Mafisadi + CCM ngao imara ya Freeman Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi + CCM ngao imara ya Freeman Mbowe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TUNTEMEKE, Sep 1, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Jamani kwa kweli nimeamini kuwa Tanzania tuna safari ndefu sana ya kufikia maendeleo endelevu. kwa sababu hata uwezo wetu wa kuchambua mambo ni mfinyu sana na mara nyingi tukiwa na upande hatutaki kufanya analysis ya kina na badala yake tunatafuta wa kumbebesha mzigo.

  katika hili ningependa tujue kuwa lazima tuweze kutofautisha kati ya Taasisi na Mtu binafsi.

  naamini taasisi kama taasisi haiwezi kufanya makosa bali watu binafsi katika taasisi wanaweza kufanya makosa na hakuna binadamu ambaye ni mkamilifu, sote tunakosea, cha msingi ni kuamua kukubaliana na kosa na kujikosoa.

  Zitto alipochukua form ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA, gazeti lake la Tanzania Daima na magazeti ya Ndugu yake Mengi yaliandika kuwa Zitto katumwa na Rostam Aziz, CCM pamoja na mafisadi wengine.

  Wangwe alipotifautiana nae, pia alikuwa katumwa na CCM + MAFISADI.

  Wanachama waliotofautiana nae hadi akawafukuza pia walikuwa wametumwa na MAFISADI + CCM.

  Je, wakati yeye anachukua pesa walizokuwa wamepewa na Conservative na kuanzisha gazeti la Tanzania Daima na miradi yake mingine alikuwa ametumwa na nani?

  Alipochukua milioni 35 za chama december 2008 na kulipia kodi ya Club Bilicanas na kumalizia ukarabati alikuwa ametumwa na nani?

  Alipopindisha na kutoa majina yaliyokuwa yameteuliwa ya Wabunge wa viti Maalum na kupeleka Wachaga watano kati ya nafasi sita na moja akampa demu wake toka Kigoma alikuwa ametumwa na nani?

  alipochukua kurugenzi zote nyeti akawapa wachaga: Kurugenzi za fedha, utawala, Rasilimali, bunge na halmashauri alikuwa katumwa na nani?

  alipolazimisha yeye na kujiweka signatory wa akaunti ya chama, na Ndugu yake Komu, John Mrema na Mweka Hazina Mchaga alikuwa katumwa na nani?

  alipopeleka tenda za kutengeneza bendera china na kumpa mchaga zabuni, na hata pikipiki za chama zikaenda nunuliwa Kilimanjaro badala ya Dar alikuwa katumwa na nani?

  aliposhindwa kufanya kazi na viongozi wenzake wakuu na hata kuwa-frustrate wengine wakarudi CCM alikuwa katumwa na nani?

  kuna na mambo mengi sana unaweza jiuliza, lakini kila mara mtu anapotofautiana na Mbowe katumwa na CCM + MAFISADI.

  kwa hiyo wanachadema tusiwe na uhuru wa kukosoa viongozi wetu?

  kwa nini makosa yanayofanywa na viongozi yanafanywa ya chama na katika kujitetea wanasema aliyesema katumwa.

  je ni kanuni za chama zinazowatuma kufanya hayo?

  kwa nini hoja zisibaki kama hoja na kama mtu akifanya kosa awajibishwe kama yeye?

  Mbona Mkapa tunasema makosa aliyoyafanya kwa biashara akiwa Ikulu siyo ya Kiofisi hivyo awajibishwe, au inapokuja kwa wengine inakuwa Mkuki kwa Nguruwe.

  Nafikiri ni vyema Wadanganyika tusiendelee kudanganyika lazima viongozi wasio na sifa hata huku kwetu (CHADEMA) wawajibishwe na sio kufumba jicho moja na kuona ya mwenzio tu.

  kwa hiyo kama kweli kila mtu anayepingana na Mbowe katumwa na CCM/MAFISADI basi Mbowe ni Malaika kutoka juu na asipingwe wala kuwajibishwa kwa makosa anayoyafaya kama kiongozi.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  ..Kama Chadema ni mali ya Wachaga kama mnavyodai basi mnapaswa kuhama na kuanzisha chame chenu cha Kitaifa.

