Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,
06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.
01total-tageta-launch-press-photos-jpg.990824
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (kushoto) akipokelewa na Meneja wa Sheria, Mawasiliano na Mahusiano wa Bibi Marsha Kileo Msuya (kulia) kuja kuzindua wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni mmiliki wa kituo hicho, Bw Vincent Lyimo
02total-tageta-launch-press-photos-jpg.990825

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakijiandaa kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
03total-tageta-launch-press-photos-jpg.990826

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakikata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
04total-tageta-launch-press-photos-jpg.990827

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, mara baada ya kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
05total-tageta-launch-press-photos-jpg.990828

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakirejesha vikatio mara baada kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
06total-tageta-launch-press-photos-jpg.990829

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
07total-tageta-launch-press-photos-jpg.990830
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akijaza mafuta ya kwanza, mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
08total-tageta-launch-press-photos-jpg.990831
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akijaza mafuta ya kwanza, mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
09total-tageta-launch-press-photos-jpg.990832
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wamiliki na menejiment ya Total Tageta mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Pembeni yake ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
10total-tageta-launch-press-photos-jpg.990833

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wamiliki na menejiment na wafanyakazi wa kituo kipya cha Total Tageta mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Pembeni yake ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
Wajameni, haya mambo mazuri ya Total kwa Tanzania, hawakuanza leo!.

P
 
nyamatala.

nyamatala.

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Messages
203
Likes
91
Points
45
nyamatala.

nyamatala.

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2015
203 91 45
Pascal sjakuelewa! Kituo cha mafuta tu kama tunavyoviona vya total nchi nzima. Total ni kampuni ya wafaransa, sasa mtanzania kuwa na kituo cha total cha kuuza mafuta ndiyo iwe habari kubwa. Labda sijaelewa. Kuna vitu pale Kongowe kinaitwa Muro, ni mwafrika, so what is strange with total. Nieleweshe please wala sina nia ya kukejeli, NO!
Tunataka vituo vingi vya mafuta,angarau bei itapungua,pia total ,wanamradi wa bomba la mafuta sasa wewe sjakuelewa ni Mgeni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined
Sep 13, 2017
Messages
172
Likes
111
Points
60
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined Sep 13, 2017
172 111 60

Nyamatala,

Demand ya mafuta ni inelastic Hata kwa kutumia a very simple managerial economics (and accounting) tool inayoitwa CVP Analysis haioneshi kama bei inaweza kupungua kwa kuwa na vituo vingi. Labda itachangamsha access ya bidhaa kwa watu wengi.
 
sodoliki

sodoliki

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,877
Likes
1,030
Points
280
sodoliki

sodoliki

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,877 1,030 280
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,
06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. View attachment 990824 View attachment 990825 View attachment 990826 View attachment 990827 View attachment 990828 View attachment 990829 View attachment 990830 View attachment 990831 View attachment 990832 View attachment 990833
Paschal hivi kuwuzia TOTAL mafuta ndiyo ukombozi, yaani walete mafuta wachukue 95% ya profit wewe upate 0.5% YA PROFIT UJISIFU, MFYUU HERI YA PUMA INASHARE YA SERIKALI, HII NI UTAPELI
 
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2010
Messages
1,064
Likes
961
Points
280
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2010
1,064 961 280
kitendo cha kupatiwa franchise ya Total ni mtaji mkubwa kuliko

Hajapatiwa franchise, amenunua franchise! Kwa cash au kwa mkopo!

Na hakuna cha fursa hapo!

Franchise zozote, ziwe TOTAL ziwe McDONALDS, zinauzwa kama pikipiki! Ni hela yako tu. Huyo Mfaransa aliyeuza jina la TOTAL ndio kapata fursa hapo! Mamilioni ya dola, jina tu!

Wengine tumetembea duniani humu na kufanya makazi ya pumping gas na ku befriend ma owner hao, what I can tell you ni kwamba faida ya gas station mara nyingi inategemea traffic ya kile ki convinience store cha kununulia sigara, engine oil za dharura na condom. Mafuta yenyewe sometimes ni hasara tupu! Why you think watu wanachakachua mafuta?

