korosho, pamba na kahawa.

  Kwavile nyingi ya kambi hizi zingekuwa vijijini na kwa kuwa hata darasa la saba wangekuwa na sifa ya kuajiriwa na ADA provided wana afya njema; basi tatizo la msingi la ukosefu wa ajira hususani vijijini lingepungua. Aidha, kwa kuwa hivi sasa kilimo kingekuwa kimepatiwa commited work force, basi uzalishaji wetu ungeongezeka kwa kiasi kikubwa. Katika situation kama hii, mazao kama mahindi na mpunga yasingekuwa tena ni mazao ya chakula bali yangekuwa ni ya biashara hasa ukiziangatia kwamba ukanda wa Afrika ya Mashariki na ule wa Maziwa Makuu ni ukanda ambao mara kwa mara umekuwa ukikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula. Hii ingekuwa ni fursa kubwa ya kuuza chakula nje ya nchi na hivyo kuiongezea nchi fedha za kigeni.

  Aidha, kwa kuwa mfumuko wa bei hapa nchini unachangiwa sana na uongezekaji wa bei ya vyakula; uongezekaji wa chakula ungepunguza kwa kiasi kikubwa mfumuko wa bei na badala yake chanzo kikuu kingebaki tu kwa nishati.

  Kwenye upande wa mazao ya biashara tungeanza kwanza kuyapa kipaumbele korosho na pamba. Hata hivyo,lengo hapa liseingekuwa kusafirisha mazao hayo nje ya nchi yakiwa ghafi; la hasha. Hakuna asiyejua jinsi sekta ya nguo ilivyo mwajiri mkubwa duniani. Hivyo basi, nchi ingeandaa mpango wa kuboresha sekta ya nguo kwakutumia pamba ilimwayo nchini. Hapa pangepaswa kuwapo viwanda vyenye uwezo wa kubuni na kutengeneza nguo zenye ubora wa hali ya juu na za kila aina na sio tu kanga na vitenge! Tungewekeza vya kutosha kwenye sekta ya ufumaji ambapo tungeweza kutengeneza vitambaa vyenye ubora mbali mbali ambavyo vingetumika kutengeneza aina zote za nguo; kuanzia za kike hadi za kiume na zenye ubora wa hali ya juu!

  Wafanyakazi wa serikali na taasisi zake wanakaribia laki nne na wataendelea kuongezeka! Hapa sheria ingepitishwa kwamba ni marufuku kwa mfanyakazi yeyote wa serikali kuvaa nguo kutoka nje ya nchi anapokuwa ofisini! Hii maana yake ni nini? Sekta ya nguo tayari ingekuwa na wateja wasiopungua laki nne kutoka serikalini. Na kwa kuwa sekta hii ingekuwa imeboreshwa na kuzalisha nguo zilizo na kiwangu cha juu basi pasingekuwa na wa kulalamika. Likewise, kwavile nguo zingekuwa zinalishwa kwa wingi na kwa kutumia malighafi zetu wenyewe; basi hapo tunge-enjoy economies of scale na uniti cost ingekuwa ndogo na hivyo kuzifanya hata nguzo zinazozalishwa zisiwe za bei ghali.

  Kwa mara nyingine, mkakati huo nao ungeongeza sana ajira kwa Watanzania wa kawaida simply becasue mara nyingi textle industry inaajiri sana hata wale wasio na elimu kubwa. Aidha, mkakati huo ungeokoa miilions of dollars ambazo zinatumika kuagiza nguo nje ya nchi wakati mwingine nguo zenyewe zikiwa na ubora dhaifu. Na kwa vile uzalishaji huu ungekuwa in large scale, sina shaka Tanzania ingebadilika kutoka kuwa mwagizaji wa nguo na kuwa msafirishaji wa bidhaa hiyo na hivyo kuingozea nchi fedha za kigeni!

