Mafukara milioni 30, Mabilionea 30

Tuambie, mbona tangu Mhando kupumzishwa hujaja na kauli, Tanzania kuingia gizani? na kumbuka mvua hazinyasha kwa muda sasa lakini megawati zipo za kutosha.
 
Mabilionea 30, na yeye yumo, halafu kwa ulafi wake kapelekea mafukara 30 kwa kutuuzia miti ya iringa na kudai eti imetokea sauth, halafu madai ya kuwepo mgao wa umeme wakati megawati zipo za kutosha. Fisadi wewe

Mkuu Tupe ushahidi au source ya habari Kama na yeye Yuko kwenye list please? Mimi najua Dogo ni ka millionear wewe unasema nili billionear which is what?? Zitto nili kwambia hapo juu watu Wana maswali mengi wanahitaji majibu kutoka kwako na ndio kilichojitokeza embu mjibu Huyu bwana kanusha au kiri tuhuma
 
Zitto,

Wewe ni mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma kwa nafasi yako tuambie hadi sasa yapi umeyafanya katika kusaidia jitihada za kupambana na huu umasikini.
 
Watendaji wa serikali,wanasiasa ndo hao wafanyabiashara wa nchi hii,kiasi kikubwa imechangiwa na chama tawala kuwafuata wafanyabiashara na kuwaomba kugombea nafasi za uongozi kama vile udiwani,ubunge nk.

Tenganisha siasa na biashara kwanza halafu tuanzie hapo kuangalia other factors
.
 
Tusikubali kuondolewa kwenye mada kuu kwa habri za kufikirika na kutungwa. Siwezi kujibu tuhuma za kufikirika pia mbazo haziwezi kufikia hata thamani ndogo ya kusadikika.

Sio tu huko ughaibuni, hata hapa nchini akiba zangu zipo benkii za makabwela NMB na CRDB. Akiba zangu zipo wazi kwenye fomu za maadili ya umma. Sina biashara yeyote ya kunifanya kuwa na mabilioni au hata mamilioni.

Wala sitegemei kuwa mfanya biashara maana mimi naamini kabisa kwenye utumishi wa umma na kwamba ukishakuwa mtumishi wa umma na ukafanya biashara lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

Nadhani tujadili mada iliyopo na tusihame mada kwa kuingiza masuala ambayo hayapo tena ya kutungwa tu. Najua wengi humu hamumjui Zitto. Mnaye Zitto wenu kichwani ambaye mnadhani ndio Zitto halisi. Iko siku mtamjua Zitto halisi ambaye hatokani na propaganda za kizushi na zenye mikakati maalumu.

Turudi kwenye mada. Tujadiliane namna ya kupambana na ufisadi ili kukuza maendeleo ya vijijini na hatimaye maendeleo ya nchi. Tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho inazidi kutanuka kutokana na mfumo wa uchumi unaozalisha 'rent seekers' badala ya wazalishaji. Tunatokaje huko? Way forward ni ipi? Mjadala uendelee
.
 
pamoja na kuwa mie sio shabiki wa chama chochote...lakini ili tanzania ipige hatua system nzima inabidi iondoke,
utawala wa ccm na sera zake zilizoshindwa ziende....
Sasa hivi tanzania haina viongozi imejaa watawala... Naam kuna watawala na si viongozi.... Watawala wanaowaza matumbo yao na ya wajukuu wao na si kuwazia watanzania kwa ujumla....

Nchi inayotegemea kodi za beer na mishahara ya wafanyakazi wakati kuna rasilimali za kutosha kuendeleza nchi hii....

Wafanyabiashara wakubwa ndo wakwepaji kodi na loopholes hizo zimefumbiwa macho maana watawala/wanasiasa ndio wafanyabiashara wenyewe......

Dhahabu toka ianze kuchimbwa imemnufaisha nani? Kama sio watawala na 10% zao?

Leo mwananchi anapokonywa ardhi anapewa "mwekezaji" kisha anaambiwa mwekezaji atatengeneza aiira, ajira gani? Kwa nini mwananchi asiwezeshwe? Akajiajiri badala ya kuwa manamba?

