Sasa nimeamini kuwa wananchi tuna safari ndefu ya kufika kanani...
Juzi CCM walikuwa na mtafaruku mkubwa kuliko huu wa CHADEMA ....wakapigana kwenye kamati kuu wametoka ..angalau hawakuja hapa kuanikana...
Wapinzani sasa mmejeuza jamboforums kuwa kamati kuu ya CHADEMA????....KWANINI mambo yenu ya ndani yasiishie ndani....hamuoni kuwa kwa mara nyingine mnawakatisha tamaa wananchi!!????
Tangu mwaka 1992 tunapambana tumeona wapinzani wakiendelea kuumizwa kwa mambo kama haya ...NCCR ya mwaka 1989 ilikuwa moto na wasomi wote ....lakini kumbe lilikuwa gari la UT la kusanya wapinzani waliokuwa wakichomoza....walishindwa kuifanya NCCR KUWA CHAMA PEKEE...
KAMAHURU na baadaye CUF ...baada ya kuungana na JAMES MAPALALA....yuko wapi mapalala?????
MREMA ..aliyevuma kama tsunami ...yupo wapi????
CHADEMA ambacho mwanzo kilikuwa chama wachache makini kisicho kuwa na watu....wengi ,miaka yote nyuma kilikuwa hakioneshi cheche..tunashukuru vijana mliochukua madaraka baada ya wazee...MTEI NA BOB MAKANI....miaka hii mitano tumeona mnapanuka na kuwapa matumaini wananchi kwa kasi ya ajabu .....sasa kwanini mnafikia kuja kuvuana nguo hapa....mmekosa vikao...
kwanini CHADEMA mnataka kuwasaliti watanzania??/
ni CHAMA gani hakina siri za ndani??? haata ndoa ina siri....na siri ni siri..???...miliosoma vitabu vya siasa mnajuwa ...wanachowashinda CCM ndio hicho...?? watu wao wameapa kutunza siri...hata waulizeni waliokuwa humo..watawambia...
chukulia mfano wa mtu kama MREMA ..Pamoja na uropokaji wake ...mambo aliyoyajuwa kwa kiapo ambayo anajuwa akiongea itakuwa kinyume hajapata kuyasema..nasema hivyo kwa sababu kuna mengi tumepata kumuuliza..anazungusha...!..anajuwa maana ya siri na adhabu ya kutowa siri anaijuwa!
Tena wapinzani mjuwe ikiwa umeenda ccm unaweza kuongea porojo zote lakini ukisema siri ambayo imekuwa rated secret...simply they kill you!!! mifano mnayo...!!!...sitaki wapinzani mfikie huuko lakini lazima mjuwe hamtakiwi kukwaruzana na kuwayumbisha wananchi namna hii......
CCM waanajuwa kuwagombanisha .....na wanaofanikiwa huzawadiwa vyeo lakini tayari wanakuwa wameshajiaharibia historia na kubeba usaliti...
watu kama ....lamwai,hizza,akwilombe.,kaborou[aliyekuwa kipenzi cha wananchi]....leo hii wakitokea mbele ya wananchi hata wanaona haya ...ukiachilia mtu kama hizza ambaye anajulikana ni mpiga domo...hawa wasomi wengine...dhamira zinawasuta....na tayari wamekosa uhalali mbele ya macho ya watu!!
....tunaomba vita dhidi ya ufisadi isitumike vibaya kuyumbisha wananchi...narejea maneno ya POLYCAP CARDINAL PENGO.."wanaopingana na ufisadi lazima wajiulize wanapigana toka moyoni au wanapigana kwa kuwa tu na wao wamekosa fursa ya kuwa mafisadi....""
CHADEMA MSIKUBALI KUTUMIWA NA MAFISADI AU HATA HAO MAKAMANDA WA MAFISADI...KWANI WANANCHI WOTE WANAJUWA NYIE NDIO WAAZILISHI WA HII VITA....MBOWE .,SLAA,...ZITTO NA WABUNGE WOTE WA CHADEMA ....SASA IWEJE LEO MNAKUBALI KUWA UNDERDOGS......ITAKUWA NI FURAHA SANA KWA MKIFARAKANA KAMA HIZI...NAPATA PICHA WANAKUNYWA MVINYO SASA.......
MSITUPELEKE HUKO!!!