  Viwanda vya korosho navyo ni aina nyingine ya viwanda ambazo huwa vinaajiri watu wengi sana sawa na textile industries. Hivyo, endapo huko nako tukiwekeza vya kutosha kwa kujenga viwanda vya kubangua korosho basi kwa mara nyingine sekta hiyo nayo ingepunguza sana ukosefu wa ajira hadi kwa wale wasio na elimu ya kutosha.


  yapo mengi ya kufanya, lakini wacha tu niishie hapa na tujaribu kujiuliza ni wapi tunaweza kupata fedha za kufanya mambo yote hayo hususani pale wakati wa kuanzisha program hizo. Generally speaking, between 15-20% ya fedha za bajeti zinapotea hivi hivi! Hivyo basi, tunaweza kuanzia kuibana hiyo hiyo bajeti kwa ku-introduce kitu ambacho tunaweza kukiita Savings Before Budget Scheme. Ninachomaanisha hapa ni kwamba, tunaweza kutenga angalau 10% ya mapato ghafi ya kila mwezi ya TRA na kisha kuyaweka kwenye mfuko maalumu na 90% itakayobaki ndiyo itaenda kwenye mzunguko wake wa kawaida. Kwavile kwa wastani makusanyo ya TRA ni kama 500bn, basi mfuko huo utakuwa unaingiziwa si pungufu ya 50bn kila mwezi na hivyo kuwa na karibu 600bn kwa mwaka ambazo zitaingia kwenye mpango huo wa makusudi.
   
 8. Root

  Root JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,853
  Trophy Points: 280
  Zitto I salute the analysis
  Najua ipo siku tutafika huko tupatakapo ila tusipokuwa makini tutafika tukiwa tumechoka sana
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Katika moja ya masimulizi ya kale yenye kuelezea mageuzi ya china toka kwenye lindi la ujamaa mufu mpaka ujamaa wa kimapinduzi ya kiuchumi, Masimulizi yaliyo kwenye makumbusho ya Szechuan yanasomeka kuwa ni matajiri 8 tu ndio walioibadili China mpaka kuja ilipo sasa.

  Najiuliza swali lakini linakosa majibu, je ni taifa gani lililoendelea bila mabilionea? bila mafisadi? bila mamafia wa ukwasi? bila WEZI?

  Mimi naamini tatizo ni mfumo wa hawa wakwasi ndio unaoliyumbisha taifa, ni vigumu kuwaondoa lakini tunaweza kupunguza spidi yao na kuwaambia wabadili mfumo wao wa ukwasi.

  Mfano nchi ya Marekani mabebari hawa wanapiga sana hela nje ya nchi na wanalipa kodi kwa wingi ndani ya nchi yao. vivyo hivyo ufaransa, Urusi, Uchina, Uingereza na Japan

  Lakini Tanzania ni matajiri wangapi biashara zao ni halali na wanalipa kodi stahiki??????
   
 10. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  You're right kwamba hakuna nchi inayoendelea pasipo na mabilionea(mafisadi?) Tatizo lililopo nchini kwetu ni aina ya mabilionea/mafisadi tulionao! Mafisadi wengi tulionao ni ama wanasiasa au watendaji serikalini na taasisi zake. Hawa, wengi wao si wajasiliamali na matokeo yake mapesa wanayokwapua hayaingii kwenye shughuli za uzalishaji ama uchumi endelevu ambazo zingetengeneza ajira kwa walio wengi. Kwavile ni wanasiasa wasio na weledi wa biashara, unakuta wengi wao wanaishia kuficha mabilioni waliyokwapua kwenye akaunti za benki nje ya nchi na wengine kuishia kuwekeza kwenye maeneo yasiyo ya uzalishaji.....kama vile kununua majumba na viwanja kila sehemu! Na hata wale wanasiasa wenye weledi na biashara bado hawawezi kuwa na ujasiri wa kuwekeza nchini kwani mwanasiasa mara zote angependa aonekane safi na kuwekeza nchini kunaweza kuzalisha maswali ya wapi alikopata mtaji wa biashara anayofanya!
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  well said.Hela zao za wizi si mtaji wakujenga uchumi mkubwa,kwa taifa au hata kwao wenyewe,kwani kwa kuongeza faida ni kuiba nyingine.Ndio maana hata wamachinga wanaofikiria kupata 3mil tuu wabadilishe biashara yao kuwa multibillion business wanapata shida kuelewa elimu inatengeneza watu gani?Au inafundisha nini?
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  China kama wan apropaganda wengine wa kijamaa hawawezi sema ukweli,ila wamefaidi sana mabilionea wa Hong Kong, Macau, na Taiwan.Wao kama wao wamepata mabilionea karibuni sana,baada ya economic boom.Na wasipokuwa karibu na serikali hali yao huwa ngumu sana.wengine walipatia ktik hizo nchi ambazo sasa zipo chini ya China.Huku mashirika yao ya kitaifa ndio yananunua makampuni ya nje, kuchukua tender za ujenzi etc,yote haya yanakuwa subsidized by the Gov.
   
