Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,
06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.
01total-tageta-launch-press-photos-jpg.990824
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (kushoto) akipokelewa na Meneja wa Sheria, Mawasiliano na Mahusiano wa Bibi Marsha Kileo Msuya (kulia) kuja kuzindua wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni mmiliki wa kituo hicho, Bw Vincent Lyimo
02total-tageta-launch-press-photos-jpg.990825

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakijiandaa kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
03total-tageta-launch-press-photos-jpg.990826

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakikata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
04total-tageta-launch-press-photos-jpg.990827

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, mara baada ya kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
05total-tageta-launch-press-photos-jpg.990828

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kushoto) na wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wakirejesha vikatio mara baada kukata utepe kuzindua kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni.
06total-tageta-launch-press-photos-jpg.990829

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
07total-tageta-launch-press-photos-jpg.990830
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akijaza mafuta ya kwanza, mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
08total-tageta-launch-press-photos-jpg.990831
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres akijaza mafuta ya kwanza, mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Katikati ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
09total-tageta-launch-press-photos-jpg.990832
Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wamiliki na menejiment ya Total Tageta mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Pembeni yake ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
10total-tageta-launch-press-photos-jpg.990833

Makamo rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika, Kaskazini, Kati na Afrika Mashariki, Jean Philippe Torres (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wamiliki na menejiment na wafanyakazi wa kituo kipya cha Total Tageta mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kwanza cha mafuta cha DODO jijini Dar es Salaam,ambacho ni kilichoko Tageta, katika tukio lililofanyika hivi karibuni. Pembeni yake ni wamiliki wa kituo hicho, Bw na Bibi Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo.
Wajameni, haya mambo mazuri ya Total kwa Tanzania, hawakuanza leo!.

P
 
REDEEMER.

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Messages
5,994
Likes
8,766
Points
280
Age
26
REDEEMER.

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2015
5,994 8,766 280
Mbona ukienda kituo cha mafuta cha Total karibu na Uwanja wa Taifa ukiwepa EFD inaandika kampuni ya kitanzania sasa sielewi hii inakuaje habari kubwa...mara kusifia awamu ya tano yani nashindwa kupata connection kabisa
Main point hapo ni "awamu ya 5" acheni unafki, ccm ina wanachama kama ilivyo upinzani, ni kama hamtaki kabisa kusikia serikali ikipewa sifa, japo hamzidi watatu lakini kelele nyingi.
img_20181023_183628-jpg.991029
 
M

Mzee Mwenzangu

Senior Member
Joined
Dec 23, 2013
Messages
133
Likes
79
Points
45
M

Mzee Mwenzangu

Senior Member
Joined Dec 23, 2013
133 79 45
Wanabodi,

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere alisema, Maendeleo ya kweli yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kumiliki njia kuu za uchumi na uzalishaji mali, ili faida yote itakayozalizwa, ibaki nchini.

Katika kulitekeleza hili, Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa mambo mapya kuhusu umiliki wa vituo vya mafuta vya Total, ambapo imekuja na mpango kamambe uitwao DODO, kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta vya Total.

Fuatilia taarifa hii.
, ,
06/01/2019. Mwaka Mpya na Mambo Mapya, Total Yaja na Kitu Kipya, Yaipongeza Tanzania Kuendelea Kuwa Nchi ya Fursa, Yawataka Watanzania Kuchangamkia Fursa.

Kampuni ya Mafuta ya Total, imeuanza mwaka mpya kwa kuwaletea Watanzania kituo kipya cha mafuta cha aina yake, na kummpongeza rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5, kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya uwekezaji, kuifanya Tanzania kuendelea kuwa ni miongoni mwa nchi za Afrika inayoongoza kwa uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuleta maendeleo, na kuwataka Watanzania kuzichangamkia fursa hizo na kuzitumia kujiletea maendeleo yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamo Rais wa kampuni ya mafuta ya Total Kanda ya Afrika ya Kaskazini, Kati na Afrika ya Mashariki, Jean Philippe Torres, wakati wa uzinduzi wa kituo kipya na cha kwanza cha mafuta cha Total ambacho kinamilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100% kwa mtindo unaoitwa DODO, cha Total Tageta Service Station kilichozinduliwa mwishoni mwa wiki (jana).