Wasitudanganye habari ya “changamkia fursa” wakati wao ndio wamepiga, wameuza franchise!
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Hii inamaana, kwa vile stock yote ya mafuta Tanzania ni bulk procured na standard quality ni unleaded, then Total wana futher treat their portion for adding value kwa kuongeza kiambata cha excellium kinachoyapa ubora wa juu zaidi.
P
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Paschal hivi kuwuzia TOTAL mafuta ndiyo ukombozi, yaani walete mafuta wachukue 95% ya profit wewe upate 0.5% YA PROFIT UJISIFU, MFYUU HERI YA PUMA INASHARE YA SERIKALI, HII NI UTAPELI
Ukombozi sio unauza mafuta ya nani bali Mtanzania kujengewa uwezo na kumiliki kituo cha mafuta chenye hadhi ya Total kwa 100%!. Kwenye chain international bussiness, the hardest thing to get is the franchise.

Umewahi kujiuliza kwa nini hatuna Macdonalds, unadhani waBongo hatupendi zile burggers zao?. Ni franchise!. Hata enzi za Steers nyama zilitoka South Africa. Sasa tuna KFC na MerryBrown, don't ask zinamilikiwa na nani, na kuku zinatoka wapi?, hivyo sisi kazi yetu ni to spend tuu money lakini faida inakwenda wapi?, lakini kwa huyu Mtanzania mwenye franchise ya Total, faida yote inabaki Tanzania!.
Hili ni jambo jema, jambo zuri.
P.
 
Mookiesbad98

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Messages
1,364
Likes
847
Points
280
Mookiesbad98

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2015
1,364 847 280
Asante kwa taarifa hii, iko very deep, na very informative. Pia sasa ndio nimeelewa sababu na maana ya bulk procurement ya fuel.

Pale mimi nimeitwa kuripoti ufunguzi wa kituo, lakini kiukweli supply chain ndio naisomea hapa kwako.

Hivyo kwa mujibu wa maelezo yako hata Total wananunua kwa bulk suppliers kisha ndio wana ya treat mafuta yao kwa kuongeza kiambata cha excellium!.

All and all, fuel ya Total, ndio the best in Tanzania, na kwa Tanzania Total ndio the giant, number one Afrika na number 3 duniani.

Nimeoa Moshi, hivyo Desemba hujiunga na timu ya kuhiji, kwa kutumia kagari kangu kadogo fuel economy, kwa trips za Dar-Moshi nikijaza full tank, nikifika Mombo ni empty. Lakini juzi nimejaza full tank ya mafuta ya Total excellium, amini usiamini sikujaza popote hadi MS!, na bado nikaround town kabla ya kupanda mgombani. Hivyo statement yangu hii ya mafuta ya Total, are the best, sio fagilia, ni testimonial.
P
Ni ukweli usio na Shaka mafuta ya Total excellium additive technology yanakaa muda mrefu na yanaongeza performance ya gari.

Huwa naweka mafuta ya GBP na Oil com
Na Kuna siku nimeleta Moshi kwenye gari baada ya kuchanganya mafuta ya oilcom na GBP. Ukijaza ya hizi kampuni zetu 2 zenye Bei poa humalizi wiki lazima uingie she'll na Kama unadrift njiani mafuta yanaisha kabisa. Total kwa mafuta yao wako na viwango vya Hali ya juu japo Bei yao huwa ni juu lakini it's worth it.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jidu La Mabambasi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Messages
4,611
Likes
3,667
Points
280
Jidu La Mabambasi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2014
4,611 3,667 280
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,
06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. View attachment 990824 View attachment 990825 View attachment 990826 View attachment 990827 View attachment 990828 View attachment 990829 View attachment 990830 View attachment 990831 View attachment 990832 View attachment 990833
Mkuu uko ile kitu inaitwa naive.
Mfano huo mmoja wa Total Fuel retailing hauwezi kuvutia wengi.

Wafanya biashara lukuki wanafunga biashara kwa matatizo makubwa katika shifting and unpredictable TRA Taxing policy, unstable investment policy, ruinous Banking policy(fedha yako yaweza kuwa attached any time), unfriendly Business climate na mengine mengi tu.

Fungua magazeti yoyote mainstream na uone benki zinavyotangaza kuuza collaterals, thats a failed business.

Kwa watanzania pengine a no stress "business" ni umachinga.