  ..pia hivi hizi kampeni unazoziendesha dhidi ya Wachaga zina baraka za Zitto Zuberi Kabwe?
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pumba tupu
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu soma btn lines utagundua muandishi ni nani. Unganisha hii na ile thread ya kifisadi eti inayodaiwa kuwa ni ya kitabu cha wangwe.
   
 5. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  itahamishwa sasa hivi kwa kisingizio cha SERVER. umemaliza kila kitu.
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  kwangu mimi ni mchele mtupu tena wa KYELA.sokoni unaitwa SUPER KYELA.
   
 7. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ni mzimu wa Marehemu Wangwe.jee maandishi ya KIBANDA NA NGURUMO KWENYE TANZANIA DAIMA YANA BARAKA ZA MBOWE?
   
 8. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Itahamishwa na nani? mbona unapenda kulialia sana kama kitoto kichanga?
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ... ndio maana Mwakalinga mnamuita super Kyela sasa hivi. Ha ha hah ha ha. Na mkianzisha mahakama ya kiislam mtaiita super kyela pia?
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  Mwafrika,

  ..unajua kama hiki ndiyo kikundi ambacho Zitto anaji-associate nacho basi sidhani kama atafika mbali ktk masuala yake ya siasa.

  ..binafsi namsihi aje akanushe kwamba hahusiki na hii vita ya kikabila inayoendeshwa kwa niaba yake.
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Jokakuu,

  Zitto ana kazi kweli huko aendako. Kuna mtu juzi alianza kudai hapa kuwa kuna mambo ya kidini kwenye hii saga. Usishangae mtu kama Kanda2 ambaye anajulikana hapa kwa chuki zake kali dhidi ya wakristo akiwa msitari wa mbele kwenye hili swala.

  Zitto atagundua haraka sana kuwa kina kanda2 wanampoteza kwenye hili.
   
 12. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  duh jamani hata kama ni propaganda basi hebu punguzeni japo kidogo jama..
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu kanda2... Nakukubali unavyoitumia haki yako ya maoni...

  Lakini nadhani ungesoma hapa usingeandika ulichoandika... Anyway, ahsante.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  SikuIkifika Member
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Join Date: Mon Jun 2009
  Posts: 23
  Thanks: 0
  Thanked 9 Times in 7 Posts

  Jina mbadala hili....haya bwana umeskika!
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  kanda2,

  ..sidhani kama makala za Ngurumo na Kibanda zimeshambulia kabila la Zitto Kabwe.

  ..unajua haya mashambulizi dhidi ya Wachaga yameendelea hapa kwa siku karibu tatu sasa.

  ..wasije wakapewa nchi hawa halafu wakasherehekea kwa kuchinja-chinja Wachaga.

  ..ZITTO NI MWANACHAMA HAPA NA ANAPASWA KUJITOKEZA NA KUTOA KAULI YA KULAANI KIKUNDI HIKI.
   
 16. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwa nini umemhusisha moja kwa moja Zitto na kuanza kumshutumu kuwa anajihusisha na kikundi kilichoandika waraka huu? Kwa nini awe Zitto pekee na si mtu mwingine ndani ya Chadema au Chama kingine chochote cha siasa. Nadhani humtendei haki Zitto kwa kutoa shutuma bila kuonyesha ushahidi wowote unaomhusisha yeye binafsi.
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Sasa nimeamini kuwa wananchi tuna safari ndefu ya kufika kanani...

  Juzi CCM walikuwa na mtafaruku mkubwa kuliko huu wa CHADEMA ....wakapigana kwenye kamati kuu wametoka ..angalau hawakuja hapa kuanikana...

  Wapinzani sasa mmejeuza jamboforums kuwa kamati kuu ya CHADEMA????....KWANINI mambo yenu ya ndani yasiishie ndani....hamuoni kuwa kwa mara nyingine mnawakatisha tamaa wananchi!!????

  Tangu mwaka 1992 tunapambana tumeona wapinzani wakiendelea kuumizwa kwa mambo kama haya ...NCCR ya mwaka 1989 ilikuwa moto na wasomi wote ....lakini kumbe lilikuwa gari la UT la kusanya wapinzani waliokuwa wakichomoza....walishindwa kuifanya NCCR KUWA CHAMA PEKEE...

  KAMAHURU na baadaye CUF ...baada ya kuungana na JAMES MAPALALA....yuko wapi mapalala?????

  MREMA ..aliyevuma kama tsunami ...yupo wapi????