Bwana Torres amesema Tanzania inazo fursa nyingi sana na uwekezaji ambazo kama zitachangamkiwa, zitataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania na taifa kwa ujumla, na maendeleo hayo yatakuwa na manufaa zaidi, endapo fursa hizo zitachangamkiwa na Watanzania wenyewe na makampuni ya Kitanzania, kitu kinachotakiwa ni kwa Watanzania kuangaziwa fursa zilizopo, kisha wahamasishwe kuchangamkia fursa hizo kwa kujengewa uwezo wa kimitaji, kiutaalam, kitekinolojia na kiuendeshaji, kuweza kuzitumia fursa hizo kuchochea maendeleo ya Watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Kituo cha Mafuta cha Total Tageta ni mfano hai wa kuigwa, ambapo Mtanzania mmiliki wa eneo hilo, ameangaziwa fursa, na yeye kuchangamkia fursa hiyo, hivyo Total Tageta Service Station ndicho kituo cha kwanza cha kujengwa Tanzania kwa kumilikiwa na Mtanzania na kuendeshwa na Mtanzania kupitia utaratibu wa Kampuni ya Total kuwawezesha Watanzania kumiliki vituo vya mafuta unaoitwa DODO.

Akifafanua kuhusu DODO, Mkurugenzi wa Sheria na Ushirikiano wa Makampuni wa Total Tanzania, Marsha Kileo Msuya, amesema DODO ni kifupi cha maneno “Dealer Owned, Dealer Operated” ambapo kampuni ya Total inawawezesha Watanzania wenye nia ya kufanya biashara ya mafuta, kwa kuwaangazia fursa na kuwajengea uwezo wa kumiliki vituo vya mafuta vya Total na kuviendesha wenyewe, Total wao wanawapatia viwango vya ubora wa kimataifa wa vituo vya Total, misaada ya kitaalamu, kuwapatia wasimamizi wa ujenzi wa viwango vyao, na mwisho kuwapatia jina kubwa la Total na bidhaa za Total kwa utaratibu wa kibiashara unaoitwa franchise, hivyo vituo hivyo vya DODO, vina jina kubwa la Total, lakini vinamilikiwa na kundeshwa na watu binafsi Watanzania wa kawaida wenye kuchangamkia fursa.

Kwa upande wao, wamiliki wa kituo hicho cha Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, kwa Total kutambua fursa walionayo, wakawaita kuwaonyesha fursa hiyo, na wao bila kuchelewa, wakaichangamkia fursa hiyo, ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho. Mama Mary Lymo amemshukuru Mungu na mume wake Vincent Lymo kwa kuwawezesha kuchangamkia fursa hiyo.

Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total

Total Kimataifa ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa kimataifa na ni moja ya makapuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi zaidi ya 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. View attachment 990824 View attachment 990825 View attachment 990826 View attachment 990827 View attachment 990828 View attachment 990829 View attachment 990830 View attachment 990831 View attachment 990832 View attachment 990833
Mkuu Pascal
Lifafanue kwa maneno machache ili hii fursa isiwe fumbo.
Kwamba kwa mtanzania anaihitaji DODO. anatakiwa kuwa na vigezo gani kwa kuanza.
Mfano:
1. Kiwanja kilichopimwa, mengine TOTAL atamalizia
2. Kiwanja na uwezo wa kujenga mwenyewe kwa std za TOTAL
3. Aweze 1,2 na aweza na mtaji, TOTAL wao ni utaalamu na ushauri
4. Weka wazi huo ushauri wa TOTAL kama ni bure au unalipiwa.
Pia weka mawasiliano wenye dukuduku wawatafute wahusika huko TOTAL maana kama ni fursa haiwezi kuwa sapuraizi kama ulivyoileta hapa

MM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Messages
1,281
Likes
464
Points
180
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2014
1,281 464 180
Kumbe Maylla presenter wa nguvu? Yupo media ipi ? maana tunagongana vikumbo humu nimeona sura ndo namkumbuka sura.
 
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Messages
1,281
Likes
464
Points
180
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2014
1,281 464 180
Main point hapo ni "awamu ya 5" acheni unafki, ccm ina wanachama kama ilivyo upinzani, ni kama hamtaki kabisa kusikia serikali ikipewa sifa, japo hamzidi watatu lakini kelele nyingi. View attachment 991029 Mmmm hapa chadema haihitahi Cardiac Arrest kweli? ama Oxygen machine itatosha.
 
