SoC02 Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

kennedy nkya

New Member
Aug 8, 2022
2
4
Kwa Utangulizi: Sayansi Ni mmarifa au ujuzi unaopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainshwa hazijathibitishwa.Sayansi imegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo ayo makundi ni kama vile;sayansi ya asili(mfano biologia na zologia), sayansi ya umbile(mfano fizikia na kemia), sayansi ya jamii(mfano siasa na saikolojia) na sayansi ya matumizi(mfano uhandisi).

Kwa upande mwingine teknolojia ina maana ya; elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi, vifaa na mbinu za uzalilishaji wa vifaa na huduma katika jamii pia teknolojia ina maana nyingine tofauti ambazo ni kama ; ni uwezo wa kubadili malighafi asilia na kuwa bidha yenye thamani inayoweza kukidhi mahitaji ya binadamu. Mfano wa mambo hayo ni kama huduma ya usafii (kama vile mwendokasi na magari mengi pia ndege mbali mbali) ambazo zamsaidia mtu kufanikiwa kiuharaka katika kufanya shughuli zake mfano mwngine ni kama huduma ya utalii(mfano igizo la “ROYAL TOUR” limesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza idadi ya watalii katika nchi ya Tanzania ikiwa na mojawapo ya manufaa ya teknologia ambayo ilifanya kusambaa kwa igizo ilo fupi na kufanya watu waliopo nje ya Tanzania kuvutiwa kuingia katika nchi ya Tanzania).

Huduma nyingine ni huduma za chakula na huduma zinazohusu vitu vyote vinavyozalishwa kiwandani. Maendeleo ya teknologia yalihusisha uvumbuzi wa chombo cha kupigia chapa, simu janja na mitandao ambayo hufanya mawasiliano kuwa rahisi.

Sayansi na teknolojia: ni jumla ya maarifa ujuzi na elimu juu ya kutumia vyombo na ubunifu wa vitu mbali mbali katika jamii na maisha ya watu kwa ujumla. Kifupi sayansi na teknologia imesaidia sana kupunguza uzito wa mambo mengi katika dunia ya sasa tuliopo.Sayansi na teknolojia imesaidia kwa namna moja ama nyingine katika jamii ya sasa mfano wa nishati ya jua na upepo. Mchango wa sayansi na teknolojia kwa jamii ya leo umesaidia kwa namna tofauti ambazo ni kama zifuatazo:

Kwa kuanza mchango hasi sayansi na teknolojia imesaidia katika wepesi wa mawasiliano: mawasiliano ni kama vile simu za mkononi na kompyuta vimesaidia sana katika kuunganisha jamii kwa pamoja kwa mfano mtu anaweza akawa nchi nyingine tofauti na Tanzania akawasiliana na mtu aliepo Tanzania, pia imesaidia kukuza soko la ajira kama inavyonekana saivi watu wengi wamejiajiri katika uuzaji wa simu na kompyuta ili ziweze kufikia jamii zote na kurahisisha mawasiliano.

Vilevile imesaidia katika kukuza maendeleo ya biashara na tasnia: katika biashara nyingi za saivi duniani zinafanywa kwa njia ya mtandaoni kwa lugha ya kingereza wanaita “online business” ambayo imesaidia katika kukuza uchumi wa dunia na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja. Mfano wa biashara ya kuagiza vitu kama nguo na simu kutoka china kuja Tanzania ni moja wapo ya biashara za mtandaoni na pia uagizaji wa nafaka kutoka Tanzania kwenda nchi kama Botswana.

Imesaidia katika maboresho ya mchakato wa elimu :katika shule mbali apa Tanzania wanapata teknolojia hii kupitia njia za ufundishaji wao, mfano shule inaweza kuwa na kompyuta na vifaa vingine vya ufanisi ambavyo viamsaidia mwanafunzi katika kukua vyema kiakili na pia humwandaa mwanafunzi katika kuwa mbunifu wa mambo mbali mbali ya kieletroniki na kisayansi mfano utengeezwaji wa mafuta halisi utengenezwaji wa vifaa vya kurahisisha kazi za nyumbani.