Viwanda vyote vimekufa/vimeuzwa kwa wawekezaji je wamewekeza nini? Leo mpaka kitenge kifuatwe china? Eti "chinese wax?" Excuse me please...

Ranchi si wameuziana wenyewe?

Hadi nyumba za serikali, ambazo zipo kwenye maeneo muhimu si wameuziana wenyewe?

Loliondo si iliuzwa kwa mwarabu? Kwa nini pasingeendelezwa wamasai wale wakapata ajira na nchi ikapata pato kutokana na utalii na uwindaji

bado zengwe la mafuta na gesi.......

Watawala wa tanzania ndo tatizo wanaona mwisho a pua zao, wanaona mwisho wa familia zao, hawa watawala ndio wa kuondoka...

Tanzania inahitaji viongozi si watawala.........
Viongozi wenye maono na wanaofanyia kazi vision zao, sio vision za kwenye makaratasi ambazo hazitekelezwi either kwa makusudi au kwa udhaifu....... Kuna watu huko vijijini anakosa shilingi mia ya kununua chumvi......miaka 50 sasa ya uhuru.......

Watawala must go..... Tunahitaji tanzania mpya yenye uwajibikaji na si tanzania ya walaji.....

Hawa wapo kwenye nchi yenye Uhuru leo ni miaka zaidi ya 230 na moja katika nchi tajiri duniani:

b-w-beggars_%7EB75-287149%2BUSA%2Bevsiz%2Bissiz%2BGenc.jpg

32191-six.jpg

[h=4]Spencer Platt/Getty Images[/h] Women walk by a panhandler along Madison Avenue, one of Manhattan's premier shopping and residential streets.
 
Sioni tatizo la Utajiri, umaskini na ufukara kuwa ni la kuumiza kichwa, ni vitu tu vilivyojengwa na mifumo ya kidunia ili kuwatia watu hofu na chuki.

Wewe ndiyo chanzo cha ufukara na umaskini wetu. I hate you
 
Tusikubali kuondolewa kwenye mada kuu kwa habri za kufikirika na kutungwa. Siwezi kujibu tuhuma za kufikirika pia mbazo haziwezi kufikia hata thamani ndogo ya kusadikika.
Sio tu huko ughaibuni, hata hapa nchini akiba zangu zipo benkii za makabwela NMB na CRDB. Akiba zangu zipo wazi kwenye fomu za maadili ya umma. Sina biashara yeyote ya kunifanya kuwa na mabilioni au hata mamilioni. Wala sitegemei kuwa mfanya biashara maana mimi naamini kabisa kwenye utumishi wa umma na kwamba ukishakuwa mtumishi wa umma na ukafanya biashara lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

Nadhani tujadili mada iliyopo na tusihame mada kwa kuingiza masuala ambayo hayapo tena ya kutungwa tu. Najua wengi humu hamumjui Zitto. Mnaye Zitto wenu kichwani ambaye mnadhani ndio Zitto halisi. Iko siku mtamjua Zitto halisi ambaye hatokani na propaganda za kizushi na zenye mikakati maalumu.

Turudi kwenye mada. Tujadiliane namna ya kupambana na ufisadi ili kukuza maendeleo ya vijijini na hatimaye maendeleo ya nchi. Tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho inazidi kutanuka kutokana na mfumo wa uchumi unaozalisha 'rent seekers' badala ya wazalishaji. Tunatokaje huko? Way forward ni ipi? Mjadala uendelee

mada ni mafukara milion 30, na mabilionea 30 au sio mkuu?

Sasa kilichopelekea ufukara wa watu mil.30, ni UFISADI wa watumishi wa umma wakishirikiana na wafanyabiashara na baadhi ya wastaafu wa utumishi wa umma. Zitto zamani ulikuwa unakuja na taarifa za TAIFA KUINGIA GIZANI, ukitoa suluhisho kwa miradi ya kijanja janja, ambayo ingeligarimu taifa. Mbona baada ya mhando kuenguliwa husikiki ukizungumzia nishati, kwamba mwezi ujao kutakuwa na upungufu wa umeme?