  CHADEMA ambacho mwanzo kilikuwa chama wachache makini kisicho kuwa na watu....wengi ,miaka yote nyuma kilikuwa hakioneshi cheche..tunashukuru vijana mliochukua madaraka baada ya wazee...MTEI NA BOB MAKANI....miaka hii mitano tumeona mnapanuka na kuwapa matumaini wananchi kwa kasi ya ajabu .....sasa kwanini mnafikia kuja kuvuana nguo hapa....mmekosa vikao...

  kwanini CHADEMA mnataka kuwasaliti watanzania??/

  ni CHAMA gani hakina siri za ndani??? haata ndoa ina siri....na siri ni siri..???...miliosoma vitabu vya siasa mnajuwa ...wanachowashinda CCM ndio hicho...?? watu wao wameapa kutunza siri...hata waulizeni waliokuwa humo..watawambia...

  chukulia mfano wa mtu kama MREMA ..Pamoja na uropokaji wake ...mambo aliyoyajuwa kwa kiapo ambayo anajuwa akiongea itakuwa kinyume hajapata kuyasema..nasema hivyo kwa sababu kuna mengi tumepata kumuuliza..anazungusha...!..anajuwa maana ya siri na adhabu ya kutowa siri anaijuwa!

  Tena wapinzani mjuwe ikiwa umeenda ccm unaweza kuongea porojo zote lakini ukisema siri ambayo imekuwa rated secret...simply they kill you!!! mifano mnayo...!!!...sitaki wapinzani mfikie huuko lakini lazima mjuwe hamtakiwi kukwaruzana na kuwayumbisha wananchi namna hii......

  CCM waanajuwa kuwagombanisha .....na wanaofanikiwa huzawadiwa vyeo lakini tayari wanakuwa wameshajiaharibia historia na kubeba usaliti...

  watu kama ....lamwai,hizza,akwilombe.,kaborou[aliyekuwa kipenzi cha wananchi]....leo hii wakitokea mbele ya wananchi hata wanaona haya ...ukiachilia mtu kama hizza ambaye anajulikana ni mpiga domo...hawa wasomi wengine...dhamira zinawasuta....na tayari wamekosa uhalali mbele ya macho ya watu!!

  ....tunaomba vita dhidi ya ufisadi isitumike vibaya kuyumbisha wananchi...narejea maneno ya POLYCAP CARDINAL PENGO.."wanaopingana na ufisadi lazima wajiulize wanapigana toka moyoni au wanapigana kwa kuwa tu na wao wamekosa fursa ya kuwa mafisadi....""

  CHADEMA MSIKUBALI KUTUMIWA NA MAFISADI AU HATA HAO MAKAMANDA WA MAFISADI...KWANI WANANCHI WOTE WANAJUWA NYIE NDIO WAAZILISHI WA HII VITA....MBOWE .,SLAA,...ZITTO NA WABUNGE WOTE WA CHADEMA ....SASA IWEJE LEO MNAKUBALI KUWA UNDERDOGS......ITAKUWA NI FURAHA SANA KWA MKIFARAKANA KAMA HIZI...NAPATA PICHA WANAKUNYWA MVINYO SASA.......

  MSITUPELEKE HUKO!!!
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Geeque,
  Mkuu tatizo lillipo sasa hivi ni kurushiana makombora tu..unajuaq tena mabomu ya siku hizi hayawezi ku chambua Taliban nani naraia ni nani unafagia kiijiji kizima kisha unadai vifo vya wasiokuwa na hatia ni Casualties of war..
  Yaani wee tazama jifunze kisha ujue jinsi kazi kubwa ilokuwa mbele yetu Ndivyo Tulivyo..
   
 19. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Geeque,

  Nadhani Jokakuu ametumia if...then statement hapo juu. Amesema kuwa kama Zitto anajihusisha (msisitizo kwenye kama) na kikundi hiki basi itakuwa si vyema.

  Sioni kama amemhusisha Zitto moja kwa moja.
   
 20. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mwafrika,

  Mwafrika jaribu kusoma vizuri maandishi ya JokaKuu na utaona jinsi ambavyo amemhusisha Zitto kuhusika na hiko kikundi kilichoandika waraka huu. Hapo chini ni quote yake.

  Ina maana ndani ya Chadema mtu yeyote atakayetoa tuhuma za ukabila ndani ya Chama basi anamuwakilisha Zitto au wanatoa hizo tuhuma kwa niaba yake?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...