Umeona Pascal, wengi walikuwa hawajui kuwa unachokiongea ni kitu kipya. Soma komenti. siyo mimi peke yangu. asanteMkuu Retired, kwanza Total sio Muingereza, Total ni Mfaransa, Muingereza alikuwa Shell akageuza jina kuwa BP. Agip ni Mtaliano etc.
Vingi ya vituo vya Total, vinamilikiwa na Total wenyewe, sasa kwa vile ni kampuni ya nje, Tanzania tunafaidika na uwekezaji, miundombinu, ajira, na kodi, lakini faida ambayo ndicho kitu kikubwa kuliko vyote, inarudi kwa wenyewe. Hivyo ndivyo ilivyo kwa FDI zote.
Lakini badala ya Total kuendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo na kuvimiliki, kupitia mpango wa DODO, wanawawezesha Watanzania kumiliki kituo kwa asilimia 100%, wao wanatoa franchise ya Total, hivyo sasa net profit yote inabaki nyumbani Tanzania. McDonald's, KFC, Merry Brown etc, wote wangefanya hivyo, Tanzania tungekuwa mbali.
P.