Huoni kuwa wewe ulitumika kuwaanda watanzania kuzoea mgao ili muuze mafuta? sasa kama si uhujumu na kusababisha hao mafisadi 30 dhidi ya mafuakara mil.30 ni nini!!!!!

TUKO KWENYE MADA, HATUJATOKA NNJE. JIBU MASWALI KWANI KWA SASA WEWE NI MIONGONI MWA WANAOTUHUMIWA KWA UFISADI
 
watendaji wa serikali,wanasiasa ndo hao wafanyabiashara wa nchi hii,kiasi kikubwa imechangiwa na chama tawala kuwafata wafanyabiashara na kuwaomba kugombea nafasi za uongozi kama vile udiwani,ubunge nk.
Tenganisha siasa na biashara kwanza....alafu tuanzie hapo kuangalia other factors

Ni kweli. Lazima tuanzie hapa. Kwamba mtu anayetaka kuwa mtumishi wa umma lakini anafanya biashara aache biashara. Aweke kwenye 'blind trust' biashara zake katika kipindi chote cha utumishi wa uuma. Mataifa makubwa tena ya kibepari duniani yanafanya hivi. Sisi Taifa lililotoka kwenye ujamaa tunashindwa kuchukua hatua hii. Mara 3 nimepeleka muswada Bungeni kutaka kutungwa kwa sheria ambayo itadhibiti mgongano wa maslahi kati ya wafanyabiashara ambao ni wanasiasa na mra zote imekataliwa hata kuchapishwa kwenye gazeti la serikali (GN).

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba hapa ndio mahala pa kuanzia. Kisha uwazi wa mali za viongozi. Hivi sasa tunatangaza mali lakini wananchi hawana access. Matokeo yake ni wananchi kuwa na mawazo tofauti kuhusu viongozi wao. Daftari la mali na madeni ya viongozi liwe wazi. Mfano kwa wabunge liwekwe pale ofisi za Bunge Dar na Dodoma. Daftari liwe wazi kwenye website ya Bunge. Ili kama kiongozi amedanganya iwe rahisi kwa wananchi kumsema na kuona kuona kama anamiliki mali zaidi ya kipato chake.

Uwazi ni msingi mkubwa sana wa kupambana na ufisadi. Uwazi utaondoa majungu na kuzushiana. Uwazi utawapa nguvu wananchi juu ya viongozi wao.
 
Bilioni huanza na milioni. Ukitaka kujua naye yumo kwenye list ya watu wanaomiliki bilioni, ni kuangalia maisha yake. Sijawahi kuliona gari lake analotumia hilo hammer, lakini naambiwa ni kati ya magari wanayotumia wenye nazo. Kama hana angelipata wapi?
 
Asante kwa kujibu swali amabalo aliulizwa Mh. JK na hakujua kwa nini watanzania ni masikini japo nchi ina lasilimali za kutosha.
 
ZZK BIG UP .Uchambuzi na maelezo mazuri sana yenye takwimu nzuri sana.

Ila umesahau kuelezea nini kifanyike kwa haraka kuokoa jahazi, maana yataongelewa kila siku kwa ustadi mkubwa na bado huyu mdudu ccm bado ataendelea kutafuna hata kile kidogo tulicho nacho na KEKI ya taifa wataendelea kuila watu wachache.
 
indeed ... we will never enjoy what we call national wealth in TZ if we don't get 'responsible' leaders

who are they and what do they posses ....

je yupi anayeweza kuiba/badhirifu/miradi kati ya tajiri/mwenyenacho na maskini/asiyenacho pindi anapopewa dhamana ya uongozi ....?
 
Nasikia kumiliki vitu hivi si jambo dogo, ni mwendo mrefu. Atupe mchanganua wake ili pia tujue thamani yake halisi tulinganishe na kipato chake kwa miaka hiyo 7 ya utumishi wake kama mbunge.
 