Nenda CBD mjini kati uone retail businesses zilizofungwa.
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,769
Likes
21,387
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,769 21,387 280
Nyamatala,

Demand ya mafuta ni inelastic Hata kwa kutumia a very simple managerial economics (and accounting) tool inayoitwa CVP Analysis haioneshi kama bei inaweza kupungua kwa kuwa na vituo vingi. Labda itachangamsha access ya bidhaa kwa watu wengi.
Nyamatala nadhani ni layman, hajaenda shule. Huyu hafai kumjibu unapoteza muda wako. Nadhani katika thread nzima ndiye ameandika rubbish!
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Mkuu uko ile kitu inaitwa naive.
Mfano huo mmoja wa Total Fuel retailing hauwezinkuvutia wengi.

Wafanya biashara lukuki wanafunga biashara kwa matatizo makubwa katika shifting and unpredictable TRA Taxing policy, unstable investment policy, ruinous Banking policy(fedha yako yaweza kuwa attached any time), unfriendly Business climate na mengine mengi tu.

Fungua magazeti yoyote mainstream na uone benki zinavyotangaza kuuza collaterals, thats a failed business.

Kwa watanzania pengine a no stress "business" ni umachinga.

Nenda CBD mjini kati uone retail businesses zilizofungwa.
Mkuu Jidu, sio being naive but ni optimastic than pesimistic, I see things with positivism wakati wengi wetu ni fault finders na much negativity. Ukifurahia maisha ya Mtanzania mmoja akiyefanikiwa, watu negatives wataponda.

Ni kweli Tanzania tunapita kipindi kigumu cha changamoto za kiuchumi, biashara zinafungwa, vyuma vinabana, hata mimi na kakampuni kangu kangu ka PR kameathirika na nilizungumza humu

Lakini pamoja na changamoto zote hizo za
matatizo makubwa katika shifting and unpredictable TRA Taxing policy, unstable investment policy, ruinous Banking policy, unfriendly Business climate na mengine mengi tu, hakutuzuii kusifia mazuri yanayofanyika kama hili la Total
P.
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,769
Likes
21,387
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,769 21,387 280
Mkuu Jidu, sio being naive but ni optimastic than pesimistic, I see things with positivism wakati wengi wetu ni fault finders na much negativity. Ukifurahia maisha ya Mtanzania mmoja akiyefanikiwa, watu negatives wataponda.

Ni kweli Tanzania tunapita kipindi kigumu cha changamoto za kiuchumi, biashara zinafungwa, vyuma vinabana, hata mimi na kakampuni kangu kangu ka PR kameathirika na nilizungumza humu

Lakini pamoja na changamoto zote hizo za
matatizo makubwa katika shifting and unpredictable TRA Taxing policy, unstable investment policy, ruinous Banking policy, unfriendly Business climate na mengine mengi tu, hakutuzuii kusifia mazuri yanayofanyika kama hili la Total
P.
Pascal, these are petty things! beneficial at individual basis not at national level. Tunataka vitu vitakavyoinua wengi... Norway walipogundua mafuta, Norway ikabadilika ikawa kama ilivyo!(nimefundisha Norway, ninasema nilicho na uhakika nacho)
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Nyamatala nadhani ni layman, hajaenda shule. Huyu hafai kumjibu unapoteza muda wako. Nadhani katika thread nzima ndiye ameandika rubbish!
Mkuu Retired, nadhani sio haki kumdegrade mtu kuwa hajaenda shule kwa kutojua the
inelasticty ya biashara ya mafuta, na katika kuheshimu the freedom of opinion, usidharau maoni ya mtu na kuyaita rubbish, kwa sababu ganda la mua la jana, ambalo kwa mmoja ni rubbish, kwa chungu ni kivuno cha mlo wa wiki nzima.
P.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Pascal, these are petty things! beneficial at individual basis not at national level. Tunataka vitu vitakavyoinua wengi... Norway walipogundua mafuta, Norway ikabadilika ikawa kama ilivyo!(nimefundisha Norway, ninasema nilicho na uhakika nacho)
Mkuu Retired, japo chururu si ndondondo, kwa upande wa speed ya kujaza ndoo, lakini kwa ndondondo hiyo hiyo, ikilala usiku kucha asubuhi ndoo inajaa.

National economic development inakuwa realized by both macro economics na micro economics, hivyo ndivyo walivyofanya Tiger nations na China, inua uchumi wa mtu mmoja mmoja na collectively watainua uchumi wa taifa. Kilichowainua Wschagga na Wahaya hadi kuongoza kwa kuelimika ni micro economics za zao la kahawa. Kama Watanzania wote, wangekuwa kama Wachagga na Wahaya kwa maendeleo, tungekuwa wapi?.

