Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station

utasemaje kuwa total ndio kituo cha kwanza kumilikiwa na mtanzania wakati kuna vituo kibao vinamilikiwa na watanzania mfano wa wanaomiliki vituo vya mafuta ni Peter zakaria, JJaphet Lema (Njake), Panone. Sango petrol station
Kituo cha kwanza cha Total kumilikiwa na mtanzania. That's the point
 
Mbona kuna vituo vingi sana vya watanzania wanavyomiliki ..bado sijaelewa Pasco kaleta mada hii kwa sababu gani
Kaja kuwafanyia matangazo hao watanzania
Kuna wabongo wangapi Wana miliki vituo vya mafuta tena zaidi ya 7
Sema mayalla kaja na style ya kuwapa kik
Labda atapewa fuel card awe anajaza bure hapo

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama ni cha mtanzania sasa iweje mseme tena ni cha total? labda mseme kinamilikiwa kati ya total na mtanzania
Ni hivi, vituo vyote vilivyoandikwa total ni mali ya kampuni ya total. Wanavimiliki wao, wewe wanakukodisha kituo chao unauza mafuta. Sasa kituo hiki ni mali ya huyo mchaga, hakodishwi, anakimili yeye. kesho anaweza kuamu kufunga na kujenga guest hapo. Vituo vya total huwezi kuvigeuza matumizi and if you mess up wanakunyanganya!
 
Ni kweli Pascal Mayala DODO ni Dealer Owned Dealer Operated.
Ila siyo utaratibu mpya wa kumiliki vituo vya mafuta ni utaratibu wa uendeshaji wa vituo vya mafuta amboa upo siku zote. Taratibu nyingine ni pamoja na CODO = Company Owned Dealer Operated, COCO=Company Owned Company Operated; DOCO=Dealer Owned Company Operated n.k.

Main disadvantage ya DODO ni kuwa lazima mafuta ununue, in this case, kutoka Total na si vinginevyo hata kama kuna kampuni inauza kwa bei ya chini kuliko Total. Lakini hili wakati mwingine huwa inakuwa relaxed kwenye mkataba. Siyo jambo jipya kabisa.
 
Pascal sjakuelewa! Kituo cha mafuta tu kama tunavyoviona vya total nchi nzima. Total ni kampuni ya wafaransa, sasa mtanzania kuwa na kituo cha total cha kuuza mafuta ndiyo iwe habari kubwa. Labda sijaelewa. Kuna vitu pale Kongowe kinaitwa Muro, ni mwafrika, so what is strange with total. Nieleweshe please wala sina nia ya kukejeli, NO!
Mkuu Retired, kwanza Total sio Muingereza, Total ni Mfaransa, Muingereza alikuwa Shell akageuza jina kuwa BP. Agip ni Mtaliano etc.

Vingi ya vituo vya Total, vinamilikiwa na Total wenyewe, sasa kwa vile ni kampuni ya nje, Tanzania tunafaidika na uwekezaji, miundombinu, ajira, na kodi, lakini faida ambayo ndicho kitu kikubwa kuliko vyote, inarudi kwa wenyewe. Hivyo ndivyo ilivyo kwa FDI zote.

Lakini badala ya Total kuendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo na kuvimiliki, kupitia mpango wa DODO, wanawawezesha Watanzania kumiliki kituo kwa asilimia 100%, wao wanatoa franchise ya Total, hivyo sasa net profit yote inabaki nyumbani Tanzania. McDonald's, KFC, Merry Brown etc, wote wangefanya hivyo, Tanzania tungekuwa mbali.

P.
 
Ni kweli Pascal Mayala DODO ni Dealer Owned Dealer Operated.
Ila siyo utaratibu mpya wa kumiliki vituo vya mafuta ni utaratibu wa uendeshaji wa vituo vya mafuta amboa upo siku zote. Taratibu nyingine ni pamoja na CODO = Company Owned Dealer Operated, COCO=Company Owned Company Operated; DOCO=Dealer Owned Company Operated n.k.

Main disadvantage ya DODO ni kuwa lazima mafuta ununue, in this case, kutoka Total na si vinginevyo hata kama kuna kampuni inauza kwa bei ya chini kuliko Total. Lakini hili wakati mwingine huwa inakuwa relaxed kwenye mkataba. Siyo jambo jipya kabisa.
ufafanuzi mzuri. hapa pascal mayala amelileta kama kitu kipya, novel invention! Pascal Mayalla . all ina ll it is good news!
 
Mkuu Retired, kwanza Total sio Muingereza, Total ni Mfaransa, Muingereza alikuwa Shell akageuza jina kuwa BP. Agip ni Mtaliano etc.

Vingi ya vituo vya Total, vinamilikiwa na Total wenyewe, sasa kwa vile ni kampuni ya nje, Tanzania tunafaidika na uwekezaji, miundombinu, ajira, na kodi, lakini faida ambayo ndicho kitu kikubwa kuliko vyote, inarudi kwa wenyewe. Hivyo ndivyo ilivyo kwa FDI zote.

Lakini badala ya Total kuendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo na kuvimiliki, kupitia mpango wa DODO, wanawawezesha Watanzania kumiliki kituo kwa asilimia 100%, wao wanatoa franchise ya Total, hivyo sasa net profit yote inabaki nyumbani Tanzania. McDonald's, KFC, Merry Brown etc, wote wangefanya hivyo, Tanzania tungekuwa mbali.

P.
asante kwa ufafanuzi. sasa nimeelewa. Nadhani wao wananufaika kwa kuuza mafuta yao kwako. Ni utaratibu mpya. Kuna mtu ameeleza humu. asante tena.
 
Back
Top Bottom