 13. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Zitto nakushukuru kwa Uzalendo wako wa hali ya juu unaoonyesha na kazi nzuri unayoifanya Tanzania kama kijana. Mimi nilisoma Galanos A-Level mwaka mmoja 1994-1995 kabla ya kwenda Tambaza kumalizia masomo. Kwa sasa naishi Texas kwa miaka kumi na tano sasa!!.

  Pamoja na hoja yako nzuri kwa sisi hasa tunaoishi nje tunaona tofauti kidogo kwenye swala la Tatizo la Tanzania. Matatizo ni Mfumo, Sheria, Elimu, Bank na Tabia. Sitasema yote leo. Mfumo ni muhimu sana mimi siamini kama serikali tofauti itaweza kukomesha rushwa au hata kuleta maendeleo kama huta badilisha hayo hapo Mafano kwasababu Tanzania haina sheria ya kuzuia serikali kujiingiza kwenye shughuliza biashara kila kiongozi mpya toka wakati wa Mwinyi anakuja na miradi mipya serikali ya Tanzania ina lipa walimu wote, madaktari karibu wote, wanajeshi, magereza , polisi, wafanyakazi wote wa serikali, wabunge wote wa bara na visiwani, Tanesco, ATC, bandari n.k huwezi kuwa na serikali kubwa hivi bila kuwa na rushwa au udikteta. Nime post baadhi ya topic zangu za nyuma naomba musome kwanza

  Class 102: Hatuwezi kuendelea bila kuchagua mfumo wa kufuata!

  Naona hii topic ni muhimu sana kuliko watu wanavyofikiria naomba nitoe some tena!

  Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?

  1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu

  2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la

  3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.

  Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze.

  Mfano niliotoa ya jinsi gani kurekebisha system ya bank kuleta maendeleo Tanzania
  Kamundu Class 101: Bank ni kikwazo cha Maendeleo Tanzania je tufanye nini kurekebisha?

  Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.

  Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo
  1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
  2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
  3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%. Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.

  Mfano:Niliwahi kutoa wa jinsi ya kutatua matatizo ya mfumo.
  Ukweli: Matatizo ya Madaktari na Walimu hayawezi kutatuliwa bila kubadilisha Mfumo

  Watanzania wenzangu ukweli unauma lakini hapa JF tunaambiana ukweli wa wazi.

  Serikali haina uwezo wa kutatua tatizo la Madaktari na Walimu bila kubadilisha mfumo kwasababu serikali kwa mfumo wa sasa haiwezi kuwa na uwezo wa kuwalipa mishahara na marupurupu mazuri Madaktari wote nchini na walimu wote nchini. Ni lazima tuelewe pesa yeyote serikali inayotumia ni lazima itoke mahali fulani na kwenye fungu fulani la Budget ya nchi. Je ni sehemu gani tunataka Budget ipunguzwe na itoshe kuwalipa zaidi walimu wote na madaktari wote?kama hatuna jibu tunategemea watalipwaje?. Mimi hapa chini nitaeleza ni jinsi gani mabadiliko ya mfumo yanaweza kusaidia kutatutua Matataizo ya madaktari. Nitaelezea Mfumo wa Afya kama mfano:

  Mfumo wa sasa:
  Mfumo wa sasa wa Afya Tanzania umetoka kwenye nchi za Ulaya. Ulaya kwasababu ya Nchi zao kuwa ndogo wana barabara ndogo, Vyuo vinakuwa kwenye eneo moja, Hospitali zinakuwa kubwa "Medical Center" kwasababu Ulaya hawana nafasi ya kuwa na Medical Center kama Muhimbili au KCMC nyingi kwasababu ya maeneo. Maisha ya Ulaya kila kitu ni kidogo hata magari ni kwasababu ya udogo wa maeneo yao. Nchi za Ulaya zilivyokuja kutawala Africa zilianzisha huu mfumo ambao wanautumia kwao kwenye nchi za Africa na ndiyo mfumo tulionao hadi sasa.