Pia sayansi na teknolojia imesaidia katika miundombinu mbali mbali ya kiafya:katika hosptali kadhaa za sasa apa Tanzania zina vifaa bora ambavyo vitasaidia katika kumtunza mgonjwa na kuhakikisha mgonjwa anapona na kuwa katika hali nzuri kiafya mfano hosptali ya taifa muhimbili ilizindua kifaa cha kumfanyia mtu upasuaji wa moyo bila kusimamisha mapafu na moyo.

Tukirudi kwenye mchango chanya sayansi na teknolojia imesababisha ongezeko kubwa la watu wasio na ajira: hii ni sababu ya ubunifu wa baadhi ya vifaa vimesaidia kupunguza baadhi ya kazi zinazofanywa na mtu mmoja mmoja kazi nyingi sasa za kutumia nguvu zmekuwa zikifanywa na mashine mbali mbali zikiwemo za kieletroniki mfano zamani watu walikuwa wana ajiriwa kulima shamba kwa kutumia jembe ambayo ilisaidia wengi kupata uchumi ila kwa sasa kuna mashine mbali ikiwemo trekta ambayo inafanya kwa wepesi Zaidi na hivo kufanya ukosefu wa ajira kwa baadhi ya watu

Pia teknolojia imesabasha kwa kiasi kikubwa mabadliko ya tabia ya nchi hii ni kulingana na kuongezeka kwa teknolojia ya viwanda na mashine nyingine ambazo zimekuwa zikiharibu hali ya hewa sababu ya kutoa hewa chafu ambayo imesababisha hali ya hewa kuzorota kwa kiasi kikubwa sana na kupelekea kuongezeka kwa joto kwa kiasi kikubwa ambalo limepelekea ukosefu wa mvua na hivyo kusababisha ukosefu wa chakula kwa sehemu zinazotegema kilimo, kupitiaa mvua zinazonyesha mfano sehemu mbali mbali Tanzania mwaka huu zmekosa mvua ya kutosha hivyo kupelekea sehemu nyingine mazao kuharibika kabisa na kukauka.

Pia sayansi na teknolojia imepelekea kuongezeka kwa upungufu wa maadili kwa baadhi ya watu; Matukio mengi ya kikatili yameripotiwa kuongezeka hii ikiwa ni sababu ya uangaliaji wa video chafu mitandaoni hii ikiwemo na kesi za ulawiti na ubakaji miongoni mwa watu na hivyo kufanya kuongezeka kwa kwa magojwa mbali mbali na watoto wa mitaani wengi wasio na elimu.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameongeza wimbi la wizi na matukio mengine ya kiuhalifu: hii ni kwasababu juu la wimbi la sayansi na teknolojia vijana wengi wamejiingiza kwenye maswala ya uvutaji bangi na sigara hii ikiwa inachangia kuzorota afya za vijana hao ikiwemo afya ya akili na hivyo kufanya taifa kupoteza nguvu kazi ya vijana katika kukuza na kuiendeleza jamii

Hivyo kwa kuangalia faida za sayansi na teknolojia kuna mambo ya kuzingatia ili kupunguza michango hasi ilioletwa na sayansi na teknolojia kwa serikali kushirikiana na jeshi la polisi ili kuzuia matukio yote ya kikatili yanayotokea hii ikiwemo kushirikiana vyema na wanajamii ili kuweza kuripoti kwa matukio mbali mbali yatakayoweza kutokea.

Pia wazazi wanaswa kuwalea watoto wao katika maadili mema ya kijamii na kuwafundisha watoto wao wasiache utamaduni wao ikiwemo na mavazi hii inaiepusha kuongezeka kwa wimbi la matukio ya ubakaji katika jamii na pia kuwaelimisha kuhusu matumizi vyema ya mitandao ya kijamii ili waweze kuelewa jema na baya kwajili ya kuwakuza watoto katik kuandaa taifa lijalo

Vile vile serikali ingeshirikiana na wakulima kuwafundisha njia mbadala za kilimo ili waweze kuchukua tahadhari juu mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo kusaidia kupata chakula ma kupunguza wimbi la ukame nchini na kupanda kwa bei ya vyakula nchini.

By

Kennedy Nkya.​
 

Attachments

  • SAYANSI NA TEKNOLOJIA.docx
    269.6 KB · Views: 12
Back
Top Bottom