Attachments

  • 2008-hummer-h2-8_600x0w.jpg
    2008-hummer-h2-8_600x0w.jpg
    37.1 KB · Views: 120
Tusikubali kuondolewa kwenye mada kuu kwa habri za kufikirika na kutungwa. Siwezi kujibu tuhuma za kufikirika pia mbazo haziwezi kufikia hata thamani ndogo ya kusadikika.

Sio tu huko ughaibuni, hata hapa nchini akiba zangu zipo benkii za makabwela NMB na CRDB. Akiba zangu zipo wazi kwenye fomu za maadili ya umma. Sina biashara yeyote ya kunifanya kuwa na mabilioni au hata mamilioni.

Wala sitegemei kuwa mfanya biashara maana mimi naamini kabisa kwenye utumishi wa umma na kwamba ukishakuwa mtumishi wa umma na ukafanya biashara lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

Nadhani tujadili mada iliyopo na tusihame mada kwa kuingiza masuala ambayo hayapo tena ya kutungwa tu. Najua wengi humu hamumjui Zitto. Mnaye Zitto wenu kichwani ambaye mnadhani ndio Zitto halisi. Iko siku mtamjua Zitto halisi ambaye hatokani na propaganda za kizushi na zenye mikakati maalumu.

Turudi kwenye mada. Tujadiliane namna ya kupambana na ufisadi ili kukuza maendeleo ya vijijini na hatimaye maendeleo ya nchi. Tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho inazidi kutanuka kutokana na mfumo wa uchumi unaozalisha 'rent seekers' badala ya wazalishaji. Tunatokaje huko? Way forward ni ipi? Mjadala uendelee
.

Hapo kwenye rangi ya blue ndio muhimu sana.
Sasa,wewe uko karibu sana na Rais Kikwete, umeshawahi kumuuliza kwa nini mafisadi hawachukuliwi hatua za kisheria wakati ufisadi wao uko wazi kabisa ?
Maana bila kuchukua hatua, watu wengi watatamani kuwa mafisadi, wakijua kuwa hawatachukuliwa hatua.
Hivi karibuni ulisema kuwa unawajua mafisadi walioficha pesa nje ya nchi, sasa, hatua gani umechukua ??
Ni kwa kuchukua hatua ndio tutakuwa tunapambana na ufisadi.
 
Tusikubali kuondolewa kwenye mada kuu kwa habri za kufikirika na kutungwa. Siwezi kujibu tuhuma za kufikirika pia mbazo haziwezi kufikia hata thamani ndogo ya kusadikika.

Sio tu huko ughaibuni, hata hapa nchini akiba zangu zipo benkii za makabwela NMB na CRDB. Akiba zangu zipo wazi kwenye fomu za maadili ya umma. Sina biashara yeyote ya kunifanya kuwa na mabilioni au hata mamilioni.

Wala sitegemei kuwa mfanya biashara maana mimi naamini kabisa kwenye utumishi wa umma na kwamba ukishakuwa mtumishi wa umma na ukafanya biashara lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

Nadhani tujadili mada iliyopo na tusihame mada kwa kuingiza masuala ambayo hayapo tena ya kutungwa tu. Najua wengi humu hamumjui Zitto. Mnaye Zitto wenu kichwani ambaye mnadhani ndio Zitto halisi. Iko siku mtamjua Zitto halisi ambaye hatokani na propaganda za kizushi na zenye mikakati maalumu.

Turudi kwenye mada. Tujadiliane namna ya kupambana na ufisadi ili kukuza maendeleo ya vijijini na hatimaye maendeleo ya nchi. Tofauti ya kipato kati ya wenye nacho na wasionacho inazidi kutanuka kutokana na mfumo wa uchumi unaozalisha 'rent seekers' badala ya wazalishaji. Tunatokaje huko? Way forward ni ipi? Mjadala uendelee
.
Mkuu Zitto, mimi ni mwanachama wa CDM kwa zaidi ya miaka 10, na miongoni mwa wengi wenye matumaini kuwa mwisho wa utawala wa CCM na sera zake mbovu ni 2015. Hata hivyo, mara mbili nimemskia mwenyekiti Mbowe akitoa kauli tata kuhusu mfumo unaofaa kusimamia uchumi wa nchi hii ili kuwanufaisha wananchi wote. Nasema tata kwa kuwa sijaona tofauti yake na hizi za CCM, na ninahofia tusije kufanya makosa hayahaya ya CCM tukidhani kuwa now it is our turn.