  Tatizo la Huu Mfumo ni nini
  Tatizo la huu mfumo ni kwamba (1)Tanzania sio Ulaya ni kubwa sana hivyo hatuna na hatutakuwa na uwezo wa kujenga Medical Center kila mahali (2) Watu wanaishi mbali mbali hivyo ni vigumu kuwa na mfumo wa Medical Center kama ulioko Tanzania (3) Barabara, Maji na Umeme Tanzania kwasababu ya umasikini na ukubwa sehemu nyingi hazina barabara za uhakika, maji ya uhakika wala umeme wa uhakika hivyo ni vigumu kutoa huduma za Afya kwenye maeneo hasa ya vijijini. Kwa ujumla huu mfumo wa Ulaya hauwezi kufanya vizuri Tanzania kwasababu Tanzania inatatizo tofauti na ulaya.

  Suluhisho ni nini:

  1. Mobile Medical Service:
  Mtanisamehe kwa lugha sijapata jina halisi kwa kiswahili lakini Tanzania inatakiwa kuwa na Hospitali ambazo zinatembea kwenye magari kama zinazotumika kwenye Majeshi ya Marekani na Canada hii itasaidia (1) Kutoa Chanjo na huduma nchi nzima (2) Kutumia madaktari wachache kwasababu wanakuwa kwenye magari na wanatembea vijiji hadi vjiji (3) Inapunguza msongamano wa watu kuja kwenye hospitali za mkoa au rufaa (4) Hakuna sababu ya kuwa na Medical Center kila mahali
  2. Hakuna Haja ya kujenga Medical Center na Hospitali nyingi
  Kwasababu ambazo nimeshazisema Tanzania haina haja ya kujenga hospitali kila mahali kwani pesa ya majengo ambayo tunayaita hospitali bila vifaa wala wataalamu tungeweza kutumia kuongeza mishahara madaktari na vilevile kuhudumisha Mobile Medical Center nchi nzima.

  3. Uhusiano wa vyuo vikuu vya Afya
  Tanzania iweke utaratibu na vyuo vingine duniani kuweza kuleta wanafunzi wao kufanya Practical Tanzania. Madaktari kabla hawajapewa vibali wanafanya kazi miaka miwili bila malipo na wenye wanalipa wenyewe ili waweze kujifunza namna ya kufanya matibabu mbalimbali. Bugando mfano walikuwa na program kama hii na vyuo fulani nafikiri vya marekani. Hawa madaktari wanatakiwa waende vijijini na vilevile gharama za shule walipe wizara na wizara itumie pesa hiyo kuongeza mishahara kwa walimu, kununua vifaa na kufanya huduma nyingine za elimu. Tanzania inaweza kupata pesa nyingi sana za wanafunzi wa udaktari kutoka nchi za nje.

  Hospitali bado zitakuwepo lakini ukufuta ushauri wangu huduma zitaongezeka, gharama zitaenda sehu muhimu na madaktari watalipwa zaidi kwani gharama za ujenzi zinaweza kutumika kwenye mishahara.
   
 14. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kuwa toka kuondoka kwa Mwalimu Nyerere hakuna juhudi zozote za makusudi ambazo zimefanywa kumkomboa mwananchi wa kawaida hasa yule anayepatikana kijijini.Miradi mingi tunayoiona ukianza na ile iliyo chini ya NGOs, TASAF, MKUKUKTA I, II & III, Kilimo Kwanza nk. haijikiti katika kumjengea uwezo maskini wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba, hailengi moja moja kumfanya mwananchi abadili maisha yake kwa kumuongezea kipato na uwezo wa kumudu gharama za maisha ya kila siku.

  Mathalan, unaweza ukarasimisha ardhi za Vijiji na hata kutoa zile hati za kimila za ardhi lakini Mkulima wa kawaida kule Mbinga hati hizi zitamsaidia nini? Akitaka mkpo ataupata kupitia benki ipi? Na je thamani ya ardhi hiyo huko kijijini itampa mkpo kiasi gani? Iko sawa na ile ya Mjini? Jipu ni Hapana.

