Zitto nakushukuru kwa Uzalendo wako wa hali ya juu unaoonyesha na kazi nzuri unayoifanya Tanzania kama kijana. Mimi nilisoma Galanos A-Level mwaka mmoja 1994-1995 kabla ya kwenda Tambaza kumalizia masomo. Kwa sasa naishi Texas kwa miaka kumi na tano sasa!!.
Pamoja na hoja yako nzuri kwa sisi hasa tunaoishi nje tunaona tofauti kidogo kwenye swala la Tatizo la Tanzania. Matatizo ni Mfumo, Sheria, Elimu, Bank na Tabia. Sitasema yote leo. Mfumo ni muhimu sana mimi siamini kama serikali tofauti itaweza kukomesha rushwa au hata kuleta maendeleo kama huta badilisha hayo hapo Mafano kwasababu Tanzania haina sheria ya kuzuia serikali kujiingiza kwenye shughuliza biashara kila kiongozi mpya toka wakati wa Mwinyi anakuja na miradi mipya serikali ya Tanzania ina lipa walimu wote, madaktari karibu wote, wanajeshi, magereza , polisi, wafanyakazi wote wa serikali, wabunge wote wa bara na visiwani, Tanesco, ATC, bandari n.k huwezi kuwa na serikali kubwa hivi bila kuwa na rushwa au udikteta. Nime post baadhi ya topic zangu za nyuma naomba musome kwanza
Class 102: Hatuwezi kuendelea bila kuchagua mfumo wa kufuata!
Naona hii topic ni muhimu sana kuliko watu wanavyofikiria naomba nitoe some tena!
Watanzania tumechukua utamaduni wa waingereza wa kupenda kulalamikia kila kitu. Mara nyingi tunapenda kutumia maneno kama wao, wale kuimanisha sio mimi. Ukweli ni kwamba nchi hazibadilishwi na viongozi pekee bali wanannchi ndiyo wanaotaka maendeleo na viongozi wazuri wanafuata matakwa ya wananchi. Ni lazima Tanzania tujibu maswali yafuatayo kama kweli tunataka mabadiliko. Je ni nchi gani tunaitaka?
1. Mfumo kama wa Marekani: Mfumo wa Marekani ni kwamba serikali kwenye katiba inatakiwa kufanya vitu tu ambavyo watu hawawezi kufanya wenyewe!. Jeshi, Barabara, mifumo tu kwenye elimu, Afya, kodi, madeni ya nchi,uhamiaji, usalama wa anga,usalama wa airports, polisi, Fire, uangalizi wa maji safi, hewa safi na kutoa vibali vya hifadhi za uchimbaji wa mafuta na kulinda hifathi za wanyama vilevile wana mahakama huru. Serikali ni ya vyama vingi na kuna ushindani wa haki. Serikali haijihusishi kwenye biashara. Kwenye Mfumo huu huwezi kusingizia au kutegemea serikali ifanye kila kitu na huwezi kulalamikia serikali kwenye kila kitu
2. Mfumo wa China: Serikali ndiyo inatoa madaraka yote na ni mfumo wa chama kimoja. Uhuru wa habari unachujwa na serikali inafanya biashara kama kampuni za ujenzi, usafirishaji, ndege, banks, shule, hospitali, ni za serikali. serikali inajihusisha na ulinzi wa nchi, mahakama. Kwenye mfumo huu faida zake ni kwamba utekelezaji wa agenda ni mrahisi lakini kama agenda na viongozi ni wa zuri. Kama agenda na viongozi ni wa baya wananchi hawana jinsi ya kuwabadilisha viongozi kwasababu hakuna demokrasia ya vyama vingi. Hakuna demokrasia ya huru ya vyombo vya habari. Mfumo huu kama tunautaka inabidi tuwape uwezo serikali na sisi wananchi tufuate wanachofanya na kuwaamini kwamba wanachofanya ni sahii na ni kwa manufaa ya nchi. China haina mchanganyiko wa utamaduni kama Tanzania hivyo inaweza ikawa ngumu na vilevile tunapenda sana demokrasia. hivyo mimi sijui kwenye hii system kama itawezekana au la
3. Mfumo wa Rwanda: Mfumo wa Rwanda unafanana na wa China lakini tofauti ni kwamba China nguvu iko kwenye chama na Rwanda nguvu iko kwenye uraisi wa nchi. Hatuwezi kuwa na mfumo huu na kuwa na demokrasia wakati huohuo! hatuwezi kutaka na kupata vyote!. Huu mfumo ni kwa raisi kama una raisi mzuri nchi inaweza kwenda kwa kasi lakini kama unaraisi mbaya nchi inaweza kwenda chini kirahisi.
Mimi kwa mawazo yangu Watanzania tunajichanganya tunataka demokrasia ya Marekani lakini mfumo wa China na hii haitawezekana. Je Watanzania wenzangu ni lazima tufanye uamuzi na kama unamawazo ya system nyingine tueleze.
Mfano niliotoa ya jinsi gani kurekebisha system ya bank kuleta maendeleo Tanzania
Kamundu Class 101: Bank ni kikwazo cha Maendeleo Tanzania je tufanye nini kurekebisha?
Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.
Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo
1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%. Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.
Mfano:Niliwahi kutoa wa jinsi ya kutatua matatizo ya mfumo.
Ukweli: Matatizo ya Madaktari na Walimu hayawezi kutatuliwa bila kubadilisha Mfumo
Watanzania wenzangu ukweli unauma lakini hapa JF tunaambiana ukweli wa wazi.
Serikali haina uwezo wa kutatua tatizo la Madaktari na Walimu bila kubadilisha mfumo kwasababu serikali kwa mfumo wa sasa haiwezi kuwa na uwezo wa kuwalipa mishahara na marupurupu mazuri Madaktari wote nchini na walimu wote nchini. Ni lazima tuelewe pesa yeyote serikali inayotumia ni lazima itoke mahali fulani na kwenye fungu fulani la Budget ya nchi. Je ni sehemu gani tunataka Budget ipunguzwe na itoshe kuwalipa zaidi walimu wote na madaktari wote?kama hatuna jibu tunategemea watalipwaje?. Mimi hapa chini nitaeleza ni jinsi gani mabadiliko ya mfumo yanaweza kusaidia kutatutua Matataizo ya madaktari. Nitaelezea Mfumo wa Afya kama mfano:
Mfumo wa sasa:
Mfumo wa sasa wa Afya Tanzania umetoka kwenye nchi za Ulaya. Ulaya kwasababu ya Nchi zao kuwa ndogo wana barabara ndogo, Vyuo vinakuwa kwenye eneo moja, Hospitali zinakuwa kubwa "Medical Center" kwasababu Ulaya hawana nafasi ya kuwa na Medical Center kama Muhimbili au KCMC nyingi kwasababu ya maeneo. Maisha ya Ulaya kila kitu ni kidogo hata magari ni kwasababu ya udogo wa maeneo yao. Nchi za Ulaya zilivyokuja kutawala Africa zilianzisha huu mfumo ambao wanautumia kwao kwenye nchi za Africa na ndiyo mfumo tulionao hadi sasa.
Tatizo la Huu Mfumo ni nini
Tatizo la huu mfumo ni kwamba (1)Tanzania sio Ulaya ni kubwa sana hivyo hatuna na hatutakuwa na uwezo wa kujenga Medical Center kila mahali (2) Watu wanaishi mbali mbali hivyo ni vigumu kuwa na mfumo wa Medical Center kama ulioko Tanzania (3) Barabara, Maji na Umeme Tanzania kwasababu ya umasikini na ukubwa sehemu nyingi hazina barabara za uhakika, maji ya uhakika wala umeme wa uhakika hivyo ni vigumu kutoa huduma za Afya kwenye maeneo hasa ya vijijini. Kwa ujumla huu mfumo wa Ulaya hauwezi kufanya vizuri Tanzania kwasababu Tanzania inatatizo tofauti na ulaya.
Suluhisho ni nini:
1. Mobile Medical Service:
Mtanisamehe kwa lugha sijapata jina halisi kwa kiswahili lakini Tanzania inatakiwa kuwa na Hospitali ambazo zinatembea kwenye magari kama zinazotumika kwenye Majeshi ya Marekani na Canada hii itasaidia (1) Kutoa Chanjo na huduma nchi nzima (2) Kutumia madaktari wachache kwasababu wanakuwa kwenye magari na wanatembea vijiji hadi vjiji (3) Inapunguza msongamano wa watu kuja kwenye hospitali za mkoa au rufaa (4) Hakuna sababu ya kuwa na Medical Center kila mahali
2. Hakuna Haja ya kujenga Medical Center na Hospitali nyingi
Kwasababu ambazo nimeshazisema Tanzania haina haja ya kujenga hospitali kila mahali kwani pesa ya majengo ambayo tunayaita hospitali bila vifaa wala wataalamu tungeweza kutumia kuongeza mishahara madaktari na vilevile kuhudumisha Mobile Medical Center nchi nzima.
3. Uhusiano wa vyuo vikuu vya Afya
Tanzania iweke utaratibu na vyuo vingine duniani kuweza kuleta wanafunzi wao kufanya Practical Tanzania. Madaktari kabla hawajapewa vibali wanafanya kazi miaka miwili bila malipo na wenye wanalipa wenyewe ili waweze kujifunza namna ya kufanya matibabu mbalimbali. Bugando mfano walikuwa na program kama hii na vyuo fulani nafikiri vya marekani. Hawa madaktari wanatakiwa waende vijijini na vilevile gharama za shule walipe wizara na wizara itumie pesa hiyo kuongeza mishahara kwa walimu, kununua vifaa na kufanya huduma nyingine za elimu. Tanzania inaweza kupata pesa nyingi sana za wanafunzi wa udaktari kutoka nchi za nje.
Hospitali bado zitakuwepo lakini ukufuta ushauri wangu huduma zitaongezeka, gharama zitaenda sehu muhimu na madaktari watalipwa zaidi kwani gharama za ujenzi zinaweza kutumika kwenye mishahara.