Kama chama, mna sera gani zitakazohakikisha kuwa wananchi wote wananufaika na hizi rasilmali zinazogunduliwa kama mafuta na gesi, na nyingine kama madini, mbuga za wanyama nk?
 
Ni kweli. Lazima tuanzie hapa. Kwamba mtu anayetaka kuwa mtumishi wa umma lakini anafanya biashara aache biashara. Aweke kwenye 'blind trust' biashara zake katika kipindi chote cha utumishi wa uuma. Mataifa makubwa tena ya kibepari duniani yanafanya hivi. Sisi Taifa lililotoka kwenye ujamaa tunashindwa kuchukua hatua hii. Mara 3 nimepeleka muswada Bungeni kutaka kutungwa kwa sheria ambayo itadhibiti mgongano wa maslahi kati ya wafanyabiashara ambao ni wanasiasa na mra zote imekataliwa hata kuchapishwa kwenye gazeti la serikali (GN).

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba hapa ndio mahala pa kuanzia. Kisha uwazi wa mali za viongozi. Hivi sasa tunatangaza mali lakini wananchi hawana access. Matokeo yake ni wananchi kuwa na mawazo tofauti kuhusu viongozi wao. Daftari la mali na madeni ya viongozi liwe wazi. Mfano kwa wabunge liwekwe pale ofisi za Bunge Dar na Dodoma. Daftari liwe wazi kwenye website ya Bunge. Ili kama kiongozi amedanganya iwe rahisi kwa wananchi kumsema na kuona kuona kama anamiliki mali zaidi ya kipato chake.

Uwazi ni msingi mkubwa sana wa kupambana na ufisadi. Uwazi utaondoa majungu na kuzushiana. Uwazi utawapa nguvu wananchi juu ya viongozi wao.

Hapo umesema sawasawa, lakini kama hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa, hayo yote ni bure tu.
Viongozi wetu hawa tunawafahamu, wanaweza kutangaza hadharani mali zao, na kuthibitika kuwa haziendani na mapato yao.
Halafu baada ya hapo tutawafanya nini ??
Hakuna hatua zozote zile zinazochukuliwa !!
Ndio pale wanapokuwa na jeuri na kejeli kuwa hawawezi kujiuzulu, hawawezi kuwajibika, na kutamba kuwa hawawezi kuchukuliwa hatua zozote zile.
Kiongozi anaweza kutangaza kuwa yeye ana mabilioni mengi sana kwenye account ya benki huko Uswisi. Halafu ndio tunamfanya nini ?? Wengi sana hapa Tanzania wanajulikana kuwa mabilionea wakubwa bila ya kuwa na mapato halali.
Kutaja mali hadharani peke yake haisaidii kitu.
Kinachotakiwa ni kuchukua hatua baada ya hapo !!
 
ZITTO machapisho mengi ya wasomi Maprofesa na ma Dr. yameandikwa nchi hii tena yamekaa vizuri kuliko hili la kwako.

Lakini yameshindwa kufanyiwa kazi kwa sababu za kisiasa nakushauri ungana na wenzio kwenye M4C ili muikomboe nchi 2015 ili tuweze kufanikisha hayo mawazo yako kama unadhani hayo yanawezekana CCM ikiwa madarakani haya endelea lakini am very sure unatwanga maji kwenye kinu kama na wewe si mmoja wao wanaotucheleweshea ukombozi.
 
Zitto,

Hoja ya kumtoa Pinda imeishia wapi??? au lengo lako lilikuwa kumwondoa Waziri wa fedha???

Inaonekana unataka kuanzisha Jeshi la mtu mmoja vp utafanikiwa???
 
Back
Top Bottom