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Messages
1,281
Likes
464
Points
180
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2014
1,281 464 180
Mkuu Pascal
Lifafanue kwa maneno machache ili hii fursa isiwe fumbo.
Kwamba kwa mtanzania anaihitaji DODO. anatakiwa kuwa na vigezo gani kwa kuanza.
Mfano:
1. Kiwanja kilichopimwa, mengine TOTAL atamalizia
2. Kiwanja na uwezo wa kujenga mwenyewe kwa std za TOTAL
3. Aweze 1,2 na aweza na mtaji, TOTAL wao ni utaalamu na ushauri
4. Weka wazi huo ushauri wa TOTAL kama ni bure au unalipiwa.
Pia weka mawasiliano wenye dukuduku wawatafute wahusika huko TOTAL maana kama ni fursa haiwezi kuwa sapuraizi kama ulivyoileta hapa

MM

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania tusipochange dunia tutaiweza kweli maana hapo Franchise standard lazima ziwe maintained na nijuavyo watz hasa customer service ni janga la kitaifa
 
Mookiesbad98

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Messages
1,364
Likes
847
Points
280
Mookiesbad98

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2015
1,364 847 280
Paskali down payment au mtaji unaotakikana mpaka ukamiliki kituo Cha total ni Bei Nani. Bond unaweka Bei gani na masharti mengine Kama ardhi. Na faida unaipataje. Tafdhali ukishindwa patch the query to Total TZ wake waainishe ili kila mwenye kuweza achunguoie hiyo fursa sio akina Msuya peke yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2010
Messages
1,064
Likes
961
Points
280
Tindikali

Tindikali

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2010
1,064 961 280
ambapo kampuni ya Total wakawajengea uwezo wa kimitaji, kitaalamu na kiuendeshaji, sasa wao ni wamiliki wa kituo hicho.
TOTAL wanauza franchise, sasa sijui wanakujengea vipi uwezo kimtaji?

Unless wamewakopesha kwa dhamana ya kiwanja chao, in which case TOTAL watakula faida ya mauzo, riba ya mkopo na kodi watalipiwa na mswahili kwa miaka 10 kama sio 30.

Hakuna kabaila, capitalist, anakuja toka Ulaya kwa dhumuni la kuwasaidieni kumiliki vituo vyao vya mafuta, hata wamishenari hawakuwa wema kiasi hicho, walimtangaza Yesu na Muhammed na wakawabeba utumwani.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
Mafuta huwa yanaletwa kwa meli moja kwa makampuni yote na yanapakuliwa kwenda depot yoyote ambayo aliyeangiza mafuta anamwelekeza TPA/TRA kuyapeleka. Quality ya mafuta hupimwa kwa kuchukua mafuta kwenye meli na kupimwa na kuthibitishwa kwamba ndiyo inayotakiwa. Kama quality haifikii viwango vya Tanzania mafuta hayawezi kupakuliwa. Baada ya hapo wahusika hutoa amri ya kupakua mafuta. Baada ya mafuta kupakuliwa sampuli huchukuliwa kutoka kwenye depot zilizopokea na kupimwa ili kuthibitisha ubora wake kama unafanana na ule wa mafuta yaliyopimwa kabla ya kupakuliwa. Kama quality ya mafuta ikosawa depot huruhusiwa kuanza kutoa mafuta. Mafuta hayo hayo ndiyo yanayopelekwa vituoni viwe vya Total au kampuni nyingine yeyote. Unleaded petrol (kama wasomaji wanaelewa maana yake) ndiyo yanayopokelewa Tanzania hata kama kituo hakijaonyesha hivyo kwenye matangazo yake. Tatizo linajitokeza pale ambapo mwenye kituo anaamua kuchanganya mafuta kama ilivyokuwa zamani ili ku take advantage ya tofauti ya bei. Kwa mfano kama bei ya lita moja ya petrol ni shilingi 2000 na dizeli ni shilingi 2300 ukichukua lita mmbili za petroli ukachanganya na lita nane za diseli utapata liata kumi za dizeli. Ukiuza lita zote kumi (dizeli) utapata shilingi 23,000 badala ya ungepta shilingi 22,400 yaani (2x2,000) petrol + (8x2,300) dizeli. Sasa piga hesabu kwa proportions hizo hizo kwa lita milioni 5 za dizeli iliyokwisha changanywa utapata shilingi ngapi? Tatizo hili siku hizi limedhibitiwa na EWURA kwa kiasi kikubwa mno. Hakuna kampuni inayochanganya mafuta yakiwa depot hata kidogo labda EWURA wafumbe macho. Mafuta kuwa kwenye kidumu kama hayajachakachuliwa ni sawa na wewe unapokuwa na mafuta kwenye tanki la gari kama hayajachakachuliwa. Ila Pascal ninkupongeza sana kwa taarifa. Ni vyema ku counter check na authorities ili kutokutoa taarifa ambazo ukweli wake una mashaka
Asante kwa taarifa hii, iko very deep, na very informative. Pia sasa ndio nimeelewa sababu na maana ya bulk procurement ya fuel.

Pale mimi nimeitwa kuripoti ufunguzi wa kituo, lakini kiukweli supply chain ndio naisomea hapa kwako.