  Lakini pia mradi huu wa TASAF una vituko vyake. Kwa mfano, unawajengea wananchi Zahanati swali ni je watawezaje kumudu gharama za matibabu ili hali ni fukara wa kutupwa? Fedha za kulipia gharama za matibabu watazitoa wapi? Ni kwa vipi Zahanati hii itabadili maisha yao? Ni ngumu sana. Maana kusambaza huduma nyingi vijijini ni jambo moja lakini kuwafanya wanakijiji hawa kuweza kupata huduma hizo ni jambo jingine.

  Mwalimu aliamini Kilimo na ufugaji ndiyo njia pekee itakayomkomboa Mwananchi maskini na kwa kweli alikiwekea mikakati kuanzia kusambaza maafisa ugani vijijini, kuanzisha Benki ya Wanakijiji (CRDB), kujenga viwanda mbavyo si tu vilikuwa soko kubwa la mazao ya kilimo bali pia vilizalisha ajira nyingi kwa vijana wengi na kubwa kuliko alianzisha vyama vya Ushirika ambavyo vilikuwa mkombozi mkubwa wa Wakulima.

  Sasa haya yote Serikali zote za CCM zilizofuata zimeshindwa kuyaendeleza, Viwanda kama Urafiki, Sunguratex, Tanganyika Packers nk. vimekufa na hata, vyama vya Ushirika almost vyote viko taabani kabisa.

  Njia moja ambayo naiona ni ya kipuuzi sana ambayo kwa sasa inaimbwa na kila mtawala ni Unzishaji wa KILIMO KWA KWANZA. Toka wimbo huu umeanza kwa kweli hakuna tija yoyote iliyopatikana. Wakulima wa pamba wanalia, wakulima wa korosho wanalia, wale wa Tumbaku ndiyo usiseme kabisa na hata janga la njaa bado limeendelea kutunyemelea. Hapa kuna matatizo makubwa katika sera hii ya Kilimo kwanza;

  1. Imejikita katika kusambaza pembejeo na mbolea kwa wakulima bila kuzingatia uwezo wa wanakijiji kwanza katika kutumia pembejeo hizi na pia kumudu gharama zake.Matokeo yake Matajiri ndiyo wanufaika wa mradi huu huku wakulima wakitupwa kando. Yaani walengwa wa sera ya Kilimo Kwanza wametupwa pembeni.
  2. Ndani ya Kilimo Kwanza kwa akili ya kawaida tungetegemea uimarishaji wa masoko ya mazao ya Kilimo ikiwa ni sambamba ana mikakati ya kufufua viwanda vinavyofukiwa kaburini sasa lakini hakuna lolote. Hauwezi kuimba chorus za Kilimo Kwanza wakati hujalijengea mguvu soko la ndani la Mazao ya kilimo na hata soko la kimataifa lenyewe. Njia moja ya kujenga soko la ndani ni kupitia kuimarisha sekta ya Viwada. For Agricultural sector to grow steadily there must be Agra-industrial linkages otherwise ni kutwanga maji kwenye kinu.
  3. Kwa sasa tungetegema kule kijijini watu wanapakimbilia kwa kasi kutokana na kilimo kuwa chenye tija lakini pia hali ya maisha kuimarika kutokana na pato la mkulima kukua lakini wapi. Hali ni tofauti.Vijiji bado ni jehanamu na watu wengi wazee kwa vijana wameendelea kuvikimbia kutokana na sababu mbalimbali. Jambo moja la kupima tija ya Sekta ya Kilimo ni mabadiliko katika maisha ya Wakulima vijijini kitu ambacho ni ndoto toka aondoke Mwalimu.

  Ninachokiona kwa sasa hapa nchini ni kuwepo kwa nchi mbili katika taifa moja. Tuna nchi ambayo inaitwa MJINI yenye Barabara nzuri, huduma zote za afya ziko safi, madaraja ya kiwango cha juu yanajengwa, flying overs zinajengwa, mabasi yaendayo kasi yanakuja, umeme upo hadi chooni. Kwa ujumla hii ina kila kitu maana hata Bajeti karibu yote ya Serikali inakombwa na na nchi hii ya MJINI.

