Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Tuko naye rais wetu make hii ni kwa faida yetu na vizazi vyetu

nyie acheni ndoto , Urais ni taasisi si Mtu mmoja ni mapema sana kuanza kumchukiza Mungu , mlisema kikwete ni wa Mungu ona aliyoyafanya , mmeanza tena ! muwe na subira hamjui siasa za nchi hii haina heri
tulia siku ziende ndo utoe sifa bado mapema.

ni sawa ulivyopata Mke ukafunga ndoa , baada ya mwezi ngumi zinapigwa tulia kwanza
 
bila shaka kikwete and co wanajisikia vibaya sana kuona jamaa anavyo wa-prove wrong ktk utendaji wao.nina shaka hao ndio watakuwa wa kwanza kupanga mikakati ya kishetani ya kummaliza.magufuli my president be extra carefully.
 
Umesahau Zile Milion 50 Kwa Kila Kijiji

tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais
Fax: 255-22-2113425




PRESIDENT?S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

? Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko?. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :

​Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.

Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.

Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.

Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.

Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).

Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.

?Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao? Amesisitiza Balozi Sefue.

???Mwisho???

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu ? Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015

OMG! It is too good to believe that after all sufferings we have a person who believes that he is the president. God bless you dr. Usibadili mwendo ukakutana nawatuhumiwa wa wizi ukasema umewomba warejeshe walichoiba
 
Jibu hili limekaa vizuri sana. Tatizo la hawa wanaojiita "wapinzani" wanafikiri maana ya upinzani ni kujitoa ufahamu.
Tatizo watu wanashabikia siasa kama wanvyoshabikia mpira. Mtu akishakua yanga basi ni yangu tu milele ndiowanavyofanya siasa, hawaangalii kazi na sera za wanasiasa.
Binafsi nilikua nimeichoka CCM lakini kwa kasi hii ya Mheshimiwa raisi inanipa matumaini. Tunamuomba mungu aje apate wasaidi na mawaziri wema wenye niya nzuri na nchi yetu.
 
Ma-Tanzania sisi majinga sana, mamburura mwanzo mwisho no wonder tunafanya uchaguzi kama tumekatwa vichwa!! Hapa kigeni ni kipi? Waliopita hawakuwahi kufanya haya maigizo? Impact yake ilikuwaje? Hapa hakuna la maana linalofanyika, hebu aende akavunje mikataba mibovu huko kwenye madini na gesi ndo tumwone kweli mwanaume!! Hebu aende Stanbic akapate orodha ya watu waliobeba hela kwenye rumbesa ndo tumwelewe! Hebu afuatlie kujua kwanini home shopping centre imefunga shughuli zake ghafla hapo ndo tutamwelewa! Vinginevyo haya mengine ni maigizo tu kama ya akina Jakaya & Co Ltd.
 
Tatizo watu wanashabikia siasa kama wanvyoshabikia mpira. Mtu akishakua yanga basi ni yangu tu milele ndiowanavyofanya siasa, hawaangalii kazi na sera za wanasiasa.
Binafsi nilikua nimeichoka CCM lakini kwa kasi hii ya Mheshimiwa raisi inanipa matumaini. Tunamuomba mungu aje apate wasaidi na mawaziri wema wenye niya nzuri na nchi yetu.
Usemacho ni kweli kabisa.
 
Sipuuzi kinachofanywa na Rais Magufuli, lakini najaribu kuwakumbusha hasa wanandoa wengi ambao walizianza safari za ndoa zao kwa mbwembwe nyingi na bashasha, kwa kulishana keki kwa midomo, kwa kushikana mikono na kutembea pamoja kila pahala n.k., ..., lakini leo ndoa hizo hazitamaniki machoni pao wala machoni pa jamii...!

Ninachosema ni hiki, utukufu wa jambo lolote uko mwisho na sio mwanzo wake. Safari ya miaka mitano IKULU sio lelemama, wacha tuendelea kungoja na kuona mwisho wa safari hii kama utafafana na mwanzo wake, vinginevyo itakuwa ni kama tu 'fungate'...!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
For sure this is the kind of president we were looking for.Hata tukimtazama usoni tunaona he real mean what he is doing.
 
Magufuli rais wetu inabidi awekewe ulinzi mkubwa na mkali. wako watu wamekaa mkao wa kutaka kuhujumu kila kitu..

Usijali mkuu ulinzi anao wa kutosha kwani hata sisi watanzania tuliotengwa, watanzania kina yahe tuliopigika na ugumu wa maisha, watanzania tunaolitakia mema taifa letu mchana na usiku tunamuombea dua Rais wetu Magufuli, Mungu amlinde ampe afya njema afanye kazi ya kuwatumikia watanzania pasipo kukata tamaa... Amin!
 
Back
Top Bottom