Hivyo kwa mujibu wa maelezo yako hata Total wananunua kwa bulk suppliers kisha ndio wana ya treat mafuta yao kwa kuongeza kiambata cha excellium!.

All and all, fuel ya Total, ndio the best in Tanzania, na kwa Tanzania Total ndio the giant, number one Afrika na number 3 duniani.

Nimeoa Moshi, hivyo Desemba hujiunga na timu ya kuhiji, kwa kutumia kagari kangu kadogo fuel economy, kwa trips za Dar-Moshi nikijaza full tank, nikifika Mombo ni empty. Lakini juzi nimejaza full tank ya mafuta ya Total excellium, amini usiamini sikujaza popote hadi MS!, na bado nikaround town kabla ya kupanda mgombani. Hivyo statement yangu hii ya mafuta ya Total, are the best, sio fagilia, ni testimonial.
P
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
TOTAL wanauza franchise, sasa sijui wanakujengea vipi uwezo kimtaji?.
Utajiri mkubwa kabisa ni utajiri wa fikra, na umasikini mkubwa zaidi ni umasikini wa fikra.

Kwenye chain bussiness yoyote, the biggest asset ni franchise. Kitendo tuu cha kuangaziwa fursa ni utajiri mkubwa, kitendo cha kupatiwa franchise ya Total ni mtaji mkubwa kuliko, ili kuweza kupata mtaji wa kujengea ni lazima uwe na bussiness mind kuitumia hiyo franchise na land yako as a colateral ya kusecure loan ya kujengea.

P.
 
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined
Sep 13, 2017
Messages
172
Likes
111
Points
60
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined Sep 13, 2017
172 111 60

excellium maana yake ni nini kwa lugha rahisi? Hakuna treatment yoyote ya mafuta inayofanyika baada ya kupokelewa depot. Labda kuweka rangi tu labda kama ndiyo unayosema ni treatment.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,603
Likes
32,143
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,603 32,143 280
excellium maana yake ni nini kwa lugha rahisi? Hakuna treatment yoyote ya mafuta inayofanyika baada ya kupokelewa depot. Labda kuweka rangi tu labda kama ndiyo unayosema ni treatment.
Excellium ni kiambata kwenye mafuta ya total kinachoboost cumbustion kwa kutumia mafuta kidogo na kudumisha engine ya gari yako idumu zaidi kwa kuzuia wear and tear.
P
 
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined
Sep 13, 2017
Messages
172
Likes
111
Points
60
T

ThnkingAloud

Senior Member
Joined Sep 13, 2017
172 111 60
Utajiri mkubwa kabisa ni utajiri wa fikra, na umasikini mkubwa zaidi ni umasikini wa fikra.

Kwenye chain bussiness yoyote, the biggest asset ni franchise. Kitendo tuu cha kuangaziwa fursa ni utajiri mkubwa, kitendo cha kupatiwa franchise ya Total ni mtaji mkubwa kuliko, ili kuweza kupata mtaji wa kujengea ni lazima uwe na bussiness mind kuitumia hiyo franchise na land yako as a colateral ya kusecure loan ya kujengea.

P.
Pascal you are partly right. Kwenye franchise huwa kuna ada ya kulipa kwa kutumia hiyo franchise. Mkataba wao unasema hivyo? Hiyo haina maana kwa sababu inaongeza gharama ya kuendesha kituo.
 
Twilumba

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Messages
6,737
Likes
1,543
Points
280
Twilumba

Twilumba

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2010
6,737 1,543 280
Duh bonge la shule.... Asante
Asante kwa taarifa hii, iko very deep, na very informative. Pia sasa ndio nimeelewa sababu na maana ya bulk procurement ya fuel.

Pale mimi nimeitwa kuripoti ufunguzi wa kituo, lakini kiukweli supply chain ndio naisomea hapa kwako.

Hivyo kwa mujibu wa maelezo yako hata Total wananunua kwa bulk suppliers kisha ndio wana ya treat mafuta yao kwa kuongeza kiambata cha excellium!.

All and all, fuel ya Total, ndio the best in Tanzania, na kwa Tanzania Total ndio the giant, number one Afrika na number 3 duniani.

Nimeoa Moshi, hivyo Desemba hujiunga na timu ya kuhiji, kwa kutumia kagari kangu kadogo fuel economy, kwa trips za Dar-Moshi nikijaza full tank, nikifika Mombo ni empty. Lakini juzi nimejaza full tank ya mafuta ya Total excellium, amini usiamini sikujaza popote hadi MS!, na bado nikaround town kabla ya kupanda mgombani. Hivyo statement yangu hii ya mafuta ya Total, are the best, sio fagilia, ni testimonial.
P
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,250,080
Members 481,222
Posts 29,720,197