  Lakini sasa tuna nchi nyingine ya KIJIJINI ambayo ni jehanamu. Maisha ni magumu kupindukia, hakuna huduma zozote za msingi za jamii,miundod mbinu ni mibovu kuoindukia, umeme wao ni vizinga vya moto, chakula chao ni cha kubahatisha, mavazi yao yamejaa viraka matakoni.Kwa kweli nchii imekosa matumaini, mbele ni giza na nyuma ni giza.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Bila kuwa na masikini utakuwa na matajiri?
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mleta mada hajui maana ya ufukara na umaskini ki undani. Umaskini na ufukara ni vitu tofauti kwa maana tofauti.

  Masikini ni yule wa kuonewa huruma, yamemkuta tu na si kwa kupenda au kujitakia. Mfano kudhulumiwa, kuumwa, kuwa na maradhi au ulema unaokufanya ushindwe kujituma. Unaweza ukawa tajiri lakini ukajikuta kwenye shida inayokufanya uitwe maskini (wa kuonewa huruma).

  Mfano mtu ajulikanae ni tajiri kama Mengi au Bakhresa leo aumwe hoi kitandani, hawezi kujisaidia mpaka kwa msaada wa mwengine basi huyo ni maskini ingawa ana utajiri.

  Mfano leo wewe unapita na vogue lako, likapata pancha njiani, hujui hata namna ya kufunguwa tairi ukaomba msaada (hata kwa kulipia) basi u maskini wako ndio huo na umehitaji msaada kwa wakati huo.

  Ufukara ni wa kujitakia au ni sifa ya watu wa aina fulani wasiojuwa thamani ya fedha au mali. Kujilimbikizia mali na vitu vya anasa za kidunia kwao haipo kabisa, wanapopata mali au fursa ya kuwa na mali, wao haina maana kwao wala haiwabadili maisha yao na hauwakuti kuomba wala kutafuta msaada, ukiwapa hawakatai, hufurahi lakini hukitoa unachowapa kwa wengine wanaoona kuwa kitawafaa zaidi. Ukimuona fukara anatafuta mali au fedha basi ujuwe hizo si kwa ajili yake, ameshaona kuna mahali akiipeleka hiyo mali kitawanufaisha zaidi.

  Mfano mzuri wa Fakiri ni Rais Ahmedinajad wa Iran.

  Mfano mzuri wa maskini ni kama ilivyokuwa kwa Gaddafi (alipokosa msaada na utajiri wake) na Hosni Mubarak (alipokuwa hawezi hata kujisaidia na utajiri wake) au Nyerere (alipoumwa na akawa wa kusaidiwa). Hao wote kwa wakati fulani walikuwa maskini wa kuonewa huruma.

  Ufukara (verb), Fakiri (noun).

  Kuwa Fakiri ni sifa njema kabisa.

  Sioni tatizo la Utajiri, umaskini na ufukara kuwa ni la kuumiza kichwa, ni vitu tu vilivyojengwa na mifumo ya kidunia ili kuwatia watu hofu na chuki.

  Tajiri ana umaskini wake wa aina fulani.
  Fukara ana utajiri wake wa aina fulani.
  Maskini haina maana hana utajiri.

  Tanzania, kama nchi yoyote nyingine duniani kuna Utajiri, Umaskini na Ufukara.

  Nitajie ni nchi ipi haina hivyo.
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  pamoja na kuwa mie sio shabiki wa chama chochote...lakini ili tanzania ipige hatua system nzima inabidi iondoke,
  utawala wa ccm na sera zake zilizoshindwa ziende....
  Sasa hivi tanzania haina viongozi imejaa watawala... Naam kuna watawala na si viongozi.... Watawala wanaowaza matumbo yao na ya wajukuu wao na si kuwazia watanzania kwa ujumla....

  Nchi inayotegemea kodi za beer na mishahara ya wafanyakazi wakati kuna rasilimali za kutosha kuendeleza nchi hii....

  Wafanyabiashara wakubwa ndo wakwepaji kodi na loopholes hizo zimefumbiwa macho maana watawala/wanasiasa ndio wafanyabiashara wenyewe......

  Dhahabu toka ianze kuchimbwa imemnufaisha nani? Kama sio watawala na 10% zao?