Maendeleo ya kweli ya Tanzania, yataletwa na Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa lao, waliopata exposure za kimataifa ughaibuni na kuleta hizo exposure nyumbani. Norway ni moja ya mataifa yenye the best oil and gas laws and regulations, sasa wewe kama umefundisha Norway, na sisi ndio tumegundua gas, kwa uzoefu wako, unalisaidiaje taifa letu sio tuwe kama Norway, but angalau tukaribiane?.

Hivi ndio vitu vya wana diaspora wa Tanzania kuifanyia nchi yao na sio kuteletea tuu makontena ya used items wanazookota huko.
P
 
Hossam

Hossam

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Messages
2,804
Likes
529
Points
280
Hossam

Hossam

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2011
2,804 529 280
Pascal sjakuelewa! Kituo cha mafuta tu kama tunavyoviona vya total nchi nzima. Total ni kampuni ya wafaransa, sasa mtanzania kuwa na kituo cha total cha kuuza mafuta ndiyo iwe habari kubwa. Labda sijaelewa. Kuna vitu pale Kongowe kinaitwa Muro, ni mwafrika, so what is strange with total. Nieleweshe please wala sina nia ya kukejeli, NO!
Pascal angebakigi na siasa tu, hivi kumbe wakala wa Voda nayeye ni kampuni kumbe bwaaahahahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
elvischirwa

elvischirwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
2,928
Likes
1,970
Points
280
elvischirwa

elvischirwa

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
2,928 1,970 280
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,
06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. View attachment 990824 View attachment 990825 View attachment 990826 View attachment 990827 View attachment 990828 View attachment 990829 View attachment 990830 View attachment 990831 View attachment 990832 View attachment 990833

Wajameni, haya mambo mazuri ya Total kwa Tanzania, hawakuanza leo!.

P
Tangazo hilo la biashara halistahili kuwa ukurasa huu wa siasa, upeleke kwenye hoja mchanganyiko. JF inatakiwa ikuletee bili ya matangazo ya biashara.
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,769
Likes
21,387
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,769 21,387 280
Mkuu Retired, japo chururu si ndondondo, kwa upande wa speed ya kujaza ndoo, lakini kwa ndondondo hiyo hiyo, ikilala usiku kucha asubuhi ndoo inajaa.

National economic development inakuwa realized by both macro economics na micro economics, hivyo ndivyo walivyofanya Tiger nations na China, inua uchumi wa mtu mmoja mmoja na collectively watainua uchumi wa taifa. Kilichowainua Wschagga na Wahaya hadi kuongoza kwa kuelimika ni micro economics za zao la kahawa. Kama Watanzania wote, wangekuwa kama Wachagga na Wahaya kwa maendeleo, tungekuwa wapi?.

Maendeleo ya kweli ya Tanzania, yataletwa na Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa lao, waliopata exposure za kimataifa ughaibuni na kuleta hizo exposure nyumbani. Norway ni moja ya mataifa yenye the best oil and gas laws and regulations, sasa wewe kama umefundisha Norway, na sisi ndio tumegundua gas, kwa uzoefu wako, unalisaidiaje taifa letu sio tuwe kama Norway, but angalau tukaribiane?.

Hivi ndio vitu vya wana diaspora wa Tanzania kuifanyia nchi yao na sio kuteletea tuu makontena ya used items wanazookota huko.
P
Well said Pascal, umeongea vizuri sana. Norway walikuwa na UONGOZI bora! Nikisema Uongozi bora ni kutoka kwenye roho zao.. the innermost chamber of their hearts full with patriotism! je sisi tuna viongozi kama hao? Mkapa aliishia kujiuzia Kiwila kwa bei ya kutupa! Wa sasa (simtaji) ameishia kujenga kwao vitu vya kula hela ya walalahoi!
You have made my day, eti used items kwenye container kuzileta huku! But remeber, from Rags to riches!
 
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined
Sep 13, 2017
Messages
172
Likes
111
Points
60
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined Sep 13, 2017
172 111 60
Hii inamaana, kwa vile stock yote ya mafuta Tanzania ni bulk procured na standard quality ni unleaded, then Total wana futher treat their portion for adding value kwa kuongeza kiambata cha excellium kinachoyapa ubora wa juu zaidi.
P
Pascal hiyo ndiyo maana ya ya unleaded seriously? Just google search it. Ni shule nzuri kidogo.
 
Forum statistics

Threads 1,250,078
Members 481,222
Posts 29,720,091