  Leo mwananchi anapokonywa ardhi anapewa "mwekezaji" kisha anaambiwa mwekezaji atatengeneza aiira, ajira gani? Kwa nini mwananchi asiwezeshwe? Akajiajiri badala ya kuwa manamba?

  Viwanda vyote vimekufa/vimeuzwa kwa wawekezaji je wamewekeza nini? Leo mpaka kitenge kifuatwe china? Eti "chinese wax?" Excuse me please...

  Ranchi si wameuziana wenyewe?

  Hadi nyumba za serikali, ambazo zipo kwenye maeneo muhimu si wameuziana wenyewe?

  Loliondo si iliuzwa kwa mwarabu? Kwa nini pasingeendelezwa wamasai wale wakapata ajira na nchi ikapata pato kutokana na utalii na uwindaji

  bado zengwe la mafuta na gesi.......

  Watawala wa tanzania ndo tatizo wanaona mwisho a pua zao, wanaona mwisho wa familia zao, hawa watawala ndio wa kuondoka...

  Tanzania inahitaji viongozi si watawala.........
  Viongozi wenye maono na wanaofanyia kazi vision zao, sio vision za kwenye makaratasi ambazo hazitekelezwi either kwa makusudi au kwa udhaifu....... Kuna watu huko vijijini anakosa shilingi mia ya kununua chumvi......miaka 50 sasa ya uhuru.......

  Watawala must go..... Tunahitaji tanzania mpya yenye uwajibikaji na si tanzania ya walaji.....
   
 18. p

  pembe JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Umenena baba. Zitto tupatie njia mbadala ya kupita yenye lami isiyokuwa na matuta. Sisi walala heri tujiulize tupambane vipi kugeuza hii hali? Tunaona serikali haina nia ya dhati kupambana na umaskini kwani inategemea sana wafadhili ambao nao wanakuja na masharti yao. Tutokeje MH Zitto? Great thinkers come up. Every achievement begins with desire. if we are determined to remove poverty we brainstorm, it takes time but success will be achieved. Elimu ianze kwanza. elimu ya kujitegemea vingine vyote vitafuata i.e. Afya, makazi, kilimo,miundo mbinu etc. Courage and cooperation also matters a lot so Tanzanians lets wake up and march to prosperity.
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Mabilionea 30, na yeye yumo, halafu kwa ulafi wake kapelekea mafukara 30 kwa kutuuzia miti ya iringa na kudai eti imetokea sauth, halafu madai ya kuwepo mgao wa umeme wakati megawati zipo za kutosha. Fisadi wewe
   
 20. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa wakuu wangu mbona mnaulizia bangi kwenye kituo cha polisi? Tehe Tehe Tehe


  By MD 25
  Tunaishia kusema, kulalamika, kulaumu na kutoa takwimu lakini tumeshindwa kuchukua hatua za ki-vitendo. 'Tanzania yenye mafukara 30m na mabilionea 30m, haikubaliki', hiyo kauli haina mashiko hata kidogo, hizo kauli za 'haikubaliki' ni kauli za kisiasa au kinafiki. Sikia Mr. Zitto, tunachotaka kutoka kwako ni 'way forward', sema hivi jamani wananchi tuingie mitaani ili tuitoe hii serikali, tupe miundombinu ya kuingia mtaani na kuitoa hii serikali. You know what, enough is enough, tumechoka na porojo, matamko maandiko sasa tunataka kuingia mtaani...

  Umenena baba. Zitto tupatie njia mbadala ya kupita yenye lami isiyokuwa na matuta. Sisi walala heri tujiulize tupambane vipi kugeuza hii hali? Tunaona serikali haina nia ya dhati kupambana na umaskini kwani inategemea sana wafadhili ambao nao wanakuja na masharti yao. Tutokeje MH Zitto? Great thinkers come up. Every achievement begins with desire. if we are determined to remove poverty we brainstorm, it takes time but success will be achieved. Elimu ianze kwanza. elimu ya kujitegemea vingine vyote vitafuata i.e. Afya, makazi, kilimo,miundo mbinu etc. Courage and cooperation also matters a lot so Tanzanians lets wake up and march to prosperity.
   
Loading...